Tuesday, December 12, 2017

Waziri Mahiga awaasa Wabunge Wateule wa Tanzania kwenye Bunge la nne (4) la Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa Wazalendo na kusimamia maslahi ya Jumuiya.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga(katikati) akiongea katika kikao cha uongozi wa Wizara hiyo na Wabunge Wateule wa Tanzania kwenye Bunge la nne (4) la Jumuiya ya Afrika Mashariki, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, tarehe 12 Disemba 2017. Pembeni yake kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba na kulia ni Mwenyekiti wa Wabunge wateule wa Bunge la Afika Mashariki, Mhe. Abdullah Makame.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda (kulia) akiongea katika kikao hicho ambapo aliwakaribisha Waheshimiwa Wabunge wateule pamoja na kuwaeleza kuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ipo tayari kuwapa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yao. Pembeni yake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi.

Mwenyekiti wa Wabunge Wateule wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe.Dkt. Abdullah Makame akiushukuru uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kikao kizuri cha utangulizi kabla ya kuanza kwa Bunge hilo na pia akaahidi kuwa wataenda kuliwakilisha Taifa vizuri sambamba na kusimamia maslahi ya Jumuiya kwa maendeleo na ustawi wa wananchi wake.

Sehemu ya Waheshimiwa Wabunge Wateule wa Bunge la Afrika Mashariki wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yakitolewa na Mhe. Waziri Mahiga (hayupo pichani)

Sehemu nyingine ya Waheshimiwa Wabunge wakifuatilia kikao hicho.
Wakurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia kikao hicho. Kutoka kulia  Bw. Eliabi Chodota, Bw. Bernard Haule na Bw.Joachim Otaru.



Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Stephen Mbundi akitoa ufafanuzi kuhusiana na taratibu na miongozo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Waheshima Wabunge Wateule. 

Mhe. Waziri na  Naibu Waziri  wakiwa katika picha ya pamoja na Wabunge Wateule wa Tanzania kwenye Bunge la nne la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Picha ya pamoja uongozi wa Wizara  na Wabunge Wateule wa Tanzania kwenye Bunge la nne la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Sunday, December 10, 2017

Spika wa Bunge la Morocco atembelea Tanzania

 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Job Ndugai akimkaribisha Spika wa Bunge la Morocco Mhe. Habib El Malki nyumbani kwake Mjini Dodoma, tarehe 9/12/2017

Mhe.Habib El Malki (wa kwanza kulia)-Spika wa Bunge la Morocco, Mhe. Job Ndugai- Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Zubeir Ali Maulid - Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Dkt. Suzan Kolimba Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Pamoja na wajumbe wengine kutoka Ofisi ya Bunge na Ujumbe wa Morocco ulioambatana na Spika wa Morocco wakiwa katika mazungumzo Bungeni Dodoma, tarehe 9/12/2017.

Katika mazungumzo hayo Mhe.El Malk alitoa mwaliko kwa Mhe. Ndugai na Mhe. Ali Maulid, Mhe. El Malki alisema amefurahishwa sana na jinsi alivyopokelewa na kwa umaalum zaidi alimshukuru Mhe. Rais kwa kumpa heshima ya kipekee kwa kumtambulisha kwa Umma wa Watanzania wakati wa sherehe za maadhimisho ya Uhuru. Mhe. El Malki alisema Morocco ina mengi ya kujifunza kwa Tanzania hasa katika eneo la Demokrasia "nimeshangazwa sana kuona Marais Waastafu wanakaa pamoja na kuunga mkono Rais aliye madarakani, hili ni jambo tunalopaswa kuiga hasa kwa nchi za Afrika, tumezoea kuiga mambo mengi kutoka nchi za Magharibi na kudharau mambo mazuri ambayo yako kati yetu" alisema Mhe. El Malki.

Mhe. Ndugai akimweleza jambo Mhe. El Malki alipomtembeza kwenye ukumbi wa Bunge, wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Suzan Kolimba na anayefuatia ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar 


Wakiwa katika picha ya Pamoja baada ya Mazungumzo, tarehe 9/12/2017
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Balozi Dkt Augustine Mahiga akiwa katika mazungumzo na Spika wa Bunge la Morocco Mhe. Habib El Malki, anayefuatilia mazungumzo hayo ni Balozi wa Morocco nchini Mhe. Mhe. Abdelilah Benryane katika ukumbi wa VIP wa Uwanja wa ndege Dodoma, tarehe 9/12/2017. 

