Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizindua mfumo wa kidigitali unaoainisha fursa za uwekezaji zinazogusa malengo ya maendeleo endelevu |
Wednesday, November 30, 2022
SERIKALI YAZINDUA MFUMO WA KIDIGITALI WA KUAINISHA FURSA ZA UWEKEZAJI
Tuesday, November 29, 2022
SERIKALI, UNAIDS WAZINDUA RIPOTI YA HALI YA UKIMWI DUNIANI 2022
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Ukimwi (UNAIDS) wamezindua Ripoti ya Ukimwi Duniani kwa Mwaka 2022 leo Jijini Dar es Salaam.
Hafla ya Uzinduzi wa ripoti hiyo imeongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Mhe. George Simbachawene kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa
Wakati wa uzinduzi huo Mhe. Simbachawene amesema idadi ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) nchini yamepungua kwa asilimia 50 kutoka 110,000 mwaka 2010 hadi 54,000 mwaka 2021.
Waziri Simbachawene amesema pia idadi ya vifo vinavyotokana na Virusi vya Ukimwi kupungua kwa zaidi ya asilimia 50 kutoka 64,000 mwaka 2010 hadi 29,000 mwaka 2021.
“Tanzania imeongeza juhudi za kuzuia maambukizi ya VVU ambapo maambukizi mapya katika miaka minne (2017-2021) iliyopita yalipungua kwa asilimia 38,” alisema Simbachawene.
“Kama nchi tunaungana na kukubaliana na kaulimbiu ya Siku ya UKIMWI Duniani ya mwaka 2022 ya ‘kukusekana kwa usawa ni hatari’ ili kuhakikisha kuwa kila mtu nchini Tanzania anapata huduma bora za afya na VVU. Ili kukabiliana na tofauti katika upatikanaji na utumiaji wa huduma za afya, Tanzania imeandaa muswada wa bima ya Afya kwa Wote kwa lengo la kuhakikisha Huduma ya Afya kwa Wote. Dhamira ya Mkakati wa Kitaifa wa Afya wa 2021 - 2026 ni kutoa huduma za afya endelevu zenye viwango vinavyokubalika kwa wananchi wote bila vikwazo vya kifedha, kwa kuzingatia usawa wa kijiografia na kijinsia, aliongeza Mhe. Simbachawene.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UKIMWI (UNAIDS), Bi. Winnie Byanyima amesema kwa mujibu wa ripoti mpya ya UNAIDS iliyozinduliwa inabainisha kuwa hatua za haraka zinahitajika ili kukabiliana na kukosekana kwa usawa katika mapambano dhidi ya UKIMWI duniani.
“Tunahitaji kushughulikia changamoto ya kukosekana kwa usawa kwa wanawake hasa wenye VVU. Asilimia 50 ya wanawake wanaofanyiwa ukatili wa kijinsia wanauwezekano wa kupata VVU. Katika nchi 33 duniani tangu mwaka 2015 - 2021 sawa na asilimia 41 ya wanawake walioolewa wenye umri wa miaka 15 - 24 wanaweza kufanya maamuzi yao wenyewe juu ya afya ya ngono. Njia pekee yenye ufanisi wa kukomesha unyanyasaji kwa waathirika wa UKIMWI na kufikia malengo ya maendeleo endelevu ni kuhakikisha afya, haki na ustawi wa pamoja vinapatikana kwa wakati,” alisema Bi. Byanyima
Tanzania imekuwa imefanikiwa kupunguza maambukizi na vifo vitokanavyo na ukimwi kwa asilimia 50, jitihada hizo zimeifanya Tanzania kuwa nchi ya mfano duniania katika udhibiti wa ugonjwa huu, ameongeza Bi. Byanyima
Bi. Byanyima ameongeza viongozi wa mataifa mbalimbali dunia wanapaswa kuhakikisha usawa katika upatikanaji wa haki, huduma, sayansi bora na dawa, kwani kwa kufanya hivyo hakutasaidia tu waliotengwa bali pia kusaidia kila mmoja.
Nae mwakilishi wa Baraza la watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi Tanzania (Nacopha), Bi. Bahati Haule amesema kuna umuhimu wa jamii kupewa elimu dhidi ya masuala ya usawa na unyanyapaa kwa waathirika wa VVU kwa kuwa wengi wa walioathirika wamekuwa wakitengwa na kunyanyapaliwa katika jamii zinazowazunguka.
“Ni wakati muafaka kwa dunia na jamii zetu zinazotuzunguka kuungana pamoja katika kupinga unyanyasji dhidi ya waathirika wa VVU pamoja na kuhakikisha usawa katika haki na huduma vinapatikana, alisema Bi. Bahati
Ripoti ya Siku ya Ukimwi Duniani 2022 inaongozwa na kauli mbiu ambayo ni kukusekana kwa usawa ni hatari.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Mhe. George Simbachawene akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Ukimwi Duniani kwa Mwaka 2022 Jijini Dar es Salaam |
Monday, November 28, 2022
MKURUGENZI MTENDAJI UNAIDS AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UKIMWI (UNAIDS), Bi. Winnie Byanyima amewasili nchini tarehe 27 Novemba , 2022.
Mkurugenzi huyo atakuwepo nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi kuanzia Tarehe 28 Novemba hadi 6 Desemba, 2022. Mara baada ya kuwasili nchini, Bi. Byanyima alipokelewa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel
Akiwa nchini Bi. Byanyima atashiriki Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yatakayofanyika Mkoani Lindi pamoja na kushiriki uzinduzi wa taarifa ya Hali ya Ukimwi nchini pamoja na kukutana na Baraza la watu wanaoishi na VVU (Nacopha).
