Monday, December 27, 2021
Friday, December 17, 2021
Thursday, December 16, 2021
Tuesday, December 14, 2021
BALOZI MULAMULA ASHIRIKI MAADHIMISHO YA MT. LUCIA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula ashiriki katika sherehe za maadhimisho ya Mtakatifu Lucia iliyoandaliwa na Ubalozi wa Sweden hapa nchini. Mbali na Balozi Mulamula, Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo pia alishiriki katika hafla hiyo iliyofanyika jana jioni jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Balozi wa Sweden hapa nchini Mhe. Anders Sjöberg katika sherehe za maadhimisho ya Mtakatifu Lucia. Sherehe hiyo iliandaliwa na Ubalozi wa Sweden.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiteta jambo na Mbunge wa Urambo (CCM), Margreth Sitta katika sherehe za maadhimisho ya Mtakatifu Lucia
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akijadili jambo na Balozi wa Norway Mhe. Elisabeth Jacobsen pamoja na Balozi wa Denmark nchini, Mhe. Mette Norgaard Spandet katika sherehe za maadhimisho ya Mtakatifu Lucia
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akijadili jambo na Balozi wa Sweden hapa nchini Mhe. Anders Sjöberg pamoja na Balozi wa Norway Mhe. Elisabeth Jacobsen
Balozi wa Denmark nchini, Mhe. Mette Norgaard Spandet akifurahia jambo na Mbunge wa Urambo (CCM), Margreth Sitta pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Swahiba Mndeme
Badhi ya watoto wakiimba nyimbo maalum ya kumbukizi ya Mtakatifu Lucia
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula, Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo pamoja na viongozi wengine akiwemo Mbunge wa Urambo Magreth Sitta wakifuatilia sherehe za maadhimisho ya Mtakatifu Lucia
Balozi wa Sweden hapa nchini Mhe. Anders Sjöberg akiongea na viongozi mbalimbali walioshiriki katika sherehe za maadhimisho ya Mtakatifu Lucia
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimkabidhi zawadi Balozi wa Sweden hapa nchini Mhe. Anders Sjöberg katika sherehe za maadhimisho ya Mtakatifu Lucia
Badhi ya watoto wakiimba nyimbo maalum ya kumbukizi ya Mtakatifu Lucia
Badhi ya viongozi wakishuhudia sherehe za maadhimisho ya Mtakatifu Lucia |
Maadhimisho ya Seherehe ya Mtakatifu Lucia yakiendelea
BALOZI SHIYO AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO AU
Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Afrika, Mhe. Innocent Eugene Shiyo amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Moussa Faki Mahamat, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa tarehe 13 Desemba 2021. Wakati wa hafla hiyo, Mhe. Mahamat amempongeza Balozi Shiyo kwa kuteuliwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Afrika. Amemkarabisha na kumtakia kheri katika utekelezaji wa majukumu yake. Mhe. Mahamat na Balozi Shiyo wamekubaliana kushirikiana katika kusimamia utekelezaji wa masuala ya kipaumbele ya Umoja wa Afrika hususan juhudi za kupambana na UVIKO-19 ikiwemo upatikanaji na utengenezaji wa chanjo za ugonjwa huo barani Afrika pamoja na mikakati ya kunasua uchumi wa Afrika dhidi ya athari za UVIKO-19. Wamekubaliana kushirikiana katika kutekeleza miradi ya kipaumbele ya Umoja wa Afrika yenye lengo la kuimarisha na kukuza Mtangamano wa Afrika hususan ujenzi wa miundombinu ya uchukuzi, kuboresha mazingira ya biashara kupitia Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) na juhudi za uimarishaji wa hali ya amani, usalama na utulivu barani Afrika. Vilevile, wamekubaliana kuhusu umuhimu wa utekelezaji wa mchakato mabadiliko ya kitaasisi ndani ya Umoja wa Afrika ili kuboresha utendaji wa umoja huo. Aidha, Mhe. Balozi Shiyo alizungumzia kwa undani umuhimu wa kutekeleza maazimio mbalimbali ya Wakuu wa Nchi na Serikali ya kuwezesha lugha ya Kiswahili kuwa miongoni mwa lugha za kikazi za umoja wa Afrika. Mhe. Mahamat alimhakikishia Mhe. Balozi Shiyo kuwa ataunga mkono ombi la Tanzania kutaka lugha ya Kiswahili kuwa miongoni mwa lugha za Kazi za Umoja wa Afrika. Mhe. Mahamat alitumia fursa hiyo kutoa salamu za shukurani kwa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kumwalika kushiriki Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara tarehe 09 Desemba 2021 na zaidi kwa kukubali kuonana naye tarehe 10 Desemba, 2021 ambapo alipata fursa ya kumwelezea Mhe. Rais kuhusu maeneo mbalimbali ya kipaombele ndani ya Umoja wa Afrika na Afrika kwa ujumla. |
Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Afrika, Mhe. Innocent Eugene Shiyo amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Moussa Faki Mahamat, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika. |
Picha ya pamoja |
Monday, December 13, 2021
CHINA YAISAIDIA WIZARA YA MAMBO YA NJE MILIONI 714/-
Na Mwandishi wetu, Dar
Serikali ya Jamhuri ya watu wa China imetoa msaada wa shilingi milioni 714/- kwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambapo msaada huo utakaotumika kuijengea uwezo Wizara ya Mambo ya Nje.
