Monday, September 30, 2013

Waziri Membe akutana kwa mazungumzo na Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania, New York


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Mhe. Tuvako Manongi, Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa mjini New York alipofika Ofisini kwake kabla ya kukutana na Wafanyakazi wa Ubalozi huo.


Mhe. Membe akizungumza na Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Mjini New York (hawapo pichani) alipokuwa mjini humo kuhudhuria Kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Mhe. Balozi Manongi akimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) alipozungumza nao. Kulia kwa Balozi ni Bi. Rose Mkapa, Kaimu Mkuu wa Utawala Ubalozi akifuatiwa na Bw. Justine Kisoka na Bi. Ellen Maduhu, Maafisa katika Ubalozi huo.

Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy  wa kwanza kushoto akimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) alipozungumza na Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania, New York. Kushoto kwa Balozi Mushy ni Dkt. Justin Seruhere akifuatiwa na Bi. Maura Mwingira na Bw. Noel Kaganda Maafisa katika Ubalozi huo.

Bw. Yusuph Tugutu (kulia), Mhasibu wa Ubalozi akimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani)akifuatiwa na Bw. Togolani Mavura, Msaidizi wa Mhe. Waziri, Bw. Grayson Ishengoma, Afisa Mambo ya Nje kutoka Wizarani na Bi. Tully Mwaipopo, Afisa katika Ubalozi.
 

Mazungumzo yakiendelea.
 




Sunday, September 29, 2013

Matukio zaidi Mhe. Rais alipolihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akielekea kwenye Jukwaa la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuhutubia Kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.


Mhe. Rais Kikwete akihutubia Kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Mjini New York ambapo katika hotuba hiyo alielezea masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na nafasi ya Tanzania katika kuchangia walinzi wa Amani, Mageuzi katika Umoja wa Mataifa, Utekelezaji wa Malengo ya Milenia na pia alitoa salamu za rambirambi kwa Serikali ya Kenya kufuatia shambulio la kigaidi lililotokea tarehe 23 Septeba, 2013 mjini Nairobi.



 

Mhe. Membe akiwa na Mhe. Haroun Suleiman, Waziri wa Kazi na Utumishi wa Umma wa Zanzibar wkimsikiliza Mhe. Rais Kikwete alipolihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.



 

Mhe. Ramadhan Mwinyi, Naibu Balozi katika Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, New York akifuatilia hotuba ya Mhe. Rais kwa pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy huku Bw. Noel Kaganda, Afisa katika Ubalozi wa Tanzania, New York akisikiliza kwa makini hotuba hiyo.
 
Balozi Tuvako Manongi wa Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, New York akiteta jambo na Mhe. Membe.

Mhe. Membe akimpongeza Mhe. Rais Kikwete mara baada ya kumaliza kulihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Mama Dorcas Membe naye akifurahia mara baada ya kumpongeza Mhe. Rais Kikwete.

Balozi Manongi akimpongeza Mhe. Rais kwa hotuba nzuri.
 

Mhe. Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri, Wabung na Watendaji mbalimbali kutoka Serikalini mara baada ya kulihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
 

Mhe. Rais Kikwete katika mahojiano na Bw. Joseph Msami, Mtangazaji kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa mara baada ya kulihutubia Braza Kuu la Umoja wa Mataifa.


Mhe. Membe akutana kwa mazungumzo na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Urusi na New Zealand na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Mhe.Sergei Lavrov walipokutana kwa mazungumzo  mjini New York wakati wa Kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
 
Mhe. Membe akiongozana na Mhe. Lavrov kuelekea kwenye meza ya mazungumzo.
Mhe. Membe na Mhe. Lavrov wakizungumza kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi hizi mbili.


               -------------------------------------------                    

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, Mhe. Deepak Obhrai walipokuna mjini New York kwa mazungumzo wakati wa Kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kinachoendelea mjini humo.

Mhe. Membe akimweleza jambo Mhe. Obhrai walipokutana.
 
Mhe. Membe akimsikiliza Mhe. Obhrai.

Mhe. Obhrai na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Balozi Dora Msechu katika picha ya pamoja.


