Friday, May 18, 2018

Balozi Dkt. Possi awasilisha Hati za Utambulisho kwa Baba Mtakatifu Papa Francis

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani ambaye anawakilisha pia na Vatican, Mhe. Dkt. Abdallah Saleh Possi, akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Baba Mtakatifu Papa Francis, Vatican tarehe 17 Mei 2018. 

Kabla ya kuwasilisha Hati za Utambulisho, Balozi Dkt. Possi alipata fursa ya kukutana na viongozi muhimu wa Vatican, wakiwemo Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu Mkuu wa Mambo ya Nchi za Nje na ushirikiano wa kimataifa, Askofu Mkuu Angelo Becciu, Katibu Mkuu Msaidizi wa Vatican.

Mabalozi wengine waliowasilisha Hati za Utambulisho ni pamoja na Balozi Ahmad Naseem Warraich kutoka Pakistan, Balozi Risto Piipponen kutoka Finland, Balozi Lundeg Purevsuren kutoka Mongolia, Balozi RetÅ¡elisitsoe Calvin Masenyetse kutoka Lesotho, Balozi Karsten Vagn Nielsen kutoka Denmark,  na Balozi Sulaiman Mohammed kutoka Ethiopia. 

Baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho, Balozi Dkt. Possi alipata fursa ya kukutana na Jumuiya ya Watanzania wanaoishi Vatican. Katika kikao hicho, Dkt. Possi aliwaeleza Watanzania hao kwamba wana jukumu kubwa la kutumia.nafasi zao kuhakikisha nchi ya Tanzania inadumu katika misingi ya uadilifu, umoja, na amani ambavyo ni misingi muhimu ya maendeleo.

Balozi Dkt. Possi akisalimiana na Katibu Mkuu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin.

Balozi Dkt. Possi na Mama Balozi, Bi. Sada Mshana, katika picha ya pamoja na Baba Mtakatifu Papa Francis. Picha kwa hisani ya Vatican


Thursday, May 17, 2018

Balozi Shiyo afunga mafunzo ya mfumo wa Ufuatiliaji na Taathmini wa SADC

Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Balozi Innocent E. Shiyo (Katikati) akifunga  Warsha ya siku tatu(3) ya Mafunzo ya Mfumo wa Ufuatialiaji na Tathmini wa SADC (SADC Results Based Online Monitoring and Evaluation System), mmoja wa Wakufunzi wa Warsha hiyo kutoka SADC Bi. Lerato Moleko(kulia) na wa mwisho  kushoto ni Bw. Meneja Mradi kutoka GIZ Bw. Robson Chakwama. 

 Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Wizara kwa kushirikiana  na Serikali ya Ujerumani chini ya Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) na Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), yametolewa kwa Maafisa wa Serikali na Taasisi za Umma, tarehe 15 - 17 Mei,2018 katika ukumbi wa Mikutano wa  Mwalimu Nyerere, Jijini Dar es Salaam.
 Hafla hiyo ikiendelea
 Sehemu ya Maafisa kutoka Wizarani wakifuatilia hafla ya kufunga mafunzo hayo
 Sehemu ya Washiriki wakifuatilia hafla ya kufunga mafunzo hayo
 Bi. Felister Rugambwa ambaye alikuwa Mshereheshaji wa shughuli hiyo akitoa utaratibu wa shughuli.
Picha ya Pamoja baada ya shughuli hiyo.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika akutana na Balozi wa Italia nchini

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Jestas Nyamanga akizungumza na Balozi wa Italia nchini, Mhe. Roberto Mengoni alipofika Wizarani kwa mazungumzo kuhusu ushirikiano baina ya Tanzania na Italia.
 Bi. Tunsume Mwangolombe, Afisa Mambo ya Nje akinukuu mazungumzo kati ya Bw. Nyamanga na Balozi Mengoni(hawapo pichani)

PRESS RELEASE-SADC VACANCY ANNOUNCEMENT






PRESS RELEASE

VACANCY ANNOUNCEMENT FROM THE SOUTHERN AFRICA DEVELOPMENT COMMUNITY SECRETARIAT (SADC)

The Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation has received 50 vacant positions from the Southern Africa Development Community Secretariat (SADC) inviting qualified Tanzanians to apply. The vacant positions are open to all 16 member countries.

