Wednesday, July 16, 2014

Membe awa mgeni rasmi siku ya Taifa ya Ufaransa

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza katika hafla ya kusheherekea siku ya Taifa la Ufaransa. Halfa iliyofanyikia katika makazi ya Balozi wa taifa hilo nchini, Mhe. Marcel Escure Jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kulia ni Mkuu wa Mabalozi ambaye pia ni Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mhe. Juma Alfani Mpango. 
Mhe. Membe akizungumza wakati wa hafla hiyo huku wageni waalikwa wakimsikiliza.


Picha na Reginald Philip

Waziri Membe azungumza na wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha St. Thomas cha Marekani

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na kiongozi wa wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha St. Thomas, Fr. Jean-Piere Bongilo kilichopo  Minessota nchini Marekani waliofika Wizarani kumsalimia. Chuo cha St. Thomas kilimtunuku Shahada ya Uzamivu wa Heshima, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mwaka 2006.
Baadhi ya Wanafunzi hao wakimsikiliza Mhe. Membe alipozungumza nao.
Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatifa, Balozi Joseph Sokoine (wa kwanza kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga (wa pili kushoto) na baadhi ya wanafunzi hao.
Mhe. Membe akiendelea na mazungumzo na wanafunzi hao.
Picha na Reginald Philip


Monday, July 14, 2014

Waziri Membe azungumza na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa hapa nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe (Mb.)  akizungumza na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa hapa nchini kuhusu masuala mbalimbali ya nchi ikiwa ni pamoja na  nia ya kikundi cha uasi cha FDLR ya kuweka silaha chini na ziara ya Mabalozi na Wawakilishi hao Butiama. Wengine katika picha ni  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.),  kulia kwa Waziri Membe,  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje Bw. John Haule (wa kwanza kulia),   Mkuu wa Mabalozi na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) , Mhe.  Juma Alfani Mpango (wa pili kulia) na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Rajabu Gamaha (wa kwanza kushoto) . Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Mabalozi wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani)
Sehemu nyingine ya Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa nchini wakimsikiliza Mhe. Membe.
Sehemu ya Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakiwa katika kikao kati ya Mabalozi wa Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa nchini.
Baadhi ya Wakurugenzi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa  na Balozi wa Sudan hapa nchini (kulia) wakifuatilia maelezo ya Mhe. Membe (hayupo pichani)
Mabalozi, Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa hapa nchini pamoja na Wakurugenzi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani)


Waziri Membe akisalimiana na Mwakilishi wa Papa Bennedict XVI hapa nchini, Balozi Francisco Montecillo Padilla mara baada ya kumaliza kikao.
Mhe. Membe akisalimiana na Balozi wa Zambia hapa nchini, Mhe. Judith Kangoma Kapijimpanga.
Mhe. Membe akitoa taarifa kwa  Waandishi wa Habari kuhusu mazungumzo kati yake na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa hapa nchini.
Sehemu ya Waandishi wa Habari wakiwa kazini
Mhe. Membe akiendelea kutoa taarifa kwa Waandishi wa Habari
Meza kuu wakimsikiliza Mhe. Membe (Picha na Reginald Philip)
--------------------------------------------------------------------

Hon. Membe urges international support to dissolve FDLR

The Minister for Foreign Affairs and International Co-operation, Hon. Bernard Membe, has urged the international community to support implementation of the Angola Declaration on the dissolution of the Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (FDLR).

The declaration to dissolve the largest remaining negative forces in the Democratic Republic of Congo (DRC) was adopted by a SADC/Great Lakes Region Ministerial meeting held in Luanda, Angola on July 2, 2014. Tanzania is a member of the SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security Cooperation.

Hon. Membe told diplomats accredited to Tanzania in Dar es Salaam today, that the Angola declaration was prompted by a letter to SADC by the FDLR, offering voluntary surrender.

“As we speak, 350 soldiers of FDLR have surrendered and are cantoned in a camp near Kinshasa,” the Minister told the foreign diplomats, adding that SADC found it logical and legally correct to accept the FDLR offer of surrender.

He said the process to dissolve the negative forces would involve five stages: Disarming the soldiers; demobilizing the group; repatriating the soldiers to Rwanda, reintegrating those meriting into the national army and resettling the rest.

This process required the participation of the United Nations, DRC government, Rwanda government, which should accept repatriation, reintegration and resettlement of  FDLR troops; SADC and the international community, which would monitor implementation.

“The monitoring teams should have truly international character, and that is where your assistance is needed,” Hon. Membe told the diplomats.

He said the FDLR had been give six months from this month to comply with the dissolution plan failing which the UN combat force in DRC would be used to disable the negative force.

Hon. Membe said the acceptance of the surrender notice would not exonerate criminal elements among FDLR ranks from punishment. “If any members of the group are found to have committed crime they will be prosecuted,” he explained.

Meanwhile, Hon. Membe has expressed Tanzania’s disapproval of ongoing killing of civilians by Israeli air strikes in Gaza, which have so far claimed over 170 lives.

Addressing a press conference after the meeting with diplomats, the Minister called on Israel and Hamas to ceasefire immediately, adding that The United Nations Security Council should step in to restore harmony in the Middle East.

In another development, Hon. Membe announced that his Ministry was organizing a “World in Butiama” expedition in October, this year, which would take foreign diplomats accredited to Tanzania to the burial site of The Father of the Nation, Mwalimu Nyerere, to pay homage.


-Ends-


PRESS RELEASE

 H.E. Francois Hollande

PRESS RELEASE

H.E. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a congratulatory message to His Excellency Francois Hollande, President of France on the occasion his country’s National Day on 14th July, 2014.

The message reads as follows;

        “His Excellency Francois Hollande,
President of France,
Paris,

FRANCE.


Your Excellency,

On behalf of the government and people of the United Republic of Tanzania and indeed on my own behalf, I wish to convey my sincere congratulations to you and through you to the Government and people of France on the occasion of your country’s National Day on 14th July, 2014.

We in Tanzania cherish the close ties of friendship, cooperation and partnership that so happily exist between our two countries. Over the years these links have increasingly strengthened to the benefit of our peoples. Together we have built bridges between our two countries in every conceivable field from education, tourism, water, sanitation, governance, regional cooperation, commerce and trade.

Please accept, your Excellency, my best wishes for your personal good health and peace and prosperity for the people of France”.

Issued by the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, Dar es Salaam
14th July, 2014
       



Friday, July 11, 2014

Katibu Mkuu azungumza na Mgombea wa Nafasi ya Jaji ICC kutoka Jamhuri ya Korea


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule akizungumza na Jaji Chang-ho Chung,  Mgombea wa Nafasi ya Jaji katika Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) kutoka Jamhuri ya Korea ambaye alimtembelea Ofisini kweke tarehe 11 Julai, 2014. Jaji Chang-ho Chung ambaye kwa sasa ni Jaji wa Kimataifa chini ya Umoja wa Mataifa katika Chemba Maalum za Mahakama nchini Cambodia ni mmoja wa Wagombea wanaowania nafasi sita za Majaji katika Mahakama ya ICC ambao uchaguzi wao utafanyika Mjini New York, Marekani mwezi Desemba 2014 wakati wa Kikao cha 13 cha Nchi Wanachama waliosaini Mkataba wa Rome ulioanzisha ICC. 
Jaji Chang-ho Chung akimweleza jambo Katibu Mkuu.
Jaji Chang-ho Chung akizungumza huku akisikilizwa na   Katibu Mkuu na wajumbe wengine akiwemo Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju (wa kwanza kulia) 
Jaji Chang-ho Chung akisaini Kitabu cha Wageni huku Bw. Haule akishuhudia.
Balozi Kasyanju na Afisa kutoka katika Kitengo cha Sheria, Bw. Abdallah Mtibora wakiwa kwenye kikao cha Jaji Chang-ho Chung na Katibu Mkuu Haule (hawapo pichani).

Picha na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali.

Thursday, July 10, 2014

Mhe. Membe akutana na Mgombea Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya FRELIMO

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb.) akisalimiana  kwa furaha mgombea Urais kwa tiketi ya  Chama cha Ukombozi cha  FRELIMO cha  nchini Msumbiji, Bw. Filipe Nyusi ambaye ametembelea nchini kwa lengo la kutafuta kura kwa wananchi wa Msumbiji wanaoishi Tanzania kufuatia kampeni za urais zinazoendelea nchini kwake . Waziri Membe alimwandalia chakula cha jioni katika Hoteli ya Hyatt Regency.
Mhe. Nyusi akisalimiana na Mbunge na Mfanyabiashara maarufu nchini, Mhe. Mohammed Dewji.
Mhe. Filipe Nyusi akisalimiana na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Marcel Escure
Waziri Membe akisalimiana na mtoto wa Rais wa Kwanza wa Msumbiji, Samora Machel, Samora Samora ambaye aliambatana na mgombea huyo wa Urais.
Waziri Membe akimkaribisha Mhe. Filipe Nyusi na Ujumbe wake (hawapo pichani) katika Chakula cha jioni kilichoandaliwa katika Hoteli ya Hyatty Regency Jijini Dar es Salaam
Mhe. Nyusi pamoja na wageni waalikwa wengine akiwemo Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Mhe. Shamim Nyanduga (kushoto) na Balozi wa Msumbiji nchini (wa tatu kushoto)  wakimsikiliza Waziri Membe (hayupo pichani)
Mhe. Filipe Nyusi akitoa neno la shukrani kwa Mhe. Membe (hayupo pichani)
Mkurugenzi wa Idara ya Afrika, Balozi Vincent Kibwana  (kulia) na  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga pamoja na wageni wengine waalikwa wakimsikiliza Mhe. Filipe Nyusi (hayupo pichani)


Picha na Reginald Philip




Mhe. Membe akutana na Msajili wa Mahakama ya Kimataifa iliyorithi shughuli za ICTR



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Bw. John Hocking ambaye ni Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Msajili wa Mahakama ya Kimataifa iliyorithi shughuli za iliyokuwa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR). Bw. Hocking alitembelea Wizarani tarehe 10 Julai, 2014 kwa ajili ya kujadiliana na Mhe. Membe masuala mbalimbali ikiwemo mpango wa kuanza ujenzi wa Makao Makuu ya Mahakama hiyo katika eneo la Lakilaki Jijini Arusha.
Maafisa waliofutana na Bw. Hocking wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani)
Bw. Hocking nae akizungumza huku Mhe. Membe akimsikiliza.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Balozi Irene Kasyanju pamoja na Bw. Abdallah Mtibora wakimsikikliza Bw. Hocking (hayupo pichani).
Bw. Hocking akimuonesha Mhe. Membe Ramani ya Jengo la Makao Makuu ya Mahakama hiyo itakayojengwa katika eneo la Lakilaki Jijini Arusha.
Mhe. Membe akimweleza jambo Bw. Hocking mara baada ya mazungumzo yao
Bw. Hocking akiagana na Balozi Kasyanju mara baada ya mazungumzo yake na Mhe. Membe.

Picha na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali



Kipindi maalumu cha Wizara ya Mambo ya Nje katika maonesho ya sabasaba - Sehemu Kwanza



Kipindi maalumu cha Wizara ya Mambo ya Nje katika maonesho ya sabasaba - Sehemu ya Pili



Mhe. Membe, Mhe. Sommonds na Mhe. Nyalandu wazungumza na Waandishi wa Habari kuhusu ushirikiano kati ya Uingereza na Tanzania



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza wakati wa Mkutano wa pamoja kati yake Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. Mark Simmonds (waliokaa kushoto), Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb.) (waliokaa katikati)  na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) uliofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Julai, 2014. Wakati wa Mkutano huo Mawaziri hao waliwaeleza waandishi wa habari masuala mbalimbali ya ushirikiano  kati ya Tanzania na Uingereza ikiwemo Vita dhidi ya Ujangili wa Wanyamapori hususan Tembo na Faru na  namna ya kukomesha biashara ya meno ya tembo duniani, Uingereza kuendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta za Kilimo, Mafuta na Gesi, Nishati endelevu na kutengeneza mazingira mazuri ya biashara. Bw. Simmonds alifanya ziara ya siku mbili nchini kuanzia tarehe 8 hadi 9 Julai, 2014.
Mhe. Simmonds nae akiongea wakati wa mkutano huo na Waandishi wa Habari juu ya ziara yake 


Waziri Nyalandu akizungumza na waandishi wa

Sehemu ya Waandishi wa Habari wakisikiliza maelezo kutoka kwa Mawaziri (hawapo pichani)

Baadhi ya Wawakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa  na Ubalozi wa Uingereza akiwemo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Wizarani, Bi. Mindi Kasiga (wa kwanza kulia) wakiwasikiliza Mawaziri (hawapo pichani)
Mmoja wa Waandishi wa Habari kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Ufaransa akiuliza swali kwa Waheshimiwa Mawaziri.
Mhe. Simmonds akijibu swali .
Waziri Membe akisisitiza jambo

Picha na Reginald Philip.


Mhe. Membe na Mhe. Simmonds wazungumzia kuimarisha ushirikiano

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.)  akisalimiana na Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya  Afrika, Mhe. Mark Simmonds kabla ya kuanza kikao kuhusu ushirikiano kati ya Tanzania na Uingereza kilichofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency (Kilimanjaro) tarehe 09 Julai, 2014. Mhe. Siimmonds alifanya ziara ya siku mbili nchini kwa lengo la kukuza na kuimarisha ushirikiano.
Mhe. Membe (kulia) na ujumbe wake pamoja na Mhe. Simmonds (kushoto) na ujumbe wake wakati wa mazungumzo kuhusu ushirikiano kati ya nchi hizi mbili.
Mhe. Membe ( katikati) na Mhe. Simmonds (wa nne kutoka kushoto) katika picha ya pamoja  na Mabalozi na baadhi ya Watendaji katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kushoto kwa Mhe. Simmonds ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Peter Kalaghe na kulia kwa Mhe. Membe ni Balozi Diana Melrose, Balozi wa Uingereza nchini. Wengine ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Balozi Joseph Sokoine (wa tatu  kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga (wa pili kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Japhet Mwaisupule (kushoto), Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Ulaya na Amerika, Bibi Victoria Mwakasege (wa pili kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Bw. Innocent Shiyo (kulia).