Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Bw. Valentino Mlowola Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU wakifurahia jambo baada ya kuasaini hati za makabidhiano |
Thursday, May 31, 2018
Wizara yakabidhiwa rasmi jukumu la kuisimamia Bodi ya Ushauri ya Masuala ya rushwa ya Umoja wa Afrika
Mkutano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji wafikiatamati
Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akifuatilia Mkutano |
Maza Kuu ikiongoza Mkutano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji uliokuwa ukiendelea jijini Arusha |
Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kushoto) akisaini taarifa ya Mkutano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara,Viwanda,Fedha na Uwekezaji. Kushoto Bw. Eliah Chilangazi Afisa Biashara kutoka Wizara ya Biashara, Viwanda, na Biashara |
Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kushoto), Mhe. Mhandisi Stella Manyanya (Mb) Naibu Waziri wa Biashara, Viwanda na Uwekezaji (Katikati), na Bw. Benard Haule Kaimu Mkurugenzi wa Biashara, Uwekezaji, na Sekta za Uzalishaji (kulia) wakishauriana jambo |
Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mhe. Dkt. Pindi Chana Balozi wa Tanzania nchini Kenya wakifuatilia mkutano |
Waheshimiwa Mawaziri, Mabalozi na Watendaji wa Serikali wa nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mkutano |
Tuesday, May 29, 2018
Tanzania itaendelea kushiriki katika ulinzi wa amani duniani, Balozi Mahiga
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akihutubia katika maadhimisho ya miaka 70 ya Siku ya Walinda Amani Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Mashujaa vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Mei 2018. |
Siku ya Walinda Amani Duniani huadhimishwa tarehe 29 Mei ya kila mwaka ambapo kaulimbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni "Ulinzi wa Amani wa Umoja wa Mataifa: Miaka 70 ya huduma na kujitoa" (UN Peacekeeping: 70 Years of Service and Sacrifice).
Katika hotuba yake, Mhe. Waziri Mahiga alieleza kuwa yapata miaka 12 tangu Tanzania ianze kushiriki katika ulinzi wa amani chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa.
Pia akasisitiza Tanzania itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha inasaidia kupatikana kwa amani katika mataifa mengine kwakuwa hakuna taifa linaloweza kufanikiwa katika maendeleo pasipo kuwepo na amani ya uhakika. " Sio jambo rahisi kukubali kutoa uhai wako kwa ajili ya mtu mwingine lakini Tanzania itaendelea kuungana na mataifa mengine duniani katika kusaidia kupatikana kwa amani ya mataifa hayo" alisema Mhe. Mahiga.
Aidha, Katika kuwakumbuka Walinda Amani wote Duniani waliopoteza maisha wakati wakitekeleza majukumu yao, pamoja na kutoa heshima kwa wale ambao bado wanaendelea na jukumu la kulinda amani, Tanzania imepoteza jumla ya askari wapatao 30 ndani ya miaka 10, pia dunia imepoteza zaidi ya askari 3500 na kwa sasa Tanzania inajivunia kuwa na jumla ya askari wapatao 2,600 wanaohudumu katika misheni sita (6) za ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez akihutubia katika maadhimisho ya siku ya Walinda Amani Duniani ambapo alieleza pamoja na kuendelea kusimamia utekelezaji wa shughuli za maendeleo, Umoja wa Mataifa utaendelea kuhakikisha Dunia inakuwa mahali salama pa kuishi ili kuweza kuyafikia malengo ya maendeleo endelevu. |
Mhe. Waziri Mahiga akiweka shada la maua katika Mnara wa Mashujaa uliopo Viwanja vya Mnazi Mmoja ikiwa ni sehemu ya kuenzi mchango wa Walinda Amani Duniani. |
Wakitoa heshima kwa ajili ya kuwakumbuka Walinda Amani Duniani, waliosimama mbele kutoka kushoto ni Mhe. Waziri Mahiga akiwa na Mwakilishi kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Maj. Gen. Henry Kamunde, Bw. Alvaro Rodriguez na Mwakilishi kutoka Jeshi la Polisi Tanzania, Kamishna Nsato Marijani. |
Mhe.Waziri Mahiga akisalimiana na Askari walioshiriki katika Misheni za Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa. |
Mhe. Waziri Mahiga akisalimiana na sehemu nyingine ya Askari walioshiriki katika Misheni za Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa. |
Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Deusdedit Kaganda pamoja na askari kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Polisi Tanzania wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi. |
Sehemu nyingine ya Askari na wageni waalikwa wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi. |
Waheshimiwa Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa nchini wakifuatilia matukio mbalimbali katika maadhimisho hayo. |
Sehemu nyingine ya Waheshimiwa Mabalozi, Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa nchini na wageni waalikwa wakifuatilia matukio mbalimbali katika maadhimisho hayo. |
Waheshimiwa Mabalozi na Wageni waalikwa wakifuatilia maadhimisho ya Siku ya Walinda Amani Duniani. |
Gwaride la heshima kwa Mgeni Rasmi. |
Askari wa JWTZ wakiingia viwanja vya Mnazi Mmoja. |
Monday, May 28, 2018
Waziri Mahiga atembelea Ubalozi wa Palestina nchini
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Augustine Mahiga akisaini kitabu cha maombolezo ya Wapelestina waliouwa kwenye Ukanda wa Gaza hivi karibuni, Mhe.Waziri Mahiga alisaini kitabu hicho alipotembelea katika Ubalozi huo tarehe 28 Mei,2018, anayeshuhudia ni Balozi wa Palestina hapa nchini Mhe. Balozi Hazem Shabat.
Mhe. Waziri Mahiga akipata maelezo kutoka kwa Mhe. Balozi Shabat kuhusu sanaa ya picha inayoelezea utamaduni wa Wapalestina, aliyesimama kushoto ni Naibu Balozi wa Palestina hapa nchini Bw.Derar Ghannam.
Mhe. Waziri Mahiga akisisitiza jambo katika mazungumzo yaliyofanyika Ubalozini hapo, lengo la mazungumzo hayo pamoja na mambo mengine ni kuzidi kuboresha mahusiano yaliyopo kati ya Tanzania na Palestina.
Mhe. Waziri Mahiga akiwa ameshikilia moja ya picha yenye maelezo ya kuhimiza haki ya Wapalestina ya kuishi.
Mhe. Balozi Shabat akimfafanulia jambo kwenye Kitabu alichomkabidhi Mhe. Waziri Mahiga kama zawadi, Kitabu hicho kinaelezea Historia ya Mji wa Yerusalem.
Mhe. Waziri Mahiga akiagana na mwenyeji wake baada ya mazungumzo.
Sehemu ya maelezo ya sanaa ya picha zilizopo Ubalozini hapo, picha hizi zinaelezea kuhusu Amani katika Palestina na Haki ya Kuishi ya Wapalestina.
Sunday, May 27, 2018
Naibu Katibu Mkuu Mambo ya Nje akutana na Balozi wa Argentina nchini
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi akizungumza na Balozi wa Argentina nchini Mhe. Gomez Bustillo alipomtembelea Wizarani Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei 2018. |
Balozi Mwinyi na Mhe. Bustillo wakijadili namna ya kuendeleza miradi ya maendeleo na kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili. |
Balozi Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Bustillo, kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya, Bw. Jestas Nyamanga. |
Saturday, May 26, 2018
Mkutano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji waendelea jijini Arusha
Bw.Benard Haule Kaimu Mkurugenzi wa Biashara, Uwekezaji na
Sekta za Uzalishaji, akizungumza kwenye mkutano wa Baraza laKisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda,Fedha na Uwekezaji
unaoendelea kufanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo katika
majengo ya ofisi za Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
jijini Arusha
|
Mkutano wa Kisekta wa Baraza la Mawaziri wa Biashara,Viwanda, Fedha na Uwekezaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaendelea kufanyika jijini Arusha. Mkutano huu unafanyika kwa kipindi cha siku saba (7) kuanzia tarehe 25 hadi 30 Mei, 2018. Pamoja na mambo mengine yatakayojili, Mkutano huu unatarajia kufanya yafuatayo:-
- Kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa maagizo na maamuzi yaliyofanywa na mkutano uliopita wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji;
- Kupokea na kajadili taarifa ya majadiliano ya awali ya bajeti ya Baraza la Mawaziri wa Fedha la Jumuiya ya Afrika Mashariki;
- Kupokea na kujadili taarifa ya Kamati ya Forodha
- Kupokea na kujadili taarifa ya Kamati ya Kisekta ya Biashara;
- Kupokea na kujadili taarifa ya Kamati ya Mamlaka ya Ushindani;
- Kupokea na kujadili taarifa ya Kamati ya Viwango ya Jumuiya ya Afrika Mashariki; na
- Kupokea na kujadili taarifa kutoka Kamati ya Kisekta ya Viwanda.
