Tuesday, November 27, 2018

Watanzania wahimizwa kuchangamkia ajira za UN



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Watanzania wahimizwa kuchangamkia ajira za UN

Tanzania licha ya kuwa miongoni mwa nchi zinazoongoza duniani kwa kuchangia vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa, lakini ajira za raia wake kwenye Sekretarieti ya Umoja huo ni ndogo mno.  Kauli hiyo ilitolewa leo na Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa, Bi. Huda Hanina ambaye yupo nchini kwa ajili ya kutoa semina kwa Watanzania itakayowawezesha kuwa na ujuzi na mbinu za kuomba ajira katika Umoja wa Mataifa.

Semina hiyo inahusisha washiriki kutoka Vyuo Vikuu, vyombo vya ulinzi na usalama, Wizara na mashirika ya umma inafanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar Es Salaam tarehe 26 hadi 28 Novemba 2018.

“Tanzania kwa sasa inashika nafasi ya 12 katika nchi zinazochangia vikosi vya kulinda amani duniani na utendaji wa vikosi hivyo unajulikana na kila mtu, hivyo, Sekretarieti inapenda kuona raia wa kawaida wanaajiriwa ndani ya Umoja wa Mataifa ili watoe mchango kama unaotolewa na vyombo vya usalama”, Alisema  

Alieleza kuwa Umoja wa Mataifa una wanachama 193 kati ya hao, nchi ambazo raia wake wameajiriwa na Umoja huo ni 168 pekee ikiwemo Tanzania yenye watumishi 91 ambao ni chini ya nusu asilimia ya watumishi wote wa Umoja huo.

Bi. Hanina aliwasihi washiriki wa semina hiyo na Watanzania kwa ujumla kuingia katika Tovuti ya Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa, https://careers.un.org ili kufuatilia ajira zinazotangazwa na kuangalia inayofaa kulingana na ujuzi mtu alio nao na kutuma maombi.

Alisisitiza umhimu wa kuandaa wasifu kulingana na sifa zilizoainishwa na nafasi husika. Alisema tatizo kubwa linalowakabili watu wengi wakiwemo Watanzania ni kuandaa wasifu unaokidhi viwango kulingana na kazi iliyotangazwa.  “Watu wengi wanaandaa historia badala ya wasifu, kitu ambacho sio sahihi. Kinachotakiwa ni kuandaa wasifu ambao unaainisha ujuzi na sifa zinazotakiwa katika kazi iliyotangazwa”. Alisema.

Washiriki wa semina hiyo wamehimizwa ujuzi waliopata wawafundishe Watanzania wengine ili katika kipindi kifupi kijacho Watanzania wengi waweze kuomba ajira na hatimaye kuajiriwa kwenye Umoja wa Mataifa.

Semina hiyo imekuja kufuatia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kupitia Ofisi yake ya Uwakilishi wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa jijini New York kufanya maombi maalum kwenye Umoja huo ya kuwapatia Watanzania mafunzo na mbinu za kupata ajira katika chombo hicho kikubwa duniani.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar Es Salaam, Tanzania
Tarehe 27 Novemba 2018

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Ellen Maduhu akitoa neno la ukaribisho  katika semina ya kuwajengea uwezo  Watanzania wakuwa na mbinu na ujuzi wa kuomba na kupata ajira kwenye Umoja wa Mataifa.
Mwakilishi kutoka Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, Bi. Huda Hanina akitoa somo kwa washiriki wa semina kuhusu ujuzi na mbinu za kuomba na kupata ajira katika Umoja wa Mataifa.
Sehemu ya washiriki wa semina kutoka vyombo vya Ulinzi na Usalama, Wizara, wahitimu wa vyuo vikuu, Wizara na mashirikia ya umma wakisikiliza kwa makini somo lililokuwa linatolewa.
Semina inaendelea
Bi. Hanina akiendelea kutoa somo kwa Watanzania ili waweze kuwa na mbinu na ujuzi za kufanya maombi na kupata ajira kwenye Umoja wa Mataifa.



