Tuesday, April 30, 2019
Monday, April 29, 2019
Ubalozi wa Tanzania nchini India waadhimisha miaka 55 ya Muungano
Mhe. Balozi Luvanda (wa pili kushoto) kwa pamoja na mgeni rasmi Mhe. Shri Sanjiv Arora ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa
India anayeshughulikia Masuala ya Kikonseli, Paspoti, Visa na Diaspora wa (kushoto) na wageni waalikwa wakionesha jarida kuhusu miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar lililoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini India na kuzinduliwa
rasmi katika hafla hiyo.
|
Mhe. Balozi Luvanda akiwa
katika picha ya pamoja na Mabalozi wa nchi mbalimbali walioudhuria hafla ya
kuadhimisha miaka 55 ya Muungano.
|
Mhe. Balozi Luvanda (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Ubalozi wa Tanzania, New Delhi wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 55 ya Muungano.
|
Mhe. Schreiber asisitiza Tanzania kutosaini mkataba wa EPA
Sehemu ya waandishi wakimsikiliza kwa makini Mhe. Schreiber |
Mhe. Schreiber akiendelea kuzungumza na waandishi wa Habari. |
Saturday, April 27, 2019
Ubalozi wa Urusi waadhimisha Muungano kwa Kutangaza bidhaa za Tanzania
Naibu Mkurugenzi wa Afrika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi, Bw. George Cherpisk akisoma hotuba katika maadhimisho hayo. |
Wageni waalikwa wakiwemo Waheshimiwa Mabalozi wa nchi mbalimbali zenye uwakilishi Urusi wakisikiliza hotuba. |
Mhe. Balozi Mumwi na Waheshimiwa Mabalozi wa mbalimbali wa nchi za Afrika zenye uwakilishi nchini Urusi wakikata keki ya kuadhimisha miaka 55 ya Muungano wa Tanzania. |
Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Mhe. Maj. Jen. Mstaafu Simon Mumwi akikabidhi cheti kwa mmoja wa wadau wanaochangia maendeleo na ukuaji wa uchumi nchini Tanzania. |
Mdau akipokea cheti chake ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wake katika maendeleo ya Tanzania. |
Picha ya pamoja ya baadhi ya Waheshimiwa Mabalozi, wageni, maafisa wa ubalozi na wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma Urusi walioshiriki katika maadhimisho hayo. |
Thursday, April 25, 2019
Vacancy announcement
PRESS RELEASE
Vacancy notice
The Ministry of Foreign Affairs and East African
Cooperation has received Vacancy Notice for the post of Director
General available at the African Development Bank (AfDB) for qualified
individuals to apply.
Application details can be found through the
following website: http://www.afdb.org. Closing
date for application is 1st May, 2019.
The
Ministry encourages qualified Tanzanians to apply.
Issued by:
Government Communication Unit,
Ministry of Foreign Affairs and East African
Cooperation,
Dodoma.
25th April, 2019.
