Thursday, February 14, 2019

Tanzania and Kazakhstan establish diplomatic relations

The Permanent Representative of the United Republic of Tanzania to the United Nations, H.E Ambassador Modest J. Mero (R) and Permanent Representative of Republic of Kazakhstan to the United Nations, H.E  Ambassador Kairat Umarov signing a communique to establish diplomatic relations between their Nations. The signing ceremonies took place in New York on 13th
  February 2019.
Ambassador Mero exchanges the signed communique with his counterpart, Ambassador Umarov.


Ambassador Mero and Ambassador Umarov posing for a photo after signing a communique to establish diplomatic relations between the two countries.

Wednesday, February 13, 2019

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje akutana na Balozi wa Namibia nchini.


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Namibia Mhe. Balozi Theresia Samaria.  Mazungumzo hayo  ambayo yalijikita kwenye masuala ya kuimarsha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili,  yamefanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam tarehe 13 Februari 2019.
Mazungumzo yakiendelea.







ZIARA YA PAMOJA YA NAIBU MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE NA FEDHA MPAKANI HOROHORO

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango  Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) kwa pamoja wamefanya ziara kwenye kijiji cha Jasini na Kituo cha kutolea huduma kwa pamoja Mpakani cha Horohoro kilichopo mpakani mwa Tanzania na Kenya Wilayani Mkinga, Mkoani Tanga. Pamoja na Mambo mengine Naibu Mawaziri hao waliweza kujionea changamoto mbalimbali ikiwamo ukusanyaji wa mapato kituoni hapo, pamoja na kuzungumza na wanakijiji cha Jasini na Watendaji wa Kituo hicho.   
Wadau walioshiriki ziara za Naibu mawaziri hao wakisikiliza  wakati Dkt. Ndumbaro (hayupo pichani) akizungumza
Sehemu nyingine ya wadau wakimsikiliza  Dkt. Ndumbaro (hayupo pichani)
Mkutano ukiendelea
Wananchi wakipata huduma kwenye kituo hicho cha kutolea huduma kwa pamoja
Dkt. Ndumbaro pamoja na Dkt. Kijaji wakimsikiliza Bw. Bilali Juma, Afisa Mkemia wa kituo cha kutolea huduma kwa pamoja mpakani Horohoro
Dkt. Ndumbaro akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mazungumzo na wadau mbalimbali
Kituo cha kutolea huduma kwa pamoja cha Horohoro kilihopo Mpakani mwa Tanzania na Kenya kama kinavyoonekana pichani 

Dkt. Ndumbaro akisaini kitabu cha wageni cha kijiji cha Jasini kilichopo wilaya ya Mkinga, Mkoani Tanga, kabla ya kuanza ziara kwenye kijiji hicho

Naibu Mawaziri pamoja na wadau mbalimbali wakiwa wamesimama kwenye moja ya jiwe ambalo linaonyesha Mpaka wa Tanzania na Kenya.
Mhe. Dkt. Ndumbaro na Mhe. Dkt.  Kijaji wakiwa kwenye Nyumba iliyojengwa mpakani mwa Tanzania na Kenya.  Horohoro. Mhe. Ndumbaro akiwa upande wa Kenya na Mhe. Kijaji akiwa upande wa Tanzania
Mhe. Dkt. Ndumbaro na Mhe. Dkt. Kijaji wakiendelea na ziara na kujionea alama za mipaka zilizopo mpakani hapo
Mhe. Dkt. Ndumbaro pamoja na Mhe. Dkt. Kijaji wakiwa kwenye moja ya alama za mpaka
Mhe. Dkt. Ndumbaro akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa ziara yao kwenye kituo cha kutoa huduma kwa pamoja cha Horohoro
Mhe. Dkt. Kijaji akitizama kitambulisho cha mjasiriamali mdogo huku Dkt. Ndumbaro akishuhudia tukio hilo. Mjasiriamali huyo aliwavuti Naibu Mawaziri hao kwa mwitikio wake chanya katika kuhakikisha kila mjasiriamali nchini anapata kitambulisho cha kufanyia biashara
Mmoja wa wanakijiji akielezea changamoto wanazokabiliana nazo kijijini hapo ikiwamo upatikanaji wa elimu kwa watoto wao ambao wanalazimika kwenda kusoma Kenya na jioni kurejea Tanzania.
Wanakijiji wakiwasikiliza kwa makini Naibu Mawaziri hawapo pichani


Naibu Mawaziri hao wakizungumza na baadhi ya wananchi wa Jasini mara baada ya kumaliza ziara kijijini hapo
Waandishi wa habari wakiwa kazini
Waheshimiwa Naibu Mawaziri wakimsikiliza Mohamed Ibrahim anayesoma Darasa la nne Shule ya Vumba Kuu iliyopo Kenya. Mohamed alikuwa amerudi nyumbani kupata chakula  wakati wa mapumziko mafupi kabla ya kurudi darasani.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

ZIARA YA PAMOJA YA NAIBU MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE NA FEDHA MPAKANI HOROHORO

Watendaji wa Kituo Cha Kutoa Huduma kwa Pamoja cha Horohoro kilichopo mkoani Tanga kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya wametakiwa kuhakikisha kuwa malengo yaliyowekwa ya kukusanya mapato kwenye kituo hicho yanafikiwa.

Kauli hiyo ilitolewa kwa pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) walipotembelea kituo hicho tarehe 10 Februari 2019.

