Wednesday, January 16, 2019

Dkt. Mahiga akagua ujenzi wa ofisi ya Wizara Ihumwa, Dodoma

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Mb) akiweka saini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye eneo linalojengwa jengo la ofisi ya Wizara Ihumwa, Dodoma.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Mb) akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la ofisi ya Wizara Ihumwa Dodoma. Mhe. Waziri alielezwa kuwa ujenzi huo unaenda katika kasi inayoridhisha ambapo wakandarasi wapo mbele ya mpangoa kazi.

Waziri Mahiga na Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bw. Hamid Mbegu wakioneshana alama za mipaka ya kiwanja cha Wizara.

Waziri Mahiga akiendelea na ukaguzi wa jengo la ofisi ya Wizara.
Waziri Mahiga akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bw. Hamid Mbegu 

Watanzania 70 wahitimu Chuo Kikuu cha Galgotias nchini India


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Watanzania 70 wahitimu Chuo Kikuu cha Galgotias nchini India

Watanzania zaidi ya 70 wakiwemo wawili wa shahada ya uzamivu wamehitumu masomo yao katika Chuo Kikuu cha Galgotias nchini India katika fani mbalimbali tarehe 14 Januari 2019.

Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika mahafali ya nne ya chuo hicho aliwatunuku vyeti wanafunzi hao na wengine kutoka nchi mbalimbali duniani na kuwasihi  kutumia ujuzi walioupata kuchangia kikamilifu maendeleo ya nchi walizotoka.

‘Ulimwengu unasubiri uongozi mpya na mawazo mapya na kanuni na miiko madhubuti kutoka kwenu. Hivyo, kifanyeni chuo kijivune kupitia kwenu kwa kutoa michango yenye tija katika mataifa na jamii zenu, hususan kwa kufanya kazi kwa bidii, ubunifu na uadilifu mkubwa katika kutimiza majukumu yenu', Balozi Luvanda alisema.

Balozi Luvanda alisema kuwa wanafunzi hao wanahitimu huku dunia ikishuhudia mapinduzi ya teknolojia mbalimbali zikiwemo za kidigitali, teknolojia ya matumizi ya sarafu za kidigitali (block chain), matumizi ya kiwango kikubwa cha data katika kufanya maamuzi (big data revolution), usalama wa mitandao (cybersecurity) na matumzi ya teknolojia katika kutekeleza kazi ambazo awali zilikuwa zinafanywa na mwanadamu (artificial intelligence). Alielezea matumaini yake kuwa chuo hicho kitakuwa kimewandaa vyema wahitimu hao  kukabiliana na changamoto za mapinduzi ya teknolojia katika kutekeleza majukumu yao.

Mhe. Balozi alihitimisha hotuba yake kwa kuwasihi wahitimu hao kuwa, kutunukiwa vyeti sio mwisho wa kujifunza. Wanatakiwa waendelee kusoma vitabu kwa kuwa kusoma vitabu ni sawa na kuufanyia matengenzo ubungo. ‘Akili ya mwanadamu ni kama bustani, bustani isipomwagiwa maji na kupaliliwa itaota magugu na kufa kabisa.   Mhe. Balozi alimaliza.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
16 Januari 2019

Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika Chuo Kikuu Galgotias kutunukuu vyeti kwa wahitimu wa chuo.
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda akitoa heshima katika picha ya Mahatma Gandhi kwa kuweka shada la maua.
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda akitoa hotuba katika mahafali ya nne ya Chuo Kikuu cha Galgotias

Umati wa wahitimu wa chuo kikuu cha Galgotias
wakisikiliza kwa makini hotuba ya Balozi Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda.
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda akipokea memento kutoka kwa mwanzilishi na mkuu wa chuo kikuu cha  Galgotias, Bw. Suneel Galgotia.






Tuesday, January 15, 2019

Dkt. Ndumbaro akutana na Mwakilishi wa UNHCR

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.), amekuatana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la kutetea wakimbizi la Umoja wa Mataifa Tanzania UNHCR, Chansa Kapaya.

