Wednesday, August 31, 2022

KAMATI YA NUU YARIDHISHWA NA MIKAKATI YA UTEKELEZAJI WA DIPLOMASIA YA UCHUMI




Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akisoma taarifa ya Mikakati ya Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU)

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akiendelea kusoma taarifa ya Mikakati ya Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) huku wajumbe hao wakimsikiliza kwa makini.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), Mhe. Victor Kawawa akisema jambo wakati wa kikao kati ya Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU). 

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) wakifuatilia kwa makini taarifa ya Mikakati ya Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi iliyokuwa ikiwasilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), Mhe. Alexander Pastory Mnyeti akichangia jambo katika kikao hicho

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), Mhe. Cosato Chumi akichangia jambo katika kikao hicho

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), Mhe. Ali Hassan Omar King akichangia jambo katika kikao hicho
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akinukuu hoja za Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU)

Kaimu Mkurugenzi wa  Idara ya Sera na Mipango katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Justin Kisoka akifafanua jambo wakati wa  kikao kati ya Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU)

Mkurugenzi wa  Kitengo cha Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi James Bwana akifafanua jambo wakati wa  kikao kati ya Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU)
Kaimu Mkurugenzi wa  Idara ya Diplomasia ya Uchumi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw.Magabilo Murobi akifafanua jambo wakati wa  kikao kati ya Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU)
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) 
walioshiriki kikao kati ya Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Kamati hiyo.
Baadhi ya Wakuu wa Taasisi, Idara na Vitengo kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki walioshiriki kikao kati ya Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Kamati ya NUU.
Sehemu ya Wakuu wa Taasisi, Idara na Vitengo kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki walioshiriki kikao kati ya Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Kamati ya NUU.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Taasisi, Idara na Vitengo kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki walioshiriki kikao kati ya Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Kamati ya NUU.




 

TANZANIA, QATAR KUSHIRIKIANA SEKTA YA AFYA

Katika jitihada za kutafuta fursa mbalimbali za ajira kwenye sekta ya afya, ujumbe wa Tanzania uliopo ziarani nchini Qatar umekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Hamad Medical Corporation (HMC) Jijini Doha, Qatar. 

Ujumbe huo wa serikali uliongozwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu kwa kushirikiana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma M. Rajab. 

Viongozi hao wamejadiliana namna ya kuanza kutoa nafasi za ajira kwa watanzania. Watalaam wa sekta ya Afya nchini Tanzania walikuwa hawajaanza kuingia kwenye soko la ajira la Qatar na hivyo endapo Tanzania itafunguliwa nafasi hizo itaweza kupeleka watalaamu wake kufanya kazi nchini humo.

Mkurugenzi Mtendaji Msaidizi, Idara ya Rasilimali Watu wa 'Hamad Medical Center', Bi. Sabeeha Amin Qasemi amesema kuwa hospitali hiyo imefurahishwa na hatua ambazo Tanzania inazichukua katika kuboresha sekta ya afya na kuahidi kuwa watatoa nafasi za ajira kwa wataalamu wa afya ambao hatimaye watapelekwa kwenye hospitali mbalimbali nchini Qatar. 

Naye, Prof. Katundu ameuhakikishia uongozi wa Shirika hilo kuwa Tanzania ina wataalamu wa afya wenye uwezo na uzoefu wa kutosha na endapo watapata fursa za ajira nchini humo watafanya kazi kwa bidii na weledi kwa kuzingatia sheria na taratibu za Qatar kwa kuwa watahiniwa hao hupatiwa mafunzo wakati na baada ya usaili wa ajira.  

Kwa upande wake, Balozi Fatma Rajab amesema kuwa Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki itaendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali ya Qatar ili kuiwezesha Serikali hiyo kupata wafanyakazi bora zaidi katika sekta mbalimbali. 

Mkurugenzi Mtendaji Msaidizi, Idara ya Rasilimali Watu wa 'Hamad Medical Corporation', Bi. Sabeeha Amin Qasemi akizungumza na ujumbe wa Serikali ya Tanzania uliongozwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu kwa kushirikiana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma M. Rajab walipokutana kwa mazungumzo Jijini Doha, Qatar

Mmoja wa Mawakala wa ajira binafsi kutoka Tanzania akichangia jambo wakati wa mazungumzo ya vuiongozi hao yaliyofanyika Jijini Doha, Qatar

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu akielezea mkakati wa Serikali kwa uongozi wa 'Hamad Medical Corporation' Jijini Doha, Qatar. Wa kwanza kulia mwa Prof. Katundu ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu akielezea mkakati wa Serikali kwa uongozi wa 'Hamad Medical Corporation' Jijini Doha, Qatar


Mazungumzo baina ya Ujumbe wa Tanzania na Uongozi wa Hamad Medical Center yakiendelea Jijini Doha, Qatar



Tuesday, August 30, 2022

MAWAKALA WA AJIRA BINAFSI WA TANZANIA, QATAR WAJADILI FURSA ZA AJIRA

Mawakala wa ajira katika sekta binafsi nchini Tanzania wamekutana na kujadili fursa za ajira na Mawakala wenzao wa ajira binafsi wa Qatar, Jijini Doha tarehe 30 Agosti, 2022.

