Friday, March 9, 2018

Katibu Mkuu akutana na Mabalozi wa Afrika waliopo nchini

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda akihutubia kwenye hafla iliyoandaliwa na Umoja wa Mabalozi wa nchi za Afrika nchini Tanzania. Katika hotuba yake Prof. Mkenda aliwashukuru Mabalozi hao kwa kumwalika kwenye hafla hiyo na kuwaahidi kushirikiana nao kwenye shughuli zao za uwakilishi wa mataifa yao hapa nchini.
Balozi wa Misri nchini Mhe. Yasser Ahmed Al Eldin Elshawaf
Balozi wa Algeria nchini, Mhe. Saad Belabeb (kushoto), pamoja na Balozi wa Msumbiji nchini, Mhe. Monica Patricio Clemente wakisikiliza hotuba ya Prof. Mkenda.

Mkurugenzi wa Idara ya Itifaki, Balozi Grace Martin pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hapa nchini, Mhe. Jean Mutamba wakimsikiliza kwa makini Prof. Mkenda hayupo pichani.
Sehemu nyingine ya wageni waalikwa wakifuatilia kwa makini hotuba.

Prof. Mkenda akiendelea kuhutubia kwenye hafla hiyo.
Balozi wa Afrika Kusini akizungumza kama mshereheshaji katika hafla iliyoandaliwa na Umoja wa Mabalozi hao wa Afrika.
Sehemu ya Maafisa kutoka Ofisi mbalimbali za Balozi za Afrika zilizopo nchini.

 


Thursday, March 8, 2018

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan afanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo ya Viwanda (UNIDO), Mh. Li Yong, ambaye yupo nchini kwa ziara ya siku tatu. 
Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage (Mb.)na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb.). Mazungumzo hayo yamefanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam, tarehe 08 Machi,2018.
Mhe. Samia Suluhu akimsikiliza Mhe. Yong wakati wa mazungumzo hayo.
Mazungumzo yakiendelea kati ya Mhe. Suluhu na Mhe. Yong, wa kwanza kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Mwijage akifuatilia mazungumzo hayo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (wa kwanza kushoto), Waziri wa Fedha  na Mipango, Mhe. Philip Mpango (katikati) na  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekaji, Bw. Ludovick J. Nduhiye nao wakifuatilia mazungumzo 
Mwakilishi wa UNIDO nchini  Bw. Stephen Kargbo akifuatilia mazungumzo hayo.
Sehemu ya watumishi wa Serikali wakifuatilia mazungumzo hayo.
Mhe. Samia Suluhu akishuhudia kusainiwa kwa makubaliano ya Mpango shirikishi baina ya nchi, UNIDO na  Washirika wengine wa Maendeleo, wanaosaini Mpango huo kushoto ni Mhe. Waziri  Mwijage na Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO Bw. Li Young. Mpango huo umesainiwa katika ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere, tarehe 08 Machi,2018.
Mhe. Waziri Mwijage na Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO Bw. Li Yong wakibadilishana Makubaliano hayo baada ya kusainiwa.
Mhe. Samia Suluhu na Mhe. Li Yong katika picha ya pamoja na Viongozi kutoka Serikalini pamoja na uongozi kutoka UNIDO.








Mheshimiwa Waziri Mahiga amkaraibisha nchini Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO alipowasili katika hafla ya jioni iliyoandaliwa na mwenyeji wake Waziri Mahiga katika Hotel ya Hyatt Regency, Dar es Salaam, tarehe 07 Machi, 2018. Anayeangalia pembeni yao ni Bw. Stephen Kargbo Mwakilishi wa UNIDO nchini. 

Mheshimiwa Waziri Mahiga akiongea kwenye hafla hiyo
Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO Bw. Li Young (Kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alvaro Rodriguez wakiwa katika hafla hiyo
Mhe. Waziri Mwijage (Kulia) akiwa na Balozi wa China nchini  Mhe.Wang Ke.
Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO Bw. Li Young akiongea katika hafla hiyo
Sehemu ya wageni wakifuatilia hafla hiyo
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Jestas Nyamanga ( wa kwanza Kulia)  na wengine ni Watumishi wa Wizara wakifuatilia hafla.

