Monday, July 6, 2015

Rais Kikwete aongoza Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi wa EAC kuhusu Burundi


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Mhe.Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na baadhi ya Wawakilishi wa Wakuu wa Nchi Wanachama wakiimba Wimbo wa Jumuiya  hiyo tayari kwa kuanza Mkutano wao Dharura wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya hiyo uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 06 Julai, 2015.
 Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt.Richard Sezibera akisoma Maazimio  yaliyofikiwa katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi wa EAC huku Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Rais Kikwete (wa tano kutoka kushoto waliokaa) pamoja na viongozi wengine wakisikiliza kwa makini. Pamoja na mambo mengine Wakuu wa Nchi wamemteua Rais Museveni kusimamia majadiliano ya makundi yanayopingana nchini Burundi na Uchaguzi wa Rais ufanyike tarehe 30 Julai, 2015 badala ya tarehe 15 Julai mwaka huu.
 Katibu mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulamula (katikati) kwa pamoja na  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afrika Mashariki, Bi.Joyce Mapunjo (kulia) pamoja na wajumbe wengine waliohudhuria mkutano huo wakiimba wimbo wa Jumuiya.
  Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Chirau Ali Mwakere pamoja na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Kenya, Mhe. Phyllis Kandie 

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Zuhura Bundala akiwa na Wajumbe wengine kabla ya mkutano kuanza
 Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Mhe.Ali Siwa (katikati) na Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe.Ladislaus Komba (kulia)  wakati wa mkutano huo.
 Afisa Mwandamizi kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Burundi, Bi. Victoria Mwakasege akiwa na Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais wakisikiliza maazimio ya wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yakisomwa.
 Afisa Mwandamizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw.Mkumbwa Ally akijadiliana jambo na Afisa wa Mambo ya Nje, Bi.Samira Diria muda mfupi kabla ya mkutano huo kuanza.
Sehemu ya Wajumbe waliohudhuria mkutano huo uliofanyika Ikulu, Jijini Dar es Salaam.
Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
 Picha ya pamoja.

Picha na Reuben Mchome
==================================

Wakuu wa Nchi wa EAC wamteua Rais Museveni kusimamia majadiliano nchini Burundi

Mkutano wa Tatu wa Dharura wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kujadili hali ya kisisasa nchini Burundi umefanyika Jijini Dar es Salaam tarehe 06 Julai, 2015 chini ya Uenyekiti wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Katika Mkutano huo ambao umehudhuriwa pia na Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni na Mawaziri wa Mambo ya Nje na wale wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki kutoka nchi zote wanachama, umeazimia masuala mbalimbali kwa ajili ya kuhakikisha hali ya kisiasa na utulivu  nchini Burundi inarejea.

Katika mkutano huo, Wakuu wa Nchi wamemteua Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kusimamia majadiliano ya makundi yanayopingana nchini Burundi.

Pia wakuu hao wa nchi wameitaka Serikali ya Burundi kuyanyang’anya silaha makundi yote nchini humo kikiwemo kikundi kinachojiita Imbonera Kure”. Aidha, wameomba Umoja wa Afrika (AU) usimamie zoezi hili kwa kupeleka Timu ya Waangalizi wa Kijeshi ili kuhakikisha linafanikiwa. 

Azimio jingine ni kuvitaka vyombo vya usalama chini ya Sekretarieti ya Maziwa Makuu (ICGLR) kutafiti na kuhakiki uwepo wa kikundi cha waasi cha FDLR nchini Burundi.

Aidha, Wakuu wa Nchi wameitaka Serikali ya Burundi kuahirisha Uchaguzi wa Rais  uliopangwa kufanyika tarehe 15 Julai, 2015 na sasa ufanyike tarehe 30 Julai, 2015 ili kutoa muda kwa msuluhishi kusimamia majadiliano kama ilivyopangwa.

Wakuu hao wa nchi pia wametaka yeyote atakayeshinda nafasi ya Urais nchini Burundi kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa itakayojumuisha vyama vilivoshiriki kwenye Uchaguzi na vile ambavyo havikushiriki.

