Sunday, November 6, 2011

Royal Highness and the Dutches of Cornwall Arrival in Dar es salaam


His Royal Highness and the Dutches of Cornwall with the Prime Minister of Tanzania Hon. Mizengo Pinda at the airport in Dar es salaam shortly after their arrival

High-ranking government officials led by the Minister for Fore ign Affairs and International Cooperation Hon. Bernard Membe at the airport





The British Royal Highness, Prince Charles has arrived this evening in Dar es salaam for the four-day Official visit to Tanzania. The Prince visit is among the series of visits to commemorate the 50Years of Tanzania Mainland Independence.
The Royal Highness is accompanied by the Dutches of Cornwall, Hon. Henry Bellingham, UK Minister for Africa Affairs and other ranking officials from the Buckingham Palace.
On arrival at the airport, the Royal Highness and the Dutchess of Cornwall were received by the Tanzanian Prime Minister, Hon. Mizengo Kayanza Pinda and other high-ranking officials including the Minister For Foreign Affairs and International Cooperation Hon. Bernard Membe.
While in the country, the Prince of Wales will have an opportunity to hold official talks with President Jakaya Kikwete and gracing the Ministry of Science and Technology 50Years Exhibition. He is also expected to visit a number of Development projects supported by the British Government and make a visit to Arusha and Zanzibar.
On the Zanzibar trip, the Prince will pay a courtesy call to Dr. Mohammed Shein, the President of Zanzibar.
In Arusha, the Royal Highness will visit Legunga School to find more about the donor and government partnership in improving access to education and get briefing on the role of Non-governmental in raising awareness.
Prince Charles and his delegation are expected to depart Tanzania from Kilimanjaro International Airport.






Saturday, November 5, 2011

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. John Haule akiwa kwenye mazungumzo leo na Maafisa wa Mambo ya Nje wa Wizara waliohitimu mafunzo ya wiki tatu ya diplomasia.

Baadhi ya Kaimu Wakurugunzi wa Wizara wakisikiliza hoja za Maafisa wa Mambo ya Nje wa Wizara walipofanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara leo tarehe 5.11.2011

Katibu Mkuu wa Wizara Bw. John Haule akiandika baadhi ya hoja za Maafisa Mambo ya Nje wa Wizara alipokutana nao leo wizarani baada ya kuhitimu mafunzo ya diplomasia.


Kaimu Mkurugenzi Idara ya Asia na Australasia Bw. Rogatus Shao akifuatilia mazungumzo ya Katibu Mkuu kwenye mkutano huo. Kulia ni msaidizi wake kwenye idara hiyo Bi. Naimi Aziz 
Bw. Robert Kahendaguza, Afisa Mambo ya Nje Ubalozi wa Tanzania Pretoria Afrika Kusini, akizungumza kwa niaba ya Maafisa wengine changamoto na mafanikio ya maafisa hao baada ya mafunzo yao.  

Thursday, November 3, 2011

Waziri Membe azungumza na Waandishi wa Habari

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake kufuatia Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Jumuiya ya Madola uliofanyika Mjini Perth Australia. Katika mkutano na waandishi wa habari Waziri Membe pia alizungumzia msimamo wa Tanzania kuhusu kauli ya Waziri Mkuu wa Uingereza Mhe. David Cameron  kuhusu utoaji wa misaada kwa nchi zinazoendelea kwa masharti. Kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Mahadhi Juma Mahadhi na Katibu Mkuu wa Wizara John Haule.



