Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John
Kabudi akitoa hotuba kama mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Taifa la
Misri.
Katika hotuba yake Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi alisifu
ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Misri, ambapo kwa sasa Misri
wanatekeleza mradi mkubwa wa Bwawa la kuzalisha Umeme Nchini ambalo Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alizindua mradi
huo hivi karibuni.
Pamoja na mambo mengine Prof. Palamagamba John Kabudi alimweleza
Balozi kuwa Tanzania inatambua mchango wa Misri kwenye sekta mbalimbali
zikiwemo Afya, Elimu na Biashara. Hafla hiyo imefanyika tarehe 29 Julai, 2019
jijini Dar es Salaam
|