Katika mazungumzo yao Mhe.  El Malki na Mhe. Waziri walizungumzia masuala mbalimbali ya kudumisha na kukuza ushirikiano wa kidiplomasia,uchumi na utalii.
                                         
Mhe. Waziri Balozi Dkt. Augustine Mahiga, akimuaga  Mhe. Spika wa Morocco katika uwanja wa ndege wa Dodoma, tarehe 9/12/2017. Kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika NMashariki, Mhe. Dkt Suzan Kolimba na anayefuata ni Katibu Mkuu Prof. Aldof Mkenda

Sherehe za Maadhimisho ya siku ya Uhuru

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akikagua gwaride wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Tanganyika tarehe 9/12/2017. Maadhimisho hayo yalifanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akimtambulisha Spika wa Bunge la Morocco Mhe. Habib El Malki katika maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Tanganyika tarehe 9/12/2017. Kulia kwake ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa. Mhe. Rais alisema Spika ametumwa na Mfalme Mohamed VI wa Morocco kuja kuangalia sehemu ambayo utajengwa Uwanja Mkubwa na wa Kisasa wa mpira Dodoma, hii ikiwa ni kati ya ahadi zilizotolewa na Mfalme MohamedVI alipotembelea Tanzania Oktoba,2016. 



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt Augustine Mahiga(wa tatu mbele), anayefuata ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dkt Suzan Kolimba pamoja na Mawaziri na Viongozi mbalimbali wa Serikali wakifuatilia sherehe za maadhimisho ya Uhuru wa Tanganyika  zilizofanyika Uwanja wa Jamhuri Dodoma, tarehe 9/11/2017



Thursday, December 7, 2017

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa afanya uzinduzi wa ofisi za Umoja wa Mataifa mkoani Dodoma

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa  akihutubia katika sherehe za uzinduzi wa majengo ya ofisi za mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini zilizofanyika mkoani Dodoma tarehe 7 Disemba 2017.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akihutubia katika sherehe za uzinduzi wa ofisi za mashirika ya Umoja wa Mataifa zilizofanyika mkoani Dodoma tarehe 7 Disemba 2018.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez akihutubia kwa lugha ya kiswahili katika sherehe za uzinduzi wa Ofisi za mashirika ya Umoja wa Mataifa mkoani Dodoma tarehe 7 Disemba 2017.


==============================================

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amezindua rasmi Ofisi za Umoja wa Mataifa, mkoani Dodoma tarehe 7 Disemba 2017. 

Ofisi hiyo ambayo ipo katika Mtaa wa Mlimwa, Area D, nje kidogo ya Mji wa Dodoma, itakuwa na Ofisi za Mashirika saba (7) kati ya 23 ya Umoja wa Mataifa yanayofanya kazi nchini Tanzania hivi sasa. Mashirika hayo ni pamoja na UNICEF, UNDP, UNFPA, UN Women, IOM, FAO na WHO.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Balozi Dkt. Augustine Mahiga, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bw. Jabir Shekimweri, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Bw. Alvaro Rodriguez, Mwakilishi wa Nchi wa UNICEF, Bi. Maniza Zaman, Maofisa wa Serikali na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa.

Akizindua Ofisi hiyo Mhe. Waziri Mkuu aliwapongeza Umoja wa Mataifa kwa hatua yao ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano(5) ya kuhamishia Makao makuu ya nchi mjini Dodoma “Serikali ya awamu ya tano(5) iliazimia kuunga mkono kwa vitendo tamko la Baba wa Taifa la Mwaka 1973 la kuifanya Dodoma kuwa Makao Makuu ya nchi". alisema.

Aidha, alifafanua kuwa hadi sasa Waziri Mkuu, Mawaziri, watendaji wa Serikali na watumishi wa umma zaidi ya 2000 wamehamia Dodoma na mwisho wa Mwezi huu Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuhamia Dodoma na Mheshimiwa Rais anatarajiwa kuhamia Dodoma mapema mwakani. 

Halikadharika, Waziri Mkuu ameyahakikishia Mashirika ya Kimataifa kuwa Serikali imeandaa utaratibu mzuri wa kuhakikisha mashirika hayo pamoja na ofisi za ubalozi zinazowakilisha nchini zinapata viwanja kwa ajili ya kujenga ofisi na makazi mkoani Dodoma.