Monday, November 26, 2018

Watanzania wajengewa uwezo wa kupata ajira kwenye Umoja wa Mataifa

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhani Mwinyi Muombwa amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi kutoka Umoja wa Mataifa, Bi. Huda Hanina ambaye yupo nchini kwa ajili ya kutoa Semina ya kuwajengea uwezo Watanzania kuhusu mbinu za kuomba ajira kwenye Umoja wa Mataifa. Balozi Mwinyi alipongeza hatua hiyo  kwa kuwa Tanznaia licha ya kuwa ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kuchangia vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa duniani, lakini idadi ya Watanzania waliojairiwa katika Sekretarieti ya umoja huo ni ndogo mno. 
Sehemu ya Uongozi wa Jeshi la Ulinzi wa Tanzania pamoja Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Bi. Hellen Maduhu wakifuatilia mazungumzo
Sehemu nyingine ya watumishi wa Serikali wakifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Balozi Mwinyi na Bi. Hanani 
Mazungumzo yakiendelea.
Balozi Mwinyi na Bi. Hanani wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi kutoka serikalini na Umoja wa Mataifa.




Majadiliano katika Meza Duara


Bi. Hanani akielezea mambo mbalimbali kwenye Mkutano na Viongozi wa Serikali na Jeshi la Ulinzi Tanzania, kabla ya kufunguliwa kwa semina za kuwajengea uwezo Watanzania ili kuweza kuchangamkia fursa zinazotolewa na Umoja wa Mataifa.  
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za SMZ - Zanzibar, Mhe. Radhia Haroub Rashid (wa kwanza kulia) akichangia jambo katika semina ya kuwajengea uwezo wa Watanzania wa kuomba nafasi za ajira kwenye Umoja wa Mataifa. 
Juu na Chini sehemu ya viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama nchini wakimsikiliza kwa makini Bi. Hanani



Mazungumzo yakiendelea.



Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway kutua Tanzania


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

VIONGOZI WA NCHI MARAFIKI WAENDELEA KUTEMBELEA TANZANIA WAKIONGOZWA NA WAZIRI WA MAENDELEO YA KIMATAIFA WA NORWAY

Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway, Mhe. Nikolai Astrup atafanya ziara ya kikazi nchini kuanzia tarehe 27 hadi 30 Novemba 2018.

Wakati wa ziara yake nchini, Waziri huyo anatarajiwa kufanya mazungumzo na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ratiba ya Waziri huyo itahusisha pia mikutano na viongozi wengine wa Serikali wakiwemo Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Phillip Mpango (Mb), Waziri wa Fedha na Mipango na Bw. Charles Kichere, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Mikutano hiyo itajadili namna ya kukuza uhusiano kati ya Tanzania na Norway hususani kwenye maeneo ya ukusanyaji wa mapato, mazingira, nishati na kilimo.
Mheshimiwa Waziri Astrup pia atatembelea Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga kwa ajili ya kukagua miradi ya umeme inayofadhiliwa na Serikali ya Norway ikiwemo iliyoanzishwa kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na mtambo wa kuzalisha umeme wa maji uliojengwa na Norway, Sweden na Finland kwenye miaka ya 1990 na kukarabatiwa hivi karibuni na Serikali ya Norway. Kwenye ziara mkoani Tanga, Waziri huyo ataambatana na Mhe. Subira Mgalu (Mb), Naibu Waziri wa Nishati.
Vilevile, Waziri huyo pamoja na Mhe. Omary Mgumba (Mb), Naibu Waziri wa Kilimo watatembelea maghala na mtambo wa kuhifadhi mbolea uliopo karibu na Bandari ya Dar es Salaam, unaomilikiwa na kampuni ya Yara kutoka Norway ambapo Waziri kutoka Norway atasaini makubaliano na uongozi wa Mpango wa Chakula Duniani (WFP) ambapo Norway itasaidia Programu inayoitwa Farm to Market Alliance (FtMA) iliyo chini ya WFP.
Ratiba ya Waziri huyo itahusisha pia hafla itakayojumuisha watanzania waliowahi kusoma na kufanya kazi nchini Norway. Akiwa ni mmoja wa viongozi waliosoma nchini Norway, Mhe. Job Y. Ndugai (Mb), Spika wa Bunge la Tanzania atakuwa mgeni rasmi kwenye hafla hiyo inayotegemewa kuhusisha washiriki wapatao 400.
Viongozi wengine wanaotarajiwa kufanya ziara nchini kati ya tarehe 27 na 30 Novemba 2018 ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. Gorge Arreaza tarehe 29 Novemba 2018, Katibu Mkuu anayesimamia maendeleo na ushirikiano kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Dernmark, Bw. Trine Rask tarehe 28 hadi 30 Novemba 2018 na Mkurugenzi anayesimamia nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara kwenye Wizara ya Mambo ya Nje ya Uswisi, Balozi Anne Lugon- Moulin tarehe 27 hadi 29 Novemba 2018. Ziara hizi zinalenga kuongeza wigo wa ushirikiano baina ya Tanzania na nchi hizo rafiki.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Tarehe 26 Novemba 2018