----------------------------------------------
 

Mhe. Membe akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa New Zealand, Mhe. Murray McCully walipokutana mjini New York wakati wa Kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
 
Mhe. Membe akimweleza jambo Mhe. McCully.
 
Ujumbe wa New Zealand wakati wa mazungumzo.
 
Balozi Msechu wakati wa mazungumzo akiwa na Bw. Grayson Ishengoma, Afisa Mambo ya Nje.

Mazungumzo  yakiendelea
 

Mhe. Membe akiagana na Mhe. McCully walipomaliza mazungumzo yao.

Saturday, September 28, 2013

Video of President Kikwete's Statement at the 68th Session of the UN General Assembly Debate


H.E. President Jakaya Mrisho Kikwete as he delivers his Statement on September 27, 2013.   

    
H.E. President Jakaya Mrisho Kikwete while addressing the 68th Session of the United Nations General Assembly Debate (video by UN file)


Thank you for visiting our blog,

posted by the Government Communication Unit in the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation.


Friday, September 27, 2013

President Kikwete's Statement at the 68th Session of the UN General Assembly Debate


Please access the below Statement by H.E. President Jakaya Mrisho Kikwete, delivered at the United Nations General Assembly Debate:








Thank you for visiting our blog,

posted by the Government Communication Unit in the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation 



LIVE - UN General Assembly debate


Watch 'LIVE' feed of the United Nations General Assembly Debate in New York, USA


Click the video to watch LIVE feed 



Thank you for visiting our blog.  

Posted by the Government Communication Unit, Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation.


The debate will resume on Monday, 30 September 2013, at 9:00 a.m. (New York time, GMT-4).


PLEASE NOTE:  H.E. President Jakaya Mrisho Kikwete has already delivered his Statement on September 27, 2013.


Waziri Membe ashiriki Mkutano wa 12 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Madola


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akiwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Mhe. Kamalesh Sharma  mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa 12 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Madola uliofanyika tarehe 26 Septemba, 2013 Mjini New York sambamba na Kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ili kujadili masuala muhimu kuhusu jumuiya hiyo.

Mhe. Membe na Mhe. Sharma wakifurahia jambo.

Mhe. Membe akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Peter Kalaghe wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Afisa Mwandamizi katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa jumuiya hiyo .

Mhe. Membe akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sri Lanka, Mhe. G.L. Peiris kuhusu maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) unaoandaliwa na nchi hiyo na kufanyika mwezi Novemba, 2013

 Mhe. Peiris akimpatia maelekezo Afisa wake huku Mhe. Membe akisikiliza.


Mhe. Membe akiteta jambo na Balozi Adonia Ayebare ambaye ni mmoja wa Wajumbe wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola

Mhe. Membe akiongozana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ghana, Mhe. Hannah Tetteh mara baada ya kuhudhuria Mkutano wa 12 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Madola.
 
----------------------------------------

 MKUTANO WA 12 WA MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE WA JUMUIYA YA MADOLAWAFANYIKA MJINI NEW YORK.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe ameshiriki Mkutano wa 12 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola uliofanyika Mjini New York sambamba na Kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kujadili masuala mbalimbali muhimu kuhusu Jumuiya hiyo.

Wakati wa Mkutano huo, Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Mhe. Kamalesh Sharma alitoa taarifa kwa Mawaziri kuhusu kupitishwa kwa Mpango Mkakati wa miaka minne  kuanzia mwaka 2013/2016 ulioandaliwa na Sekretarieti ya Jumuiya hiyo ili kuiwezesha kukidhi mahitaji ya nchi wananchama. Mpango Mkakati huo umezingatia masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuhakikisha nchi wanachama zinafuata utawala wa sheria, zinaimarisha demokrasia, zinaheshimu haki za binadamu pamoja na kuzingatia usawa wa kijinsia.

Katika maelezo yake, Mhe. Sharma alisema kuwa, Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola inaendeleza jitihada zake kuzisaidia nchi wanachama kuimarisha demokrasia na maendeleo endelevu ambapo pamoja na mambo mengine waangalizi katika chaguzi mbalimbali zinazofanyika katika nchi wanachama wamekuwa wakipelekwa ikiwa ni pamoja chaguzi zilizofanyika hivi karibuni katika nchi na Ghana, Maldives na Sri Lanka.