Msaada huo umekabidhiwa Wizarani na Balozi wa China nchini Mhe. Chen Mingjian na kupokelewa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Kabla ya kukabidhi msaada huo, Mhe. Mingjian pamoja na Balozi Sokoine wamesaini Mkataba wa Makubaliano kati ya China na Tanzania kuhusu msaada huo pamoja na Hati ya Makabidhiano ya msaada huo.
Msaada huo unafuatia ahadi iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Wang Yi alipofanya ziara ya kikazi hapa nchini tarehe 7 na 8 Januari 2021.
Balozi wa China nchini Mhe. Chen Mingjian pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine wakionesha Mkataba wa Makubaliano mara baada ya kusainiwa katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Balozi wa China nchini Mhe. Chen Mingjian akibadilishana Mkataba wa Makubaliano kati ya China na Tanzania kuhusu msaada wa milioni 714 na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine mara baada ya kusainiwa katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Balozi wa China nchini Mhe. Chen Mingjian pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine wakisaini Mkataba wa Makubaliano kati ya China na Tanzania kuhusu msaada huo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
UZINDUZI WA MATANGAZO YA VIVUTIO VYA UTALII KATIKA MABASI NCHINI ISRAEL
Balozi wa Tanzania nchini Israel, Mhe. Job Masima akionesha tangazo kwenye basi linalohusu fukwe za Zanzibar likisomeka "Zanzibar - Splendid Unspoiled White Sand Beaches" |
Tangazo kwenye basi linalohusu Mlima Kilimanjaro likisomeka "Glorious Mt. Kilimanjaro - The roof of Africa only in Tanzania" |
Tangazo kwenye basi linalohusu Ngorongoro likisomeka "Magnificent Ngorongoro Crater- World's wildest Nature" |
Tangazo kwenye basi linalohusu Serengeti likisomeka "Outstanding Serengeti Wildlife- The Largest Wild Migration in the World" |
Saturday, December 11, 2021
MAWAZIRI WA AFYA KUTOKA NCHI ZA EAC WAKUTANA MJINI ZANZIBAR
Mkutano wa 21 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta (BLM) la Afya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki umefanyika tarehe 10 Desemba 2021 katika Hotel Verde mjini Zanzibar.
Mkutano wa Baraza la Mawaziri ulitanguliwa na mikutano miwili ya awali iliyofanyika tarehe 6 hadi 8 Desemba 2021na tarehe 9 Desemba 2021 katika ngazi ya Wataalamu na Makatibu Wakuu mtawalia.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Nassor Ahmed Mazrui (Mb) aliwakaribisha wajumbe wa mkutano huo mjini Zanzibar na kupongeza maamuzi yaliyofikiwa na sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ya kwamba mkutano huo ufanyike mjini humo ili kuwapa fursa wajumbewa mkuano huo kuyafahamu maeneo ya utalii ndani ya kanda.
Vilevile alieleza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kufanyia kazi maamuzi na mapendekezo mbalimbali yanayotolewa na vikao hivyo ili yaweze kuwa na tija kwa masalahi ya wananchi ndani ya jumuiya.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia Sekta ya Uzalishaji na Jamii, Mhe. Christophe Bazivamo katika ufunguzi wa mkutano huo aliipongeza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mapokezi mazuri kwa wajumbe wa mkutano huo na kwa kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Aidha, alitumia nafasi hiyo kupongeza jitihada mbalimbali zinazofanywa na Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kurasimisha lugha nyingine zitakazotumiwa kwenye mikutano ya jumuiya hiyo ambapo, alieleza mpaka sasa Sekretarieti ya Jumuiya hiyo inafanyia kazi taratibu za kuifanya lugha za Kiswahili na kifaransa kuwa lugha rasmi kwa ajili ya matumizi ya mikutano ya jumuiya.