Mawakala hao wameongozana na Ujumbe wa Serikali ya Tanzania ulioongozwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu kwa kushirikiana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab.

Akifungua mkutano huo, Mkuu wa Kitengo cha Uratibu kutoka Wizara ya Kazi nchini Qatar, Bw. Hamad Ali Elfaifa amesema Qatar na Tanzania zina uhusiano wa muda mrefu na wa kihistoria ambao umedumu hadi sasa na wanapenda kuuendeleza kwa kushirikiana katika nyanja mbalimbali ikiwemo sekta ya ajira.

Bw. Elfaifa amewataka Mawakala wa ajira kutoka Tanzania kuzingatia sheria na taratibu za ajira pamoja na kushirikiana na Mawakala wenzao wa Qatar ili kuweza kupata wafanyakazi wenye ujuzi, maarifa na weledi kwa maslahi ya pande zote mbili.

Vilevile, Bw. Elfaifa ameeleza kuwa katika kutekeleza Mkataba wa Ajira kati ya Tanzania na Qatar, sasa Tanzania imeingizwa kwenye mfumo wa ajira nchini Qatar ambapo mawakala wa Tanzania wataweza kupokea oda za kazi kutoka kwa Mawakala wa Qatar, hatua itakayowezesha watanzania wengi wenye sifa kunufaika na nafasi za kazi nchini Qatar

Kwa upande wake, Kiongozi wa ujumbe wa Serikali ya Tanzania, Prof. Katundu amesema Tanzania inajivunia kuwa na vijana wenye ujuzi na uzoefu katika fani mbalimbali hivyo wanaamini kuwa endapo vijana hao watapatiwa fursa za ajira nchini Qatar watasaidia kuboresha zaidi uchumi wa Qatar pamoja na Maisha yao.

Naye Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Ajira (TaESA), Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. Joseph Nganga amesema kuwa lengo kubwa la kuwakutanisha mawakala wa ajira binafsi wa Tanzania na wa Qatar ni kufahamishana taratibu za ajira kwa pande zote mbili ili kuweza kufanya kazi kwa ushirikiano na kupata waajiriwa wenye sifa stahiki.

“Mkutano wa leo umesaidia kufahamu taratibu zinazotakiwa ili kumpata mfanyakazi na stahiki zake hivyo mawakala wa nchi zote watumie fursa hiyo ipasavyo ambapo Mawakala wa Qatar wameonesha kuridhishwa na nidhamu ya vijana wanaoajiriwa kutoka Tanzania na kuahidi kuendelea kushirikiana na mawakala kutoka Tanzania ili kuwapata wafanyakazi kwenye sekta mbalimbali,” alisema Bw. Nganga.

Mwaka 2014 Tanzania ilisaini mkataba wa makubaliano ya ajira na Qatar, ambapo kwa sasa Serikali ya Tanzania inaangalia namna ya kupata nafasi za ajira kwa Watanzania ili waende kufanya kazi nchini humo.

Ujumbe wa Chemba ya Biashara ya Qatar ukizungumza na Ujumbe wa Serikali ya Tanzania ulioongozwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu kwa kushirikiana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab Jijini Doha tarehe 30 Agosti, 2022

Ujumbe wa Chemba ya Biashara ya Qatar ukizungumza na Ujumbe wa Serikali ya Tanzania ulioongozwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu kwa kushirikiana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab Jijini Doha tarehe 30 Agosti, 2022

Mkuu wa Kitengo cha Uratibu kutoka Wizara ya Kazi nchini Qatar, Bw. Hamad Ali Elfaifa akizungumza na Mawakala wa ajira binafsi kutoka Tanzania na Qatar walipokutana Jijini Qatar kujadili fursa za ajira nchini humo

Kikao cha Mawawakala wa ajira binafsi kutoka Tanzania na Qatar kikiendelea Jijini Qatar

Kamishna wa Kazi, Wizara ya Kazi Zanzibar, Bw. Rashid Khamis Othman akizungumza na Mawakala wa ajira binafsi kutoka Tanzania na Qatar walipokutana Jijini Qatar kujadili fursa za ajira nchini Qatar

Mmoja kati ya Mawakala wa ajira binafsi kutoka Tanzania akieleza jambo kwa mawakala walioshiriki katika mkutano ulifanyika leo Jijini Doha, Qatar

Mmoja kati ya Mawakala wa ajira binafsi kutoka Qatar akieleza jambo kwa mawakala walioshiriki katika mkutano ulifanyika leo Jijini Doha, Qatar



TANZANIA NA SINGAPORE KUIMARISHA DIPLOMASIA YA UCHUMI

Serikali ya Tanzania na Singapore zimeahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na kihistoria uliopo baina yao ili kutekeleza kwa ufanisi malengo ya kiuchumi ya mataifa hayo.