Akizungumza katika uzinduzi huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Mb), alisema "Umoja wa Mataifa umeonesha dira na kuwa nyota kwa Mashirika mengine ya Kimataifa na Balozi mbalimbali zinazowakilisha hapa nchini kwa kufungua ofisi zao hapa Dodoma".

Vilevile Mhe. Waziri Mahiga alielezea mchango wa Tanzania kwa kushiriki katika mchakato wa maboresho ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa ili yaweze kufanya kazi kwa Pamoja, pia  alifafanua kuwa Tanzania na Ireland ndio walipewa jukumu la kukusanya maoni na kuja na andiko la kuboresha utendaji kazi wa Masharika ya Umoja wa Mataifa na andiko hilo ndilo lilozaa “United Nation delivering as One”, na kwa sasa utaratibu huu unatoa fursa ya mashirika ya Umoja wa Mataifa kutoa huduma zao katika jengo moja.

Kwa upande mwingine, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Bw. Rodriguez, alisema, “ Uzinduzi wa Ofisi hii utawezesha kukuza ushirikiano wa Umoja wa Mataifa na Serikali hasa katika kipindi hiki muhimu Serikali inapohamia Dodoma na kwamba mashirika ya Umoja wa Mataifa yamekuwa yakifanya kazi kwa karibu na Serikali"


Malengo ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa tangu miaka 72 iliyopita ni pamoja na kusimamia na kuleta maelewano baina ya nchi na nchi,kuhamasisha na kuleta maendeleo hasa kwa nchi zinazoendelea, kulinda, kuleta heshima kwa watu wote hasa kwa watu wanaonyanyaswa na wale wa makundi maalum na kusimamia na kulinda haki za binadamu ikiwemo haki ya kujitawala. Umoja wa Mataifa  una jumla ya Mashirika 50 Duniani na hapa Tanzania inawakilishwa na jumla ya Mashirika 23.

Mhe.Waziri Mkuu akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa majengo ya ofisi za mashirika ya Umoja wa Mataifa mkoani Dodoma. Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bw.Jabir Shekimweri, Mhe. Waziri Mahiga na wengine ni wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini.
Bw. Alvaro Rodriguez akikabidhi zawadi ya ngao kwa Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.



Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Dodoma wakitumbuiza katika sherehe za uzinduzi wa ofisi za Mashirika ya Umoja wa Mataifa Mkoani Dodoma.

Vikundi vya ngoma vikitumbuiza.

Picha ya pamoja meza kuu pamoja na wawakilishi wa Taasisi za Serikali.
Picha ya pamoja meza kuu pamoja na watumishi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa.



Wednesday, December 6, 2017

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje akutana na Naibu Mkurugenzi wa Kamati ya Mambo ya Nje wa Bunge la China

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba akizungumza na Naibu Mkurugenzi wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la China, Mhe. CAO Weizhou alipofika Wizarani tarehe 06 Desemba, 2017. Katika mazungumzo yao pamoja na mambo mengine walijadili kuhusu kuimarisha ushirikiano wa kindugu uliopo kati ya Tanzania na China. Pia Mhe. Dkt. Kolimba alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya China kwa misaada mbalimbali inayotoa kwa Tanzania hususan katika sekta ya ujenzi wa miundombinu.
Sehemu ya ujumbe uliofuatana na Mhe. CAO Weizhou wakifuatilia mazungumzo. Wa pili kutoka kulia ni Balozi wa China nchini, Mhe. Wang Ke.
Sehemu nyingine ya Ujumbe uliofuatana na Mhe. CAO Weizhou.
Sehemu ya ujumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kutoka kushoto ni Bi. Justa Nyange, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia,  Bw. Charles Faini, Katibu wa Naibu Waziri,  na Bw. Halmesh Lunyumbu, Afisa  Mambo ya Nje 
Mhe. Dkt. Kolimba akiagana na Mhe. CAO mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.
Picha ya pamoja

Waziri Mahiga apokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Nigeria nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Nigeria nchini, Mhe. Dkt. Sahabu Isah Gada. Tukio hilo limefanyika Wizarani tarehe 06 Desemba, 2017.
Mhe. Dkt. Mahiga akionesha Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Gada mara baada ya kuzipokea.
Mhe. Dkt. Mahiga akiwa katika mazungumzo rasmi na Dkt. Gada
Sehemu ya ujumbe kutoka Ubalozi wa Nigeria.
Sehemu ya ujumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ukifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Mahiga na Balozi Gada (hawapo pichani). Kushoto ni Bw. Suleiman Saleh, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika na Bw. Nicholaus Joseph, Afisa Mambo ya Nje.
Mhe. Dkt. Mahiga akiagana na Balozi Mteule wa Nigeria nchini, Mhe. Dkt. Gada mara baada ya kumaliza mazungumzo yao
Mhe. Dkt. Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi Gada na Mkewe mara baada ya kupokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi huyo.

