Friday, March 6, 2015

Wizara ya Mambo ya Nje yajipanga kutekeleza Sera ya Elimu n Mafunzo ya Mwaka 2014

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Prof.Sifuni Mchome akiwasilisha mada kuhusu Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 kwa Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika warsha fupi iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa  Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 06 Machi, 2015.

Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya (kushoto) akiwa na Mkurugenzi Idara ya Asia na Austaralasia, Balozi Mbelwa Kairuki (katikati) na Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Sera na Mipango  Bw. Joachim Otaro wakifuatilia kwa makini warsha hiyo
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Prof. Mchome ambaye hayupo pichani wakati akiwasilisha mada kuhusu Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014
 Prof. Mchome akiendelea na mada yake
 Balozi Kairuki akichangia hoja kuhusu sera hiyo mpya ya elimu.
  Kaimu Mkureugenzi wa Idara ya Diaspora, Bibi Rosemary Jairo akiuliza swali wakati wa warsha hiyo.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,  Bi.Mindi Kasiga akitoa maoni yake kuhusu Sera ya Elimu.
Katibu wa Waziri wa Mambo ya Nje,  Bw.Thobias Makoba akiuliza swali juu ya sera mpya ya elimu
 Afisa Mambo ya Nje, Bw. Bartholomeo Jungu akitoa mchango wake kuhusu sera hiyo ya Elimu.

Picha na Ruben Mchome

================================


Wizara ya Mambo ya Nje yahamasishwa kutekeleza Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Sifuni Mchome ametoa wito kwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuishirikisha Jumuiya ya Kikanda na Kimataifa kuisaidia Tanzania katika kutekeleza Sera mpya ya Elimu  na Mafunzo ya Mwaka 2014.

Prof. Mchome aliyasema hayo wakati akiwasilisha mada kuhusu Sera mpya ya Elimu kwa Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika warsha fupi iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa  Julius Nyerere, Dar es Salaam hivi karibuni.

Prof. Mchome alisema kuwa ili kutekeleza Sera hii kikamilifu, upo umuhimu mkubwa wa kuwashirikisha wadau mbalimbali ikiwemo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambao kwa kutumia nafasi  ya ushirikiano na mataifa mbalimbali watahamasisha upatikanaji wa vifaa vya kufundishia hususan katika maabara, vitabu na wataalam wa masuala mbalimbali.

 “Lengo la kukutana nanyi leo ni kuwapatia mwelekeo wa Sera mpya ya Elimu na Mafunzo ni kwa kutambua umuhimu wa Wizara hii katika kutekeleza Sera hiyo hususan katika nyanja za kikanda na kimataifa” alisema Prof. Mchome.

Aidha, aliongeza kuwa Sera hiyo ambayo ilianza kuandaliwa mwaka 2008 imejikita katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na inalenga kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali katika sekta ya elimu nchini ikiwemo uhaba wa walimu, vifaa na ithibati ambavyo kwa kiasi fulani vimechangia kushuka kwa ubora wa elimu na mafunzo hapa nchini.
Alifafanua kuwa, Sera hiyo pia inalenga  kuangalia viwango vya elimu vya Watanzania ili viendane na  vile vya kimataifa na kikanda na pia kutoa fursa sawa kwa watoto wote nchini kupata elimu na hatimaye kupata Watanzania wachapakazi, weledi na wenye vipaji kupitia elimu bora.

“Lengo kubwa la elimu ni kupata rasilimali watu yenye weledi, ujuzi na maarifa ya hali ya juu kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu na hiyo ndiyo dhamira yetu, alisisitiza Prof. Mchome.

Akielezea masuala muhimu katika Sera hiyo, Prof. Mchome alisema kuwa kwa sasa Elimu ya Msingi itakuwa ni ya lazima na itatolewa bure kwa kipindi cha miaka 10 ikijumuisha Elimu ya Sekondari.

