Wednesday, September 14, 2016

Wizara ya Mambo ya Nje yachangia waathirika wa tetemeko Mkoani Kagera

Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akipokea mfano wa hundi ya Shilingi milioni 10 kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (katikati) ikiwa ni mchango wa Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera hivi karibuni. Mkutano huo wa kuhamasisha uchangiaji  ulifanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 13 Septemba, 2016 na kuwashirikisha Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini na Wafanyabiashara. Kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Charles Mwijage na kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Aziz Mlima
Sehemu ya Mabalozi na Wafanyabiashara walioshiriki mkutano huo
Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa akitoa hotuba wakati wa mkutano wa kuhamasisha uchangiaji kwa maafa yaliyotokea Kagera kufuatia tetemeko la ardhi.
Sehemu nyingine ya wafanyabiashara akiwemo Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Dkt. Reginald Mengi (wa kwanza kushoto)
Sehemu ya wageni waalikwa walioshiriki mkutano huo wakiwemo Wakurugenzi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Mhe. Dkt. Kolimba akitoa neno la ukaribisho wakati wa mkutano huo
Mwenyekiti wa TPSF, Dkt. Mengi akizungumza wakati wa mkutano huo
Mkutanoo ukiendelea


Tuesday, September 13, 2016

TAMKO (COMMUNIQUE); Mkutano wa Dharula wa 17 wa Viongozi Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

COMMUNIQUE: 17TH EXTRA-ORDINARY SUMMIT OF HEADs OF STATE OF THE EAST AFRICAN COMMUNITY
1. THE EAST AFRICAN COMMUNITY HEADS OF STATE, THEIR EXCELLENCIES PRESIDENT DR. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA AND CHAIRPERSON OF THE SUMMIT, PRESIDENT YOWERI KAGUTA MUSEVENI OF THE REPUBLIC OF UGANDA, PRESIDENT PAUL KAGAME OF THE REPUBLIC OF RWANDA, DEPUTY PRESIDENT WILLIAM RUTO OF THE REPUBLIC OF KENYA; AND AMB. ALAIN AIMÈ NYAMITWE, MINISTER OF EXTERNAL RELATIONS AND INTERNATIONAL COOPERATION OF THE REPUBLIC OF BURUNDI REPRESENTING PRESIDENT PIERRE NKURUZINZA HELD THE 17TH EXTRA-ORDINARY SUMMIT MEETING OF THE EAST AFRICAN COMMUNITY HEADS OF STATE ON 8TH SEPTEMBER, 2016 IN DAR ES SALAAM, TANZANIA. IN ATTENDANCE WERE H.E ALI MOHAMED SHEIN, PRESIDENT OF ZANZIBAR, AND HON AGGREY TISA SABUNI, SPECIAL ENVOY OF GENERAL SALVA KIIR MAYARDIT, PRESIDENT OF THE REPUBLIC OF SOUTH SUDAN.

2. THE HEADS OF STATE AND GOVERNMENT MET IN A WARM AND CORDIAL ATMOSPHERE.

3. THE HEADS OF STATE CONSIDERED A REPORT OF THE COUNCIL OF MINISTERS ON EU-EAC ECONOMIC PARTNERSHIP AGREEMENT (EPA) AND NOTED THAT TWO PARTNER STATES HAVE SIGNED THE EPA. THE SUMMIT REQUESTED FOR THREE MONTHS TO FINALISE ON THE CLARIFICATION OF THE CONCERNS OF SOME OF THE REMAINING PARTNER STATES BEFORE CONSIDERING THE SIGNATURE OF EPA AS A BLOC. THE SUMMIT CALLED UPON EU NOT TO PENALISE THE REPUBLIC OF KENYA AND DIRECTED THE SECRETARIAT TO COMMUNICATE TO EU ON THIS MATTER.

4. THE HEADS OF STATE RECEIVED A REPORT FROM H. E. BENJAMIN WILLIAM MKAPA, THE FACILITATOR OF THE INTER- BURUNDI DIALOGUE. THE SUMMIT ENDORSED ALL THE RECOMMENDATIONS AS PROPOSED IN H. E BENJAMIN WILLIAM MKAPA’S REPORT ON THE INTER BURUNDI DIALOGUE AND DIRECTED THE COUNCIL OF MINISTERS TO AVAIL A BUDGET FOR THE INTER BURUNDI DIALOGUE.

