Friday, October 30, 2015

BALOZI ZOKA AWASILISHA HATI ZA UWAKILISHI KWA MAKAMU WA RAIS WA CUBA

Balozi wa Tanzania Ottawa-Canada na Mwakilishi nchini Cuba, Mhe. Jack Mugendi Zoka pamoja na ujumbe wake wakiwasili katika Ikulu ya Makamu wa Rais ijulikanayo kama Revolutionary Palace.
Mhe. Balozi Jack Mugendi Zoka akikabidhi Hati za Uwakilishi kwa Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Salvador Valdes Mesa katika Ikulu ijulikanayo kama Revolutionary Palace.
Mara baada ya kukabidhi hati, yalifuata mazungumzo ya pamoja kuhusu ushirikiano wa nchi za Tanzania na Cuba. Kutoka kushoto ni Mama Balozi, Esther Nyanzila Zoka, Balozi wa Tanzania Ottawa-Canada na Mwakilishi nchini Cuba, Mhe. Jack Mugendi Zoka, Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Salvador Valdes Mesa, na maafisa wa Ikulu ya Cuba. 
Picha ya pamoja. Kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania Ottawa-Canada na Mwakilishi nchini Cuba, Mhe. Jack Mugendi Zoka, Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Salvador Valdes Mesa, Mama Balozi, Esther Nyanzila Zoka na mshauri wa Makamu wa Rais wa Cuba.
Mhe. Balozi Jack Mugendi Zoka akiweka shada la maua katika eneo la kumbukumbu (memorial square) kwa heshima ya mwanamapindizu, Jose Marti, shujaa na mhasisis wa Cuba.
Picha ya kumbukumbu mara baada ya kuweka shada la maua. Kutoka kushoto ni askari wa Cuba mwenye mkumbulu, Balozi wa Tanzania Ottawa-Canada na Mwakilishi nchini Cuba, Mhe. Jack Mugendi Zoka, Mama Balozi, Esther Nyanzila Zoka, Afisa wa Mambo ya Nje, Bw. Paul James Makelele na mshauri wa Makamu wa Rais wa Cuba. Wa nyuma ni maaskari wa Cuba.

*******************************
Balozi wa Tanzania nchini Canada na Cuba Mhe. Jack Mugendi Zoka aliwasilisha Hati za Uwakilishi kwa Makamu wa Rais wa Cuba Mhe. Salvador Valdes Mesa katika Ikulu ya nchi hiyo ijulikanayo kama ´Revolutionary Palace´. 

Mhe. Balozi aliambatana na Mama Balozi Bibi Esther Zoka na Afisa wa Ubalozi Bw. Paul Makelele. Sherehe hiyo pia ilihudhuriwa na Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Cuba, Mhe. Balozi Miguel Lamazares Puello na Maafisa wengine kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na ofisi ya Makamu wa Rais.
Baada ya zoezi hilo, Mhe. Balozi Zoka alipata fursa ya kuwa na mazungumzo na Mhe. Makamu wa Rais.
Baada ya zoezi la kuwasilisha Hati na mazungumzo, Balozi alitembelea eneo la kumbukumbu - Memorial Square ijulikanayo kama Jose Marti ambapo aliweka Shada la Maua, kutembezwa na kupewa maelezo ya historia kuhusu ukombozi wa nchi hiyo inayomtambua Jose Marti kama shujaa na muasisi wa ukombozi wa Cuba.

APOKEA UONGOZI WA KILIMANJARO FC UBALOZINI NA KUKUBALI KUWA MLEZI WA TIMU HIYO

Mhe. Balozi Dora Msechu ameupokea Ubalozini  Ujumbe wa timu maarufu  ya soka ya watanzania waishio Sweden,  Kilimanjaro FC, ambao walikuja kumkabidhi Mhe. Balozi makombe waliyoshinda kwenye mashindano mbalimbali hapa Sweden. Mhe. Balozi Dora Msechu ameipongeza na kuishukuru Kilimanjaro FC kwa kuiwakilisha vyema nchi yetu kwenue fani ya michezo hapa Sweden na kuwahamasisha waongezee bidii zaidi na wasibweteke na mafanikio wanayoyapata.

Aidha, Mhe. Balozi Dora Msechu amekubali ombi la Kilimanjaro FC la kuwa Mlezi wa timu hiyo na kuahidi ushirikiano wake pale itakapowezekana.