Mkutano huu anafanyika katika ngazi tatu ambazo ni ngazi ya waalam, ngazi Makatibu Wakuu, na ngazi ya Mawaziri.
Mkutano huu umehudhuriwa na wajumbe kutoka nchi zote wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Bw. Benard Haule Kaimu Mkurugenzi wa Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji akichangia wakati wa Mkutano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda,Fedha na Uwekezaji unaondelea jijini Arusha |
Bw. Raymond Agaba Kamishna wa Biashara za Ndani (kushoto) kutoka Jamhuri ya Uganda akiongoza mkutano. Kulia ni Bibi Flavia Busingye Afisa Mkuu wa Forodha,ufuatiliaji na utekelezaji kutoka Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki |
Mkutano ukiendelea |
Wednesday, May 23, 2018
Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki yapitishwa na Bunge
Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akisoma hotuba ya bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2018/2019 bungeni jijini Dodoma. Mapema leo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepisha kiasi cha Shilingi Bilioni Mia Moja Sabini na Saba, Milioni Sita na Mia Mbili Thelathini na Mbili Elfu. Kati ya fedha hizo Shilingi Bilioni Mia Moja Sitini na Sita, Milioni Mia Sita na Sita, na Mia Mbili Thelathini na Mbili Elfu ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida, na Shilingi Bilioni Kumi na Milioni Mia Nne ni kwa ajili ya bajeti ya maendeleo. |
Pro. Adolf F. Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,(wa kwanza kushoto) akifuatilia uwasilishwaji wa hotuba ya bajeti ya Wizara. Wa pili kutoka kushoto, ni Naibu Katibu Mkuu Balozi Ramadhani Mwinyi akifuatilia hotuba. |
Sehemu ya Watendaji wa Wizara wakifuatilia hotuba ya bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2018/2019 iliyowasilishwa na kupishwa bungeni jijini Dodoma |
Mhe.Balozi Dkt. Augustine Mahiga akijibu maswali bungeni mara baada ya kuwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2018/2019 |
Mhe. Dkt. Susan Kolimba Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kushoto), akifuatilia hotuba ya bajeti bungeni jijini Dodoma |
Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akifafanua jambo mara baada ya kuwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara. |
Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akisalimiana na Dkt. Stergomena Tax Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) walipokutana katika viunga vya Bunge jijini Dodoma mara baada kuwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara. |
Mhe. Waziri Mahiga akijadili jambo na Mhe. Zitto Kabwe Mbunge wa Kigoma Mjini katika viunga vya Bunge jijini Dodoma mara baada ya kupitishwa kwa hotuba ya bajeti ya Wizara |
Mhe. Waziri Mahiga na Mhe. Naibu Waziri Kolimba wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Waheshimiwa Mabalozi na Watendaji wa Wizara waliohudhuria tukio la uwasilishwaji wa bajeti ya Wizara bungeni jijini Dodoma
HOTUBA YA MHESHIMIWA BALOZI DKT. AUGUSTINE PHILIP MAHIGA
(MB), WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI AKIWASILISHA
BUNGENI MAKADIRIO YA BAJETI YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA
2018/2019
iii
Stabilisation
Mission in the Central African Republic
MK-ICC Mt. Kilimanjaro International
Convention
Centre
MONUSCO United Nations Organisation
Stabilisation
Mission
in the Democratic Republic of the Congo
NPT Non – Proliferation Treaty
PSPF Public Sector Pension Fund
RFI Radio France International