5. THE HEADS OF STATE RECEIVED A REPORT OF THE COUNCIL OF MINISTERS ON MATTERS RELATING TO THE REPUBLIC OF SOUTH SUDAN AND CONGRATULATED THE PEOPLE AND THE GOVERNMENT OF THE REPUBLIC OF SOUTH SUDAN FOR THE TIMELY DEPOSITING OF THE INSTRUMENTS OF RATIFICATION OF THE TREATY OF ACCESSION OF THE REPUBLIC OF SOUTH SUDAN INTO THE EAST AFRICAN COMMUNITY WITH THE SECRETARY GENERAL. THE HEADS OF STATE DIRECTED THE COUNCIL OF MINISTERS TO PRESENT THE ROADMAP FOR THE ACCELERATED INTEGRATION OF THE REPUBLIC OF SOUTH SUDAN INTO THE EAC AT THE 18TH SUMMIT OF THE EAC HEADS OF STATES SCHEDULED FOR NOVEMBER, 2016.

6. THE HEADS OF STATE RECEIVED THE REPORT OF THE 33RD EXTRA-ORDINARY MEETING OF THE COUNCIL OF MINISTERS RECOMMENDING TO THE SUMMIT THE APPOINTMENT OF HON. CHRISTOPHE BAZIVAMO FROM THE REPUBLIC OF RWANDA AS A DEPUTY SECRETARY GENERAL OF THE EAST AFRICAN COMMUNITY.

7. THE HEADS OF STATE APPOINTED HON. CHRISTOPHE BAZIVAMO AS DEPUTY SECRETARY GENERAL OF THE EAST AFRICAN COMMUNITY TO A THREE YEAR TERM WITH EFFECT FROM 8TH SEPTEMBER, 2016 AND PRESIDED OVER HIS SWEARING IN CEREMONY.

8. THEIR EXCELLENCIES PRESIDENT YOWERI KAGUTA MUSEVENI OF THE REPUBLIC OF UGANDA, PRESIDENT PAUL KAGAME OF THE REPUBLIC OF RWANDA, DEPUTY PRESIDENT WILLIAM RUTO OF THE REPUBLIC OF KENYA AND AMB. ALAIN AIMÉ NYAMITWE MINISTER OF EXTERNAL RELATIONS AND INTERNATIONAL COOPERATION OF THE REPUBLIC OF BURUNDI THANKED THEIR HOST, HIS EXCELLENCY PRESIDENT DR. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA AND CHAIRPERSON OF THE SUMMIT, FOR THE WARM AND CORDIAL HOSPITALITY EXTENDED TO THEM AND THEIR RESPECTIVE DELEGATIONS DURING THEIR STAY IN DAR ES SALAAM.


……………………........…....
H.E DR. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI
PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

…………….................……
H.E YOWERI KAGUTA MUSEVENI
PRESIDENT OF THE REPUBLIC OF UGANDA

…………………........…
H.E PAUL KAGAME
PRESIDENT OF THE REPUBLIC OF RWANDA

….………….……..…..…..
H.E WILLIAM RUTO
DEPUTY PRESIDENT OF THE REPUBLIC OF KENYA

……………………....…
AMB. ALAIN AIMÉ NYAMITWE
MINISTER OF EXTERNAL RELATIONS AND INTERNATIONAL COOPERATION
REPUBLIC OF BURUNDI


Friday, September 9, 2016

Mkutano wa 17 wa Dharura wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wamalizika Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika Mkutano wa 17 wa Viongozi Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akizungumza katika Mkutano wa 17 wa Viongozi Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Rwanda Mhe. Paul Kagame akizungumza katika Mkutano wa 17 wa Viongozi Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akizungumza katika Mkutano wa 17 wa Viongozi Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Ikulu, Jijini Dar es Salaam
Naibu Rais wa Kenya Mhe. William Ruto akizungumza katika Mkutano wa 17 wa Viongozi Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Ikulu Jijini Dar es Salam
Sehemu ya wageni waalikwa wakifuatilia Mkutano

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu Wengine wa Nchi Wanachama wa Jumuiya na Wawakilishi.

