Tuesday, June 20, 2017

Balozi Migiro amtunuku kijana aliyeshinda shindano la kimataifa la kugiga picha.


Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Asha-Rose Migiro (kulia) akimvisha begi ya bendera ya Taifa kijana wa miaka 18 Samwel Mwanyika, aliyeshinda shindano la kimataifa la kupiga picha kwa vijana wenye utindio wa Ubongo maarufu kama "The Stephen Thomas Awards" lililofanyika mapema wiki hii Jijini London, Uingereza.

Kijana Samwel Mwanyika akiwa ameshika picha iliyompa ushindi katika shindano la Tuzo za Stephen Thomas, mara baada ya kuwasili katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza, kwaajili ya hafla iliyoandaliwa na Mhe. Balozi Migiro kwa lengo la kumpongeza kijana huyo ambaye aliweza kuibuka mshindi miongoni mwa vijana wengi walioshindanishwa.
Mhe. Migiro akizungumza na Mony Teri Petitte mwasisi wa Taasisi inayohudumia watu wenye mtindio wa Ubongo “Pearl of People with Down Syndrome” anayejitolea kuendesha Jumuiya ya Watanzania wenye matatizo ya ubongo sambamba na kuratibu tuzo ya Stephen Thomas.

Picha ya pamoja kutoka kulia Mhe. Balozi Migiro, kijana Samweli ambaye aliambatana na rafiki yake Penina Haika Petitte na  Mkuu wa  Utawala wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza Bi.  Rose Kitandula.

Monday, June 19, 2017

Balozi wa Tanzania nchini Israel awasilisha Hati za Utambulisho

Balozi wa Tanzania nchini Israel, Mhe. Job Masima (kulia) akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Taifa la Israel, Mhe. Reuven Rivlin  Ikulu ya nchi hiyo mjini Jerusalem 
Balozi wa Tanzania nchini Israel, Mhe. Job Masima akikaribishwa rasmi kwa toast baada ya kuwasilisha salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  pamoja na kusoma salamu maalumu za mwanzo wa urafiki mpya wa ushirikiano wa karibu kwa ki-Hebrew baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Taifa la Israel, Mhe. Reuven Rivlin  Ikulu ya nchi hiyo mjini Jerusalem.


Akiwa amevaa baragashia ya kitamaduni ya Kiyahudi maarufu kama "Kippah" Balozi wa Tanzania nchini Israel, Mhe. Job Masima akiwasilisha salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Thursday, June 15, 2017

Balozi wa Sweden atembelea Wizara ya Mambo ya Nje

 Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga (Kulia)akiwa  katika mazungumzo na Balozi wa Sweden Nchini Mhe. Katarina Rangnitt katika ukumbi wa mikutano wa Wizara Juni 14,2017. Katika mkutano huo walijadiliana masuala mbalimbali kuhusu ushirikiano wa Tanzania na Sweden pamoja na hali ya usalama nchini Burundi.
Mheshimiwa Waziri Mahiga, Balozi wa Sweden nchini pamoja na Wataalam kutoka Wizarani wakiwa katika mkutano huo,

Mwakilishi Mkaazi wa UNIDO awasilisha Hati za Utambulisho

 Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mwakilishi Mkaazi wa UNIDO nchini, Bw.Stephen Bainous Kargbo, Juni 14,2017, katika ukumbi wa Mikutano Wizarani. 
 Mhe. Waziri Balozi Augustine Mahiga (Katikati), Mwakilishi Mkaazi wa UNIDO, Bw. Stephen Bainous Kargbo (Kushoto) na kulia ni Balozi Grace Martin, Mkurugenzi Idara ya Itifaki wakiwa katika mazungumzo.

Mhe. Waziri Balozi Mahiga, Mwakilishi Mkaazi wa UNIDO na Wataalam kutoka Wizarani na Ofisi za UNIDO wakiwa katika picha ya pamoja baada ya makabidhiano ya Hati za Utambulisho..