Pia, ufundishaji utaimarishwa hususan katika masomo ya hisabati, sayansi na teknolojia; kuhakikisha uwepo wa vifaa, nyenzo na zana muhimu za kufundishia; kuwa na kitabu kimoja cha kiada kwa kila somo na kila mwanafunzi; kuimarisha ithibati na udhibiti wa ubora wa elimu na kuimarisha mbinu za ufundishaji.

Vile vile alisema kuwa bado kuna haja ya kuhamasisha Watanzania kujiunga na elimu ya juu na vyuo vya ufundi ambapo alisema kati ya Watanzania milioni 11.5 ambao ni wanafunzi wa ngazi mbalimbali ni asilimia 1 pekee wapo elimu ya juu ikiwemo elimu ya juu.

“Hadi sasa kuna jumla ya Watanzania milioni 11.5 ambao ni wanafunzi kwa ngazi mbalimbali.  Kati yao asilimia 71 wapo katika elimu ya msingi, asilimia 15 elimu ya Sekondari, asilimia 10 vyuo ya ufundi na nyinginezo, asilimia 1 elimu ya juu na ufundi na asilimia 0.7 Elimu ya Sekondari kwa kidato cha tano na sita,” alifafanua Prof. Mchome.

Kwa mujibu wa Prof. Mchome, Tanzania imeridhia Itifaki ya SADC (1997) kuhusu elimu na mafunzo inayozitaka nchi wanachama kuwa na elimumsingi ya lazima isiyopungua miaka tisa; Itifaki ya Dakar (2000) kuhusu Elimu kwa wote; Makubalinao ya Perth chini ya UNESCO (2007) kuhusu Elimu ya Sayansi na Teknolojia na mafunzo ya ufundi.

Awali akimkaribisha Prof. Mchome kuwasilisha mada yake, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Balozi Simba Yahya alisema kuwa anayo imani kubwa na mabadiliko ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 na kwamba Wizara itashirikiana kikamilifu na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kutekeleza Sera hiyo.

Sera hiyo ilizinduliwa rasmi na Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 13 Februari, 2015.


-Mwisho-

Thursday, March 5, 2015

Waziri Membe azungumza na Balozi wa Oman nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard K. Membe (Mb.) akifanya mazungumzo na Balozi wa Oman hapa nchini, Mhe. Saoud Al Ruqaishi alimpomtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kuzungumzia masuala mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Oman.
Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya (kushoto) akiwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Bi. Mindi Kasiga (kulia) pamoja na Bi. Asha Mkuja, Afisa Mambo ya Nje.
Mazungumzo yakiendelea

Picha na Reginald Philip




Wednesday, March 4, 2015

Waziri Membe akutana kwa mazungumzo na Balozi wa China hapa nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), akizungumza na Balozi wa China nchini Mhe. Lu Youqing alipofika Wizarani kwa ajili ya mazungumzo  ya kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na China 

Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya (kushoto), akiwa na  Mkurugenzi Idara ya Asia na Australasia Balozi Mbelwa Kairuki (wa pili kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano,  Bi. Mindi Kasiga na  Afisa Mambo ya Nje, Bw. Imani Njalikai (kulia) wakifuatilia mazungumzo kati ya Waziri Membe na Mhe. Lu Youqing ambao hawapo pichani.
Balozi Lu Youqing akizungumza na Mhe. Membe
Maafisa walioambatana na Balozi Lu wakinukuu mazungumzo akiwemo Kaimu Mkuu wa masuala ya Siasa katika Ubalozi huo, Bw. Li Xhuhang (kulia).   
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Asia na Australasia, Bw. Nathaniel Kaaya (kulia)  na Katibu wa Waziri, Bw. Thobias Makoba nao wakisikiliza mazungumzo hayo.
Mazungumzo yakiendelea
WaziriMembe akiagana na Balozi Lu Youqing mara baada ya mazungumzo yao.
Picha na Reginald Philip.