Tanzania na China zaadhimisha miaka 55 ya ushirikiano
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako (Mb.) akitoa hotuba kama mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya miaka 55 ya Ushirikiano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Watu wa China yaliyofanyika kwenye ukumbi uliopo kwenye Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam tarehe 24 Aprili, 2019. Katika hotuba yake, Prof. Ndalichako ameipongeza China kwa kuimarisha ushirikiano na Tanzania hususan katika sekta za Elimu, Biashara na Ujenzi wa miundombinu. Aidha, amesema kuwa mahusiano kati ya Tanzania na China ni ya muda mrefu na mchango wa nchi hiyo kwenye maendeleo ya Tanzania ni dhahiri akitolea mfano ujenzi wa Reli ya TAZARA pamoja na ujenzi wa viwanda mbalimbali vya nguo nchini. Vilevile China imeendelea kushirikiana na Tanzania kwenye Sekta ya Afya kwa kubadilishana uzoefu. Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda, Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Bw. Caesar Waitara, na viongozi mbalimbali kutoka Taasisi za umma na binafsi nchini. |
Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda akiwa na mke wake Mhe. Tunu Pinda (kushoto) pamoja na viongozi mbalimbali kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia hotuba iliyokuwa ikitolewa na Prof. Ndalichako (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho ya miaka 55 ya ushirikiano kati ya Tanzania na China. |
Juu na Chini ni sehemu ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini wakifuatilia hotuba hiyo. |
Prof. Ndalichako akiendelea kuhutubia kwenye maadhimisho hayo. |
Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini, Mhe. Wang Ke naye akihutubia kwenye maadhimisho hayo. |
Wageni waalikwa wakifuatilia maadhimisho hayo. |
Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda pamoja na mke wake Mhe. Tunu Pinda (kushoto) pamoja na viongozi wengine kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakipitia kitabu chenye kuonyesha ushirikiano wa Tanzania na China kwenye sekta mbalimbali. |
Mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Zanzibar, Balozi Mohammed Hamza (kushoto) kwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Bw. Caesar Waitara (kulia) wakipitia kitabu kinachoonesha namna Tanzania na China zinavyoshirikiana kwenye sekta mbalimbali. |
Maafisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakijadiliana jambo wakati wa maadhimisho hayo. |
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe akitambulishwa kwa wageni walioshiriki maadhimisho hayo. |
Mshehereshaji, Bi. Bertha Makilagi akitoa mwongozo wa ratiba ya maadhimisho hayo kwa wageni waalikwa. |
Juu na chini ni maonyesho mbalimbali yakiendelea kuonyeshwa na vikundi mbalimbali kwenye maadhimisho hayo
Mgeni Rasmi pamoja na wageni waalikwa wakiwa wamesimama wakati nyimbo za mataifa ya Tanzania na China zikiimbwa. |
Kikundi chenye mchanganyiko wa wanafunzi kutoka Tanzania na China wakiongoza kuimba wimbo wa Taifa wa Tanzania na China kabla maadhimisho hayo kuanza. |
Naibu Waziri, Mhe. Dkt. Ndumbaro akimpa mkono wa pongezi mmoja wa wasanii aliyekuwepo kwenye maadhimisho hayo |
Mhe. Prof. Ndalichako na wageni waalikwa wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa maadhimisho hayo. |
Mgeni rasmi pamoja na Viongozi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja. |
Wednesday, April 24, 2019
Nafasi za Ajira Katika Shirika la Kuzuia Silaha za Kemikali
Dodoma, 24 Aprili 2019
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Nafasi za Ajira
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki inapenda kuwahimiza Watanzania wenye sifa kuomba fursa ya ajira
iliyotangazwa na Sekretarieti ya Shirika la Kuzuia Silaha za Kemikali
(Organization for the Prohibition of Chemicals Weapons-OPCW) iliyopo The Hague,
Uholanzi. Nafasi hiyo ni ya Technical
Support Officer-P3 ambapo mwisho wa kufanya maombi ni tarehe 06 Juni 2019.
Wenye sifa zinazohitajika, wanashauriwa
kufanya maombi kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya sekretarieti; www.opcw.org
Imetolewa
na:
Kitengo
cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki,
Thursday, April 18, 2019
Fursa ya Ajira.
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
NAFASI
YA AJIRA KATIKA SEKRETARIETI YA JUMUIYA YA UKANDA WA MAZIWA MAKUU (ICGLR).
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, inawahamasisha Watanzania wenye sifa, kuomba nafasi ya
ajira katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR).
Ajira hiyo ni Mtaalam wa Uhakiki wa Nyaraka. Taarifa zote muhimu kuhusu fursa hiyo ya ajira zinapatikana kwa kupitia tovuti www.icglr.org.
Maombi yote yatumwe kwenda katika
barua pepe jobs@icglr.org na nakala itumwe
katika barua pepe gerard.nayuburundi@icglr.org
yakiwa na kichwa cha habari Maombi ya
nafasi ya Mtaalam wa Uhakiki wa Nyaraka.
Mwisho wa kutuma maombi kwa nafasi
hiyo ni tarehe 25 Aprili, 2019.
Imetolewa na:
Kitengo cha
Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.