Maelezo ya Mhe. Bernard K. Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa baada ya kuwasili nchini kutoka kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Jumuiya ya Madola
1.    Nimewaita ili kuwaeleza kwa kifupi kuhusu kikao kilichofanyika Perth Australia kuhusu Jumuiya ya Madola, lakini pia nitazungumzia suala la ‘ushoga’ ambalo limejitokeza hapa na ndio maana wengi wenu mmenyoosha vidole kutaka kuuliza maswali.
2.    Kikao cha Viongozi wa Jumuiya ya Madola kilikwenda vizuri Mjini Perth, kilifanyika vizuri sana kati ya tarehe 28-30 mwezi Oktoba.
3.    Katika kikao kile kulikuwa na masuala matatu makubwa yaliyojitokeza:
a.   La kwanza ni pendekezo la Jumuiya ya Madola kuwa na charter. Charter ni utaratibu wa kuwa na kanuni, taratibu na muongozo wa kufuatwa na wananchi wa Jumuiya ya Madola. Jumuiya hii ni kubwa kwa sababu ina watu bilioni mbili kutoka nchi 54. Kuna dini zote kubwa duniani Wahindu milioni mia saba, Waislamu milioni mia sita, Wakristu milioni mia nne. Hivyo ni Jumuiya kubwa inayostahili kuwa na charter (kanuni) kama ilivyo kwenye Umoja wa Mataifa. Hili lilizungumzwa na kukubaliwa kimsingi na kupitishwa kwenye vikao vya Mawaziri na baadaye kupitishwa na Wakuu wa nchi.
b.   Suala la pili kwenye kikao hicho lilikuwa ni kuimarisha demokrasia, utawala bora, na haki za binadamu.Hili nalo lilizungumzwa kwa pendekezo kwamba tuwe na kamishana, ambaye atashughulikia mambo hayo matatu. Baada ya mjadala mkali kwenye ngazi ya mawaziri na baadae kwa viongozi wan chi, suala hilo halikukubalika kwa sababu Jumuiya ya Madola ina vyombo viwili:-
                                         i.    Ofisi ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola
                                       ii.    Kamati maalum ya Mawaziri wa Jumuiya ya Madola (CMAG)
Vyombo vyote hivi vinahusika na uratibu wa demokrasia, utawala bora na haki za binadamu. Kwa hivyo kuunda chombo kipya cha Kamishna kuratibu mambo haya haya, itaonekana kama ni kupoteza fedha na muda (redundant). Kwa hiyo hilo lilikataliwa.

c.    La tatu lilikuwa linahusu mabadiliko ya tabia nchi au hali ya hewa. Huko nyuma jumuiya ilijikita zaidi kwenye masuala ya haki za binadamu, utawala bora na masuala ya demokrasia. Safari hii viongozi wakasema pamoja ya kwamba mambo haya ni muhimu ni vizuri masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa pamoja na masuala ya maendeleo ya nchi wanachama wa jumuiya yapate uzito kwani bado nchi nyingi za Jumuiya ya Madola ziko kwenye maendeleo sasa na zinakumbwa na zinakumbwa na mabadiliko ya hali ya hewa.

4.    Serikali na Tanzania imesikia tamko la Waziri Mkuu wa Uingereza kwenye Vyombo vya Habari, kuhusu suala la ushoga. Na katika matamko hayo, ushoga unaunganishwa na msaada wa maendeleo “development aid”. Kwamba ili upate msaada wa maendeleo basi ukubali sheria za ushoga zinazoruhusu watu wa jinsia moja kufunga ndoa, na kuishi pamoja.

5.    Suala la ushoga halikuwa sehemu ya ajenda, na wala halikuzungumziwa kwenye kikao cha Viongozi wa Jumuiya ya Madola. Katika Mkutano wa ngazi ya Maafisa Waandamizi kulikuwa na jaribio la Serikali ya Uingereza kuwasilisha pendekezo la kuingizwa aya katika Charter (kanuni) ya Jumuiya ya Madola inayosisitiza kulinda na kuheshimu haki za binadamu kwa ujumla wake, ikiwemo haki za Mashoga. Pendekezo hilo lilipata upinzani mkali na kutupiliwa mbali kwenye ngazi ya Mawaziri na pia halikujitokeza kabisa kwenye ngazi ya Wakuu wa Nchi.

6.    Tamko hili ni la Chama Tawala cha Conservative, na ndiyo sera yao ambapo sasa kwa tamko hili inashinikiza mataifa wanayowapa misaada kuafikiana na suala hili.

