Monday, June 30, 2014

Mhe. Membe amuaga rasmi Balozi wa Afrika Kusini nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumuaga aliyekuwa Balozi wa Afrika Kusini hapa nchini, Mhe. Thanduyise Henry Chiliza ambaye amemaliza muda wake wa kazi. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency (Kilimanjaro) Jijini Dar es  Salaam.
Balozi Chiliza (kulia) akiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha (katikati) pamoja na Balozi wa Nigeria hapa nchini, wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kumuaga Balozi Chiliza.
Balozi Chiliza nae akizungumza 
Mhe. Membe na Balozi Chiliza wakigonganisha glasi kutakiana afya njema na ushirikiano imara kati ya Tanzania na Afrika Kusini
Mhe. Membe akimkabidhi Balozi Chiliza zawadi ya picha ya kuchora ya Mlima Kilimanjaro.
Picha ya pamoja

Picha na Reginald Philip

Mhe. Membe amuaga rasmi Balozi wa Somalia nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Balozi wa Somalia hapa nchini, Mhe. Abdihakim Ali Yasin ambaye alifika Ofisini kwake  kwa ajili ya kumuaga rasmi baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini.
Mhe. Membe akimsikiliza Mhe. Balozi Yasin alipofika Ofisini kwake kwa lengo la kumuaga.
Mhe. Membe akiagana na Balozi Yasin
Mhe. Membe akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Yasin pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga (kushoto), Bi. Faduma Abdullahi Mohamud (wa pili kutoka kulia), Afisa kutoka Ubalozi wa Somalia hapa nchini na Bw. Bujiku Sakila (kulia), Afisa Mambo ya Nje.



Saturday, June 28, 2014

Hon.Membe Guest of Honour at Pope's anniversary


The Minister for Foreign Affairs and International Co-operation, Hon. Bernard Kamilius Membe (MP), speaking at the ceremony, hosted by the latter in Dar es Salaam on Friday evening to mark the first anniversary of the pontificate of Pope Francis. Hon. Membe praised Pope Francis for his "focused direction on world peace and harmony." He said the word of GOD upheld by all faiths preached love, which was the cornerstone for world peace, stability and development. "I believe that the voice of the Pope will remain strong and continue to be heard and provide guidance to us and to the people of the world," he said.
Bishops and invited guests listen to the speech by Hon. Membe
Hon. Bernard Membe listens to the speech by the Apostolic  Nuncio in Tanzania, Archbishop Francisco Montecillo Padilla.
Retired President Benjamin Mkapa (Right)  follows events at the ceremony to mark the first anniversary of the pontificate of Pope Francis. Left is the Dean of Diplomatic Corps, Ambassador Juma-Alfani Mpango
Members of the diplomatic community follow the speech by Hon. Membe
 Minister Membe, exchanges views with the Apostolic Nuncio in Tanzania, H.E. Archbishop Francisco Montecillo Padilla (Centre) during the ceremony. Left is retired President Benjamin Mkapa. 
Minister Membe greets Bishop Methodius Kilaini at the function
Hon. Membe has a word with Bishops.
Invited guests follow the proceedings
The Director of Europe and America in the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation, Ambassador Joseph Edward Sokoine  exchanges views with the British High Commissioner to Tanzania, Ambassador Dianna Melrose, at the ceremony.
The Minister for Lands and Human Settlements Development, Prof. Anna Tibaijuka, meets the Swedish Ambassador to Tanzania, H.E. Lenarth Hjelmaker.
Hon. Membe, Prof. Tibaijuka and Ambassador Mpango (Left) pose with the bishops
Archbishop Padilla bids farewell to Hon. Membe at  the end of the ceremony