Wizara ya Mambo ya Nje yapokea mashine ya kutengeneza vitambulisho

Mkuu wa Kitengo cha Usajili wa Taasisi ya United Nation Mechanism for International Criminal Tribunal (MICT), iliyorithi shughuli za Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda, Bw. Samuel Akorimo (kulia) akiwa katika harakati za kukabidhi mashine ya kutengeneza vitambulisho iliyotolewa na taasisi hiyo kwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wengine katika picha watatu kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Ramadhan Mwiny; wakwanza kushoto ni Mkuu wa Itifaki, Balozi Grace Martin na Mtaalamu wa Sheria wa MICT, Bi. Tully Mwaipopo.

Balozi Ramadhan Mwinyi (kushoto) akipeana mkono na Bw. Akiromo mara baada ya kupokea mashine ya kutengeneza vitambulisho

Picha ya pamoja, kutoka kulia ni Bi. Angela Ngaillo, Afisa kutoka Idara ya Itifaki, Bw. Akiromo kutoka MICT Arusha, Bi. Tully Mwaipopo kutoka MICT, Balozi Ramadhan Mwinyi na Balozi Grace Martin.

TANGAZO KWA UMMA

TAARIFA KUHUSU KUTHIBITISHA VYETI


Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuufahamisha Umma ya kwamba, wale wote wanaohitaji na watakaohitaji kupata huduma ya kuthibitisha vyeti na nyaraka mbalimbali kama ifuatavyo:

(1)  KuanziaTarehe 01/07/2017 malipo yote ya huduma ya kuthibitisha vyeti/nyaraka yatafanyika kwa njia ya benki, kupitia akaunti namba 0150275408200, Foreign Collection Account, CRDB Bank na hati ya malipo ya benki iwasilishwe wizarani kuthibitisha malipo hayo.

(2)  Wizara haitapokea pesa taslimu kama ilivyokuwa inafanyika hapo awali bali hati ya malipo kutoka benki.Kila nakala itakayothibitishwa na kugongwa muhuri italipiwa kiasi cha Shillingi Elfu Kumi na Tano tu (TSHS 15,000/=) benki.

(3)  Vyeti vyote vinavyoletwa Wizarani kwa ajili ya kuthibitishwa, havinabudi kupelekwa kwanza katika Taasisi zilizotoa vyeti/nyaraka hizo ili vihakikiwe na kuthibitshwa.

(4)  Baada ya kutekeleza maelekezo katikak ifungu cha tatu (3) hapo juu, Mteja anatakiwa kuandika barua kwa Katibu Mkuu,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiomba nyaraka hizo zithibitishwe na kueleza matumizi tarajiwa ya nyaraka hizo nje ya nchi. Aidha, barua hiyo iambatishwe na nakala (copies) za nyaraka zilizothibitishwa na Taasisi husika.

(5)  WATEJA WOTE WANAOMBWA KUZINGATIA RAI KWAMBA HUDUMA HIZI ZITAKUWA ZINATOLEWA SIKU YA JUMANNE NA ALHAMISI TU, KUANZIA SAA 3.00 - 5.00 ASUBUHI.

Imetolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

PUBLIC ANNOUNCEMENT


PUBLIC ANNOUNCEMENT

The Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation of the United Republic of Tanzania wishes to inform the General Public in need of Certificationof Documents to be used outside the country, that;

(1)From 1stJuly, 2017 all payments for Certification of Documents shall be made via CRDB bank account number0150275408200, Foreign Collection Account and the bank slip be submitted to the Ministry.

(2)It is stressed that, no cash payment will be accepted at the Ministry as per the previous practice except bank payment slip. Cost for certification remains unchanged,Tanzania Shillings Fifteen Thousands only (Tshs.15, 000/=) per copy.

(3)Before any document is brought to the Ministry for certification, it has to be first verified by the issuing authority for authentication.

(4)After complying with the directive provided under clause three (3) herein above, the applicant must write a letter to the Permanent Secretary, Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation requesting for certification of the documents. The said letter must be accompanied with copies of all the documents to be certified after being firstly verified by the issuing authority.

(5) IT IS REMINDED THAT, DOCUMENTS CERTIFICATION SERVICE IS AVAILABLE ONLY ON TUESDAY AND THURSDAY FROM 0900HRS TO 1100HRS.

ISSUED BY MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS

 AND EAST AFRICAN COOPERATION