Tuesday, June 23, 2015

Balozi Simba apongezwa na iliyokuwa Idara yake kwa kuteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya akipokea zawadi kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Bw. Elibariki Maleko katika hafla fupi ya kumpongeza Balozi Simba kwa kuteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo. Kabla ya uteuzi huo Balozi Simba alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati. Hafla hiyo ilifanya katika Hoteli ya Southernsun Jijini Dar es Salaam 
Balozi Simba akitoa neno la shukrani kwa Watumishi wa Idara ya Mashariki ya Kati wakati wa hafla hiyo.
 Balozi Simba  (wanne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Idara ya Mashariki ya Kati. 


Picha na Reginald Philip

Monday, June 22, 2015

Katibu Mkuu Kiongozi atembelea Banda la Mambo ya Nje kwenye Wiki ya Utumishi wa Umma

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushiriano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya akimkaribisha Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue kwenye Banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakati wa maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Habu Mkwizu.
Balozi Sefue akisaini Kitabu cha Wageni katika Banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Balozi Sefue akisoma Kitabu cha Sera ya Mambo ya Nje huku akisikiliza maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Yahya.
Katibu Mkuu Kiongozi,  Balozi Sefue (katikati), Naibu Katibu Mkuu Balozi Simba Yahya (kushoto) wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Manejimenti ya Utumishi wa Umma,  Bw. Habu Mkwizu alipokuwa akiwaelezea jambo.
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Taasisi zake wakifurahia jambo na Naibu Katibu Mkuu mara baada ya Katibu Mkuu Kiongozi  kutembelea Banda la Mambo ya Nje.

Juu na Chini ni Balozi Yahya akihojiwa na Mwandishi wa Habari kutoka TBC kuhusu mafanikio ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Mkufunzi kutoka Chuo cha Diplomasia Bw. Ally Masabo naye akihojiwa na Mwandishi wa TBC
Afisa Mambo ya Nje, Bw. Batholomeo Jungu akitoa maelezo kwa mmoja wa wananchi waliojitokeza kutembelea Banda la Wizara ya Mambo ya Nje wakati wa Maonesho ya Utumishi wa Umma.  
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu katika Wizara ya Mambo ya Nje, Bi. Glory Mboya akisaini Kitabu katika Banda la Maonyesho la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililopo katika maonyesho Utumishi wa Umma Jijini Dar es Salaam
Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya akitizama mfano wa Majengo yanayojengwa katika Banda la Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolijia.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa tatu kulia), na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje Balozi Simba Yahya (wa nne kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa kutoka Wizarani na Taasisi zake. 
Naibu Katibu Mkuu Balozi Simba Yahya akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Wizara na Taasisi zake.

Picha na Reginald Philip

Rais Kikwete aongea na Watanzania wanaoishi India

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Watanznia wanaoishi India katika Hotel ya Taj Palace jijini Delhi. Rais Kikwete aliwaeleza mambo ya maendeleo yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya nne ikiwemo ujenzi wa miundombinu kama vile barabara, maji, umeme na uboreshaji wa bandari ya Dar es Salaam. Aidha, aliwambia mipango iliyopo ya kujenga bandari ya Bagamoyo na reli ya kati ya kisasa. Aliwaeleza pia hali ya kisiasa, hususan maandalizi ya uchguzi mkuu ambapo zoezi la kuchukua fomu za kuwania nafasi ya Rais linaendelea.

Baadhi ya Watanzania waliohudhuria mkutano wa Rais Kikwete

Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe (Mb) kulia na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb) nao waliongozana na Rais Kikwete katika mkutano na Watanzania.
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekzaji Tanzania (TIC), Bi. Juliet Kairuki akitoa ufafanuzi wa masuala ya uwekezaji kwa Watanzania wanaoishi India.

Dada wa Kitanzania ambaye kwa sasa ni mwanafunzi wa Shahada ya Uzamili ya masuala ya Teknolojia ya Kilimo nchini India akimuuliza swali Rais Kikwete. Dada huyo alitaka kujua Serikali imejipngaje kuhakikisha kuwa mazao yanayolimwa nchini Tanzania yanasindikwa kabla ya kusafirishwa nje ya nchi. Rais Kikwete alieleza kuwa katika awamu ya pili ya mpango wa maendeleo wa mwaka 2025 ambao unaanza kutekelezwa mwaka 2015/2016 unalenga maendeleo ya viwanda. 

Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na watoto wa wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini India.
Rais Kikwete (kushoto) akiwa pamoja na Balozi wa Tanzania nchini India, Me. Mhandisi John Kijazi


Mama Salma Kikwete (katikati) akiwa na baadhi ya Watanzania wanawake wanaoishi India.