Bi Ramla Hamisi akitoa utaratibu wa hafla hiyo




Waziri wa Viwanda na Biashara Bw. Charles Mwijage ampokea Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO

Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage (katikati), akimpokea Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO Bw. Li Young, mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Bw. Young ambaye yupo nchini kwa ziara ya siku tatu. 
Bw. Li Young anatarajia kukutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustino Mahiga (Mb.) hayupo pichani, Waziri wa Fedha Mhe. Philip Mpango (Mb.).
Mhe. Mwijage akifurahia jambo na Li Young.


Tuesday, March 6, 2018

Naibu Katibu Mkuu akutana kwa mazungumzo na Balozi wa Uholanzi nchini

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan M. Mwinyi akizungumza na Balozi wa Uholanzi nchini, Mhe. Jeroen Verheul. Katika mazungumzo yao walisisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Uholanzi. Mazungumzo hayo yamefanyika Wizarani tarehe 06 Machi, 2018
Maafisa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ulaya na Amerika wakinukuu mazungumzo. Kutoka kushoto ni Bw. Hassani Mwamweta na Bw. Anthony Mtafya.
Mazungumzo yakiendelea
Balozi Mwinyi akiagana na Balozi Verheul

Monday, March 5, 2018

Serikali ya Tanzania na Palestina zasaini Hati ya Makubaliano kuhusu masuala ya Afya.



 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na watoto, Mhe. Ummy Mwalimu na Balozi wa Palestina nchini Mhe. Balozi Hazem Shabat  wakisaini Hati ya Makubaliano (MOU)  katika eneo la afya. 
Makubaliano hayo yana lengo la kuboresha mahusiano kati ya Tanzania na Palestina, katika Makubaliano hayo nchi ya Palestina wamekubali kuisaidia Tanzania  katika masuala ya afya hasa katika maeneo ya kuimarisha mifumo ya afya, matibabu ya kibingwa ya moyo, mifupa ya fahamu na saratani, kubadilishana wataalam katika matibabu ya kibingwa na uboreshaji wa mifumo ya TEHAMA.  Makubaliano hayo  yamesainiwa tarehe 05 Machi,2018, katika ukumbi wa Wizara ya Afya, Dar es Salaam
                                    
   Mheshimiwa Waziri Ummy na Mhe. Balozi Shabat wakiendelea kusaini Hati  hiyo ya Makubaliano, wanaoshuhudia  kulia ni Wataalam kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Wizara ya Afya na kushoto ni Naibu Balozi kutoka Ubalozi wa Palestine nchini Bw. Derar Ghannam
                                          
Mhe. Waziri Ummy na Mhe. Balozi Shabat wakibadilishana Mikataba ya Makubaliano hayo baada ya kusaini, wanaoshuhudia ni waandishi wa Habari pamoja na Wataalam kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Wizara ya Afya.

Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu akiongea baada ya kusaini Hati ya Makubaliano.


 
                                   





Friday, March 2, 2018

Tanzania yashiriki Mkutano wa Kwanza wa Global Dryland Alliance

Balozi wa Tanzania nchini Qatar, Mhe. Fatma M. Rajab (wa kwanza kulia walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe walioshiriki mkutano wa kikao cha Kwanza cha Wajumbe wa Global Dryland Alliance. Balozi Rajab alimwakilisha  Mhe. Dkt. Charles Tizeba, Waziri wa Kilimo. Mkutano huo ulifanyika kwenye Makao Makuu ya Umoja iliyopo Doha, Qatar hivi karibuni. Umoja huo ambao ulianzishwa rasmi mwaka 2017  unaangalia namna ya kutatua majanga ya njaa yanayosababishwa na ukame, upungufu wa mvua na mabadiliko ya hali ya hewa.
Kikao hicho kilizinduliwa rasmi na mwenyewe wa mkutano huo Mhe. Mohammed bin Abdullah Al Rumaihi Waziri wa Manispa na Mazingira wa Qatar. Na baadae kuendeshwa na Mwenyekiti mpya wa Umoja huo ambae pia ni Waziri wa Kilimo wa Benin.
Balozi Fatma M. Rajab akifuatilia  mkutano wa kikao cha Kwanza cha Wajumbe wa Global Dryland Alliance Tanzania ambapo alimwakilisha, Mhe. Dkt. Charles Tizeba, Waziri wa Kilimo. Mkutano huo umefanyika Kwenye Makao Makuu ya Umoja huo yaliyopo Doha, Qatar. 
Mkutano ukiendelea.
Wajumbe wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutembelea jengo jipya la Makao Makuu ya Global Dryland Alliance mjini Doha.




