Friday, July 31, 2015

Marais wastaafu wajadili uongozi wa Afrika

Rais Yoweri Museveni na Mhe. Rais Mstaafu, Benjamin William Mkapa wakiwa na baadhi ya  marais wastaafu wa Afrika waliohudhuria mkutano huo akiwemo Mhe. Festus Mogae (wa kwanza kushoto), Rais Mstaafu wa Botswana, Mhe, Olusegun Obasanjo (wa pili kushoto), Rais Mstaafu wa Nigeria,  Mhe. Jerry Rawlings (wa tatu kutoka kulia), Rais Mstaafu wa Ghana, Mhe. Bakili Muluzi (wa pili kulia), Rais mstaafu wa Malawi na Mhe. Hifikepunye Pohamba (wa kwanza kulia), Rais Mstaafu wa Namibia
===========================================
MARAIS WASTAAFU WAJADILI UONGOZI WA AFRIKA

Marais wastaafu wa nchi sita za Afrika wamekutana Jijini Dar es Salaam jana kutafakari mustakabali wa Bara lao wakizingatia mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa na kiteknolojia ulimwenguni. Mjadala huo ulioitishwa na Rais Mstaafu wa Tanzania, Mhe. Benjamin Mkapa, ulifunguliwa rasmi na Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Museveni.

Ulihudhuriwa na Marais Wastaafu wa Nigeria, Mhe. Olusegun Obasanjo, Ghana, Mhe Jerry Rawlings, Malawi, Mhe. Bakili Muluzi; Botswana, Mhe. Festus Mogae, na Namibia, Mhe. Hifikepunye Pohamba.

Marais wastaafu pamoja na wanazuoni na watu mashuhuri wa Afrika walisisitiza muhimu wa kujenga mtangamano wa bara hilo ili kuleta maendeleo ya haraka ya kiuchumi. Washiriki walikubaliana kuwa juhudi za pamoja zifanywe kudhibiti vikwazo dhidi ya mtangamano, ikiwa ni pamoja na historia ya tawala tofauti za kikoloni; elimu na teknolojia duni, na ukosefu wa utashi wa kisiasa.

Pamoja na kusifia hatua zilizofikiwa kuboresha demokrasia barani Afrika, washiriki walisema maendeleo ya uchumi yanahitaji kasi kubwa zaidi ili wananchi wafaidike na rasilimali nyingi zilizopo.

Uongozi wa nchi za Afrika ulikosolewa kwa kushindwa kutoa kipaumbele kwa maendeleo ya kiuchumi na kuzembea utekelezaji wa maamuzi yanayochukuliwa kwenye majukwaa mbalimbali ya pamoja, kama vile Umoja wa Afrika na Jumuiya za Maendeleo za kikanda.

Ilishauriwa jumuiya za kikanda ziimarishwe kwa kutengewa rasilimali za kutosha na kupewa uwezo zaidi wa kufanya maamuzi ili ziwe misingi ya kujenga umoja wa kiuchumi.

Washiriki walisifia Mpango Mkakati wa Umoja wa Afrika wa kulifanya bara hilo liongoze  duniani kiuchumi na kiteknolojia ifikapo mwaka 2063, lakini wakasisitiza uwekwe mpango madhubuti wa utekelezaji ili kufikia azma hiyo.

Katika hotuba yake, Rais Museveni alisema Afrika inayo misingi imara ya umoja. Alitupilia mbali madai kuwa bara hilo lina mgawanyiko mkubwa wa kijamii. "Bara hili lina makundi manne tu ya kilugha," alisema.
Kiongozi huyo wa Afrika Mashariki alihimiza juhudi zaidi kuleta mtangamano wa kiuchumi na kisiasa Afrika. "Lazima tujenge mtangamano wa kiuchumi. Pale inapowezekana, tuungane kisiasa pia."

Alisema Afrika ilitawaliwa na wakoloni kwa sababu haikuwa na mtangamano, kitu kinacholifanya bara hilo liendelee kubaki nyuma kimaendeleo. Alitaka hatua za pamoja zichukuliwe kuendeleza viwanda na maliasili za Afrika, ikiwapo madini, mafuta na gesi.
Jana usiku, Mhe. Mkapa aliwaandalia wageni wake hafla ya  chakula cha jioni ambapo pia Jukwaa la Uongozi Afrika lilikabidhi zawadi kwa washidi wa shindano la kuandika insha lililoshirikisha vijana 522 kutoka nchi 11 za bara hilo.

Mshindi wa kwanza ni Munyaradzi Shifetete kutoka Zimbabwe, ambaye alikabidhiwa cheti na fedha taslim. Wengine waliokabidhiwa zawadi na Rais Mstaafu wa Botswana, Mhe. Mogae, ni Vicky Mbabaazi kutoka Uganda, Sholopelo Sholopelo kutoka Botswana, Joseph Wanga kutoka Kenya na Omolo Juema kutoka Uganda

(mwisho)

Press Release

H.E Simonetta Sommaruga, President of Switzerland

 PRESS RELEASE 

H.E. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a congratulatory message to H.E. Simonetta Sommaruga, President of the Swiss Confederation on the occasion of the National Day of Switzerland on 1st August, 2015.