Katika mazungumzo yao Bi. Chansa alitumia fursa hiyo kujitambulisha kwa mara ya kwanza pamoja na Kumpongeza Dkt. Ndumbaro kwa Kuteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Wizara wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kwa upande wake Dkt. Ndumbaro alimshukuru kwa kuja ofisini kwake na kumwahidi kumpatia ushirikiano wa kutosha wakati wote wautendaji wa majukumu yake akiwa hapa nchini. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi Ndogo ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.  
Mazungumzo yakiendelea.
Dkt. Ndumbaro akimkaribisha Bi. Shansa ofisini kwake walipokutana kabla ya kuanza kwa mazungumzo yao. 




Waziri Mahiga akutana kwa Mazungumzo na Balozi wa Misri.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Misri hapa nchini Mhe. Mohamed Gaber Abouelwafa. Katika mazungumzo yao Balozi Abouelwafa alimweleza Dkt. Mahiga kuwa wanafurahishwa na mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na Misri, ambapo kwa sasa Misri wanatekeleza mradi mkubwa wa Bwawa la kuzalisha Umeme Nchini, vilevile Misri itaendelea kuboresha miundombinu ya uzalishaji wa maji kwa kuchimba visima vingine vya maji Nchini.
Pamoja na Mambo mengine Dkt. Mahiga alimweleza Balozi Abouelwafa kuwa Tanzania itaendelea kumpa ushirikiano wa kutosha  katika utekelezaji wa majukumu yake hapa nchini.
Aidha, Dkt. Mahiga alimweleza Balozi kuwa Tanzania inatambua mchango wa Misri kwenye sekta mbalimbali zikiwemo Afya, Elimu na Biashara. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, zilizopo jijini Dar Es Salaam 
Katibu wa Waziri Bw. Magabilo Murobi (wa kwanza kushoto), pamoja na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Afrika Bw. Wilbroad Kayombo wakifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Dkt. Mahiga na Balozi Abouelwafa (hawapo pichani).
Mazungumzo yakiendelea kati ya Dkt. Mahiga na Balozi Abouelwafa
Maafisa kutoka Ubalozi wa Misri nchini Tanzania wa kwanza kushoto ni Bw. Ahmed Elghoul na Bi. Nevine Elsaeed nao wakifuatilia kwa makini mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea kati ya Dkt. Mahiga na Balozi Abouelwafa (hawapo pichani).



Monday, January 14, 2019

Dkt. Ndumbaro awaaga Watanzania wanaokwenda Japan kujifunza masuala ya Uongozi

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Japan, Mhe. Shinichi Goto aliyeambatana na washiriki kutoka Tanzania wanao kwenda Nchini Japan kwa ajili ya kupata mafunzo ya Uongozi katika sekta mbalimbali. Mafunzo hayo yatadumu kwa muda wa siku 50. Aidha, Dkt. Ndumbaro amemshukuru Balozi Goto kwa kuendelea kuiwakilisha vyema nchi ya Japan hapa nchini ambapo aliahidi kuwa Japan itaendelea kuchangia maendeleo katika sekta mbalimbali.
 Dkt. Ndumbaro amewaasa Washiriki wanaokwenda katika mafunzo hayo kuitumia fursa hiyo vyema kwa kujifunza mambo mampya kutoka Taifa hilo. 


Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Bw. Caesar Waitara (hayupo pichani) yamefanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  jijini Dar Es Salaam.
Mazungumzo yakiendelea 
Dkt. Ndumbaro akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Goto
Dkt. Ndumbaro pamoja na Balozi Goto wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki kutoka Tanzania wanao kwenda nchini Japani.  