Aidha, Mawaziri hao walipata fursa pia ya kupitia utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na Jopo la Watu Mashuhuri wa Jumuiya hiyo (EPG) kuhusu mageuzi katika Jumuiya hiyo. Vile vile ilielezwa kuwa, Katika kutekeleza mapendekezo hayo, Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola imeanzisha mipango mbalimbali  ikiwa ni pamoja na kuunda Kikundi cha Wataalam kwa ajili ya kutafuta fedha  ili kuiwezesha Sekretarieti kuzisaidia nchi wanachama zilizoathiriwa na mabadiliko ya tabianchi na zile zinazoendelea.

Katika hatua nyingine, Mawaziri  hao  walipokea  taarifa kuhusu maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali (CHOGM) unaotarajiwa kufanyika mjini Colombo, nchini Sri Lanka mwezi Novemba, 2013.

Akizungumza kuhusu maandalizi ya mkutano huo wa CHOGM ambao hufanyika kila baada ya miaka miwili, Waziri wa Mambo ya Nje wa Sri Lanka, Mhe. G.L. Peiris alisema kuwa, nchi yake imekamilisha maandalizi yote muhimu kwa ajili ya mkutano huo na kuwahakikishia Mawaziri hao kuwa hali nchini kwake ni ya amani na usalama tofauti na taarifa zinazotolewa na baadhi ya nchi kuwa hali si shwari nchini humo.

Tanzania ni miongoni mwa nchi wanachama 54 wa Jumuiya ya Madola ambayo Kiongozi wake Mkuu ni Malkia Elizabeth II wa Uingereza.

-Mwisho-
 
 
 
 

Thursday, September 26, 2013

Konseli Mkuu wa China awasilisha Hati za Uwakilishi


Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akimkaribisha Bw. Xie Yunliang, Konseli Mkuu (Consul General) wa Jamhuri ya Watu wa China kule Zanzibar. 

Mhe. Maalim akisoma Hati za Uwakilishi wa Konseli (Exequatur) baada Konseli Mkuu Xie Yunliang kuziwasilisha.

Konseli Mkuu XieYunliang akiongea na Mhe. Naibu Waziri Maalim.

Kikao kikiendelea.


Picha na Reginald Phillip

Ujumbe kutoka Japan watembelea Wizara ya Mambo ya Nje


Balozi Mbelwa Kairuki (kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia akielezea maendeleo ya miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Serikali ya Japan.  Balozi Kairuki alikutana mapema leo na Profesa Takahashi Motoki kutoka Taasisi ya Masomo ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Kobe, nchini Japan.  Profesa Motoki na Ujumbe wake hupo nchini kutathmini malengo ya misaada inayotolewa na Serikali ya Japan kwa Tanzania. 

Mkutano ukiendelea.

Profesa Takahashi Motoki (kushoto) akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo hayo.  

Balozi Kairuki (watatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Wataalamu kutoka Japan, ikiongozwa na Profesa Takahashi Motoki kutoka Taasisi ya Masomo ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Kobe, nchini Japan.


Picha na Reginald Phillip


Wednesday, September 25, 2013

Waziri Membe akutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kosovo

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kosovo, Mhe. Enver Hoxhaj walipokutana Mjini New York kwa mazungumzo kuhusu ushirikiano baina ya nchi hizi mbili.
Mhe. Membe akizungumza na Mhe. Hoxhai.
Ujumbe wa Tanzania uliofuatana na Mhe. Membe wakati wa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kosovo. Kulia ni Grayson Ishengoma, Afisa Mambo ya Nje, Bi. Tully Mwaipopo, Afisa katika Ubalozi wa Tanzania, New York na Bw. Tolani Mavura, Msaidizi wa Waziri.
Mhe. Hoxhaj akizungumza na Mhe. mhe. Membe ambapo aliishukuru Tanzania kwa kuitambua nchi yake na kuomba ushirikiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili uimarishwe.
Mazungumzo yakiendelea.
Mhe. Membe akiagana na Mhe. Hoxhaj mara baada ya mazungumzo.