Photo: Reginald Philip






Friday, June 27, 2014

Naibu Katibu Mkuu afunga rasmi mafunzo ya SOFREMCO

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili katika Chuo cha Diplomasia (CFR) kilichopo Kurasini Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuwakabidhi Vyeti Wahitimu 30 wa Mafunzo Maalum kwa Maafisa Waandamizi  wa Mambo ya Nje (SOFREMCO) kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, (kushoto) ni Kaimu mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia Dr. Bernard Archiula.
Balozi Gamaha akihutubia kabla ya kutoa vyeti kwa wahitimu hao (hawapo pichani)
Wahitimu wakimsikiliza Balozi Gamaha (hayupo pichani) alipozungumza nao.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Diplomasia, Balozi Mwanaidi Maajar naye akizungumza na Wahitimu wa Mafunzo Maalum kwa 
Sehemu ya Wahitimu hao wakimsikiliza Balozi Maajar (hayupo pichani)
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Diplomasia, Dkt. Bernard Achiula akizungumza na wahitimu hao.
Sehemu nyingine ya wahitimu hao.
Mwakilishi wa Wahitimu hao, Bw. Hassan Mwamweta  akitoa neno la shukrani.
Balozi Gamaha akimkabidhi Cheti  kwa mmoja wa Wahitimu hao Bi. Rose Kitandula.
Balozi Gamaha akimkabidhi cheti Bw. Idd Bakari mbaye ni mmoja wa Wahitimu hao
Picha ya pamoja

Picha na Reginald Philip

Makamu wa Rais wa China amaliza ziara yake nchini


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mohamed Gharib Bilal akiagana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao baada ya kukamilisha ziara yake ya siku sita hapa nchini. Wakati wa ziara hiyo Mhe. Li alisaini mikataba mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na China pia alipata fursa ya kutembelea sehemu mbalimbali ikiwemo Zanzibar, Ngorongoro pamoja na kukabidhi gari la kurushia matangazo ya Televisheni  nje ya studio (OB Van) kwa Shirika la Utangazaji la Tanzanaia (TBC).
Mhe. Li Yuanchao akiagana na Mhe. George Mkuchika, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utawala Bora kabla ya kuondoka nchini.
Mhe. Li Yuanchao akiagana na Mhe. Fenella Mukangara (Mb.), Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Mhe. Li Yuanchao akiagana na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Philip Mangula
Mhe. Li Yuanchao akiagana na Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Abdulrahman Shimbo.
Kikundi cha burudani kikitumbuiza wakati Mhe. Li akiondoka nchini.


Thursday, June 26, 2014

Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Umoja wa Afrika, Malabo Equatorial Guinea

Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, kiongozi wa ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Umoja wa Afrika akiwa amesimama na kupiga makofi baada ya kuimba wimbo wa taifa wa Umoja wa Afrika kuashiria kuanza rasmi kwa mkutano huo. 

Ujumbe wa Tanzania: Kutoka kushoto ni Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Christopher Chiza, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika; (Mstari unaofuatia nyuma kutoka kulia kwenda kushoto) Mhe. Binilith Mahenge, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira; Mhe. Ummy Mwalimu, Naibu Waziri - Mazingira; na Mhe. Haji Sereweji, Mmbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Mhe. Ban Ki Moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiwasilisha salamu zake rasmi wakati wa ufunguzi wa mkutano huo ambapo moja ya masuala aliyozungumzia ni mabadiliko ya tabia nchi na athari zake. Aidha alizisifu nchi za Afrika tisa zinazounda Kamati ya Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi chini ya uenyekiti wa Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania.
Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Mambo ya Nje Mhe. Membe wakifanya majadiliano kabla ya ufunguzi wa mkutano huo.
Meza kuu wakiwa wamesimama wakati Wimbo wa Taifa wa Umoja wa Afrika ukiimbwa. 
Mhe. Abdul Fatah el-Sisi, Rais wa Misri akielekea kwenye kipaza sauti kabla ya kuhutubia kwa Mara ya kwanza tangu atwae madaraka nchini Misri, ambapo Umoja wa Afrika umeirudisha nchi hiyo kwenye Umoja baada ya uchaguzi kufanyika.

Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa na Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Afrika na Addis Ababa Ethiopia, Mhe. Naimi Aziz; wakielekea Nje ya ukumbi kwa picha ya pamoja ya viongozi waliohudhuria mkutano huo (chini )