7.    Hapa Tanzania, dini zetu na tamaduni za makabila yetu haziruhusu ndoa za jinsia moja. Sheria yetu ya Ndoa ya Mwaka 1971 na sheria ya makosa ya jinai ambazo kwa kiasi kikubwa tulizirithi kutoka kwa Waingereza, zinatambua tu mahusiano kati ya mume na mke, yaani jinsia mbili tofauti. Na Watanzania tunajua kama msingi wa Taifa ni familia, ambayo kwa kanuni na sheria za asili ni muungano wa mwanaume na mwanamke. Matokeo ya muungano huu ni vizazi, ambavyo ndio nguvu kazi na uhai wa taifa. Hivyo basi sheria zetu zinachukulia ndoa za jinsia moja kama kinyume cha maumbile na kosa la jinai ambalo mwenye hatia anaweza kuhukumiwa hadi miaka 30 jela.

8.    Tanzania inafuata utamaduni wa familia ya mume na mke, na kamwe hatutapokea amri wala ushauri wa mtu yoyote nje ya nchi yetu kuja kuingilia masuala ya nchi yetu.

9.    Huu utamaduni mpya wa kuunganisha misaada ya maendeleo na ushoga, kwamba ili upate hiki, fanya hili, inavunja uhusiano wa kimataifa. Ni tamko hatarishi linaloweza kuvunja uhusiano kati ya nchi na nchi. Muhimu zaidi ni kwamba tamko hili linatoka Uingereza ambao ndio walezi wa Jumuiya ya Madola na tumetoka nalo kwenye Mkutano, likitaka kupenyezwa. Tamko hili ni hatari kwa Jumuiya ya Madola na Jumuiya inaweza kuvunjika kwa matamko ya aina hii. Na ikivunjika, Waziri Mkuu wa Uingereza atawajibika na usambaratishaji au kuvunjika kwa Jumuiya ya Madola.  

10. Suala la Mashoga halikubaliwi kwenye Jumuiya ya Madola na iwapo Waziri Mkuu wa Uingereza akililazimisha ndani ya Jumuiya, atahatarisha uhai wa Jumuiya yenyewe. Jumuiya ya Madola ina nchi 54 na ni nchi 13 tu ndio zinaabudu suala hili. Nchi 41 haziabudu suala hili, na hawa ndio wengi. Hili si suala la Uingereza kulishabikia, wala si suala la Uingereza kulitamka wazi leo. Wanaweza kujuta.

11. Tanzania hatuwezi kuyumbishwa wala kupindisha utaifa wetu kwa maagizo wala masharti ya aina hii, tuko tayari kwa lolote lile, bora tuitunze heshima yetu. Tanzania ni nchi maskini sana, na tuna tofauti zetu nyingi za ndani (ya nchi) lakini kamwe hatutaruhusu mtu, au kundi la watu wa nchi yoyote iwe kubwa tajiri itakayokuja kutupa masharti ya kubadilisha utaifa wetu eti kwa sababu tuwe na tumbo lililoshiba, tunakataa. Natamka sasa, tutakataa. Kama wanadhani kuwa misaada kwa nchi zinazoendelea na nchi ya Tanzania itatolewa kwa masharti kwamba sisi tuanze sasa kukubaliana na masuala nje ya sheria na kanuni zetu kama suala hili la mashoga, wakae na hela zao.

Mwisho.
 

Sunday, October 30, 2011

Closing CHOGM Press Conference Official Photos

Commonwealth Heads of Government Meeting, Perth 2011

CHOGM 2011- The Prime Minister of Trinidad and Tobago The Honourable Kamla Persad Bissessar, The Prime Minister and Minister of Foreign Affairs for Samoa The Honourable Tuilaepa Lupesoliai Sailele Malieliegaoi, The Commonwealth Secretary-General His Excellency Kamalesh Sharma, The Australian Prime Minister Julia Gillard, The President of The United Republic of Tanzania His Excellency Jakaya Kikwete, The President of Maldives His Excellency Mohamed Nasheed at CHOGM 30 October 2011.
Photograph by John Donegan/CHOGM.
CHOGM 2011-Concluding Press Conference-The President of Tanzania His Excellency Mr Jakaya Kikwete at a press conferece at the conclusion of The CHOGM 2011 meeting in Perth.
Photograph by Mike Bowers/CHOGM




CHOGM 2011-Concluding Press Conference-FROM LEFT-The Prime Minister of Australia Julia Gillard, The President of Tanzania His Excellency Mr Jakaya Kikwete and The President of The Maldives His Excellency Mr Mohamed Nasheed at a press conference at the conclusion of The CHOGM 2011 meeting in Perth.
Photograph by Mike Bowers/CHOGM



Saturday, October 29, 2011

Waziri Membe akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe na Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada Mhe. John Baird baada ya mazungumzo yao tarehe 29-10-2011
 
“Serikali ya Tanzania imedhamiria kutatua tatizo la ajira kwa vijana kwa kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika nyanja ya elimu ya mafunzo ya ufundi”.

