Friday, October 3, 2014

Mkutano wa DICOTA wafunguliwa rasmi mjini Durham

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akifungua rasmi Mkutano wa Tano wa Mwaka wa Baraza la Watanzania waishio Marekani (DICOTA 2014) Mkutano huo wa siku tatu unafanyika katika Hoteli ya Millenium mjini Durham, North Carolina. Washiriki kwenye mkutano huo ni pamoja na Watanzania kutoka Majimbo mbalimbali ya Marekani, Wajumbe kutoka Serikalini na Sekta Binafsi na Serikali ya Marekani. Katika hotuba yake ya ufunguzi Balozi Sefue alilipongeza Baraza la DICOTA kwa juhudi na mafanikio mbalimbali na pia alisema Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi hizo.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula (mwenye scarf) kwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Rosemary Jairo, Mwalimu Christopher Mwakasege na Wajumbe wengine wakimsikiliza Balozi Sefue (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa DICOTA 2014
Balozi Mulamula akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa DICOTA 2014


Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Alphayo Kidata (wa kwanza kushoto) pamoja na wajumbe wengine akiwemoo Dkt. Joe Masawe (wa kwanza kulia) kutoka Benki Kuu ya Tanzania wakimsikiliza Balozi Mulamula (hayupo pichani)
Meya wa Mji wa Durham, Mhe. William Bell akiwakaribisha Wajumbe wa Mkutano wa DCOTA 2014 mjini hapo wakati wa sherehe za ufunguzi


Meya wa Durham Mhe. Bell akimkabidhi Balozi Sefue Cheti Maalum cha kuitambua DICOTA mjini Durham.
Rais wa DICOTA, Dkt. Ndaga Mwakabuta nae akikaribisha Wajumbe kwenye ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Mwaka wa DICOTA 2014
Wajumbe kwenye mkutano wakifuatilia matukio
Sehemu nyingine ya Wajumbe kwenye mkutano
Wajumbe wengine akiwemo Bi. Susan Mzee kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia hafla ya ufunguzi
Wajumbe mbalimbali kwenye ufunguzi wa mkutano

Mkutano ukiendelea na wajumbe wakifuatilia
Sehemu ya Wajumbe wakijadiliana jambo
Wajumbe zaidi kutoka Tanzania wakifuatilia hafla ya ufunguzi
Balozi Sefue akishangiliwa na kina mama wa DICOTA waliokuwa wamevalia sare kumkaribisha kufungua mkutano wa DICOTA 2014
Balozi Sefue akizungumza na Meya wa Durham, Mhe. Bell
Kina mama wa DICOTA wakati wa shamrashamra za ufunguzi wa mkutano
Balozi Sefue, Balozi Mulamula, Mama Jairo, Mwalimu Mwakasege na Wajumbe wengine wakifurahia nyimbo kutoka kwa kina Mama wa DICOTA kabla hala ya ufunguzi haijaanza.
Kijana wa DICOTA, John Mmanywa akiimba kwa ufasaha kabisa Wimbo wa Taifa la Tanzania.

 ----------Matukio kabla ya ufunguzi wa Baraza la DICOTA

Balozi Sefue akipata maelezo kutoka kwa Mjumbe kutoka Benki ya CRDB kuhusu huduma yao ya Tanzanite Account maalum kwa Diaspora. Kulia ni Dkt. Sweetbert Mkama kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Balozi Sefue akiendelea kupata maelezo katika meza za maonesho ya bidhaa mbalimbali kwa ajili ya Diaspora na nchi
Balozi Mulamula akisalimiana na Mwalimu Mwakasege huku Balozi Sefue akishuhudia.
Balozi Sefue katika picha ya pamoja na Mwalimu Mwakasege
Balozi Mulamula katika picha ya pamoja na Bibi Jairo