Thursday, September 8, 2016

Rais Museveni awasili nchini kuhudhuria Mkutano wa Dharura wa EAC

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango akimpokea Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tayari kwa kuhudhuria Mkutano wa 17 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika Ikulu,  Jijini Dar es Salaam tarehe 8/09/2017
Rais Museveni akisalimiana na Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Mhe. Simon Sirro mara baada ya kuwasili nchini.
Rais Museveni akipita kwenye Gwaride la heshima lililoandaliwa kwa mapokezi yake

Wednesday, September 7, 2016

Waziri Mahiga azungumza na Vyombo vya Habari kuhusu Mkutano wa dharura wa EAC

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Dkt Augustine Mahiga (Mb) akiongea katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 7 Septemba, 2016.
Katika Mkutano huo Mhe. Mahiga aliwaarifu waandishi kuhusu Mkutano wa 17 wa Dharura wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaotarajiwa kufanyika tarehe 08 Septemba , 2016, Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na nchi wanachama wote wa Jumuiya hiyo.
Sehemu ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano.
Sehemu nyingine ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano.






TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mkutano wa 17 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kufanyika Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameitisha Mkutano wa 17 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi Wanachama Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) utakaofanyika Ikulu, Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Septemba, 2016.

Mkutano huo ambao ulitanguliwa na vikao vya maandalizi vya Makatibu Wakuu na Mawaziri vilivyofanyika Jijini Arusha utajadili agenda kuu nne ambazo ni:- Mahusiano ya kibiashara na uwekezaji kati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Umoja wa Ulaya (EU) kupitia Mkataba wa Ushirikiano wa Kibiashara (EPA).

Agenda zingine ni Kupokea Taarifa ya Mwezeshaji wa mazungumzo ya Amani nchini Burundi, Mhe. Benjamin William Mkapa, Rais Mstaafu wa Tanzania; Kupata taarifa ya hatua za kukamilisha uanachama wa Sudan Kusini kwenye EAC; na
Kuapishwa kwa Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Rwanda.

Akizungumzia mkutano huo kwa Waandishi wa Habari, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga amesema kuwa mkutano huu umeitishwa kwa dharura ili kuzungumzia agenda hizo muhimu hususan ile ya nchi wanachama kukubaliana kwa pamoja kusaini au kutosaini Mkataba wa EPA ifikapo tarehe 1 Oktoba, 2016.

Kuhusu Mkataba wa EPA, Mhe. Waziri Mahiga alisema kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ilianza mazungumzo na Jumuiya ya Ulaya ya kushirikiana kibiashara kupitia EPA miaka 14 iliyopita na kuingia makubaliano ya awali mwaka 2014. Alieleza kuwa kwa mujibu wa makubaliano hayo ya awali EU na EAC zilikubaliana Mkataba huo usainiwe kwa pamoja na nchi zote za Jumuiyamwezi Julai 2016 kabla ya kuanza utekelezaji wake. 

Hata hivyo Tanzania ilitangaza kutosaini makubaliano hayo kwa sababu mkataba huo unaweza kukwamisha juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano ya kuifanya Tanzania nchi ya Viwanda na Uchumi wa kati ifikapo 2025.
Aidha, Tanzania inahitaji kujadiliana zaidi na nchi wanachama ili kujiridhisha kuwa mkataba huo hautoathiri Mkataba ulioanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki hususan hatua ya mwanzo ya mkataba ambayo ni Umoja wa Forodha. 

Kuhusu nchi nyingine wanachama Mhe. Mahiga alieleza kwamba, tayari Kenya na Rwanda zimesaini mkataba huo huku Uganda ikisubiri majadiliano ya nchi wanachama kabla ya kusaini na Burundi ikijitoa kusaini mkataba huo kwa vile tayari nchi za Ulaya zimeiwekea vikwazo vya kiuchumi.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam, 07 Septemba 2016.