Hayo yamebainishwa leo na Mhe. Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa alipofanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, Mhe. John Baird mjini Perth, Australia pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Jumuiya ya Madola (CHOGM).
Katika mazungumzo hayo, Waziri Membe alisisitiza umuhimu wa Tanzania na Canada kushirikiana katika kuendeleza Sekta ya Elimu ya Ufundi nchini Tanzania ili kusaidia kutatua tatizo la ajira kwa vijana.
Waziri Membe alisema Wizara yake ina dhamana ya kushughulikia masuala ya ushirikiano na mataifa mbalimbali duniani kwenye sekta tofauti ili kuleta maendeleo kwa Watanzania. Sekta ya Elimu ya Ufundi imepewa kipaumbele katika mahusiano hayo, ili kuwajengea vijana wengi zaidi nchini Tanzania uwezo wa kujiajiri baada ya kupata elimu ya ufundi.
Kwa kutambua hatua kubwa iliyopigwa na Canada katika sekta ya elimu ya ufundi, Waziri Membe aliiomba Serikali ya Canada kuisaidia Serikali ya Tanzania kujenga uwezo wa taasisi za elimu ya ufundi nchini Tanzania  ili kukuza ujuzi na hatimaye uwezo wa vijana kujiajiri na kuajiriwa.
Kwa upande wake, Waziri Baird alipongeza hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania katika kupiga vita umasiki na aliahidi kuwa Serikali ya Canada itakuwa tayari kuisaidia Tanzania katika Sekta ya Elimu ya Ufundi.
Pia alielezea uzoefu wa Canada kwenye sekta hiyo ambapo wahitimu wa vyuo vya Elimu ya Ufundi wamefanikiwa kupata ajira kwa urahisi zaidi kuliko wahitimu wa Elimu ya Juu.
Katika Mkutano huo mawaziri hao pia walizungumzia umuhimu wa  kudumisha uhusiano mzuri uliopo kati ya Canada na Tanzania katika nyanja mbalimbali za ushirikiano na masuala ya kimataifa. 
Mhe. Baird aliishukuru Tanzania kwa mchango wake mkubwa katika Tume ya Kimataifa inayoshughulikia masuala ya afya ya wakina mama wajawazito na watoto iliyoundwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  ikiongozwa na wenyeviti wenza Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mhe. Steven Harper, Waziri Mkuu wa Canada.
Mawaziri hao pia walijadili  masuala ya ushirikiano katika ulinzi wa amani na suala la ugaidi katika bahari ya hindi.
 

Friday, October 28, 2011

Speech - Her Majesty the Queen at the CHOGM 2011 Opening Ceremony

Rais Kikwete ahudhuria Ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Jumuiya ya Madola Leo

Jina la Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete likitangazwa kabla hajaingia ukumbuni.

Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akitembea kwenye jukwaa kuu kuelekea sehemu ya kukaa pamoja na wakuu wengine wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola.

Wanakwaya wa kikundi cha wanafunzi wakiimba wimbo wa Taifa wa Australia kabla ya ufungunguzi kuanza.

Sehemu ya burudani zilizopamba shughuli nzima ya ufunguzi

Rais Kikwete (aliyeketi mstari wa katikati wa tatu kutoka kulia) akifuatilia salamu za kiasili zilizotolewa na wananchi wa Australia wenye asili ya "aborigine" kutoka Kusini Magharibi mwa nchi hii kwenye Jamii ya Wanoongar.

Burudani za asili zilipendezesha sherehe za ufunguzi huo.

