Wednesday, October 5, 2016

Naibu Waziri akutana na Wabunge wa Tanzania Bunge la Afrika Mashariki

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba akizungumza wakati wa kikao cha pamoja kati ya Uongozi wa Wizara na Wabunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki (hawapo pichani) walipofika Wizarani kwa ajili ya kujadili suala la EPA na masuala mbalimbali yenye maslahi kwa Tanzania yanayoendelea katika Bunge hilo.
Baadhi ya Wabunge hao wakimsikiliza Mhe. Kolimba (hayupo pichani). Kutoka kulia ni Mhe. Shy-Rose Bhanji (Mb.), Mhe. Abdallah Mwinyi (Mb.) na Mratibu kutoka EALA.
Sehemu ya Wajumbe kutoka Wizarani waliohudhuria kikao hicho. Kushoto ni Bw. Stephen Mbundi, Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Bw. Joachim Otaru, Mkurugenzi Msaidizi.
Mhe. Shy-Rose Bhanji akizungumza jambo wakati wa kikao hicho
Mhe. Naibu Waziri kwa pamoja na Waheshimiwa Wabunge hao wakifuatilia mada zilizowasilishwa wakati wa kikao hicho
Wabunge wakifuatilia uwasilishwaji wa mada. Kushoto ni Mhe. Angela Kizigha
Mhe. Kolimba (kushoto) pamoja na Wakurugenzi wa Wizara. Kutoka kulia ni Bw. Oswald Kiamani, Mkurugenzi Msaidizi, Sera na Mipango, Balozi Baraka Luvanda, Mkurugenzi wa Sheria na Bw. Bernard Haule, Kaimu Mkurugezni wa Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji.
Maafisa walioshiriki kikao hicho.

Rais Kabila aweka Jiwe la Msingi la Jengo la Bandari ya Dar es Salaam nchini Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mhe. Joseph Kabila Kabange akikata utepe pamoja na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli (wa kwanza kulia), na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Pro. Makame Mbarawa (wa kwanza kulia) wakati wa kuweka jiwe la msingi katika Jengo la Mamlaka ya Bandari lililopo nchini Jijini Dar es Salaam. Mhe. Magufuli amatumia nafasi hiyo kumuhakikishia Mhe. Kabila kuwa wafanyabiashara kutoka Congo hawatopata matatizo kwa kutumia Bandari ya Dar es Salaam, kwa kuwa Serikali imerekebisha mapungufu yaliyokuwepo kipindi cha nyuma.
Rais Kabila na Dkt. Magufuli pamoja na Prof. Mbarawa wakifurahia kwa pamoja kwa kupiga makofi mara baada ya kumaliza uwekaji wa Jiwe la msingi la Jengo la Mamlaka ya Bandari Jijini Dar es Salaam
Marais wakiangalia michoro ya jengo jipya la Mamlaka ya Bandari
Mhe. Kabila pamoja na Mwenyeji wake Rais Magufuli wakipata maelezo juu michoro ya Ghorofa hilo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu Mhandisi, Deusdedit Kakoko (aliyeshikilia kipaza sauti).


Rais Kabila akipokea zawadi inayoonesha mwonekano wa Bandari ya Dar es Salaam 
Viongozi mbalimbali wa Serikalini wakishuhudia tukio la hilo la uwekwaji wa Jiwe la Msingi wa Jengo la Mamlaka ya Bandari. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Aziz Mlima.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo Mhe. Joseph Kabila Kabange pamoja na viongozi mbalimbali alioongozana nao. 

Tuesday, October 4, 2016

Rais Dkt. Magufuli akutana na Rais Kabila Ikulu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mhe. Joseph Kabila. Mazungumzo hayo yalifanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Oktoba, 2016. Mhe. Rais Kabila yupo nchini kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu.
Mhe. Rais Magufuli akipeana mkono na Rais Kabila mara baada ya mazungumzo kati yao
Mhe. Rais Magufuli akizungumza na Waandishi wa  Habari (hawapo pichani) kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano waliyokubaliana na Rais Kabila.
Mhe. Rais Kabila naye akizungumza na Wanahabari na Wageni waaalikwa
Wakuu wa Vyombo vya Usalama nchini wakifuatilia mkutano Ikulu
Balozi wa DRC nchini, Mhe. Jean Pierre Mutamba (kushoto) na wageni wengine waalikwa wakiwa Ikulu
Rais John Pombe Magufuli na Rais Joseph Kabila wakishuhudia uwekwaji saini wa Makubaliano kati ya Tanzania na DRC kuhusu Utafiti na Uendelezaji wa Utafiti wa Mafuta katika Ukanda wa Ziwa Tanganyika.
Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Mhongo na Mwenzake wa DRC wakibadilishana Mkataba huo wa Makubaliano mara baada ya kuusaini
Mazungumzo rasmi
Mhe. Rais Magufuli akimpatia Rais Kabila zawadi ya Kinyago mashuhuri cha Umoja kinachoonesha Umoja na Mshikamano wa Watanzania.
Rais Kabila naye akimpatia Rais Magufuli zawadi
Picha ya pamoja
Rais Kabila akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga
Rais Kabila akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, . Dkt. Aziz Mlima
Rais Kabila akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samwel Shelukindo
Mhe. Rais Magufuli akiwa ameongozana na mgeni wake Mhe. Rais Kabila alipompokea Ikulu