The message reads as follows;

“H.E. Simonetta Sommaruga,
President of the Swiss Confederation,
Bern,

SWITZERLAND


Your Excellency,

It is my pleasure and privilege to extend to you, my heartfelt congratulations on the occasion of your country’s National Day. As you celebrate this important occasion, allow me to take this opportunity to express my gratitude on the good relations that exist between our two countries and peoples.

The Government of Tanzania highly values the existing ties and is ready to work with the Government of Switzerland in deepening the friendship between our two countries and strengthening collaboration in bilateral and multilateral frameworks.
        Please accept, Your Excellency, my best wishes for your personal good health and continued peace and prosperity for the people of Switzerland”.

Issued by the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, Dar es Salaam

31st July 2015

Kaimu Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje akutana kwa mazungumzo na Katibu Mtendaji wa SADC

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Yahya  Simba akimkaribisha Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Dkt. Stergomena Lawrence Tax alipotembelea Wizarani na kuzungumzia masuala mbalimbali ikiwemo uanachama wa Tanzania kwenye Jumuiya hiyo.
Balozi Simba akizungumza na Dkt. Tax
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Bw. Innocent Shiyo (Kushoto) na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Upendo Mwasha kwa pamoja wakifuatilia mazungumzo yaliyo kuwa yakiendelea kati ya Balozi Simba na Dkt. Tax (Hawapo pichani).
Mkutano ukiendelea
Naibu Katibu Mkuu Balozi Simba (Kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)



Picha na Reginald Philip

Thursday, July 30, 2015

Rais Museveni awasili nchini kuhudhuria Mkutano wa Jukwaa la Uongozi la Afrika

Rais wa Uganda, Mhe.Yoweri Kaguta Museveni akipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw.Said Meck Sadiq mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius  Nyerere, tayari kwa kuhudhuria mkutano wa Jukwaa la Uongozi la Afrika unaofanyika Jijini Dar es Salaam tarehe 30 na 31 Agosti, 2015
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Zuhura Bundala akisalimiana na Rais Museveni baada ya kuwasili uwanjani hapo .

Mhe. Rais Museveni akikagua gwaride rasmi lililoandaliwa kwa ajili yake.
Rais Mstaafu, Mhe.Benjamin William Mkapa ambaye ni Mwenyeji wa mkutano huo akimpokea Rais Museveni katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam tayari kuanza kwa mkutano huo. 
Mhe. Mkapa akimkaribisha Rais Museveni tayari kuhutubia mkutano.
Rais  Museveni akihutubia mkutano huo.
 Mkutano huo ukiendelea.
Rais Museveni na Mhe. Mkapa wakiwa na baadhi ya  Viongozi wastaafu wa Afrika waliohudhuria mkutano huo akiwemo Mhe. Festus Mogae (wa kwanza kushoto), Rais Mstaafu wa Botswana, Mhe, Olusegun Obasanjo (wa pili kushoto), Rais Mstaafu wa Nigeria,  Mhe. Jerry Rawlings (wa tatu kutoka kulia), Rais Mstaafu wa Ghana, Mhe. Bakili Muluzi (wa pili kulia), Rais mstaafu wa Malawi na Mhe. Hifikepunye Pohamba (wa kwanza kulia), Rais Mstaafu wa Namibia.

Wednesday, July 29, 2015

Wizara ya Mambo ya Nje yamuaga rasmi Balozi wa India aliyemaliza muda wa kazi nchini


Balozi wa India nchini Tanzania anayemaliza muda wake wa kazi, Mhe.Debnath Shaw akitoa hotuba yake ya kuaga mbele ya wageni waalikwa wakiwemo  baadhi ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini wakiongozwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyofanyika katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Julai, 2015.

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya (kushoto) pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hapa nchini ambaye pia ni mkuu wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, Mhe.Juma Halfan Mpango wakifuatilia hotuba ya Mhe.Debnath Shaw (hayupo pichani).
Balozi wa China hapa nchini, Mhe.LU Youqing (kulia) pamoja na Afisa  Mambo ya Nje, Bi.Eliet Magogo (katikati) pamoja na mmoja wa wageni waalikwa wakisikiliza hotuba.

Mabalozi pamoja na Maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje wakifurahia hotuba ya Balozi huyo wa India hapa nchini.
 Maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje wakifuatilia kwa makini hotuba ya balozi huyo wa India anayemaliza muda wake.
 Afisa  Mambo ya Nje, Bw.Emmanuel Ruhangisa (kulia) pamoja na Mgeni mwalikwa nao wakisikiliza kwa makini hotuba hiyo.
Balozi Yahya kwa pamoja na  Balozi Shaw wakitakiana afya njema
 Mshereheshaji akiendelea kusherehesha wakati wa hafla hiyo.
Balozi Yahya akiwaongoza Balozi  Shaw (kulia) na Balozi  Mpango kupata chakula wakati wa hafla fupi ya chakula cha mchan akumuaga Balozi Shaw.
 Balozi Yahya akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Shaw na Balozi Mpango
 Picha ya Pamoja.
 Balozi Simba akibadilishana mawazo na Balozi Debnath Shaw mara baada ya hafla hiyo.
Balozi Simba akiagana na Balozi Juma Mpango baada ya hafla hiyo