BALOZI DORA MSECHU ASHIRIKI KWENYE SHEREHE YA MIAKA 10 YA JUMUIYA YA WATANZANIA JIMBO LA FYN, DENMARK

Balozi Dora Msechu  amekutana na watanzania wanaoishi kwenye Jimbo la Fyn nchini Denmark na kuwapongeza kwa kutimiza miaka 10 ya Umoja wao. na kuwashukuru kwa mchango mkubwa wanaotoa kwenye maendeleo ya nchi yetu. Amewaasa waendeleze mshikamano wao na kuwahakikishia kuwa  milango ya Ubalozi ipo wazi katika kuwahudumia na kushirikiana kwa  karibu na watanzania wote wanaoishi kwenye nchi za Nordic na Baltic.

Sherehe hiyo iliandaliwa na Jumuiya ya Watanzania Jimbo la Fyn kwa kushirikiana na familia ya Bibi Dorthe Nielsen, rafiki mkubwa wa Tanzania na mtoto wa aliyekuwa Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Denmark, marehemu Robert Andersson.





Katibu Mkuu akutana kwa mazungumzo na Balozi wa Sudan nchini

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Balozi wa Sudan hapa nchini, Mhe. Dkt. Yasir Mohammed Ali alipofika Wizarani kwa mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Sudan. 
Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Samwel Shelukindo (kushoto) akifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Mulamula na Balozi Ali (hawapo pichani). Kulia ni Afisa Mambo ya Nje. 
Balozi Ali nae akichangia jambo wakati wa mazungumzo na Balozi Mulamula
Mazungumzo yakiendelea
Balozi Mulamula akiagana na  Balozi Ali mara baada ya kumaliza mazungumzo baina yao.


Wednesday, October 28, 2015

Rais Kikwete apokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mabalozi wa Misri, Singapore, Israel na Ufilipino

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Ufilipino nchini Tanzania mwenye makazi nchini Kenya,  Mhe. Bayani V. Mangibin. Hafla hiyo imefanyika Ikulu Dar es Salaam tarehe 28 Oktoba, 2015. 
Balozi Mangibin akizaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam
Balozi Mangibin (kulia) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberatta Mulamula (kushoto) mara baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Rais Jakaya Kikwete (katikati mwenye tai nyekundu)
Balozi Mangibin (kulia) akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Khatibu Makenga (wa kwanza kushoto) alipokuwa akitambulishwa na Mhe. Rais. 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga (wa kwanza kushoto) akisalimiana na Balozi Mangibin (kulia).
Mhe. Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mangibin.
Picha ya pamoja

=========Balozi wa Singapore
Balozi wa Singapore nchini Tanzania, Mhe. Tan Puay Hiang akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Mhe. Rais.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Singapore mwenye kazi yake nchini Singapore,  Mhe. Tan Puay Hiang (kulia)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberatta Mulamula (kushoto) akisalimiana na Balozi Tan Puay Hiang (kulia)
Mhe. Rais Kikwete akizungumza na Balozi Hiang mara baada ya kupokea hati zake za utambulisho kama Balozi mpya wa Singapore hapa nchini. Kushoto ni Afisa aliyefuatana na Balozi Hiang.

.......Balozi wa Misri 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi mpya wa Misri hapa nchini, Mhe. Yasser Ahmed Al Eldin Elshawaf. Hafla hiyo imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Oktoba, 2015.
Mhe. Rais Kikwete akimkaribisha Balozi Elshawaf.
Mhe. Rais Kikwete akimtambulisha kwa Balozi Elshawaf, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula.
Balozi Elshawaf akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Samwel Shelukindo 
Balozi Elshawaf akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. 
Picha ya pamoja
Mhe. Rais Kikwete akiwa kwenye mazungumzo na Balozi mpya wa Misri hapa nchini Mhe. Elshawaf
Mazungumzo yakiendelea

