Friday, April 10, 2015

Rais Mstaafu Mkapa atoa elimu ya uchumi kwa Mabalozi, Maofisa na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje

Rais wa Awamu ya Tatu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa akitoa mada katika semina ya masuala ya diplomasia ya uchumi kwa Mabalozi, Maofisa na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (hawapo pichani). Semina hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam tarehe 9 Aprili 2015.
Mkaguzi Mkuu wa ndani Bw. Mathias Abisai (wakwanza kushoto), Mkurugenzi Idara ya Ununuzi Bw.Elias Suka (Katikati), wakiwa pamoja na Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje Bw. Paul Kabale wakati wa Semina hiyo 
Sehemu ya Watumishi wakisikiliza kwa makini elimu iliyokuwa ikitolewa na Rais Mstaafu Benjamini Mkapa.
Waziri Membe akitoa Ufafanuzi katika moja ya mambo yaliyo jadiliwa
Mkurugenzi Idara ya Asia na Australasia Balozi Mbelwa Kairuki (Kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Bi. Mindi Kasiga
Sehemu nyingine ya walioudhuria Semina Hiyo.
Balozi Mstaafu Mhe. Simon Mlay akiuliza swali meza kuu
Mkurugenzi wa Masomo wa Chuo cha Diplomasia Dkt. Watengere Kitojo akiuliza swali. 


Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Simba Yahya (mbele kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria Balozi Irene Kasyanju wakifuatilia semina hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mambo ya Nje Bi. Mindi Kasiga 
Muhadhiri kutoka Chuo cha Diplomasia Dr. Lucy Shule akiuliza swali
Rais Mstaafu Mkapa akiteta jambo na Mhe. Membe wakati wa semina hiyo ambapo alizungumzia changamoto za ushirikiano wa kiuchumi na diplomasia nchini Tanzania, na nje ya nchi na kwenye Jumuiya za Kimataifa. Andiko la mada hii litapatikana baada ya muda mfupi kwenye tovuti ya Wizara www.foreign.go.tz
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mjadala wa semina hiyo.
Rais Mstaafu Benjamini W. Mkapa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb.), na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Rajab Gamaha, kwenye Picha ya Pamoja na Watumishi Wizara ya Mambo ya Nje na Chuo cha Diplomasia 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), akimpokea Rais wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa mara baada ya kuwasili Mwalimu Nyerere kwa ajili ya semina hiyo. 

Picha na Reginald Philip

Thursday, April 9, 2015

Rais Mstaafu Mkapa atoa elimu ya uchumi kwa Mabalozi, Maofisa na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje

Rais wa Awamu ya Tatu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa akitoa mada katika semina ya masuala ya diplomasia ya uchumi kwa Mabalozi, Maofisa na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (hawapo pichani). Semina hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam tarehe 9 Aprili 2015.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), akimpokea Rais wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa mara baada ya kuwasili Mwalimu Nyerere kwa ajili ya semina hiyo. 

 ...Waheshimiwa wakielekea ukumbini.
 Rais Mstaafu Mkapa akiteta jambo na Mhe. Membe wakati wa semina hiyo ambapo alizungumzia changamoto za ushirikiano wa kiuchumi na diplomasia nchini Tanzania, na nje ya nchi na kwenye Jumuiya za Kimataifa. Andiko la mada hii litapatikana baada ya muda mfupi kwenye tovuti ya Wizara www.foreign.go.tz
 Mabalozi, Maofisa na Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje pamoja na Walimu na Wanachuo cha Diplomasia wakimsikiliza kwa makini Mhe. Benjamin W. Mkapa. 

 Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Simba Yahya (mbele kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria Balozi Irene Kasyanju wakifuatilia semina hiyo.
 Wajumbe wa semina wakimsikiliza kwa makini Balozi Mlay (Mstaafu) (mbele kushoto aliyesimama) akitoa maoni yake kuhusu mada iliyowasilishwa katika semina hiyo.
 Balozi (Mstaafu) Bertha Semi Somi akichangia katika semina hiyo.
 Mhadhiri wa Chuo cha Diplomasia Dkt. Kitojo akiuliza swali katika semina hiyo. 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma wa Wizara ya Mambo ya Nje Bi. Mindi Kasiga akiuliza swali kufuatia mada iliyotolewa na Rais Mstaafu Mhe. Mkapa katika hiyo semina hiyo.
  Baadhi ya washiriki wakifuatilia mjadala wa semina hiyo.
Rais Mstaafu Benjamin W. Mkapa (katikati), Waziri wa Mambo ya Nje Mhe. Bernard Membe na Kaimu Katibu Mkuu wa  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Rajab Gamaha,  kwenye picha ya pamoja na Maafisa Mambo ya Nje.

Sunday, April 5, 2015

Waziri Membe awaasa vijana nchini kumcha Mungu

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akihutubia wakati wa Maadhimisho ya miaka 15 ya Tamasha la Pasaka. Tamasha hilo linaloandaliwa kila mwaka na Kampuni ya Msama Promotions lilifanyika katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam tarehe 05 Aprili, 2015.
Sehemu ya umati wa watu ukimshangilia Waziri Membe alipokuwa akihutubia
Waziri Membe (wa pili kushoto), Askofu David Mwasota a kushoto),  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angella Kairuki pamoja na  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Paul Makonda wakimtazama mmoja wa waimbaji wa nyimbo za injili Bibi  Upendo Nkone (hayupo pichani) wakati wa tamasha hilo ambalo huwakusanya waimbaji wa injili kutoka ndani na nje ya nchi
Bibi Upendo Nkone akitoa burudani wakati wa  Tamasa la Pasaka

Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Balozi Mbelwa Kairuki (wa Pili kutoka kushoto Mstari wa juu) akitazama waimbaji mbalimbali wa nyimbo za injili katika Tamasha la Pasaka lililofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Bi Christina Shusho akitumbuiza katika Tamasha la Pasaka.
 Nae Bw. Joshua Mlelwa mwimbaji wa nyimbo za injili akitoa burudani Katika Tamasha la Pasaka
Mhe. Membe  akifurahia nyimbo za injili zilizokuwa zikiimbwa katika Tamasha la Pasaka 
Mwimbaji Rebeca Malope kutoka Afrika Kusini nae hakuwa nyuma kwenye Tamasha la Pasaka

Waimbaji Upendo Nkone (wa pili kushoto) na Rose Mhando (wa pili kulia) pamoja na mashabiki wao wakicheza kwa furaha mbele ya Mgeni Rasmi, Mhe. Membe (hayupo pichani)
Waziri akiangalia waimbaji jukwaani

Waziri Membe akishirikiana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara na Askofu David Mwasota kukata keki kusherehekea miaka 15 ya Tamasha la Pasaka
Waziri Membe akitoa tuzo kwa mmoja wa wawakilishi kutoka vyombo vya habari
Mhe. Membe akipokea Tuzo ya Heshima kwa mchango wake katika kusaidia jamii

Picha na Reginald Philip
================================
Waziri Membe awaasa vijana nchini kumcha Mungu

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe amewaasa vijana wa Tanzania kumcha na kumheshimu Mungu kwani wao ndio nguzo ya amani na maendeleo ya nchi.

Waziri Membe ametoa rai hiyo tarehe 05 Aprili, 2015 katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam wakati akihutubia mamia ya watu waliofika uwanjani hapo kuadhimisha miaka 15 ya Tamasha la Pasaka lililoandaliwa na Kampuni ya Msama Promotions.

Mhe. Membe ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha hilo alisema kuwa amani ya nchi inawategemea kwa kiasi kikubwa vijana wenye uadilifu na wanaomcha Mungu, kwani pasipo kufanya hivyo ni rahisi kurubuniwa na kujiunga na makundi mabaya na hatari yakiwemo ya ugaidi.

“Ndugu zangu upo uhusiano kati ya dini, vijana na amani ya nchi. Ni wajibu wa  viongozi wa dini zote na Serikali kuhimiza vijana sasa waipende dini kwa sababu ndio msingi wa nchi tunayotaka kuijenga na ni msingi wa uongozi bora na uadilifu ambao utakabidhiwa mikononi mwenu”, alisema Waziri Membe.

Mhe. Membe aliongeza kusema kuwa dini zote duniani zimejikita katika kuleta amani na kusisitiza kuwa  vijana wasiende makanisani kwa ajili ya ndoa, misiba na ibada za wagonjwa pekee bali pia  waende kwa lengo la kupata mafundisho ya kumcha Mungu  kwani taifa lenye vijana wasio waadilifu  haliwezi kuwa na viongozi bora.

Awali akimkaribisha Waziri Membe kuzungumza, Askofu David Mwasota wa Kanisa la Naioth Gospel Assembly alisema kuwa anampongeza na kumshukuru Waziri Membe kwa kuwa tayari wakati wote anapoalikwa kushiriki Tamasha la Pasaka pamoja nao.

“Mhe. Waziri umati huu umefurahishwa sana na uwepo wako. Tunatambua kuwa unazo kazi nyingi za kulitumikia taifa na hata familia yako. Lakini umetambua na kuheshimu umuhimu wa Tamasha la Pasaka  na kukubali mwaliko wetu. Ni kwa upendo wako huo katika kushirikiana na watu katika shughuli mbalimbali za kijamii ndio uliokusukuma kuacha mambo mengine yote muhimu na kuja kushirikiana nasi leo, kwa hili tunasema asante sana”, alisema Askofu Mwasota.

Aidha, wakati wa Tamasha hilo tuzo mbalimbalii zilitolewa ikiwemo Tuzo ya Heshima kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutambua mchango wake katika Sanaa, Tuzo kwa Rais Mstaafu, Mhe. Ali Hassan Mwinyi, Tuzo ya Heshima kwa Mhe. Membe kwa kutambua mchango wake katika kujishughulisha na shughuli za kijamii na Tuzo kwa Vyombo mbalimbali  vya Habari.

Viongozi wengine wa Serikali waliohudhuria Tamasha hilo ni pamoja na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Fenella Mukangara, Naibu Waziri wa  Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angela Kairuki na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Paul Makonda.

Tamasha la Pasaka ambalo lilianzishwa rasmi mwaka 2000 huwashirikisha Waimbaji wa Nyimbo za Injili kutoka nchini na nje ya nchi ambapo Tamasha la mwaka huu limewashirikisha waimbaji kutoka hapa nchini, Afrika Kusini, Uingereza na Zambia.

-Mwisho-

Waziri Membe atoa wito kwa Watanzania kuwasaidia watu wasiojiweza kwenye jamii

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb)  akimtazama kwa furaha mmoja wa watoto yatima wanaolelewa kwenye kituo cha Nyumba ya Furaha na Amani kilichopo Kigogo Mburahati, Jijini Dar es Salaam. Waziri Membe alikitembelea kituo hicho wakati wa Siku Kuu ya Pasaka. 
Mhe. Membe pamoja na Mkewe Mama Dorcas Membe wakipata maelezo juu ya watoto waishio katika kituo hich kutoka kwa Sista Mary Bakhita


Mhe Membe akizungumaza wakati wa ziara yake kituoni hapo. Kulia ni Mama Dorcas Membe. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Paul Makonda akifuatiwa na Padri Timoth Maganga wa Kanisa Katoliki la Kigogo Mburahati
Watoto yatima wakiwa na walezi wao 
Sehemu ya Wazee  wanaolelewa na Kituo hicho wakimsikiliza Mhe. Waziri (hayupo pichani) alipowatembelea
Sehemu nyingine ya Wazee na Watoto
Waziri Membe akikata keki pamoja na Sista Bakitha kama ishara ya kusherehekea Siku Kuu ya Pasaka pamoja na  Watoto Yatima na Wazee wanaolelewa kwenye kituo cha Nyumba ya Furaha na Amani. Pembeni ni Mama Dorcas Membe nae akifurahia
Mhe. Wazriri akijumuika kwa chakula cha mchana pamoja  na watoto Kituoni hapo.
Watoto hao nao wakifurahia chakula cha mchana na Mgeni wa aliyewatembelea na kusheherekea nao Sikukuu ya Pasaka
Waziri Membe akitoa  msaada kwenye kituo hicho
Waziri Membe pamoja na Mkewe Mama Dorcas Membe katika picha ya Pamoja na Masista wanaolea watoto yatima katika kituo hicho
Waziri Membe akisaini kitambu cha wageni alipowasili katika kituo hicho.
Baadhi ya Watoto wanaolelewa katika kituoni hapo wakitoa burudani mbele Waziri Membe (Hayupo pichani).
Waziri Membe akizungumza na Waandishi wa Habari.
 Picha na Reginald Philip>


====================================================================
Waziri Membe atoa wito kwa Watanzania kuwasaidia watu wasiojiweza kwenye jamii

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe ametoa wito kwa Watanzania kujenga utamaduni wa kuwasaidia watu wasiojiweza waliopo kwenye jamii wakiwemo watoto yatima, walemavu, wazee na wajane.

Waziri Membe ametoa wito huo hivi karibuni alipotembelea Kituo cha Kulelea Watoto Yatima na Wazee cha Nyumba ya Furaha na Amani kilichopo Mburahati Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Membe alisema kuwa katika jamii za watu kumekuwa na makundi ambayo yanahitaji msaada mkubwa kutoka kwa watu wengine ambao kwa namna moja au nyingine wamejaaliwa kipato kidogo na afya. Alisema kuwa ni wajibu wa watu wa aina hiyo kuwasaidia wale wanaohitaji kama vile watoto yatima, walemavu, wazee na wajane.

Waziri Membe ambaye alikuwa amefuatana na Mke wake, Mama Dorcas Membe aliguswa sana na historia ya baadhi ya watoto yatima aliowatembelea kituoni wakiwemo wale waliotupwa jalalani na kuokotwa wakiwa kwenye hali mbaya.
 “Lipo kundi linalopata mateso na matatizo katika jamii zetu tunazoishi. Ni vizuri Watanzania tukajenga utamaduni wa  kutembelea sehemu kama hizi ili kujionea wenyewe hali halisi. Kwa kweli ni hali ya kusikitisha kuona baadhi ya watoto walitupwa na kuokotwa jalalani na wengine tayari wakiwa wamepata majeraha ya kung’atwa na mbwa. Hivyo ni wajibu wetu sote kuwasaidia kwa chochote kidogo tunachojaaliwa kupata”, alisema Waziri Membe.

Aidha, Mhe. Membe aliwapongeza na kuwasifu Masista wa Shirika la Mama Theresa  ambao ndio wasimamizi wa kituo hicho kwa kuwalea watoto, vijana na wazee wenye matatizo mbalimbali na kuwaomba waendelee kujipa moyo katika kazi hiyo kwani ni njia moja wapo ya kumtumikia Mungu.

Awali akimkaribisha Waziri Membe kituoni hapo, Sista Mkuu wa Kituo hicho, Sista Mary Bakhita, alisema kuwa wamefurahia sana ziara hiyo ya Mhe. Membe hususan katika Siku Kuu ya Pasaka kwani ni faraja kubwa kwao kwa Watoto na Wazee wanaolelewa kituoni hapo.

“Tumefarijika sana kula pasaka pamoja nawe Mhe. Waziri. Watoto na Wazee hawa wanajisikia vizuri pale wanapotembelewa na tunaomba uendelee na moyo huo huo”, alisema Sista Bakhita.

Wakati wa ziara hiyo Mhe. Membe na familia yake walitoa zawadi mbalimbali kwa kituo hicho ikiwemo vyakula, sabuni na fedha kiasi cha shilingi milioni 10 kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali kituoni hapo.



-Mwisho-