Picha na Reuben Mchome

Friday, July 24, 2015

Kaimu Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje afunga rasmi mafunzo ya SOFREMCO

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju (kulia) akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Diplomasia, Balozi Mwanaidi Maajar wakati wa hafla fupi ya kufunga Mafunzo Maalum ya  Maafisa  Waandamizi wa Mambo ya Nje (SOFREMCO)  iliyofanyika Chuoni hapo Jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Kaimu Katibu Mkuu, Balozi Kasyanju na Balozi Maajar wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Chuo na Wizara pamoja na Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Waandamizi wa Mambo ya Nje.
Baadhi ya wahitimu wa kozi hiyo ya SOFREMCO wakifurahia
Wahitimu wengine wakiwa wenye nyuso za furaha
Kundi jingine la wahitimu hao

Wakufunzi wa Chuo cha Diplomasia wakibadilishana mawazo wakati wa hafla hiyo
Wahitimu nao wakipata wasaa wa kujadili namna kozi ilivyokuwa
Wahitimu wakipata picha za pamoja kwa kumbukumbu
Picha ya pamoja ya Maafisa waliohitimu Kozi ya Maafisa Waandamizi wa Mambo ya Nje
Wakifurahia
Picha zaidi

Kaimu Katibu Mkuu, Balozi Kasyanju akiongozana na Balozi Maajar na Viongozi wengine mara baada ya hafla  fupi ya kuwapongeza Wahitimu wa Mafunzo ya SOFREMCO kukamilika.


Thursday, July 23, 2015

Wizara ya Mambo ya Nje yamuaga Balozi wa Ubelgiji aliyemaliza muda wa kazi nchini



Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju akitoa hotuba wakati wa kumuaga Balozi wa Ubelgiji ambaye amemaliza muda wake wa kazi hapa nchini, Mhe. Adam Koeler huku Balozi huyo (wa kwanza kulia waliketi) na wageni waalikwa wakimsikiliza. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Julai, 2015. Katika hotuba yake Balozi Kasyanju alimsifu Balozi Koeler kwa kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Ubelgiji.
Balozi Koeler pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine wakimskiliza Balozi Kasyanju wakati wa hafla fupi ya kumuaga Balozi Koeler.
Balozi Koeler nae akizungumza wakati wa hafla ya kumuaga. Katika hotuba yake Balozi huyo aliishukuru Serikali ya Tanzania  kwa ushirikiano alioupata katika kipindi chote alichokuwepo hapa nchini  na kusifu ukarimu wa Watanzania.
Balozi Kasyanju kwa pamoja  na Mkuu wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini ambaye pia ni Balozi wa Congo (DRC), Mhe. Juma Halfan Mpango na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Bw. Alvaro Rodrigues wakimsikiliza Balozi Koeler (hayupo pichani) akihutubia.
Balozi Sokoine nae akizungumza machache wakati wa hafla ya kumuaga Balozi Koeler
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Zuhura Bunndala (katikati) akiwa na wageni waalikwa wengine wakati wa hafla ya kumuaga Balozi wa Ubelgiji ambaye amemaliza muda wake wa kazi hapa nchini
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga (katikati) akiwa na Balozi wa Ujerumani hapa nchini, Mhe. Egon Kochanke (kushoto) pamoja na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Felister Rugambwa wakati wa hafla ya kumuaga Balozi wa Ubelgiji.
Balozi wa Ireland hapa nchini, Mhe. Fionnuala Gilsenan (kulia) akiwa na Bw. Rodrigues (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Maulidah Hassan wakati wa hafla ya kumuaga Balozi wa Ubelgiji 
Wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo
Bi. Kasiga ambaye alikuwa msheheshaji (MC) katika hafla hiyo akiwakaribisha  Mabalozi na wageni waalikwa kwenye hafla hiyo
Kaimu Katibu Mkuu, Balozi Kasyanju (kushoto) na Balozi Koeler (kulia) pamoja na wageni waalikwa wakimsikiliza Bi. Kasiga ambaye haonekani pichani
Juu na Chini ni Maafisa Mambo ya Nje wakifuatilia matukio kwenye hafla ya kumuaga Balozi wa Ubelgiji.
Balozi Koeler akiteta jambo na Balozi Sokoine
Balozi Kasyanju, Balozi Koeler na wageni waalikwa wakitakiana afya njema
Balozi Koeler akifurahia zawadi ya picha ya kuchora ya Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro aliyokabidhiwa na Kaimu Katibu Mkuu, Balozi Kasyanju huku akitamka kuwa "nitarudi Tanzania kuja kupanda Mlima Kilimanjaro".
Balozi Koeler akimshukuru Balozi Kasyanju kwa zawadi hiyo nzuri
Picha ya Pamoja.