Friday, November 23, 2018

Waziri Mahiga amuaga Balozi wa Jamhuri ya Korea


Balozi wa Jamhuri ya Korea, Mhe. Song Geum Young (kushoto) akifurahia zawadi aliyopewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga jana. Mhe. Balozi Song amemaliza muda wa uwakilishi nchini, hivyo alikutana na Mhe. Waziri kwa ajili ya kuagana.

Ukumbusho wangu huu, Mhe. Waziri. Hayo ni maneno yanayosadikiwa kutamkwa na Mhe. Balozi Song wakati akimkabidhi zawadi Mhe. Mahiga jana.

Thursday, November 22, 2018

Mhe. Dkt. Ndumbaro awa mgeni rasmi maadhimisho ya Mshikamano na Taifa la Palestina


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) ambaye pia alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya Siku ya Mshikamano na Taifa la Palestina akitoa hotuba yake kwenye maadhimisho hayo ambayo yalifanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam tarehe 21 Novemba, 2018.  Katika hotuba yake, Mhe. Naibu Waziri alisisitiza umuhimu wa kuendelea kushirikiana na Taifa la Palestina ili kuhakikisha taifa hilo linaondokana na hali zote za kuonewa na kugandamizwa na kuwa huru.
Sehemu ya wageni waalikwa wakifuatilia hotuba ya Mhe. Dkt. Ndumbaro (hayupo pichani).
Sehemu nyingine ya wageni waalikwa akiwemo Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM). Dkt. Bashiru Ali (wa pili kushoto) wakifuatilia hotuba ya Mhe. Dkt. Ndumbaro wakati wa maadhimisho ya siku ya mshikamano na Taifa la Palestina.
Wageni waalikwa wakiwemo watoto ambao ni raia wa Palestina wanaoishi nchini wakiwa kwenye maadhimisho hayo


Balozi wa Palestina nchini, Mhe. Hamdi Abu Ali akitoa hotuba yake wakati wa maadhimisho ya siku ya mshikamano na Taifa la Palestina yaliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam

Mhe. Naibu Waziri, Dkt. Ndumbaro kwa pamoja na Mhe. Dkt. Salim Ahmed Salim, Waziri Mkuu Mstaafu wakifuatilia hotuba ya Balozi Abu Ali (hayupo pichani).


Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Bashiru Ali naye akizungumza wakati wa maadhimisho hayo

Afisa Habari kutoka Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) nchini, Bi. Stella Vuzo nae akitoa salamu za Ofisi hiyo kuhusu maadhimisho hayo


Mhe. Dkt. Ndumbaro akimsikiliza Mhe. Dkt. Salim alipokuwa akimweleza jambo wakati wa maadhimisho ya siku ya mshikamano na Taifa la Palestina


Mhe. Dkt. Ndumbaro akimsikiliza Mhe. Dkt. Salim. Pembeni ni Balozi wa Palestina nchini, Mhe. Hamdi Abu Ali


Viongozi wa meza kuu wakiwa wamesisima kwa heshima wakati nyimbo za Taifa la Tanzania na Palestina zikiimbwa wakati wa maadhimisho hayo

Katibu Mkuu wa CCM, Mhe. Dkt. Bashiru Ali (kulia) akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan M. Mwinyi (katikati) na mmoja wa wageni waalikwa kwenye maadhimisho ya siku ya mshikamano na Taifa la Palestina

Balozi Mwinyi akimweleza jambo  Katibu wa Naibu Waziri, Bw. Charles Faini wakati wa maadhimisho hayo

Sehemu ya Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki walioshiriki maadhimisho hayo

Mhe. Naibu Waziri akimkabidhi zawadi Bi. Zaheeda Alishan ambaye ni mshindi wa kwanza wa shindalo la uchoraji wa picha zinazoelezea matukio mbalimbali kuhusu  Palestina

Viongozi wakiwa kwenye picha ya pamoja na Bw. Jaykesh Rathod (mwenye mfuko) ambaye ni mshindi wa pili wa  shindano la kuchora picha zinazoelezea matukio mbalimbali ya Palestina

Mhe. Dkt. Ndumbaro akizungumza na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Bw. Alvaro Rodriguez ambaye nae alishiriki maadhimisho ya siku ya mshikamano na Taifa la Palestina


Mhe. Dkt. Ndumbaro akipata maelezo ya picha kutoka kwa mshindi wa kwanza, Bi. Alishan

Mshindi wa kwanza, Bi.Alishan (kulia) akiwa pamoja na wageni waalikwa kwenye picha yake iliyompatia ushindi.

Mhe. Dkt. Ndumbaro akipata maelezo kutoka kwa mshiriki mwingine wa shindano la kuchora

Mhe. Dkt. Ndumbaro akimsikiliza mshiriki wa maonesho hayo ya picha kuhusu Palestina

Mhe. Dkt. Ndumbaro akipata maelezo kutoka kwa mshiriki mwingine
Mhe. Dkt. Ndumbaro akikaribishwa na Mhe. Balozi Hamdi mara alipowasili kwa ajili ya kushiriki maadhimisho ya siku ya mshikamano na Taifa la Palestina

Mhe. Dkt. Ndumbaro akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho hayo

Wednesday, November 21, 2018

Tanzania wins the Best Tourist Destination Award in Russia


 PRESS RELEASE

Tanzania wins the Best Tourist Destination Award in Russia

Tanzania has won the Award for the ‘’Best Destination to the World’’ in the Category of Exotic Destination 2018.

Today, on 21st November, 2018, the Ambassador of Tanzania to Russia, His Excellency Maj. Gen. (Rtd) Simon Mumwi on behalf of the Government of the United Republic of Tanzania will be receiving a Russian National Geographical Traveler Award at the ceremony scheduled to be held in Moscow.

Tanzania won the Award after online voting conducted by the Russian version of National Geographic Magazine that involved 263,000 online readers.

Tanzania is winning this Award for the third time since 2011 where Zanzibar was chosen as the Best Beach Tourist Destination in Africa and therefore awarded the Star Travel Award. Last year, Tanzania also received a National Geographical Travel Award as the second best destination in the world in the category of exotic destination.

These achievements reflect efforts made by the Government of Tanzania through its Embassy in Russia, Ministries of Tourism and Natural Resources both in Tanzania Mainland and Zanzibar and other Institutions in tourism industry.

Through these efforts, the volume of Russian tourists visiting Tanzania has been increasing. For instance; last year (2017) 10,060 tourists from Russia visited Tanzania as compared to only 4,021 tourists in 2012.