Zimbabwe yamzawadia Dola za Marekani 100,000.00 Brig. Jen. Hashim Mbita

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe Bernard K. Membe (Mb) (katikati) akikabidhi hundi yenye thamani ya Dola za Marekani laki moja kwa mtoto wa Brigedia Jen. Mstaafu Hashim Mbita, Bibi Shella Mbita. Bibi Mbita alipokea zawadi hiyo kwa niaba ya Baba yake ambayo imetolewa na Rais wa Zimbabwe, Mhe. Robert Mugabe kutokana mchango mkubwa alioutoa Brig. Jen. Mbita katika harakati za ukombozi Kuisini mwa Afrika. Mwingine katika picha ni Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Mhe. Edzai Chimonyo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Tuzo iliyotolewa na Rais Mugabe kwa Brig. Jen. Hashim Mbita wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa SADC uliofanyika Victoria Falls nchini Zimbabwe mwezi Agosti 2014. Waziri Membe alieleza kuwa Rais Mugabe alitoa Tuzo ya Munhumutapa kwa Brig. Jen Hashim Mbita kutokana na mchango wake mkubwa katika harakati za kutafuta uhuru Kusini mwa Afrika. Brig. Jen. Mbita anakuwa mtu wa kwanza sio Mkuu wa Nchi kutunukiwa Tuzo hiyo ambayo kwa kawaida hutukiwa Wakuu wa Nchi pekee. Wengine katika picha ni Balozi wa Zimbawe nchini Tanzania na binti yake Brig. Jen. Mbita, Bibi Shella. 
Bibi Shella akitoa neno la shukrani kwa Serikali ya Zimbabwe kutokana na zawadi ya Dola 100,000.00 kwa Baba yake mzazi
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Shiyo Innocent (tai nyekundu) na Afisa wa Ubalozi wa Zimbabwe nchini Tanzania wakifuatilia kwa makini mkutano wa waandishi wa habari
Waandishi wa habari wakiwa kazini.



Picha na Reginald Philip

Balozi Mbelwa kairuki afanya mazungumzo na Balozi wa China nchini

Mkurugenzi Idara ya Asia na Australasia Balozi Mbelwa Kairuki (Kulia) kulia akimsikiliza Balozi wa China nchini Lu Youqing alipokutana nae na kufanya mazungumzo juu ya mahusiano juu kati ya Tanzania na China
Wakwanza kutoka kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Mambo ya Nje Bi. Mindi Kasiga, wakwanza kulia ni Bw. Imani Njalikai afisa Mambo ya Nje na wapili kutoka kulia ni Bw. Medadi Ngaiza afisa Mambo ya Nje wakinukuu mazungumzo hayo.
Maafisa kutoka Ubalozi wa China nchini walioambatana na Balozi Lu Youqing
Mazungumzo yakiendelea.


Picha na Reginald Philip

Taarifa kwa vyombo vya Habari




TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Bwana Samwel William Shelukindo  kuwa Balozi na pia kuwa Msaidizi wa Rais (Diplomasia).

Kabla ya uteuzi huu, Bwana Samwel William Shelukindo alikuwa Mkuu wa Utawala kwenye Ubalozi wa Tanzania Mjini Addis Ababa Ethiopia.

Uteuzi huu unaanza tarehe 01 Oktoba, 2014.

“Mwisho”

Imetolewa na;

Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu – Dar es Salaam.
02 Oktoba, 2014

Balozi Sefue kufungua rasmi Mkutano wa Baraza la DICOTA

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula  na Viongozi wa Baraza la Watanzania waishio Marekani (DICOTA) (hawapo pichani) mara baada ya kukutana nao Hotelini kwake kwa ajili ya kupata taarifa za maandalizi ya Mkutano wa Mwaka wa Baraza hilo atakaoufungua leo tarehe 03 Oktoba, 2014 mjini Durham, North Carolina.

Balozi Mulamula, Viongozi wa DICOTA pamoja na Maafisa kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani wakimsikiliza Balozi Sefue (hayupo pichani)


Mkutano wa Tano wa Baraza la Watanzania waishio Marekani (DICOTA 2014) kuanza rasmi mjini Durham
============================================

Na Mwandishi Wetu, Durham

Mkutano wa Tano wa Mwaka wa Baraza la Watanzania waishio Marekani (DICOTA 2014) utafunguliwa rasmi na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue tarehe 03 Oktoba, 2014 mjini Durham nchini Marekani.

Kaulimbiu ya mkutano wa mwaka huu ni “Kuwawezesha Watanzania waishio ughaibuni (Diasporas) kufikia Mabadiliko ya Kiuchumi na Kijamii Kule Waliko  na Nyumbani”.