Naibu Waziri akutana na mgombea uenyekiti wa IPCC na Balozi wa Comoro nchini

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akizungumza na Mgombea wa nafasi ya Uenyekiti kwenye Kundi la Wataalam chini ya Umoja wa Mataifa linaloshirikisha wadau kutoka sekta ya umma na binafsi kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi-Intergovernmental Panel on Climate Change-IPCC, Prof. Jean-Pascal Van Ypersele kutoka Ubelgiji ambaye alifika Wizarani kwa ajili ya kumsalimia Mhe. Maalim. Katika mazungumzo yao Prof. Ypersele alielezea dhamira yake ya kushirikiana na nchi zinazoendelea katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kuongeza wataalam kwenye kundi hilo pindi atakapochaguliwa kwenye nafasi hiyo.
Prof. Ypersele nae akichangia jambo wakati wa mazungumzo yao. Kushoto ni Balozi wa Ubelgiji hapa nchini, Mhe. Koenraad.
Mazungumzo yakiendelea
Balozi Adam akisaini Kitabu cha Wageni Ofisini kwa Mhe. Mahadhi
Prof. Ypersele nae akisaini Kitabu cha Wageni
Mhe. Mahadhi katika picha ya pamoja na Prof. Ypersele
Mhe. Maalim akiwa na Prof. Ypersele pamoja Balozi....na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kulia)

.....Mkutano kati ya Mhe. Mahadhi na Balozi wa Comoro hapa nchini

Mhe. Dkt. Mahadhi akimkaribisha ofisini kwake Balozi wa Comoro hapa nchini, Mhe. Dkt. Ahamada Al Badaoui Mohamed alipofika kwa ajili ya mazungumzo ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili. 
Balozi Mohamed akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na  Mhe. Dkt. Mahadhi
Mhe. Dkt. Mahadhi akifafanua jambo kwa Mhe. Dkt. Mohamed. Wengine ni Bw. Adam Issara, Katibu wa Naibu Waziri na Bi. Zuleikha Tambwe, Afisa Mambo ya Nje
Mhe. Dkt. Mahadhi akiagana na Dkt. Mohamed

Picha na Reuben Mchome

Tuesday, March 3, 2015

Waziri Membe azungumza na Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa hapa nchini



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataiafa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (hawapo pichani) waliopo hapa nchini kuhusu masuala mbalimbali yanayoendelea hapa nchini. Masuala hayo ni pamoja na hatua zinazochukuliwa na Serikali kukabiliana na mauaji ya Albino, Mkataba wa Makubaliano ya Chama cha SPLM cha Sudan Kusini na  Hali katika nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu  kama DRC. Kulia  ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.), Mkuu wa Mabalozi ambaye pia ni Balozi wa DRC hapa nchini, Mhe. Juma Khalfan Mpango na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam tarehe 03 Machi, 2015
Sehemu ya Mabalozi  na Wajumbe wengine waliohudhuria mkutano kati yao na Waziri Membe (hayupo pichani) wakifuatilia mazungumzo. Mwenye tai nyekundu ni Balozi wa Marekani hapa nchini, Mhe. Mark Childress.
Sehemu nyingine ya Mabalozi na Wawakilishi.
Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakifutilia mazungumzo  kati ya Waziri Membe na Mabalozi.
Balozi wa Finland hapa nchini, Mhe. Sinikka Antila akichangia jambo wakati wa mkutano kati ya Mabalozi na Mhe. Waziri Membe. 
Balozi wa Kenya nchini, Mhe. Chirau Mwakwere akifuatilia mkutano kati yao na Waziri Membe.
Balozi wa Cuba nchini, Mhe. Jorge Luis Lopez Tormo (kushoto) akiwa na  Balozi wa China hapa nchini, Mhe. Lu Youqing pamoja na  Balozi wa Uingereza, Mhe. Diana Melrose.
Mabalozi wakati wa mkutano
Mkutano ukiendelea huku Mabalozi wakifuatilia
Mmoja wa Mabalozi akichangia hoja wakati wa mkutano
Mkutano ukiendelea
Picha ya Pamoja

Picha na Reginald Philip