Wednesday, October 26, 2011

Tanzanian President in Perth, Australia For CHOGM

Mkuu wa Jumuiya ya Watanzania waishio Mjini Perth Asimwe Kabunga akimsikiliza Rais wakati wa hafla fupi ya kumkaribisha Rais Kikwete aliyewasili Mjini Perth kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa  Jumuiya ya Madola.

By Ichikaeli Maro

President Jakaya Kikwete of Tanzania has arrived in this Western Australia capital to join leaders of the member states of the Commonwealth for the Commonwealth Heads of State and Government Meeting (CHOGM) beginning on Friday.

The president is accompanied by Minister for Foreign Affairs and International Co-operation Bernard Membe, Minister of State at the President's Office responsible for Good Governance, Mr Mathias Chikawe and Zanzibar's Minister of State at the Second Vice-President's Office Mohamed Aboud.

The official opening of the summit on Friday is expected to be attended by 54 Heads of State and Government of Commonwealth members. Queen Elizabeth II, as the Head of the Commonwealth, will officially open the biennial summit.

Security has been intensified in Perth with major streets closed to traffic as delegates arrive here for the summit.

The Commonwealth Heads of Government Meeting takes place every two years to discuss issues pertaining to the Member States of the Commonwealth and agree on collective policies and initiatives.

The theme for this year's summit is 'Building national resilience, building global resilience at a time of global economic and political challenges". Among the issues to be discussed are international peace and security, democracy, good governance, sustainable development, debt management, education, the environment, gender equality, health, human rights, information and communication technology (ICT), law, multilateral trade issues, and small states and youth affairs.

The Commonwealth objectives are outlined in the 1971 Singapore Declaration which committed the Commonwealth to institute world peace, promoting representative democracy, individual liberty and free trade, pursuing equality and opposing racism as well as fighting poverty, ignorance and disease.

Further objectives are included in the 1979 Lusaka (Zambia) Declaration opposing discrimination on the basis of gender and the Langkawi (Malaysia) Declaration of 1989 emphasising environmental sustainability.

According to a programme issued here Tuesday by the CHOGM Organizing Committee, pre-summit activities have been taking place since Monday. They include the Commonwealth Business Forum in which participants will have opportunity to sign new business deals, make contacts and networking.

Other activities of the day included meetings of the Commonwealth and Small States Foreign Ministers, Commonwealth and Small Developing States Foreign Ministers.