Ahadi hiyo imetolewa wakati wa mazungumzo kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula na Balozi wa Singapore nchini mwenye makazi yake Singapore, Mhe. Douglas Foo yaliyofanyika tarehe 30 Agosti 2022 katika ofisi za Wizara jijini Dodoma.

Katika mazungumzo hayo Mhe. Balozi Mulamula alieleza kuwa ni muhimu kwa Tanzania na Singapore kuuenzi ushirikiano ulioasisiwa na waasisi wa mataifa yao kwa manufaa ya wananchi wake.

Pia alieleza Tanzania ina nia ya kushirikiana na Singapore katika maeneo mbalimbali ikiwemo: Kukuza shughuli za bandari, kilimo cha mbogamboga na matunda, usafirishaji wa mazao ya biashara kama vile kahawa na chai, biashara, utalii, ufadhili wa masomo na ushirikiano katika masuala ya utamaduni hususan kuanzisha makubaliano ya kufundisha lugha ya Kiswahili nchini Singapore.

Maeneo mengine ya ushirikiano ni pamoja na: Kujenga uwezo katika masuala ya teknolojia ya habari na mawasiliano, uwekezaji katika maeneo maalum ya viwanda, usafiri wa anga na ushirikiano katika masuala ya kikanda.

“Tanzania inawekeza katika kujenga uwezo wa rasilimali watu kwenye masuala ya teknolojia ya habari na mawasiliano, pia kupitia uwepo wa mkongo wa mawasiliano wa taifa ina dhamira ya kutoa huduma ya mawasiliano nje ya mipaka yake” alisema Balozi Mulamula.

Kwa upande wa Mhe. Douglas Foo alieleza kuwa uhusiano kati ya Tanzania na Singapore unatimiza miaka 40 tangu ulipoanzishwa hivyo, ni muhimu kuangalia maeneo yenye fursa za kiuchumi ili kuendelea kuimarisha ushirikiano kwa manufaa kwa pande zote mbili.

Tanzania na Singapore zinaunganishwa na uanachama wao katika Umoja wa nchi za jumuiya ya madola na hivyo ni fursa kwa mataifa hayo kuongeza maeneo ya ushirikiano kupitia makubaliano yatakayowezesha usimamizi wa karibu wa utekelezaji wa malengo katika maeneo husika ya maendeleo.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula amefanya mazungumzo na Balozi wa Singapore nchini mwenye makazi yake nchini Singapore, Mhe. Douglas Foo alipomtembelea katika ofisi za Wizara tarehe 30 Agosti 2022 jijini Dodoma.

Mhe. Douglas Foo akifafanua juu ya uzoefu wa Singapore katika kusimamia makubaliano mbalimbali yanayoanzishwa na serikali yake kwa lengo la kukuza uchumi na kuinua maendeleo ya Taifa kwa ujumla.
Mazungumzo yakiendelea.
 Mhe. Balozi Mulamula akiagana na Mhe. Foo baada ya mazungumzo. 

MIRADI NANE YA KIPAUMBELE YAWASILISHWA TICAD8


Serikali ya Tanzania imewasilisha miradi nane ya kipaumbele yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 1.334 katika Mkutano wa Nane wa Kimataifa wa Wakuu wa Nchi na Serikali unaohusu Maendeleo ya Japan na Afrika (TICAD8) uliohitimishwa tarehe 28 Agosti 2022 jijini Tunis nchini Tunisia. 

Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (Mb.) aliyaeleza hayo jana tarehe 29 Agosti, 2022 akiwa nchini Tunisia ambako alimwakilisha Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo. 

Miradi hiyo nane ambayo itatekelezwa Tanzania Bara na Tanzania - Zanzibar imetajwa kuwa ni; ukarabati wa bandari ya uvuvi ya Wete, ujenzi wa bwawa la kusambaza maji la Lugoda, Mufindi Mkoani Iringa, ukarabati wa barabara ya Morogoro-Dodoma kwa kiwango cha lami, mradi wa umwagiliaji katika bonde la Ziwa Victoria, ujenzi wa njia ya umeme ya Songa-Fungu-Mkuranga, uanzishwaji wa maabara ya kuthibitisha ubora kwenye sekta ya uvuvi, kujenga uwezo wa kituo cha utafiti cha ufugaji wa samaki Dar es Salaam na ujenzi wa bandari nne za kisasa za uvuvi

Sambamba na miradi hiyo, Waziri Mkuu ameeleza kuwa, licha ya Tanzania kunufaika na ujenzi wa daraja la Mfugale, mradi wa kufua umeme wa Kinyerezi II kupitia TICAD, vilevile amewasilisha maombi ya kukamilishiwa miradi mitatu ya ujenzi wa barabara ya Arusha - Holili, Bandari ya Kigoma na mradi wa maji wa Zanzibar yenye thamani ya dola za Marekani milioni 343.8.