Makamu wa Rais wa Cuba ahitimisha ziara yake nchini

Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Salvador Valdes Mesa akipungia wananchi wa Zanzibar waliojitokeza kumuaga katika uwanja wa ndege wa Abeid Aman Karume, Zanzibar. Mhe. Mesa aliondoka Zanzibar mapema leo asubuhi na kuwasili Dar es Salaam  ambapo alielekea Kibaha kutembelea mradi unaofadhiliwa na Cuba  nchini wa kuzalisha dawa za kuua viluwiluwi wa mbu wanaoeneza Malaria.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ameambatana na Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Salvador Valdes Mesa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakati akiondoka nchini baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku tatu.

Makamu wa Rais wa Cuba atembelea Kiwanda cha Dawa za Mbu kilichopo Kibaha

Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Salvador Valdes Mesa akisalimiana na Dkt. Samuel Nyantahe,  Mwenyekiti wa Bodi ya Kiwanda cha Dawa za Kuua Viluwiluwi wa Mbu kilichopo Kibaha, Pwani mara baada ya kuwasili Kiwandani hapo kwa ajili ya kukitembelea. Katikati yao ni Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu.
Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Bw. Mkucha akitoa taarifa fupi kuhusu Kiwanda hicho ambapo alisema kitaanza uzalishaji mwezi Oktoba, 2016 na tayari kimeajiri watu 126. Kiwanda hicho ambacho kimejengwa kwa ushirikiano wa Tanzania na Cuba kina uwezo wa kuzalisha lita milioni 6 za dawa ambazo zitatosheleza matumizi ya Tanzania na nchi nyingine jirani.
Sehemu ya Wananchi na Wageni waalikwa waliohudhuria tukio hilo
Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Salvador Valdes Mesa akizungumza kuhusu umuhimu wa Kiwanda hicho katika kupambana na malaria na kwamba Serikali ya Cuba itaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali ya Tanzania katika kupambana na ugonjwa huo.
Mhe. Mesa akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa Viongozi wa Wataalam kutoka Cuba wanaofanya kazi Kiwandani hapo
Mtaalam mwingine kutoka Cuba akitoa maelezo ya namna maabara kiwandani hapo zinavyofanya kazi
Mhe. Mesa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali na Wataalam wanaofanya kazi kiwandani hapo
Mhe. Mesa akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Kiwanda hicho.



Monday, October 3, 2016

Makamu wa Rais wa Cuba awasili Zanzibar

Makamu wa Rais wa Cuba Mhe. Salvador Valdes Mesa akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Abed Aman Karume, Zanzibar. Mhe. Mesa alipokelewa na Makamu wa Rais wa Pili Mhe. Balozi Seif Ali Iddi. Mhe. Mesa anatarajia kuondoka Zanziba tarehe 4 Oktoba, 2016. 
Mhe. Mesa akikagua gwaride maalum mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Abed Aman Karume Zanzibar


Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein (kulia) akiwa katika mazungumzo na Mhe. Mesa (kushoto) alipomtembelea Ikulu Zanzibar
Rais Mhe.Dkt. Shein akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali na ujumbe wa Mhe. Mesa
Mazunguzo yakiendelea Ofisini kwa Makamu wa Rais wa Pili  wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi.
Makamu wa Rais wa Pili  wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika picha ya pamoja
Makamu wa Rais wa Pili  wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akiaagana na  Mhe. Nyusi mara baada ya mazungumzo.
Naibu wa Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Susan Kolimba (wapili kulia) akifuatilia mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea kati ya Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais wa Cuba Mhe. Mesa (hawako pichani)  


Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika  Balozi Joseph Sokoine akifuatilia mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea kati ya Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais wa Cuba Mhe. Mesa (hawako pichani)


Sunday, October 2, 2016

Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Salvador Valdes Mesa awasili Nchini


Makamu wa Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpokea Makamu wa Rais wa Cuba Mhe. Salvador Valdes Mesa mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Mhe. Mesa atakuwa Nchini kwa ziara ya siku tatu kuanzia tarehe 2- 4 Oktoba, 2016.

Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Mesa akipokea ua kutoka kwa mtoto Atkah Omary mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.