Pia, Wakuu wa nchi wameitaka Serikali ya Burundi kuheshimu Mkataba wa Amani na Maridhiano wa Arusha wa mwaka 2000 na kutoifanyia marekebisho ya aina yoyote Katiba ya Burundi.

Vilevile, Wakuu hao wa nchi wameiomba AU kuidhinisha na kupitisha maamuzi haya ya EAC na kwamba Jumuiya hiyo ya Afrika Mashariki itatuma Timu ya Waangalizi katika Uchaguzi wa Rais nchini Burundi.

-Mwisho-








Rais Museni awasili nchini kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa EAC

Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  Jijini Dar es Salaam. Mhe. Rais Museveni yupo nchini kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu hali ya kisisasa nchini Burundi utakaofanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 06 Julai, 2015.
Mhe. Rais Museveni akisilimiana na Wakuu wa Vyombo vya Usalama waliofika Uwanjani kumpokea.
Mhe. Rais Museveni akiongozana na mwenyeji wake Waziri Membe mara baada ya kuwasili
Mhe. Rais Museveni akikagua Gwaride la Heshima
Rais Museveni kwa pamoja na Waziri Membe wakifuatilia burudani kutoka kwa moja ya kikundi kilichokuwepo uwanjani hapo kwa mapokezi
Mhe. Rais Museveni akimsikiliza Mhe. Membe  katika mazungumzo mafupi kabla ya kuondoka Uwanjani hapo. Wengine katika picha ni Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Ladislaus Komba (kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe. Sofia Mjema (mwenye kitambaa kichwani) na Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Uganda hapa nchini.

Picha na Reginald Philip


Sunday, July 5, 2015

Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa EAC wafunguliwa Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb.) akifungua Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki ambao pamoja na mambo mengine utapokea na kujadili taarifa ya ziara ya Mawaziri nchini Burundi kuhusu hali ya kisisasa nchini humo. Mkutano huo ambao ni maandalizi ya Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi utakaofanyika tarehe 06 Julai, 2015, umefanyika kwenye Hoteli ya Serena, Jijini Dar es Salaam tarehe 05 Julai, 2015.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Dkt. Richard Sezibera naye akizungumza wakati wa mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula (kulia) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Joyce Mapunjo wakifuatilia kwa makini ufunguzi wa Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam
Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa nao wakifuatilia kwa makini ufunguzi wa Mkutano huo
Waziri wa Afrika Mashariki nchini Rwanda, Mhe. Valentine Rugwabiza (wa pili kushoto)  pamoja na wajumbe wengine waliohudhuria Mkutano huo. 
Balozi wa Tanzana nchini Burundi Mhe. Rajab Gamah (Kushoto) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Mhe. Henry Okello Oryem 
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Zuhura Bundara (Kushoto) akiwa na  Afisa Mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Burundi, Bi. Victoria Mwakasege wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri.
Maafisa Mambo ya Nje nao wakifuatilia kwa makini ufunguzi wa Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri. Kutoka kushoto ni Bw. Ally Ubwa, Bi. Grace Martin na Bw. Mudrick Soraga
Mkutano ukiendelea

Picha na Reginald Philip

Friday, July 3, 2015

Rais Kikwete aweka jiwe la msingi kuzindua ujenzi wa jengo la MICT

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete (mwenye tai nyejundu) akiwa pamoja na viongozi mbalimbali katika eneo la Lakilaki jijini Arusha linalojengwa jengo la taasisi ya Mechanism for International Criminal Tribunals (MICT) inayorithi shughuli za Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR). Mhe. Rais aliweka jiwe la msingi la ujenzi huo jijini Arusha tarehe 01 Julai 2015

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete wa tano kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Serikali na viongozi wa Umoja wa Mataifa waliopo Arusha na waliomwakilisha Katibu Mkuu wa Umoja huo katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi


Balozi Irene Kasyanju, Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje (wa pili kulia), Bi. Tully Mwaipopo, Afisa wa Uabalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa pamoja na Amer Jandu wa pili kutoka kushoto na Bw. Samuel Akorimo, Afisa Mkuu wa MICT, Arusha wakiwa eneo la Lakilaki. Bw. Jandu ni mmiliki wa kampuni ya kitanzania iliyoshinda kandarasi ya kujenga jengo hilo.