Saturday, January 12, 2019

Tanzania yatafuta Soko la Utalii Uholanzi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tanzania yatafuta Soko la Utalii Uholanzi

Taasisi za Serikali na kampuni binafsi mbalimbali za utalii zipo nchini Uholanzi kushiriki maonesho ya utalii ya kimataifa kwa lengo la kutafuta fursa mpya za soko la utalii nchini humo.
Maonesho hayo maarufu kama Holday Fair 2019 (Vakantiebeurs2019) yalianza tarehe 9 Januari na yatakamilika tarehe 13 Januari 2019, hufanyika kila mwaka katika mji wa Utrecht na kushirikisha taasisi mbalimbali kutoka duniani kote.
Taasisi za Serikali zinazoshiriki ni Bodi ya Utalii Tanznaia (TTB), Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA). Kwa upande wa kampuni binafsi ni into Africa Eco Travel Ltd, Migada Adventures, Mbalaget Tented Camp Ltd, Kili Fair Promotions Ltd, East Africa Camps na Makasa Tanzania Safaris.
Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Irene Kasyanju amesema kuwa maonesho hayo ni fursa adhimu kwa nchi kutangaza vivutio vya utalii ambapo kwa mwaka 2019, waandaji kwa mara ya kwanza wametoa nafasi kwa Balozi za nje zilizopo nchini humo kutangaza pia fursa za biashara na uwekezaji.
Balozi Kasyanju ambao Ubalozi wake unashiriki katika maonesho hayo alieleza kuwa maonesho hayo yataenda sanjari na Vakantiebeurs Travel Congress, Vakantiebeurs Consumer Day na Vakantiebeurs Trade Day ambapo washiriki watapata fursa ya kupeana taarifa muhimu kuhusu mwelekeo na maendeleo ya biashara ya utalii katika maeneo mbalimbali duniani, vivutio vipya pamoja na kufanya biashara.
Ushiriki wa Tanzania katika maonesho hayo utasaidia washiriki kukutana na wadau na kuanzisha uhusiano wa kibiashara unaotarajiwa kufungua soko la utalii nchini baada ya wadau hao kupata maelezo ya kutosha kuhusu vivutio vilivyopo nchini na faida zake. 

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma, Tanzania
11 Januari 2019

Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Irene Kasyanju (mwenye miwani) akiwa na washiriki wengine katika Maonesho ya Utalii ya Kimataifa yanayofanyika nchini Uholanzi kuanzia tarehe 9 hadi 13 Januari 2019.

Wageni mbalimbali wanatembelea banda la Tanzania ili kupata maelezo kuhusu vivutio vya uwekezaji nchini

Banda la Tanzania linatia fora kwa kutembelewa na idadi kubwa ya watu wanaotaka kupata maelezo kuhusu fursa na vivutio vya utalii nchini.

Wageni katika banda la Tanzania.

Balozi Kasyanju na washiriki wenzake wakiwa katika badna la Tanzania tayari kuanza kazi ya kuuza vivutio vya utalii nchini Uholanzi.

Dkt. Ndumbaro akutana na Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi, Mhe. Rwegasira Mukasa Oscar  (kushoto) akiwakaribisha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi katika kikao na uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Bunge Dodoma tarehe 11 Januari 2019.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro aliongoza ujumbe wa Wizara katika kikao na Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Bunge Dodoma tarehe 11 Januari 2019. Wengine katika picha, kuli ni Bw. Hamid Mbegu, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu na kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani, Bw. Japahary Kachenje.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro aliwasilisha taarifa mbili katika kikao hicho. Taarifa ya kwanza ilihusu hatua zinazochukuliwa na Wizara katika mapambano dhidi ya Ukimwi na taarifa ya pili ilihusu namna Wizara inavyoshirikiana na mashirika ya kimataifa, kikanda na nchi mbalimbali katika kukabiliana na biashara haramu ya dawa za kulevya.

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi na uongozi wa Wizara ukisikiliza kwa makini taarifa zilizokuwa zinawasilishwa na Mhe. Naibu Waziri.

Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi walioshiriki kikao hicho.