More concerted efforts will be made by the Ministry of Foreign Affairs and other stakeholders to promote Tanzania as the best tourist destination in the world and looking forward to see more Russian tourists choosing Tanzania as their best destination for tourism.





Issued by;
Government Communication Unit,
Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation,
Dodoma
21st November 2018.



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tanzania yashinda Tuzo ya Utalii nchini Urusi

Tanzania imeshinda tuzo ya utalii kwa kuonekana ni eneo bora zaidi la utalii duniani nchini Urusi kwa mwaka 2018 (The Best Destination to the World in the Category of Exotic Destination 2018).

Leo tarehe 21 Novemba 2018, Balozi wetu nchini Urusi Mhe. Maj. Gen. (Mst). Simon Mumwi atapokea Tuzo hiyo kutoka Jarida la kirusi la “National Geographic Magazine” jijini Moscow kwa niaba ya nchi.   

Tanzania imepata ushindi huo kutokana na kura zilizopigwa kwenye mtandao wa jarida hilo la “National Geographic Magazine” lililoshirikisha wapiga kura 263,000 kwa njia ya mtandao.

Hii ni mara ya tatu katika kipindi cha miaka saba tokea mwaka 2011, raia wa Urusi kupitia jarida hilo wanaichagua Tanzania kama eneo bora zaidi la utalii. Mwaka 2011, Zanzibar ilipata tuzo ya ‘Star Travel’ kama eneo bora zaidi la utalii wa ufukweni katika bara la Afrika na mwaka jana, Tanzania ilipata tuzo ya NGT na Tanzania ilishinda nafasi ya pili katika tuzo hiyo  katika kundi la eneo bora la utalii duniani.

“National Geographic Traveller Awards” (NGT Awards) ni tuzo ya kifahari zaidi katika sekta ya utalii nchini Urusi na hutolewa na Jarida la kirusi la “National Geographic Magazine”.

Mafanikio hayo yanatokana na jitihada zinazofanywa na Serikali ya Tanzania kupitia Ubalozi wetu Urusi, Wizara za Utalii za Tanzania Bara na Zanzibar, na Taasisi zote zinazosimamia masuala ya utalii za ndani na nje ya nchi katika kutangaza vivutio vya utalii kwa nchi mbalimbali duniani ikiwemo Urusi.

Kupitia juhudi hizi, idadi ya watalii wanaokuja Tanzania kutoka Urusi imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka. Kwa mfano, idadi hiyo imeongezeka kutoka watalii 4,021 mwaka 2012 hadi watalii 10,060 mwaka 2017.  

Wizara kupitia Ubalozi wetu itaendelea kuongeza juhudi za kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania na tunategemea kwa kushirikiana na wadau wengine katika juhudi hizi, idadi ya watalii kutoka Urusi wanaokuja nchini itaongezeka zaidi.




Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
21 Novemba 2018


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje akutana na Balozi wa Iran nchini


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) akisalimiana na Balozi wa Iran nchini, Mhe. Mousa Farhang alipofika kwenye Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumpongeza Mhe. Naibu Waziri kwa kuteuliwa kwenye wadhifa huo na kuzungumzia uhusiano kati ya Tanzania na Iran.
Mhe. Dkt. Ndumbaro akizungumza na Mhe. Balozi Farhang kuhusu namna ya kuimarisha ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya Tanzania na Iran.
Ujumbe uliofuatana na Balozi Farhang kutoka Ubalozi wa Iran hapa nchini ukifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Dkt. Ndumbaro na Mhe. Balozi Farhang (hawapo pichani)


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Zainab Angovi (kushoto) kwa pamoja na Katibu wa Naibu Waziri, Bw. Charles Faini na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Kisa Mwaseba wakifuatilia na kunukuu mazungumzo kati ya Mhe. Dkt. Ndumbaro na Mhe. Balozi Farhang (hawapo pichani).

Mazungumzo yakiendelea

Balozi Farhang akimpatia Mhe. Dkt. Ndumbaro zawadi ya sanaa ya kutengenezwa kwa mkono kutoka Iran