Balozi Celestine Mushy, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda wa kwanza kulia na Balozi Kasyanju wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa Umoja wa Mataifa mbele ya jiwe la msingi lililowekwa na Rais Kikwete.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Hassan Simba Yahya wa pili kushoto, Balozi Kasyanju, Balozi Mushy na Bw. Akorimo wakikagua eneo la ujenzi kabla ya shughuli za uwekaji wa jiwe la msingi kuanza.

Rais Kikwete azindua rasmi Kiwanda cha Viuadudu Wilayani Kibaha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe.Hailemariam Desalegn wakikata utepe kwenye uzinduzi wa Kiwanda cha kuzalisha Viuadudu vya kuua Viluwiluwi vya Mbu wanaoeneza Malaria kilichopo eneo la viwanda-TAMCO Kibaha Mkoani Pwani. Uzinduzi huo ulifanyika tarehe 02 Julai, 2015. Wanaoshuhudia pembeni ni Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda na Balozi wa Cuba nchini, Mhe. Jorge Tormo.
Rais Kikwete pamoja na Waziri Mkuu wa Ethiopia wakizindua rasmi Kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza ugonjwa wa Malaria.
Mhe. Rais Kikwete akizungumza na wananchi waliohudhuria  uzinduzi wa kiwanda hicho.Wanaomsikiliza ni Mhe. Desalegn, Mhe. Pinda na Mhe. Tormo.
Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe.Hailemariam Desalegn akihutubia umati wa watu wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho kilichopo Wilayani Kibaha.
Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria uzinduzi wa kiwanda hicho,wakimsikiliza kwa makini Mhe. Rais Kikwete (hayupo pichani) 
Mhe. Rais Kikwete kwa pamoja na Mhe. Desalegn, Mhe. Pinda, Mama Salma Kikwete na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Abdallah Kigoda wakifurahia jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kiwanda cha kuzalisha Viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria kilichopo Wilayani Kibaha
Balozi Joseph Sokoine (wa kwanza mstari wa mbele kulia) akiwa na Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini wakiwa wamesimama wakati wa hafla ya uzinduzi wa kiwanda hicho.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,  Balozi Liberata Mulamula akifurahia jambo na Mhe. Rais Kikwete pamoja na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Desalegn wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho.
Rais Kikwete pamoja na Waziri Mkuu wa Ethiopia wakipata maelezo kutoka kwa mmoja wa Wataalam wa kiwanda hicho cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza Malaria
 Juu na Chini ni baadhi ya mitambo ya kuzalisha Viuadudu hivyo vya kuulia viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria.

Picha na Reuben Mchome

Thursday, July 2, 2015

Wizar yaidhinisha Michoro ya Makao Makuu

Balozi Hassan Simba Yahya, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (kulia), na Bibi Li Xi, Mkurugenzi wa Idara ya Nje ya Taasisi ya Michoro ya Majeno na Utafiti ya Citic ya China, wakitia saini makubaliano ya michoro ya Makao Makuu Mapya ya Wizara jijini Dar Es Salaam jana.
Balozi Yahya na Bibi Li wakibadilishana hati za makubaliano waliyosaini.
Balozi Yahya na Bibi Li wakionyesha hati za makubaliano ya michoro ya Makao Makuu mapya ya wizara ya Nje.

Wizara ya Mambo ya Nje kujenga jengo jipya

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Hassan Simba Yahya kulia na Mwakilishi wa Kampuni itakayojenga jengo la Wizara ya Mambo ya Nje wakiweka saini Makubaliano ya mchoro wa jengo hilo.
Balozi Yahya akibadilishana nyaraka za makubaliano ya michoro ya jengo la Wizara na Mwakilishi wa Kampuni itakayojenga jengo hilo.
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, imeidhinisha michoro ya Jengo jipya la wizara hiyo, litakalojengwa jirani na Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, jijini Dar Es Salaam.
Makubaliano kuhusu michoro hiyo ya jengo la ghorofa sita, litakalogharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China, yametiwa saini jana baina ya wizara na mwakilishi wa mkandarasi wa ujenzi.
Akiongea baada ya kutia saini makubaliano hayo kwa niaba ya wizara, Naibu Katibu Mkuu, Balozi Hassan Simba Yahya, alisema hatua hiyo inatoa fursa kwa matayarisho ya ujenzi kuanza, na kuwa kazi ya ujenzi inatarajiwa kuanza kabla ya mwisho wa muhula wa Serikali ya Awamu ya Nne.
"Tumekamilisha hatua muhimu katika matayarisho ya ujenzi wa Jengo la Wizara," alisema, na kuongeza kuwa mradi huu ulianzishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete.
Utiaji saini wa makubaliano ya michoro hiyo ulishuhudiwa na wawakilishi wa Wakala wa Majengo (TBA).