Interested Tanzanians are required to present their application letters not later than or on 30th May 2018 through the following address:-

Permanent Secretary,
President's Office,
Public Services Management
University of Dodoma,
P.O.Box 670,
40404 DODOMA.

Applicants may also send their application letters through this Email address: - ps@utumishi.go.tz or shiyo27@yahoo.co.uk.  

For further details please visit the following websites: - www.sadc.int or www.utumishi.go.tz or www.foreign.go.tz. We are sending  an attachment of the stated positions with this press release.

NB: The SADC positions are highly competitive. Thus, interested candidates are advised to send their Curriculum Vitae that meets regional and international standards.

Issued by:
Government Communication Unit,
 Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation,
Dar es Salaam.
17th May 2018

=========================================================



Wednesday, May 16, 2018

THE COMMONWEALTH SECRETARIAT-NOTIFICATION OF VACANCY





Kaimu Mkurugenzi wa Ulaya na Amerika akutana na Kaimu Balozi wa Finland nchini

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya  Ulaya na Amerika amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini, Bi. Sarah Cooke kuhusu ushirikiano kati ya nchi hizi mbili. Katika mazungumzo yao walijadilikwenye ushirikiano katika sekta mbalimbali. 
Mhe.Cooke akimwelezea jambo Bw. Nyamanga.
Mazungumzo yakiendelea



Tuesday, May 15, 2018

SADC watoa mafunzo kwa Maafisa wa Serikali.

Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Balozi Innocent E. Shiyo akifungua  Warsha ya Mafunzo ya Mfumo wa Ufuatialiaji na Tathmini wa SADC (SADC Results Based Online Monitoring and Evaluation System) kwa niaba ya Katibu Mkuu Prof. Aldof Mkenda, kulia kwake ni Meneja Mradi kutoka GIZ Bw. Robson Chakwama na wa mwisho ni  mmoja wa Wakufunzi wa Warsha hiyo kutoka SADC Bi. Lerato Moleko 

 Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Wizara kwa kushirikiana  na Serikali ya Ujerumani chini ya Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) na Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), yametolewa kwa Maafisa wa Serikali na Taasisi za Umma, tarehe 15 - 17 Mei,2018 katika ukumbi wa Mikutano wa  Mwalimu Nyerere, Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo
Sehemu ya Maafisa kutoka Wizarani wakifuatilia mafunzo hayo.
Mkutano ukiendelea
Picha ya pamoja baada ya mkutano

===============================================
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KUHUSU WARSHA YA MAFUNZO JUU YA MFUMO WA UFUATILIAJI NA TATHMINI WA SADC KWA MAAFISA WA SERIKALI NA TAASISI ZA UMMA
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana  na Serikali ya Ujerumani chini ya Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) na Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) imeandaa Warsha ya Mafunzo ya Mfumo wa Ufuatialiaji na Tathmini wa SADC (SADC Results Based Online Monitoring and Evaluation System) kwa maafisa wa Serikali na taasisi za umma. Warsha hii inafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam kuanzia tarehe 15 hadi 17 Mei, 2018.

Lengo la warsha hii ni kuwezesha wizara na taasisi mbalimbali za Serikali kufahamu utendaji kazi wa mfumo huu wa SADC ambao unalenga kukusanya taarifa za utekelezaji wa itifaki na programu mbalimbali za maendeleo za SADC ambazo zinatekelezwa ndani ya nchi na kikanda kwa ujumla. 

Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini wa SADC uliridhiwa na Kikao cha Baraza la Mawaziri wa SADC kilichofanyika katika Falme ya Eswatini (Swaziland) mwezi Machi, 2017. Pamoja na mambo mengine, mfumo huu utawezesha pia nchi wanachama kufanya tathmini ya kina ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Maendeleo ya Kanda uliofanyiwa maboresho wa mwaka 2015-2020 (Revised Regional Indicative Strategic Plan, 2005 – 2020). Mpango huu ndio mkakati mkuu (blueprint) unaosimamia programu zote za kisiasa, kiuchumi na kijamii zinazotekelezwa SADC. 