......Balozi wa Israel

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Balozi mpya wa Israel hapa nchini mwenye Makazi yake nchini Kenya, Mhe. Yahel Vilan mara baada ya kupokea Hati zake za utambulisho. Hafla hiyo imefanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 28 Oktoba, 2015.
Mhe. Rais Kikwete akimtambulisha kwa Balozi Vilan, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula.
Balozi Vilan akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Elibariki Maleko.
Balozi Vilan akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga
Balozi Vilan akisalimiana na Bw. Batholomeo Jungu, Afisa Mambo ya Nje
Mhe. Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Vilan
Mhe. Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Vilan na Balozi Mulamula
Balozi Elshawaf (katikati) akipokea heshima ya wimbo wa taifa mara baada ya kuwasili Ikulu. Kulia ni Mkuu wa Itifaki Balozi Juma Maharage na kushoto Mnikulu.
Bendi ya polisi ikipiga wimbo wa taifa wa Misri kwa heshima ya Balozi Elshawaf
Balozi Elshawaf akisalimiana na Bw. Celestine Kakele, Afisa Mambo ya Nje
Balozi Elshawaf akisalimiana na Kiongozi wa Bendi ya Polisi
Picha na Reginald Philip

Taarifa kwa Vyombo vya Habari - Uhamisho wa Kituo

Balozi Peter A. Kallaghe 


Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemuhamisha kituo Balozi Peter A. Kallaghe aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza kwenda kuwa Balozi wa Tanzania nchini Brazil.

Uhamisho huo unaanzia tarehe 23 Oktoba, 2015.


Imetolewa na:
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam

28 Oktoba, 2015

Tuesday, October 27, 2015

Timu za Waangalizi za AU, SADC na Jumuiya ya Madola waisifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Kiongozi wa Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi Mkuu wa Tanzania kutoka Umoja wa Afrika (AU), ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Msumbiji Mhe. Armando Emilio Guebuza, akitoa ripoti ya timu hiyo mbele ya Waandishi wa Habari na Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini  tarehe 27 Oktoba, 2015 katika Hoteli ya White Sands Jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine, timu hiyo ya Waangalizi ya Umoja wa Afrika (AU) imeisifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kuendesha uchaguzi katika hali ya haki na uwazi bila upendeleo wowote.
Kamishna anayeshughulikia masuala ya Siasa katika Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Dkt. Aisha Abdulahi nae akizungumza wakati wa uwasilishaji ripoti ya Umoja huo kuhusu Uchaguzi Mkuu wa hapa nchini.
Baadhi ya Waheshimiwa Mabalozi  wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini wakimpigia makofi kiongozi wa timu ya Waangalizi ya Afrika Mhe. Armando Guebuza (hayupo pichani).
Kiongozi wa Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi Mkuu kutoka  Jumuiya ya Madola, ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Nigeria, Mhe. Goodluck Jonathan akitoa ripoti ya timu yake  mbele ya Waandishi wa Habari na Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini tarehe 27Oktoba, 2015 katika Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.
Mheshimiwa Goodluck Jonathan ameisifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Vyombo vya Dola, Wagombea, Viongozi wa vyama vya siasa pamoja na Watanzania wote kwa ujumla kwa kuendesha uchaguzi katika mazingira ya haki, uwazi na amani.
Mkurugenzi wa Idara ya Afrika, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Samwel Shelukindo (katikati), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga (kulia) pamoja na Afisa wa Wizara hiyo Bw. Celestine Kakere, wakifuatilia ripoti hizo.
Baadhi ya Waheshimiwa Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini wakifuatilia ripoti ya kiongozi wa timu ya Waangalizi ya Jumuiya ya Madola Mhe. Goodluck Jonathan.
Wajumbe wa timu za Waangalizi wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC)Umoja wa Afrika (AU) na Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola nao wakifuatilia Ripoti ya Mhe. Goodluck Jonathan.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Msumbiji ambaye pia ndiye Kiongozi wa Timu ya Waangalizi wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Mhe. Oldemiro Baloi naye akitoa taarifa ya timu yake ya uangalizi wa Uchaguzi Mkuu hapa nchini tangu kipindi cha kampeni hadi siku ya uchaguzi.

Baadhi ya Waheshimiwa Mabalozi  wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini wakifuatilia ripoti ya kiongozi wa timu ya waangalizi ya SADC.
Mkutano huo ukiendelea.
Waheshimiwa Mabalozi wakiendelea kufuatili uwasilishwaji wa ripoti hizo za waangalizi wa Kimataifa wa Uchaguzi Mkuu nchini Tanzania.

Mmoja wa Waandishi wa Habari akiuliza swali juu ya ripoti hizo.
Waandishi wa Habari wakiendelea kuwajibika kuchukua kila kinachoelezwa na timu hizo za kimataifa za waangalizi wa Uchaguzi Mkuu unaoendelea hapa nchini.
Mkutano ukiendelea.
===========================
PICHA NA: REUBEN MCHOME.