Mbali na kushiriki TICAD 8, Waziri Mkuu kwa nyakati tofauti alifanya mikutano ya pembezoni na Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) Dkt. Akihiko Tanaka, Makamu wa Rais wa Kampuni ya Mitsubishi Bw. Yasuteru Hirai na Mwenyekiti wa Bodi ya Japan Tobacco Incorporation (JTI) Bw. Mutsuo Iwai 

Katika mazungumzo hayo Waziri Mkuu amewashukuru na kuwapongeza wadau hao kwa kuchangia katika shughuli mbalimbali za maendeleo nchini ikiwemo ujenzi wa shule ya bweni ya wasichana wilayani Urambo iliyojengwa na JTI, ambapo pia ametoa rai kwa kampuni hiyo kuendelea kununua zao la tumbaku nchini sambamba na kuongeza kiwango cha ununuzi wa zao hilo kutoka kwa wakulima.

Waziri Mkuu vilevile amewapongeza watendaji wa Kampuni ya Mitsubishi kwa kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya umeme mkoani Kilimanjaro na akatoa rai waangalie uwekezekano wa kujenga kiwanda cha uzalishaji mbolea nchini.

Kwa upande wake Rais wa JICA Dkt. Tanaka, amemuahidi Waziri Mkuu kuendelea kufanya kazi kwa karibu na Serikali katika kuibua na kutekeleza miradi mbalimbali inayogusa maisha ya kila siku ya Watanzania, pia ameahidi kuwarudisha wafanyakazi waliokuwa wakijitolea katika sekta mbalimbali nchini ambao walilazimika kurudi Japan kwa sababu ya janga la UVIKO-19. 

Rais wa JICA Dkt. Tanaka alitumia fursa ya mazungumzo hayo kuelezea furaha yake na kufikisha shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuchangia makala ya chapisho kuhusu TICAD 8. 

Miradi hiyo nane iliyowasilishwa TICAD8 ni yakipaumbele kwa mujibu wa Mpango wa Taifa wa Tatu wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP III).
Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.) akisalimiana na Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) Dkt. Akihiko Tanaka walipokutana kwa mazungumzo jijini Tunis nchini Tunisia.
Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.) akiwa katika mazungumzo na Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) Dkt. Akihiko Tanaka yaliyofanyika jijini Tunis nchini Tunisia
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Mbarouk (Mb.) akichangia jambo wakati wa mazungumzo yaliyofanyika baina ya Waziri Mkuu na Rais wa JICA.
Balozi wa Tanzania nchini Japan Mhe. Baraka Luvanda akifuatilia mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea baina ya Waziri Mkuu na Rais wa JICA
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango - Zanzibar Bw. Aboud Mwinyi, akichangia jambo wakati wa mazungumzo yaliyofanyika baina ya Waziri Mkuu na Rais wa JICA
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na ujumbe wake akiwa na katika picha ya pamoja na ujumbe wa JICA. 

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na ujumbe wake akiwa na katika picha ya pamoja na ujumbe wa JICA

Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Mitsubishi Bw. Yasuteru Hirai, yaliyofanyika jijini Tunis nchini Tunisia

8. 




Monday, August 29, 2022

UJUMBE WA SERIKALI YA TANZANIA WAENDELEA NA ZIARA NCHINI QATAR

 




Ujumbe wa Serikali ya Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu kwa kushirikiana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab ukiwa katika mazungumzo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kazi Qatar, Mhe. Mohammed Hassan Al-Obaidly Jijini Doha Tarehe 29 Agosti,2022

Kikao baina ya ujumbe wa Serikali ya Tanzania na ujumbe kutoka Wizara ya Kazi nchini Qatar kikiendelea Jijini Doha


Ujumbe wa Serikali ya Tanzania na ujumbe kutoka Wizara ya Kazi nchini Qatar ukiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza kikao chao Jijini Doha

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu akimueleza jambo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Elimu ya Juu Qatar Mhe. Ibrahim bin Saleh Al Nuaimi wakati ujumbe wa Serikali ya Tanzania ulipofanya ziara katika Ofisi za Wizara hiyo Jijini Doha. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab akimkabidhi zawadi Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Usafirishaji ya MOWASALAT ya Qatar wakati ujumbe wa Tanzania ulipofanya ziara katika Ofisi hizo Jijini Doha