Ubalozi wa Tanzania, The Hague wawapokea Wanafunzi wa Al Muntazir

Balozi wa Tanzania uliopo The Hague, Uholanzi, Mhe. Irene Kasyanju akizungumza na wanafunzi na walimu kutoka Shule ya Sekondari ya Al Muntazir ya Jijini Dar es Salaam walipomtembelea Ofisi kwake wakati wa ziara yao nchini humo ya kushirki Kongamano la Wanafunzi linalojulikana kama Farel Model United Nations-FAMUN 2018 lililofanyika Mjini Amersfoort, Uholanzi hivi karibuni.
Mhe. Balozi Kasyanju akimpongeza Mwalimu Getrude Mtenga kwa ushiriki na uwakilishi mzuri wa Tanzania katika Kongamano la FAMUN 2018
Mhe. Balozi Kasyanju akimpongeza Bi. Zainab Sumar ambaye ni Mwanafunzi aliyepokea Tuzo ya "Best Delegate Award in ECOSOC at FAMUN 2018".
Mhe. Balozi Kasyanju akiwa kwenye picha ya pamoja na Wanafunzi na Walimu kutoka Shule ya Sekondari ya Al Muntazir waliotembelea Ubalozi hivi karibuni.
========================================================================
WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI YA ALMUNTAZIR WATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA THE HAGUE, UHOLANZI

Ubalozi wa Tanzania, The Hague, Uholanzi umewapokea Wanafunzi 10 na Walimu wawili (2) kutoka Shule ya Sekondari ya Almuntazir ya Jijini Dar es Salaam waliofika nchini Uholanzi kuhudhuria Kongamamo la Wanafunzi, linalojulikana kama Farel Model United Nations –FAMUN 2018, lililofanyika Mjini Amersfoort, Uholanzi hivi karibuni.

Wakiwa nchini Uholanzi, wanafunzi hao Fatima Jiwan, Zeinab Mehboob Pyarali Sumar, Saleha Munavarali Virani, Jeet Kirti Hirwania, Waqaas Mahsen Mahdi, Saloha Said Aboud, Sakina Mohamed Akhtar Walji, Kadhim Mahmood Kara, Zahra Imtiyaz Gulamhussein, Neha Dharmendra Makwana pamoja na walimu; Bibi Getrude Mtenga na Bi. Zainab Muslim Dharsee walipata fursa ya kutembelea Ubalozi wa Tanzania uliopo The Hague Uholanzi.

Kongamano la FAMUN hutoa fursa nzuri kwa wanafunzi wa shule za sekondari kuongeza ujuzi wa kuendesha mijadala kuhusu masuala mbalimbali ya kimataifa yanayoendelea ulimwenguni katika lugha ya Kiingereza, kujenga uwezo katika kufanya tafiti pamoja na kuunda urafiki mpya miongoni mwao. Ushiriki wa wanafunzi hao pia umeitangaza vizuri Tanzania kwenye Kongamano hilo.

PRESS RELEASE





Thursday, March 1, 2018

Waziri Mahiga akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt Augustine Mahiga akimkaribisha Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi Mhe. Alain Aime Nyamitwe alipomtembelea Wizarani, tarehe 1 Machi,2018, Dar es Salaam.

 Mhe. Waziri Mahiga,(Kulia) akizungumza jambo na Mhe. Waziri Nyamitwe katika mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Wizara, Dar es Salaam. Katika mazungumzo hayo pamoja na mambo mengine walizungumzia jinsi ya kuboresha mahusiano kati ya Tanzania na nchi ya Burundi.
Balozi wa Burundi nchini Mhe. Balozi Gervais Abayeho (wa kwanza kushoto), akifuatilia mazungumzo hayo, wengine wanaofuatilia mazungumzo, kutoka kulia  ni , Bw. Suleiman Saleh, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Afrika. Bw. Wilbroad Kayombo na Bw. Erick Ngilangwa, Maafisa Mambo ya Nje,  na mwisho ni Katibu wa Waziri, Bw. Magabilo Murobi wakifuatilia mazungumzo hayo

Waziri Mahiga akiagana na mgeni wake Waziri Nyamitwe  baada ya kumaliza mazungumzo