Mkutano huu ambao utahudhuriwa na Watanzania kutoka Majimbo yote ya Marekani, Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Kimarekani, unalenga kuwakutanisha wadau hao na wajumbe kutoka Serikalini, Taasisi za Umma na Sekta Binafsi ili kubadilishana mawazo na uzoefu na kuangalia namna bora ya kutumia fursa na rasilimali zilizopo katika kukuza uchumi na kupata maendeleo endelevu ya Jumuiya hiyo ya Diaspora na Taifa kwa ujumla.

Wakati wa Mkutano huu mada mbalimbali za ueleimishaji zitatolewa  kwa lengo la kueleza kwa kina fursa mbalimbali za uwekezaji, biashara na utalii zilizopo nchini. Mada hizo ni pamoja na Uhamiaji na Uraia, Mchakato wa Katiba mpya, Vitambulisho vya Uraia kwa Dispora, Mifuko ya Hifadhi za Jamii na Pensheni, masuala ya Ardhi na Nyumba, umuhimu wa Bandari ya Dar es Salaam kwa Diaspora, Usajili wa Makampuni na upatikanaji wa Leseni za Biashara kwa Diaspora, masuala ya Kodi, Masoko ya Mitaji na Hisa, masuala ya Nishati ya Mafuta na Gesi, Bima, Uwekezaji katika Kilimo na mada kuhusu Uchumi na Fedha zinazotumwa kutoka nje na Diaspora (Remittances).
Baraza la DICOTA lilianzishwa rasmi mwaka 2008 na kikundi cha watu 30 wakiwa na lengo la kushirikiana na Serikali na Sekta Binafsi katika kuleta maendeleo endelevu kwa kutumia ujuzi, elimu, maarifa na mitaji waliyoipata wakiwa ughaibuni. Baraza hilo linaongozwa na Dkt. Ndaga Mwakabuta na Katibu wake ni Bi. Lyungai Mbilinyi.

Mkutano wa kwanza wa DICOTA ulifanyika mwaka 2009 mjini Houston, Texas ukifuatiwa na ule wa mwaka 2010 uliofanyika mjini Minneapolis, Minnesota. Mkutano wa Tatu ulifanyika mwaka 2011 mjini Dulles, Virginia ukifuatiwa na mkutano wa mwaka 2012 uliofanyika Chicago, Illinois.

Mbali na Balozi Sefue, Viongozi Waandamizi wengine kutoka Serikalini wanaohudhuria mkutano huu ni pamoja na Mhe. Liberata Mulamula, Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Bw. Alphayo Kidata, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bibi Rosemary Jairo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Bi. Susan Mzee, Mshauri wa masula ya Diaspora kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu.

-mwisho-

Thursday, October 2, 2014

Balozi mpya wa Ufaransa awasilisha nakala za Hati za Utambulisho

Balozi mpya wa Ufaransa nchini Tanzania Mhe. Malika Berak akiwasilisha Nakala za Utambulisho kwa Mkuu wa Itifaki Balozi Juma Maharage  
Mhe. Beraki akiweka saini katika kitabu cha wageni
Balozi Malika Berak akizungumza na Balozi Maharage mara baada ya kuwasilsha nakala za Hati za Utambulisho
Kushoto ni mkurugenzi msaidizi Idara ya Itifaki Bw. James Bwana, kulia ni Afisa Mambo ya Nje Bi. Mona Mahecha wakifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Balozi Malika Berak na Balozi Maharage

Picha na Reginald Philip

PRESS RELEASE


  
  

PRESS RELEASE

H.E. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a congratulatory message to H.E. Joachim Gauck, President of Federal Republic of Germany on the occasion of the Unity Day of Germany. The message reads as follows:-

The message reads as follows;

“H.E. Joachim Gauck,
President of the Federal Republic of Germany,
Berlin,
GERMANY.

Your Excellency,

It gives me great pleasure, on behalf of the Government and people of the United Republic of Tanzania, and indeed on my own behalf, to extend cordial congratulations to You, the Government and people of Germany on the occasion of your country’s Unity Day.

Our historical bilateral relations are multifaceted and we cooperate in many areas such as education, energy, tourism, water and sanitation. 

On this special occasion, I wish to cherish and celebrate these excellent bilateral relations that exist between our two countries. Let me also take this opportunity to assure you that the Government of Tanzania remains committed to maintaining and consolidating these relations for the mutual benefit of the people of our two countries.