Aidha, Bi. Byanyima, anatarajia kukutana kwa mazungumzo na viongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Mapinduzi.
Saturday, November 26, 2022
DKT. TAX AWAASA VIJANA KUIGA FALSAFA ZA UONGOZI WA NYERERE
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax amewaasa vijana kutumia vyema Taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation kujifunza, kubadilishana mawazo juu ya falsafa za Mwalimu Nyerere pamoja na kuimarisha amani na umoja katika jamii.
Dkt. Tax ametoa wito huo alipokuwa akifungua mafunzo yanayotolewa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation kwa kundi la kwanza la viongozi vijana 60 kutoka nchi zaidi ya 40 Barani Afrika tarehe 25 Novemba, 2022 usiku Jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine, Dkt. Tax aliwasisitiza vijana hao kutumia mafunzo hayo kuinufaisha jamii inayowazunguka.
“Napenda kutumia fursa hii kuwasihi vijana wa kizazi kipya cha Viongozi wa Afrika na watu wa Afrika, kufanya kazi kwa umoja, ushirikiano, na imani thabiti, kwani bila kufanya hivyo ni vigumu kuwa na mustakabali wa Afrika tunayoitaka,” alisema Dkt. Tax.
Dkt. Tax aliongeza kuwa, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Uongozi Imara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, imejipanga kuhakikisha vijana wanawezeshwa ili kuendeleza amani, usalama na maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
“Katika kuenzi mchango mkubwa wa Mwalimu Nyerere katika kukuza umoja, amani na maendeleo ya watu nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla, Serikali inaendelea kuunga mkono mipango ya amani kwa kuchangia Misheni za ulinzi wa amani Barani Afrika na Kikanda. Leo hii Tanzania ni nchi ya 13 kwa ushiriki katika Operesheni za Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa Duniani,” aliongeza Dkt. Tax
Bara la Afrika limebarikiwa rasilimali nyingi, tuchanganye maarifa, ujuzi wa uongozi, na maliasili ilizonazo ili kupeleka bara la Afrika katika ngazi za juu zaidi. Kwa kufanya hivyo, vijana mtakuwa mmeenzi falsafa za uongozi za Mwalimu Nyerere, aliyeongoza mapambano ya kupigania uhuru, umoja, na kujenga misingi imara ya Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Awali akizungumza kabla ya ufunguzi wa mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation, Bw. Joseph Butiku alisema kuwa programu ya Mafunzo ya Uongozi kwa Vijana yanayotolewa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere ni mpango unaolenga kushirikisha viongozi vijana katika kutoa mafunzo, changamoto, kufafanua na kubadilisha mtazamo wa kizazi kipya cha Afrika kuwa viongozi wanaowajibika, wanaojitolea na wapenda amani.
“Malengo ya taasisi yetu ni kutafiti na kueneza falsafa ya uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere, amani, umoja na maendeleo ya watu. viongozi wazuri na wenye tija wa sasa na wa siku zijazo wa bara hili,” alisema Bw. Butiku.
Mafunzo hayo yametolewa kwa vijana 60 kutoka mataifa mbalimbali ambayo ni Botswana, Burundi, Cameroon, Djibouti, Misri, Ethiopia, Gabon, Guinea, Kenya, Libya, Liberia, Namibia, Nigeria, Rwanda, Sudani, Sudani Kusini, Afrika Kusini, Tanzania, Uganda, na Zambia.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation, Bw. Joseph Butiku akielezea mkakati wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere wa kuwaendeleza na kuwajengea vijana viongozi uwezo |
Friday, November 25, 2022
Thursday, November 24, 2022
DKT. TAX AFANYA MAZUNGUMZO NA MENEJIMENTI YA UDOM
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) na Mkuu wa Chuo cha Dodoma akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Chuo Kikuu cha Dodoma. |
MABALOZI WARIDHISHWA NA MIPANGO YA HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA
Waheshimiwa Mabalozi wa Tanzania katika nchi za Ufaransa, Japan na Brazil wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika |
Waheshimiwa Mabalozi wa Tanzania katika nchi za Urusi na Austria wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika |
Waheshimiwa Mabalozi wa Tanzania wakiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika |
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika akiwa katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Mabalozi wa Tanzania |
Wednesday, November 23, 2022
DKT.TAX AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA URUSI NA IRAN
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akimkaribisha Balozi wa Iran nchini Mhe. Hossein Alvandi Bahineh wakati wa mazungumzo yaliyofanyika jijini Dodoma. |
Sunday, November 20, 2022
MABALOZI WAHIMIZWA KUBIDHAISHA KISWAHILI
Saturday, November 19, 2022
RAIS SAMIA AWATAKA MABALOZI KUENDANA NA MABADILIKO YA DUNIA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwahutubia Mabalozi wa Tanzania Nje ya Nchi wakati wa mkutano uliofanyika Zanzibar tarehe 19 Novemba, 2022 |
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akitoa neno la utangulizi wakati wa mkutano kati ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na Mabalozi |
Sehemu ya Mabalozi wakifuatilia mkutano kati yao na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan uliofanyika Zanzibar 19 Novemba 2022 |
Meza kuu ikiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja |
Meza kuu ikiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na uongozi wa Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki |