Friday, May 29, 2015

Kaimu Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kikanda akutana Ujumbe wa EU hapa nchini

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Innocent Shiyo (kulia) akizungumza na Naibu Balozi wa Ujerumani hapa nchini Bw. John Reyels  ambaye pia aliongoza Ujumbe wa Jumuiya ya Ulaya (EU), kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Jumuiya hiyo pamoja na masuala mengine yanayohusu Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu. Mazungumzo hayo yalifanyika Wizarani tarehe 29 Mei, 2015.
Balozi wa Ubelgiji hapa nchini, Mhe. Adam Koeler naye akichangia jambo wakati wa kikao chao na Bw. Shiyo na kulia ni Balozi wa Uholanzi hapa nchini, Mhe. Jaap Frederiks.
Wajumbe wengine walioshiriki kikao hicho akiwemo Balozi wa Ufaransa hapa nchini Mhe. Malika Barak (kulia)
Bi. Upendo Mwasha (kushoto), Afisa Mambo ya Nje akinukuu mazungumzo.
Balozi wa Uholanzi nchini, Mhe. Frederiks akichangia hoja
Mkutano ukiendelea 
Bw. Shiyo akiagana na Balozi Koeler
Bw. Shiyo akifafanua jambo kwa Maafisa walioshiriki kikao kati yake na Ujumbe wa EU



Wednesday, May 27, 2015

Rais Kikwete awaapisha Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Balozi wa Tanzania Saudia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha  Balozi Liberata Mulamula kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Balozi Mulamula anakuwa Katibu Mkuu wa kwanza mwanamke kuongoza Wizara hiyo na kabla ya uteuzi huo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani. Hafla hiyo fupi ya uapisho imefanyika Ikulu tarehe 27 Mei, 2015.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akishuhudia Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi  Mulamula  akisaini Hati ya Kiapo mara baada ya kumwapisha. 
Mhe. Rais Kikwete akimkabidhi Balozi Mulamula Vitendea Kazi mara baada ya kumwapisha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Balozi Hassan Simba Yahya  kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kabla ya uteuzi huo Balozi Yahya alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Hafla hiyo fupi ya uapisho imefanyika Ikulu tarehe 27 Mei, 2015.
 Mhe. Rais Kikwete akishuhudia Naibu Katibu Mkuu  mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,  Balozi Yahya  akisaini Hati ya Kiapo mara baada ya kumwapisha. 
Mhe. Rais Kikwete akimpongeza Balozi Yahya mara baada ya kumwapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha, Mhe. Hemed Iddi Mgaza kuwa Balozi  wa Tanzania nchini Saudi Arabia. Kabla ya uteuzi huo Balozi Mgaza alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu  na Mkuu wa Utawala katika Ubalozi wa Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Hafla hiyo fupi ya uapisho imefanyika Ikulu tarehe 27 Mei, 2015.

Rais  Kikwete akishuhudia Balozi  Mgaza  akisaini Hati ya Kiapo mara baada ya kumwapisha.

Mhe. Rais Kikwete akimkabidhi Balozi Mgaza Vitendea Kazi mara baada ya kumwapisha.
Mhe. Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mulamula, Balozi Yahya na Balozi Mgaza mara baada ya kuwaapisha katika nyadhifa zao mpya
Mhe. Rais Kikwete kwa pamoja  na  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Mohamed Gharib Bilal (wa nne kushoto), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) (wa tatu kushoto), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) (wa tatu kutoka kulia), Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (wa pili kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mulamula, Balozi Yahya na Balozi Mgaza muda mfupi baada ya kuapishwa.
Mhe. Rais Kikwete akiwa katika Picha ya Pamoja na Balozi Mulamula, Balozi Yahya,  Balozi Mgaza na baadhi ya Wakurugenzi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mabalozi wa Tanzania.
Mhe. Rais Kikwete katika picha ya pamoja na viongozi aliowaapisha pamoja na baadhi ya Wakurugenzi wa Idara za Mambo ya Nje na Watumishi wa Wizara hiyo
Mhe. Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mulamula (kushoto) na mumewe, Bw. George Mulamula (kulia)

Picha na Reginald Philip

Watumishi Wizara ya Mambo ya Nje wawapokea kwa shangwe Katibu Mkuu mpya na Naibu Katibu Mkuu


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akikabidhiwa ua na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Bi Amisa Mwakawago alipowasili Wizarani mara baada ya kuapishwa.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Balozi Simba Yahya naye akipokea ua kutoka kwa Bi. Lilian Mushi mara baada ya kuapishwa.
Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Balozi Mulamula na Naibu Katibu Mkuu Balozi Simba wakipokelewa na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa walipowasili Wizarani hapo baada ya kuapishwa.




Picha na Reginald Philip 

Tuesday, May 26, 2015

RAIS KIKWETE AFUNGUA RASMI MKUTANO WA NNE WA MABALOZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati akifungua rasmi Mkutano wa Nne wa Mabalozi wa Tanzania nje ya nchi. Mkutano huo umefanyika katika Hoteli ya Ramada Jijini Dar es Salaam ukiwa umebeba Kaulimbiu isemayo "Diplomasia ya Tanzania Kuelekea Dira ya Taifa 2025".
Mhe. Rais Kikwete akizungumza huku Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (katikati) pamoja na Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula wakimsikiliza.
Sehemu ya Mabalozi wakifuatilia hotuba ya ufunguzi ya Mhe. Rais Kikwete (hayupo pichani)
Wajumbe wengine wakiwemo Wakuu wa Vitengo katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakifutilia hotuba ya Mhe. Rais Kikwete ambaye haonekani pichani.
Rais Kikwete akiendelea na hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo ambapo pamoja na mambo mengine aliwakumbusha Mabalozi  kuwathamini Watanzania waishio nje ya nchi, kuendelea kusaidia upatikanaji wa misaada ya maendeleo, masoko ya bidhaa za Tanzania, wawekezaji na teknolojia bora 

Mhe. Rais Kikwete akimsikiliza kwa makini Waziri Membe wakati akimweleza jambo kabla ya kuwahutubia Mabalozi
Waziri Membe akijadiliana jambo na Katibu Mkuu, Balozi Mulamula huku Balozi Sefue akisikiliza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Nne wa Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi.
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Sekretarieti ya Mkutano wa Nne wa Mabalozi 
Mhe. Rais Kikwete akiwa ameongozana na Balozi Mulamula kuelekea eneo la kupata picha ya pamoja.
Mhe. Rais Kikwete kwa pamoja na Waziri Membe, Naibu Waziri, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.), Balozi Sefue,  Balozi Mulamula, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Simba Yahya, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, Mhe. Mussa  Zungu, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Paul Makonda wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wote .
Mhe. Rais Kikwete na Viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi Wanawake
Mhe. Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.


Picha na Reginald Philip

Monday, May 25, 2015

Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi wa EAC kuhusu Burundi kufanyika mwishoni mwa mwezi Mei

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo tarehe 25 Mei, 2015 kuhusu Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaotarajiwa kufanyika Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Mei, 2015 kuhusu masuala ya amani na usalama nchini Burundi. Mkutano huo ambao umeitishwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya EAC, Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete utatanguliwa na Mkutano wa Baraza la Mawaziri.
Mhe. Membe akiendelea na mkutano wake na Waandishi wa Habari


Picha na Reginald Philip

Mkutano wa Nne wa Mabalozi kujadili mchango wa Diplomasia ya Tanzania kuelekea Dira ya Maendeleo 2025 waanza

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) na Katibu Mkuu Mteule wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula wakati wa Mkutano wa Nne wa Mabalozi wanaowakilisha Tanzania nje ya nchi uliofanyika katika Hoteli ya Ramada, Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2015. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akiwasilisha mada kuhusu Mafanikio ya Wizara katika Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi wakati wa Mkutano wa Nne wa Mabalozi wanaowakilisha Tanzania nje ya nchi uliofanyika katika Hoteli ya Ramada, Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2015. 
Mkutano ukiendelea
Sehemu ya Mabalozi wa Tanzania wakimsikiliza Mhe. Membe ambaye haonekani pichani. Kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Mhe. Naimi Aziz, Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Mhe. Aziz Ponary Mlima, Balozi wa Tanzania nchini Congo, Mhe. Anthony Cheche, Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Mhe. Nassor Mbarouk na Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Mhe. Chabaka Kilumanga.
Mhe. Membe akiwa na Katibu Mkuu, Balozi Mulamula pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. John Haule (wa pili kulia) na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Mhe. Philip Marmo
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Peter Kalaghe akiwasilisha mada kwa niaba ya Mabalozi wa Tanzania Kanda ya Ulaya na Marekani huku Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Ali Saleh (kulia) ambaye aliwakilisha kanda ya Mashariki ya Kati, Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. John Kijazi (kushoto) aliyewakilisha kanda ya Asia na Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Mhe. Radhia Msuya aliyewakilisha kanda ya Afrika wakimsikiliza.
Mabalozi wengine wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi wakifuatilia mada wakati wa mkutano wao wa nne. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi Mhe. Wilson Masilingi, akifuatiwa na Balozi wa Tanzania nchini Canada, Mhe. Mugendi Zoka na Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Mhe. Deodorus Kamala
Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Mhe. Daniel Ole Njoolay (wa kwanza kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. James Lugaganya (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Mashariki, Bw. Elibariki Maleko (katikati) wakifuatilia mada.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Musa Azan Zungu akizungumza wakati wa Mkutano wa Nne wa Mabalozi kuhusu jitihada zinazofanywa na kamati hiyo kuhakikisha maslahi ya Mabalozi na Watendaji wote katika Balozi za Tanzania yanalindwa ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao vizuri.
Wakuu wa Vitengo katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nao wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa Mkutano wa Nne wa Mabalozi. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,   Bw. Isac kalumuna  akifuatiwa na Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani, Bw. Mathias Abisai na Mkurugenzi wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi, Bw. Lucas Suka
Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Mhe. Rajabu Gamaha akichangia wakati wa majadiliano ya mada mbalimbali zilizowasilishwa

Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar, Balozi Silima akizungumza wakati wa majadiliano kwenye mkutano wa nne wa mabalozi. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Uswisi, Mhe. Modest Mero
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Zuhura Bundala akichangia katika mjadala kuhusu kanda ya Afrika
Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Balozi Mbelwa Kairuki akizungumza wakati wa kuchangia mada kuhusu Kanda ya Asia na Australasia. 
Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Mhe. Begum Taj naye akichangia hoja
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) akizungumza wakati wa Mkutano wa Nne wa Mabalozi. Pembeni yake ni Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Bi. Victoria Mwakasege
Sehemu ya Sekretarieti wakinukuu mazungumzo wakati we mkutano wanne wa Mabalozi
Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Mhe. Aziz Ponary Mlima akichangia mada huku Balozi Cheche na Balozi Mbarouk
Mkutano ukiendelea

Picha na Reginald Philip