Please accept, Your Excellency, my best wishes for your good health and continued peace and prosperity for the people of Germany.


Jakaya Mrisho Kikwete
PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA


Issued by the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation of the United Republic of Tanzania
2nd October, 2014


Wednesday, October 1, 2014

Mhe. Membe Aahidi Kuendeleza Diplomasia ya Michezo


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Kamiliusi Membe (Mb.) akizungumza na baadhi ya wanamichezo walioshiriki michezo ya Jumuiya ya Madola Glasgow, Scotland mwezi Agosti, alipo kutana nao na kufanya kikao cha kutathmini matokeo ya timu ya Tanzania katika kituo cha michezo cha Filbert Bayi kilichopo Kibaha Mkuza.

Wanamichezo wakimsikiliza kwa makini Waziri Membe (Hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao.
  Viongozi mbalimbali wa vyama vya michezo wakimsikiliza                   Waziri Membe (hayupo pichani).                     
Wakwanza Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mambo ya Nje, Bw.Mkumbwa Ally, na wapili kutoka kushoto ni Afisa Mambo ya Nje Bw. Imani Njalikai wakifuatilia kikao kati ya Waziri Membe na wanamichezo walio shiriki michezo ya jumuiya ya madola Glasgow, Scotland. 
                                         Kikao kikiendele
  
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb.) akisaini kwenye kitabu cha wageni alipo wasili katika kituo cha Filbert Bayi kilichopo Kibaha Mkuza. 
Katikati ni Mama Bayi akielezea jambo kwa waziri Membe (wa kwanza kulia)  mara baada ya kusaini kitabu cha wageni, wakwanza kulia ni Bw. Filbert Bayi naye akisikiliza.
Bw. Filbert Bayi akimwonyesha na kumwelezea Waziri Membe Ramani ya eneo lililo na Shule ya awali, msingi, Sekondari na kituo cha michezo cha Filbert Bayi, lililopo Kibaha Mkuza.
Waziri Membe akizungumza alipokuwa akitazama kiwanja cha mpira wa miguu (hakipo pichani), kiwanja hicho cha mpira ni moja kati ya viwanja vinavyotumiwa na wanamichezo waliopo katika kituo hicho cha Filbert Bayi.
Kiwanja cha mpira wa miguu kilichopo katika kituo cha michezo cha Filbert Bayi.
Waziri Membe akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa vyama vya michezo mbalimbali nchini, mara baada ya kumaliza kikao na wanamichezo.
Picha na Reginald Philip


          

=========================================



Mhe. Membe Aahidi  Kuendeleza Diplomasia ya Michezo

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe, amewataka wanamichezo wa Tanzania kutokata tama kwa kufanya vibaya kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola mwaka huu, na kuahidi kuendelea kupigania maendeleo ya sekta hiyo.

Akiongea katika kiko cha kutathmini matokeo ya timu ya Tanzania, ambayo haikushinda medali yoyote kwenye michezo hiyo ya Madola, iliyomalizika mjini Glasgow, Scotland mwezi Agosti, Mhe. Membe alisema wizara yake itafanya juhudi zaidi kutafuta wadhamini wa matayarisho ya timu ya taifa ndani na nje ya nchi, chini ya mkakati wa diplomasia ya michezo.

 Kikao hicho kilichohudhuriwa na viongozi wa vyama vya michezo na baadhi ya wanamichezo walioshiriki michezo ya Glasgow, kilifanyika leo kwenye kituo cha michezo cha Filbert Bayi Mkuza.

''Msikatishwe tamaa na matokeo mabaya ya Glasgow, kwani mara nyingi mafanikio huja mara ya pili,'' alisema Mhe. Membe, na kuongeza: ''Tutumie yale yuliyojifunza kwa kushindwa hukokupanga wakati wa ushindi katika mashindano yajayo.''

Mhe. Waziri aliisifu timu ya Tanzania kwa kuonyesha nidhamu ya hali ya juu iliposhiriki michezo ya Madola, lakini akasisitiza kuwa nidhamu peke yake haitoshi. ''Nidhamu hiyo ituletee ushindi.'' alisema.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, kwakushirikiana na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, ilitafuta udhamini wa kambi za mazoezi kwa miezi miwili kwa wanamichezo wa timu ya taifa huko Uturuki, China, Ethiopia, na New Zeland, kabla ya kwenda Glasgow.