Tuesday, December 5, 2017

Mhe. Waziri afanya mazungumzo na Balozi wa Korea nchini

    Mhe. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Augustine Mahiga (Mb) akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Serikali ya Jamhuri ya Korea nchini Mhe. Balozi Song,Geum-Young, alipomtembelea Wizarani, Dar es Salaam, tarehe 05/12/2017. Mazungumzo hayo yalijikita katika kuimarisha mahusiano kati ya Korea na Tanzania.
 
    Mazungumzo yakieendelea


Mhe. Waziri na Mhe. Balozi wakipeana mkono baada ya mazungumzo

Waziri Mahiga apokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Poland nchini


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Poland, Mhe. Krzysztof Buzalski. Makabidhiano hayo yamefanyika leo katika ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Waziri Mahiga akiongea na Mhe.Buzalski ambapo katika mazungumzo yao amemuhakikishia kumpa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake awapo nchini.


Mazungumzo yakiendelea.

Waziri Mahiga amuaga balozi wa U.A.E aliyemaliza muda wake wa uwakilishi nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiongea na Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu nchini (U.A.E), Mhe Abdulla Ibrahim Alsuwaidi alipomtembelea katika ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 05 Disemba 2017.

Mhe. Abdulla Ibrahim Alsuwaidi amemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini ambapo pamoja na mambo mengine Waziri Mahiga amemshukuru kwa ushirikiano mzuri aliouonyesha alipokuwa nchini. Pia amemtakia safari njema na utekelezaji mwema wa majukumu mapya atakayopangiwa.

Mhe. Abdulla Ibrahimu Alsuwaidi akitoa neno la shukrani kwa Mhe. Waziri Mahiga ambapo alitumia fursa hiyo kutoa shukrani kwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa ujumla kwa kumwezesha kutekeleza vema majukumu yake katika muda wake wote wa uwakilishi hapa nchini. Pia akaahidi U.A.E itaendeleza kudumisha ushirikiano wa kidiplomasia pamoja na ushirikiano katika sekta za miradi ya maendeleo.

Mazungumzo yakiendelea.

Waziri Mahiga akimuga Balozi wa U.A.E aliyemaliza muda wake wa Uwakilishi nchini.

Mhe. Waziri akutana na Ujumbe wa Kamati ya Haki za Wapalestina

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga(Mb) akiongea katika mkutano na Ujumbe wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Msingi za Wapalestina(Committee on the exercise of Inalienable rights of the Palestinian People), kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mwakilishi wa kudumu wa Senegal katika Umoja wa Mataifa, kushoto kwake ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Bw. Deusdedit Kaganda. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam, tarehe 04/12/2017.

Ujumbe huo uliwasili nchini tarehe 02/12/2017, dhumuni la ziara hiyo ni kuendeleza mahusiano ya kisiasa na kidiplomasia kati ya Tanzania na Palestina, pamoja na kutoa elimu ya uelewa kwa jamii ya Watanzania kuhusu hali ya Wapalestina chini ya utawala wa Israel.
 
    Mhe. Waziri akipokea kitabu chenye  kuelezea Historia ya Watu   
  wa  Wapelestina kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati,
   Mhe. Riyad Mansour ambaye pia ni mwangalizi wa kudumu 
   kutoka Umoja wa Mataifa wa hali ya Palestina.

    Mhe. Waziri akiwa na Ujumbe wa Tanzania na Ujumbe wa  
   Kamati wakieendelea na Mazungumzo
   Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Bi. Mindi Kasiga wa  
   kwanza   kushoto, anayefuata ni Bi. Ellen Maduhu kutoka Idara 
   ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Gerald Mbafu Msaidizi wa 
   Waziri na nyuma yao ni waandishi wa Habari wakifuatilia    
  mazungumzo hayo.

   Ujumbe wa Kamati ukifuatilia mazungumzo hayo.

    Mhe. Waziri akizungumza na vyombo vya habari (hawako   
   pichani) baada ya Mkutano.