Warsha hii itatuwezesha kufuatilia kwa karibu zaidi maendeleo ya utekelezaji wa itifaki na programu mbalimbali za SADC katika sekta zao na kutoa tathmini, na kubainisha fursa zinazopatikana kupitia uanachama wetu. Hadi sasa nchi za Lesotho, Mauritius, Falme ya Eswatini (Swaziland), Zambia na Zimbabwe tayari wameshapata mafunzo ya mfumo huu. Tanzania itakuwa ni nchi ya sita. 
 
Tanzania kama mwanachama hai na mwanzilishi wa Jumuiya hii, hadi kufikia Machi, 2018 imesaini jumla ya Itifaki 28 kati ya itifaki 31. Kati ya Itifaki zilizowekwa saini, jumla ya Itifaki 23 zimesharidhiwa na itifaki 5 ziko katika hatua mbalimbali za kuridhiwa. 

Aidha, kuna Itifaki nyingine tatu ambazo Tanzania bado haijaweka saini ambazo ni itifaki ya Ajira na Kazi 2014; Itifaki ya Utunzaji wa Mazingira kwa Maendeleo Endelevu 2014 na itifaki ya kulinda aina Mpya ya Mimea, 2017. Itafaki hizi zinatarajiwa kusainiwa wakati wa Mkutano wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali utakaofanyika mwezi Agosti, 2018 Windhoek, Namibia.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam, 15 Mei ,2018

Monday, May 14, 2018

Waziri Mahiga aelezea ziara yake Israel kuwa ya mafanikio

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), amefanya mkutano na waandishi wa habari kuwaelezea yaliyojiri kuhusu ziara yake ya kikazi nchini Israel. Wakati wa ziara hiyo Mhe. Waziri Mahiga alikutana na Waziri Mkuu wa Israel, Mhe. Benjamin Netanyau na kufanya nae mazungumzo kuhusu kuimarisha ushirikiano. Mhe. Waziri Magiga pia alifungua rasmi Ubalozi wa Tanzania nchini humo.
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki waliohudhuria mkutano huo wa Waziri na waandishi wa habari, wa kwanza kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati Bw. Suleiman Saleh, wa pili kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga,  kushoto ni Katibu wa Waziri Bw. Magabilo Murobi na Afisa Mambo ya Nje Bi. Kisadoris Mwaseba.
Sehemu ya waandishi wa habari waliohudhuria kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea



Waziri Mahiga akutana na Kaimu Balozi wa Marekani nchini



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Bi. Inmi Patterson alipotembelea katika ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Mei 2018.
    Mazungumzo yao yalijikita katika kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na uchumi hususan katika sekta ya elimu, afya na ujenzi wa miundombinu.
 
Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ulaya na Amerika wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Jestus Nyamanga, Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Gerald Mbwafu na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Redemptor Tibaigana wakifuatilia mazungumzo.

Mazungumzo yakiendelea.

Friday, May 11, 2018

Wizara Kushiriki Maadhimisho ya siku ya Afrika


Mkurugenzi wa Idara ya Afrika, Balozi Grace Mujuma amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi wa nchi za Afrika wanao wakilisha nchi zao hapa nchini,Mabalozi hao ni kutoka nchi za Namibia na Malawi, pamoja na mambo mengine katika mazungumzo hayo walijadiliana kuhusu maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya Umoja wa Afrika.
Umoja huo ulioanzishwa Mwaka 1963 kwa lengo la kutetea maslahi mbalimbali ya Bara la Afrika, kuongeza umoja zaidi katika kutetea uhuru na kulinda mipaka yake. Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Namibia Mhe. Theresia Samaria, akimwelezea Balozi Mujuma (hayupo pichani), namna wanavyotarajia kuadhimisha hafla hiyo kwa hapa nchini, kulia ni Balozi wa Malawi Mhe. Hawa Olga Ndilowe akimsikiliza kwa makini.

Sehemu ya watumishi waliohudhuria mazungumzo hayo, wa kwanza kulia ni Bw. Salvatory Mbilinyi, Bw. Makamba Dahari na mwisho kushoto ni Bi. Zulekha Tambwe .
Mazungumzo yakiendelea.