Katibu Mkuu wa kamati ya Olimpiki ya Tanzania, Bw. Filbert Bayi, alisema kufanya vibaya kwa timu hiyo kulichangiwa na muda mfupi wa kukaa kambini na kukosa mashindano ya kujipima nguvu. Ali9shauri idadi ya washiriki na michezo vipunguzwe kulingana na uwezo wa taifa kifedha.

Mkurugenzi wa Michezo, ambaye aliongoza msafara wa Glasgow, Bw. Leornard Thadeo, alisema timu ya Tanzania ilikuwa na ushindani hafifu kutokana na mafunzo hafifu, viwango vya chini vya wachezaji, ukosefu wa vifaa na kuchelewa kutolewa fedha za uwezeshaji.

Walimu wa michezo na wachezaji walisisitiza matayarisho ya muda mrefu zaidi, mazingira mazuri ya mazoezi na udhamini mpana zaidi utakaohusisha taasisi za umma na binafsi.




Maafisa Wakuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa cha Afrika Kusini watembelea Wizara ya Mambo ya Nje



Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Joachim Otaru akitoa hotuba kuhusu Sera ya Mambo ya Nje ya Tanzania, nafasi ya Tanzania katika kutekeleza majukumu ya kimataifa na uwakilishi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa kwa Maafisa Wakuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa cha Afrika Kusini. Maafisa hao wapo nchini kwa ziara ya mafunzo hadi tarehe 02 Oktoba 2014. 

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Shiyo Innocent mwenye tai nyekundu akifafanua jambo kwa maafisa hao kuhusu nafasi ya Tanzania katika Jumuiya za Kikanda (SADC, EAC na ICGLR). Kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Bw. Elibariki Maleko.

Bw. Shiyo akiendelea na ufafanuzi wa masuala mbalimbali.


Bw. Maleko akitoa neno la shukrani kwa maafisa wa Chuo hicho kwa uamuzi wao wa kuitembelea Wizara ya Mambo ya Nje. 

Ujumbe kutoka Marekani wataembelea Wizara ya Mambo ya Nje



Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha (katikati) akizungumza na ujumbe wa wafanyabiashara na Mabalozi wa Heshima wa Tanzania nchini Marekani uliokuja kumtembelea Ofisini kwake. Ujumbe huo uliongozwa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya TANAS Energy Group ya Marekani, Bw. William Crawford wa kwanza kulia kwa Kaimu Katibu Mkuu upo nchini kwa madhumuni ya kuangalia fursa za uwekezaji na vivutio vya utalii. 
Ujumbe wa Marekani ukimsikiliza kwa makini Kaimu Katibu Mkuu hayupo pichani. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya TANAS Energy Group ya Marekani, Bw. William Crawford, Balozi wa Heshima wa Tanzania, California, Bw. Ahmed Issa;  Rais wa Automated Transmission Rebuilding California, Bw.  Steve Horgan; Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Seafarers inc, Bibi Deborah Owens; na  Rais na Mwanzilishi wa Shirika la Women Empowered to Achieve the Impossible (WETATI), Bibi Margret Dureke,
Ujumbe mwingine ukifuatilia mazungumzo hayo. Kutoka kulia ni Mhandisi wa Tiba, San Francisco, California, Bw. Robert Reynolds; Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Bw. Suleiman Saleh; Bw. Andy Math na Balozi wa Heshima wa Tanzania, Michigan, Bw. Robert Shumake.


Kaimu Katibu Mkuu, Balozi Gamaha akiagana na Kiongozi wa Msafara, Bw. William Crawford.

Picha ya pamoja

















TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI



Rais Kikwete ateua Balozi mpya wa Tanzania nchini Canada 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Bw. Jack Mugendi Zoka kuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Canada.

Bw. Zoka anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Alex Masinda, ambaye amestaafu kwa mujibu wa sheria.

Kabla ya uteuzi huu, Bw. Zoka alikuwa Ofisa Mwandamizi Ofisi ya Rais, Ikulu.

IMETOLEWA NA KATIBU MKUU, WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, Dar es Salaam.

Tarehe 30 Septemba 2014