Mhe. Amina Mollel, Mbunge wa Viti Maalum akichangia jambo wakati wa kikoa kati ya Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi na Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Mhe. Masoud Abdallah akichangia jambo katika kikao hicho.

Ujumbe wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ulioshiriki kikao kati ya Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi na uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje.

Sehemu nyingine ya Ujumbe wa Wizara ulioshiriki kikao hicho.

Waheshimiwa Wabjumbe wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi wakisalimiana na Mhe. Naibu Waziri kabla ya kikao kuanza.

Mhe. Allan Kiula, Mbunge wa Iramba Mashariki akisalimiana na  Mhe. Naibu Waziri.

Mheshimiwa Mbunge akibadilishana mawazo na Mhe. Naibu Waziri kabla ya kuanza kikao.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Joyce Kimey akiongea machache na Mhe. Naibu Waziri kabla hawajaingia katika kikao na Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi.

Monday, January 7, 2019

Dkt. Ndumbaro Apokea Nakala za Hati za Utambulisho


Zao la Korosho lapata soko Nchini Algeria

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.), amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Algeria, Mhe. Saad Belabed. Katika mazungumzo hayo Mhe. Balozi alieleza kuwa Algeria ipo tayari kununua korosho ya Tanzania. Dkt. Ndumbaro amesema mazungumzo hayo ni moja ya jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli za kuwakomboa kiuchumi Watanzania kwa kutafuta masoko ya mazao ya wakulima nje ya nchi. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki zilizopo jijini Dar es Salaam. 
Balozi Belabed akiendelea kumwelezea jambo Dkt. Ndumbaro 
Mazungumzo yakiendelea.
Dkt. Damas Ndumbaro akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Saad Belabed mara baada ya kumaliza mazungumzo yao. 

Dkt. Ndumbaro Apokea Nakala za Hati za Utambulisho

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amepokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Brazil, Mhe. Antonia Augusto Cesar leo jijini Dar Es Salaam. Baada ya kupokea hati hizo, Dkt. Ndumbaro alifanya mazungumzo na Balozi Mteule, Mhe. Cesar ambapo aliahidi kuwa Serikali itampa ushirikiano ili aweze kutimiza majukumu yake kwa ufanisi. Aidha, alimweleza vipaumbele vya Serikali ya awamu tano na kuiomba Brazil iunge mkono katika kufanikisha vipaumbele hivyo.

Balozi Mteule Cesar akizungumza jambo mara baada ya kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho.

Maafisa ubalozi wa Brazili wakisikiliza kwa makini mazungumzo kati ya Balozi Mteule Mhe. Cesar na Dkt. Ndumbaro (hawapo pichani).

Amb. Nassor Present Letters of Credence to the President of Palestine

The Ambassador of Tanzania to Egypt, H.E Issa Suleiman Nassor (R) who is also accredited to the State of Palestine  present his letters of credence to the President of Palestine, H.E Mahmoud Abbas in Cairo Yesterday. H.E  Nassor presented the letters of Credence when President Abbas was in a working visit in Egypt.

Friday, January 4, 2019

Tangazo la Nafasi za Kazi


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tangazo la Nafasi za Kazi
Sekretarieti ya Shirika la Kuzuia Silaha za Kemikali (Secretariat of the Organization for the Prohibition of Chemical Weapons- OPCW) imetangaza nafasi za kazi za Afisa Mwandamizi wa Masuala ya Umma na Afisa wa Masuala ya Umma (Public Affairs Officer P-4 and Public Affairs Officer P-2).  

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inawahimiza Watanzania, hususan wanawake kuchangamkia nafasi hizo ambapo mwisho wa kufanya maombi kwa nafasi ya Public Affairs Officer P-4 ni tarehe 24 Januari 2019 na ile ya Public Affairs Officer P-2 ni tarehe 9 Januari 2019.  

Maombi yafanywe kwa njia ya mtandao kupitia tovuti www.opcw.org ambayo pia ina maelezo zaidi kuhusu nafasi hizo.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
4 Januari 2019