RMB Renminbi
SADC Southern African Development
Community
SDGs Sustainable Development
Goals
TAZARA Tanzania-Zambia Railway Authority
TBC Tanzania Broadcasting Corporation
TEHAMA Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano
TIC Tanzania Investment Centre
TMEA Trademark East Africa
UKIMWI Upungufu wa Kinga Mwilini
iv
UNDP
United Nations Development Progamme
UNDAP
United
Nations Development Assistance Plan
UNEP
United Nations Environment Progamme
UNESCO
United
Nations Educational Scientific and Cultural Organization
UNFPA
United Nations Population Fund
UN-HABITAT
United
Nations Human Settlement Programme
UNHCR
United
Nations High Commission for Refugees
UNICEF
United
Nations Children’s Emergency Fund
UN-ICTR
United
Nations International Criminal Tribunal for Rwanda
UNIDO
United
Nations Industrial Development Organization
UNIFIL
United Nations Interim Force in Lebanon
UNISFA
United
Nations Interim Security Force for Abyei
v
of South Sudan
UTT Unit Trust of Tanzania
VoA Voice of America
WHO World Health Organization
WTO World Trade Organization
WWF World Wildlife Fund
vi
1.
Mheshimiwa Spika, baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuwasilisha Taarifa ya
Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara, naomba sasa kutoa hoja kwamba Bunge
lako Tukufu likubali kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa mpango na
bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa mwaka
wa fedha 2017/18. Aidha, naomba Bunge lako Tukufu lijadili na kupitisha Mpango
na Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2018/19.
2.
Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kumshukuru
Mwenyezi Mungu, mwingi wa fadhila na rehema, kwa
kutujalia afya njema na kutuwezesha kukutana tena katika Bunge lako Tukufu, kujadili Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya
Wizara yangu.
3.
Mheshimiwa Spika, naungana na wenzangu walionitangulia
kuwashukuru na kuwapongeza watoa hoja waliozungumza kabla yangu, hususan Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mheshimiwa Dkt. Philip Isdory
Mpango (Mb), Waziri wa Fedha na Mipango ambao kwa hakika hotuba zao sio tu
zimezungumzia mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano, bali pia zimetoa dira
katika mustakabali wa taifa letu kwa kuainisha masuala muhimu ya kitaifa,
kikanda na kimataifa ambayo baadhi yake yanagusa majukumu ya Wizara yangu.
1
4.
Mheshimiwa Spika, naomba pia nitumie fursa hii kutoa
shukrani zangu kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama
chini ya uongozi wa Mhe. Mussa Azan Zungu (Mb) na Makamu wake Mhe. Salum Mwinyi
Rehani (Mb). Kamati hii imetoa mchango mkubwa na imekuwa muhimili muhimu katika
kuiwezesha Wizara yangu kutekeleza majukumu yake kwa kutoa ushauri kuhusu
masuala mbalimbali ya kiutendaji.
5.
Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee naomba nitumie
nafasi hii kuwashukuru Mheshimiwa Dkt. Susan Alphonce Kolimba (Mb), Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki; Prof. Adolf Faustine
Mkenda, Katibu Mkuu; Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi, Naibu Katibu Mkuu;
mabalozi wa Tanzania nje ya nchi; Wakuu wa Idara na Vitengo; watumishi wa
Wizara; na taasisi zilizo chini ya Wizara yangu kwa kujituma na kutekeleza
majukumu yao kwa weledi na kufanikisha kwa kiwango cha juu utekelezaji wa
bajeti ya mwaka wa fedha 2017/18, pamoja na kuandaa Bajeti ya Wizara ya mwaka
wa fedha 2018/19.
|