Viongozi Jumuiya ya Madola Wapewa Changamoto

Na Anna Nkinda – Perth, Australia
Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuia ya Madola wameombwa kuchukua hatua na kuwasaidia mamilioni ya wasichana wanaoozwa kilazima huku wakiwa na umri mdogo na hivyo kukosa haki zao za msingi.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya Habari vilivyohudhuria maandalizi ya mkutano wa Viongozi wa Nchi wanachama wa Jumuia ya Madola (CHOGM) unaotarajia kuanza tarehe 28 hadi 30 mjini Perth nchini Australia inasema kuwa hivi sasa kuna mamilioni ya wasichana wananyanyasika kijinsia kutokana na ndoa za utotoni.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa leo na Plan International na Royal Commonwealth Society inasema kuwa ndoa za lazima na za utotoni ni moja ya vikwazo vikubwa kwa wasichana katika elimu, afya ya uzazi, na uchumi wa mwanamke hivyo basi kuna ulazima kwa jumuia ya madola kuchukua hatua zaidi ili kuzuia wasichana wasilazimishwe kuolewa wakiwa bado au wakiwa tayari kuolewa.
“Jumuia ya madola inatetea haki za binadamu na kaulimbiu yake ya mwaka 2011 ni “Wanawake ni wakala wa mabadiliko” hivyo basi viongozi wa Jumuia hiyo wafanye haraka kuhakikisha kuwa yanapatikana mabadiliko makubwa kwa wanawake na si kubaki kama walivyo”, ilisema taarifa hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Plan Internationa nchini Australia Ian Wishart alisema kuwa ndoa za lazima na za utotoni zinamuweka msichana katika umaskini, kutokuwa na afya njema na ukosefu wa elimu.
“Hivi sasa katika Dunia takwimu zinaonyesha kwamba kuna wasichana milioni 10 wenye umri wa chini ya miaka 18 ambao wanaolewa kila mwaka hii inamaana kuwa kila msichana mmoja anaolewa kila baada ya sekunde tatu”, alisema Wishart.
Aliendelea kusema kuwa wasichana wanaoolewa mapema wanauzoefu wa ukatili wa kijinsia, wanadharauliwa na kulazimishwa kufanya mapenzi hii inawasababishia matatizo ya kijinsia na afya ya uzazi na zaidi wanakosa elimu na hivyo kuwa wajinga..
Wishart alisema, “Ndoa za utotoni na za kulazimishwa ni moja ya vitu vinavyozuia kufika malengo ya milinia ya kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto , upatikanaji wa elimu ya msingi kwa wote, kupunguza umaskini , usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Royal Commonwealth Society Peter Kellner alisema kuwa Jumuia ya madola iko makini kuhusiana na maendeleo ya wanawake na haki za binadamu, na ina mipango kazi ya kuhakikisha kuwa suala la ndoa za lazima na za utotoni linachukuliwa hatua za haraka na linapata ufumbuzi.
“Wanachama wote wa Jumuia ya Madola wamekubaliana kulinda haki za watoto na wanawake kwani nchi 12 kati ya 20 ambazo zilikuwa na kiwango kikubwa cha ndoa za lazima na za utotoni ni nchi za Jumuia ya madola”, alisema Kellner.
Mwenyekiti huyo aliendelea kusema kuwa mamilioni ya wasichana kila mwaka kupitia Jumuia ya madola wanapata nafasi ya kuondokana na matokeo ya ndoa za lazima na za utotoni hii si kwao tu bali katika familia zao, jamaa zao na jumuia ya madola.
Jumla ya viongozi wa nchi 53 ambao ni wanachama wa Jumuia ya Madola wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo ambao utafunguliwa na Malkia Elizabeth wa pili akiwemo Rais Jakaya Mrisho Kikwete .
Serikali nchini Tanzania kupitia wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto ,Taasisi mbalimbali za Kiserikali na zisizo za Kiserikali zinafanyakazi ya kuelimisha jamii ili kuhakikisha kuwa tatizo la ndoa za lazima na za utotoni linamalizika.
Mwisho.

Mhe. Rais na Mama Kikwete wakutana na Jumuiya ya Watanzania waishio Perth Australia Leo



Rais Kikwete akihutubia Watanzania wanaoishi Perth Australia kwenye hafla fupi waliyomuandalia leo tarahe 26-10-2011





Rais Kikwete akipokea zawadi kutoka kwa Mwekahazina wa Jumuiya Maryam Powell iliyotolewa na Watanzania hao kwa Rais kama ishara ya kumbukumbu ya mkutano huo. Walimshukuru Rais Kikwete kwa kuwatembelea na kuahidi kuleta fursa mbalimbali haswa za uwekezaji ili kuendeleza uchumi.




Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bwana John Haule akisalimiana na Mahir Meghji, Mtanzania anayeishi Perth Australia. Ujumbe wa Watanzania uko Mjini Perth kuhudhuria mkutano wa Jumuiya ya Madola.

Balozi wa Tanzania Nchini Japan na Australia Mhe. Salome Sijaona akisalimiana na mwakilishi wa Jumuiya ya Watanzania waishio Australia.

Katibu wa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi Perth Australia Pendo Mwaiteleke (wa pili kulia) akiwakaribisha wageni kumsikiliza Rais Kikwete kwenye hafla fupi iliyoandaliwa na Jumuiya hiyo leo Mjini Perth Australia.

Baadhi ya Wabunge na Waziri walioongozana na msafara wa Mhe. Rais Kikwete kuhudhuria mkutano wa Jumuiya ya Madola

Baadhi ya Watanzania na marafiki wa Tanzania waliohudhuria hafla hiyo.

Wana habari walioongozana na msafara wa Rais Kikwete Anna Nkinda (maelezo) na Jaffar Haniu (TBC) nao hawakuwa nyuma kuhakikisha wanapata matukio yote muhimu ya hafla hiyo.

Mama Salma Kikwete akiwa na baadhi ya Watanzania waliohudhuria hafla hiyo.

















Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwa na Wanajumuiya kwenye picha ya pamoja na viongozi wao