Wednesday, July 1, 2015

Press Release


H.E. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent congratulatory message to The Right Honourable Stephen Harper, Prime Minister of Canada on the occasion of the National Day of Canada.

The message reads as follows.

“The Right Honourable Stephen Harper,
  The Prime Minister of Canada,

          Rt. Honourable and Dear colleague,

On behalf of the People and the Government of the United Republic of Tanzania, and indeed on my own behalf, I extend to you and through you to the People of Canada, my sincere congratulations on the occasion of Canada's National Day.

Tanzania and Canada continue to enjoy excellent bilateral relations that date back to the early years of our independence. Throughout the years, our two nations have continued to work together to strengthen our friendship, cooperation and partnership both at the individual and Government levels. As you celebrate your county's National Day, I take this opportunity to reiterate my personal commitment and that of my Government to work closely with you and Your Government in elevating to greater heights, the cordial bilateral relations that happily exist between our two countries and peoples.

I wish you, Rt. Honourable, personal good health and prosperity as you lead the people of Canada.

May I once again congratulate you on your National Day. Please accept, Rt. Honourable Prime Minister, the assurances of my highest consideration.


Issued by the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation. Dar es Salaam, 30th June, 2015
 

Waziri Mkuu wa Ethiopia awasili nchini kwa ziara ya kikazi

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Peter Pinda (kulia) akimtambulisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) kwa Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Hailemariam Desalegn (Katikati) mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Mhe. Desalegn yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ambapo pamoja na mambo mengine atashiriki uzinduzi wa Kiwanda cha Viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria.
Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Desalegn akisalimiana na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mkurugenzi Idara ya Asia na Australasia, Balozi Mbelwa Kairuki mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam
Waziri Mkuu, Mhe. Pinda akimtambulisha Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Mhe. Naimi Aziz kwa Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Desalegn.
 Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Desalegn. akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Zuhura Bundala
Afisa Mambo ya Nje, Bw. Mudrick Soraga naye akisalimian na Mhe. Desalegn 
Waziri Mkuu wa Ethiopia akikagua Gwaride la Heshima mara baada ya kuwasili huku akisindikizwa na Mhe. Pinda
Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Desalegn kwa pamoja na Mhe. Pinda wakimsikiliza Mhe. Membe wakati wa mazungumzo mafupi mara baada ya Mhe. Desalegn kuwasili.


............Matukio zaidi ya ziara ya Waziri Mkuu wa Ethiopia nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mhe. Desalegn, Mhe. Pinda na Bi. Joyce Phumaphi, Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Viongozi wa Afrika walio mstari wa mbele katika  kupambana na Malaria  (ALMA). Mhe. Desalegn ndiye Mwenyekiti wa sasa wa Taasisi hiyo wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa Ikulu kwa heshima ya Mhe. Desalegn.
Balozi wa Cuba (kushoto), Mhe. Jorge Luis Lopez Tormo akiwa pamoja na Mkurugenzi  wa Idara ya Ulaya na Amerika, Balozi Joseph Sokoine (wa pili kushoto), wakimsikiliza Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki, Balozi Juma Maharage wakati wa hafla ya chakula cha jioni kwa heshima ya Waziri Mkuu wa Ethiopia.
Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Mhe. Naimi Aziz (mwenye kitambaa kichwani) akiwa na Kaimu Mkurugenzi  wa Idara ya  Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,  Bi. Zuhura Bundala pamoja na wageni wengine waalikwa wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa Ikulu kwa heshima ya Waziri Mkuu wa Ethiopia.

Picha na Reginald Philip