Tuesday, September 6, 2016

Kamati ya Sheria na Kinga ya Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki yakusanya Maoni ya Wadau, Dar es Salaam

Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Sheria na Kinga ya Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe mara baada ya mkutano wa kukusanya maoni ya wadau kuhusu  Mswada wa Sheria ya kuzuia usafirishaji haramu wa Binadamu.
Mbunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki na Mjumbe wa Kamati ya Kinga na Sheria, Mhe. Maryam Ussi (katikati) akizungumza na wadau (hawapo pichani), kushoto ni Mhe. Twaha Taslima,  Mbunge na Mjumbe wa Kamati hiyo na Kulia ni Bw. Ashery Wimile Karani Mwandamizi EALA
Mkurugenzi Msaidizi wa Siasa, Ulinzi na Usalama, Bw. Amani Mwatonoka (Wa kwanza kulia) akichangia hoja kwenye mjadala uliokuwa ukiendelea. 
Mdau akichangia jambo

Monday, September 5, 2016

Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati akutana kwa mazungumzo na Kaimu Balozi wa S. Arabia nchini

Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Abdallah Kilima (kulia) akisalimiana na Kaimu Balozi wa Saudi Arabia nchini, Bw. Bandau Abdullah Al hazani. Kaimu Balozi huyo alikuja Wizarani kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia.
Balozi Kilima akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Kaimu Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania.
Mazungumzo yakiendelea

Saturday, September 3, 2016

Waziri Mahiga aongoza Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi ya SADC

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE, USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
Coat of Arms
Simu: 255-22-2114615, 211906-12 
Barua pepe: nje@nje.go.tz
Barua pepe: gcu@nje.go.tz

Nukushi: 255-22-2116600

               

                20 KIVUKONI FRONT,
                           P.O. BOX 9000,
                  11466 DAR ES SALAAM,  
                                    Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Waziri Mahiga aongoza Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi ya SADC -Uchaguzi wa Jamhuri ya Shelisheli

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine P. Mahiga (Mb.), jana tarehe 2 Septemba, amezindua Misheni ya Waangalizi wa Uchaguzi wa SADC kwenye uchaguzi wa Jamhuri ya Shelisheli kwa niaba ya Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa  Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika -SADC Organ.
Misheni hiyo ya waangalizi wa uchaguzi  itakayojumuisha waangalizi kutoka nchi za SADC, itashiriki kwenye uangalizi katika vituo vyote 25 vya upigaji kura nchini Shelisheli. Pamoja na kuongoza misheni hiyo, Tanzania kama Mwenyekiti wa SADC Organ itaongoza timu za uandishi wa taarifa ya SADC pamoja na ufuatiliaji wa taarifa za vyombo vya habari kuhusu mwenendo mzima wa uchaguzi nchini humo unaotarajiwa kufanyika tarehe 8-10 Septemba, 2016.
Tanzania ilikabidhiwa nafasi ya uenyekiti wa kuongoza asasi hii muhimu ya Jumuiya, wakati wa Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali uliofanyika huko Mbabane, Swaziland tarehe 29 – 31 Agosti, 2016. Mara baada ya kukamilika kwa Mkutano huo, Mhe.  Dkt. Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alielekea Jamhuri ya Shelisheli kumwakilisha Mhe. Dkt. Magufuli, katika kuongoza ujumbe wa Waangalizi wa SADC.
Wajibu wa Tanzania kuongoza Misheni hya Waangalizi wa Uchaguzi imetokana na misingi na muongozo wa Jumuiya ya SADC ya kuwa na chaguzi za kidemokrasia katika nchi wanachama wa Jumuiya hiyo ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika.
Waziri Mahiga anatarajiwa kutoa taarifa ya awali ya Misheni hiyo ya waangalizi  wa SADC Septemba 12, 2016.
Mwisho



Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki.



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akifungua Misheni ya timu ya Uangalizi wa Uchaguzi wa Wabunge tarehe 2 Septemba, 2016 Mahe-Shelisheli. Mheshimiwa Waziri anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, ambaye ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika picha ya pamoja na Misheni ya timu ya Uangalizi wa Uchaguzi wa Wabunge tarehe 2 Septemba, 2016 huko Mahe-Shelisheli.