Pia amepongeza juhudi zilizooneshwa na Shirika
la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kutangaza tarehe 7 Julai kuwa siku ya Kiswahili.
“UNESCO imeonesha ni namna gani lugha ya Kiswahili ambayo ndio lugha pekee ya kiafrika yenye watumiaji wengi imeweza kuthaminiwa ulimwenguni, sisi kama jumuiya tutaendeleza jitihada za kukuza Kiswahili” alisema Mhe. Bazivamo.
Kadhalika, Mhe. Bazivamo amezisisitiza Nchi wanachama wa jumuiya hiyo kukamilisha zoezi la uandaaji wa Hati za Kusafiria za Kielekronik za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC e-Passport) ambapo, ameeleza mpaka sasa ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pekee ndio imefanikiwa kukamilisha zoezi la ugawaji wa Hati hizo za kusafiria kwa wananchi wake.
Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo umeongozwa na Mhe. Nassor Ahmed Mazrui (Mb.) Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambaye ameambatana na Mhe. Dkt. Godwin Mollel (Mb.) Naibu Waziri, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa Tanzania Bara.
Viongozi wengine walioshiriki mkutano huo ni pamoja na; Dkt. Fatma H. Mrisho, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar; Dkt. Othman Mohamed Ahmed, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia - Tanzania Bara, Bw. Eliabi Chodota, Mkurugenzi Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki; na Dkt. Abdul S. Ali, Mganga Mkuu na Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia Wazee na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Pamoja na Mambo mengine Mkutano wa 21 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Afya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki umepokea taarifa ya utekelezaji wa maamuzi/maagizo ya mikutano iliyopita; hali ya mlipuko wa janga la UVIKO-19 Kikanda; na Utekelezaji wa program na miradi ya Afya.
Mkutano huo umehudhuriwa na nchi zote wanachama isipokuwa Jamhuri ya Rwanda na Jamhuri ya Sudan Kusini ambao walishiriki mkutano kwa njia ya mtandao.
Ujumbe wa Tanzania |
Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania |
Ujumbe kutoka Burundi |
Ujumbe kutoka Uganda |
Picha ya pamoja viongozi wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Mawaziri wa Afya wa Jumuiya hiyo walioshiriki mkutano. |
Mkutano ukiendelea |
Thursday, December 9, 2021
MAKATIBU WAKUU WA WIZARA ZA AFYA KUTOKA NCHI ZA EAC WAKUTANA MJINI ZANZIBAR
Mkutano wa 21 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta (BLM) la Afya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika ngazi ya Makatibu Wakuu unafanyika leo tarehe 9 Desemba 2021katika Hotel Verde mjini Zanzibar.
Mkutano huu na mkutano wa ngazi ya Maafisa Waandamizi ambao ulifanyika tarehe 6 hadi 8 Desemba 2021 ni sehemu ya mikutano ya awali yenye jukukumu la kupitia na kuwasilisha agenda na mapendekezo ya masuala ya afya ya kikanda yatakayo wasilishwa katika Mkutano wa 21 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Afya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika tarehe 10 Desemba 2021.
Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huu unaongozwa na Dkt. Fatma H. Mrisho, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Viongozi wengine walioambatana naye ni pamoja na Dkt. Othman Mohamed Ahmed, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia - Tanzania Bara, Bw. Eliabi Chodota, Mkurugenzi Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Dkt. Abdul S. Ali, Mganga Mkuu na Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Mkutano huu unafanyika mjini Zanzibar kwa lengo la kuendeleza jitihada za jumuiya katika kutangaza maeneo ya utalii ndani ya jumuiya. Vilevile kuvutia wageni na kuhamasisha utalii wa ndani kama ilivyosisitizwa katika maonesho ya Utalii ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC-Tourism Expo) yaliyofanyika mapema mwezi Oktoba 2021 Jijini Arusha.
==============================
Ujumbe wa Tanzania |
Ujumbe wa Tanzania |
Ujumbe wa Tanzania |
Sehemu nyingine ya Ujumbe wa Tanzania |
Ujumbe kutoka Kenya |
Ujumbe kutoka Uganda |
Ujumbe kutoka Burundi |