 

Saturday, June 20, 2015

Ifanyeni Tanzania kuwa chaguo la kwanza katika uwekezaji, Rais Kikwete


Rais wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiwa katika mazungumzo na Wakuu wa Makampuni makubwa ya India hawapo pichani. Aliwahimiza kuchangamkia fursa za uwekezaji nchini Tanzania. kushoto kwa Mhe. Rais ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Abdallah Kigoda (Mb) na kulia ni kiongozi wa Chama cha Wafanyabiashara nchini India. Mazungumzo hayo yakifanyika katika Hoteli ya Taj Palace jijini Delhi 

Wakuu wa Makampuni Makubwa ya India wakimsikiliza Rais Kikwete. Baadhi ya Makampuni hayo tayari yalishawekeza nchini Tanzania na Makampuni mengine yalionesha dhamira ya kuja kuwekeza.

Mkurugenzi Mkuu  wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bi. Juliet Kairuki akiteta jambo na Mhe. Rais kabla ya mazungumzo na Wakuu wa Makampuni ya India.

Kiongozi wa Chama cha Wafanyabiashara wa India akimkabidhi, Mhe. Rais zawadi.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Abdallah Kigoda (Mb) kulia akizungumza jambo na mmoja wa Wakuu wa Makampuni ya India. Mwingine kushoto ni Waziri wa Maji, Mhe. Prof. Jumanne Maghembe (Mb). 

Afisa Dawati wa India katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Emmanuel Luangisa akisalimiana na mmoja wa viongozi wa TIC kabla ya kuanza mazungumzo kati ya Mhe. Rais na Wakuu wa Makampuni.
Mkurugenzi Msaidizi katika Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Nathaniel Kaaya  naye akiwa katika kubadilishana mawazo na wawakiishi wa India

Mikutano ya Rais Kikwete na baadhi ya Wakuu wa Makampuni
 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, knlia akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya IFLS inayojishughulisha na uwekezaji katika miundombinu na huduma za kifedha. Rais aliiomba kampuni hiyo iangalie uwezekno wa kuja kuwekeza nchini Tanzania, hususan katika ujenzi wa barabara na miundombinu ya  maji kwa kutumia mfumo wa PPP. 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa tatu kutoka kushoto akiwa katika mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Hospitali za Apollo aliyenyoosha mikono. Mtendaji huyo alieleza kuwa taratibu zipo katika hatua za mwisho ili hospitali hiyo ifungue zahanati ya kwanza nchini Tanzania katika miezi miwili ijayo.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa tatu kushoto akiwa katika mazungumzo na Mkurugeenzi Mwendeshaji na Mwenyekiti wa Shirika la Ndege la India. Mhe. Rais aliliomba shirika hilo lirudishe safari za kuja Tanzania jambo ambalo walikubaliana nalo.
Rais Kikwete akiwa pamoja na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya ICICI. Rais Kikwete aliiomba benki hiyo ije kuwekeza Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Posta. Benki ya ICICI ina mtaji unaozidi Dola bilioni 100 imesambaa nchi nzima ya India hadi vijijini.



Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje akutana kwa mara ya kwanza na Watumishi wote wa Wizara


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Libarata Mulamula akizungumza katika kikao chake cha kwanza na Watumishi wote wa Wizara tangu alipoteuliwa na Rais hivi karibuni kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Mkutano huo ulifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Jijini  Dar es Salaam tarehe 20 Juni, 2015. Pamoja na mambo mengine Balozi Mulamula aliwahimiza Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje kufanya kazi kwa bidii, kuwa  na utii, nidhamu pamoja na unyenyekevu ili kufikia malengo katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara.
Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na Watumishi wa  Wizara wakimsikiliza Balozi Mulamula (hayupo pichani)
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje  wakimsikiliza Balozi Mulamula (Hayupo pichani).
Sehemu nyingine ya Watumishi wa Mambo ya Nje wakimsikiliza Balozi Mulamula


Juu na Chini ni baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakiwa katika kikao na Balozi Mulamula

Baadhi ya Watumishi wakichangia hoja wakati wa mkutano kati yao na Katibu Mkuu, Balozi Mulamula ambaye hayupo pichani


Mkutano ukiendelea 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya nae akizungumza machache mbele ya Watumishi wakati wa mkutano huo 
Balozi Mulamula kwa pamoja na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya wakishangilia  kwa furaha  wakati walipokutana na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Watumishi wa Wizara wakiwashangilia Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wakati wa mkutano pamoja nao.

Picha na Reginald Philip