Dkt. Ndumbaro alishangazwa na mwenendo wa ukusanyaji wa mapato wa kituo hicho ambapo takwimu zimekuwa zikipungua badala ya kuongezeka kila mwaka. ‘Kwa miaka mitatu mfululizo takwimu za ukusanyaji wa mapato ya kodi katika Kituo hiki zimekuwa zikishuka badala ya kupanda, jambo ambalo si zuri kiuchumi na linakwenda kinyume kabisa na malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli’; Dkt. Ndumbaro alimwambia Meneja wa TRA kituoni hapo.

Kwa mujibu wa takwimu hizo mwaka wa fedha 2017/2018, makusanyo ya kodi kwenye kituo hicho ni asilimia 81 ya malengo na mwaka wa Fedha 2018/2019 inatarajiwa makusanyo yatafikia asilimia 76 ya malengo yaliyowekwa.

Mhe. Naibu Waziri aliwataka watendaji hao kuwa wabunifu kuhakikisha kuwa malengo ya Serikali yanafikiwa bila kumuonea mtu ikiwemo ubunifu wa kutatua changamoto zinazokikabili kituo hicho. Changamoto hizo ni pamoja na ukosefu wa maji ambapo yananunuliwa kwa gharama ya Shilingi milioni sita kwa mwezi. Naibu Waziri alishangazwa na uamuzi huo wa kutumia fedha nyingi kwa ajili ya maji wakati kuchimba kisima hakiwezi kugharimu zaidi ya milioni 10.

Dkt. Ndumbaro pia hakuridhishwa na ubora wa jengo la kituo hicho na kubainisha kuwa ndio sababu zinazofanya kituo hicho kutozinduliwa rasmi hadi leo.

Kwa upande wake, Dkt. Kijaji alisikitishwa na utendaji usiokuwa na kiwango wa mamlaka zote zilizopo kwenye kituo hicho na kusisitiza kuwa, kwa kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ipo chini ya himaya yake atachukua hatua zinazostahili. Moja ya maeneo yenye udhaifu katika kituo hicho ni uchukuaji wa takwimu zikiwemo za magari yanayoingia na kutoka ambapo kila mamlaka iliyopo hapo ina takwimu tofauti.

Aidha, Mhe. Kijaji alipiga marufuku kwa wafanyabiashara wa Wilaya ya Mkinga kwenda Wilaya ya Muheza kufuata huduma za kodi zikiwemo za kulipia kodi mbalimbali. Mhe. Naibu Waziri alimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Mkinga kuwatangazia wafanyabiashara wa Mkinga marufuku hiyo na kuagiza watumishi wa TRA wa Mkoa kwenda Mkinga kutoa huduma za kikodi angalau mara tatu kwa wiki.

Kuhusu ubora wa jengo hilo, Dkt. Kijaji aliagiza apatiwe nyaraka za jengo hilo ifikapo tarehe 15 Februari 2019 ili aone majukumu ya kila mmoja katika ujenzi wa jengo hilo kwa madhumuni ya kuchukua hatua stahiki.
Mhe. Dkt. Ndumbaro na Mhe. Dkt. Kijaji walifanya ziara ya pamoja kwenye kituo hicho cha Horohoro kwa lengo la kujionea changamoto ili ziweze kutafutiwa ufumbuzi.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
13 Februari 2019




Tuesday, February 12, 2019

Job Announcement at the Commonwealth Secretariat

PRESS RELEASE

Job Announcement at the Commonwealth Secretariat
The Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation has received vacancy notification from the Commonwealth Secretariat inviting qualified Tanzanians to apply for the post of Legal Adviser (Natural Resources) available at the Commonwealth Secretariat.

In line with the Commonwealth’s commitment to gender equality, the Commonwealth Secretariat encourages applications from appropriately qualified women for this post.

Application details can be found on the Secretariat’s website, http://thecommonwealth.org/jobsClosing date for application is Wednesday 20th February, 2019 at 17:00 GMT.

Issued by;
Government Communication Unit,
Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation,
Dodoma.
12th February  2019.


Saturday, February 9, 2019

Tanzania na Azerbaijan kuanzisha Ushrikiano wa Kidiplomasia


Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Modest J. Mero (kushoto) akisalimiana na Mwakilishi wa Kudumu wa Azerbaijan katika Umoja wa Mataifa, Balozi Yashar Aliyev jijini New York Marekani. Viingozi hao walikutana kwa ajili ya kusaini Makubaliano ya kuanzisha ushirikiano wa kidiplomasia baina ya Mataifa yao. 

Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Modest J. Mero (kulia) na Mwakilishi wa Kudumu wa Azerbaijan katika Umoja wa Mataifa, Balozi Yashar Aliyev wakiweka saini Makubaliano ya kuanzisha ushirikiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na Azerbaijan jijini New York, Marekani. Wengine katika picha ni maafisa wa ofisi za Balozi, Bi, Lilian A. Mukasa na Bw. Tofig F. Musayev. 

Balozi Mero na Balozi Aliyev wakiagana baada ya kusaini makubaliano ya kuanzisha ushirikiano wa kidiplomasia baina ya mataifa yao.

Friday, February 8, 2019

Naibu Mawaziri watembelea Kituo cha kutoa huduma kwa pamoja cha Mtukula.


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) amekutana na Naibu Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki wa Uganda, Mhe. Julius Wandera Maganda katika Kituo cha kutoa huduma kwa pamoja mpakani cha Mutukula mpakani mwa Tanzania na Uganda Tarehe 7 Februari 2019. Mara baada ya kukutana walipata fursa ya kutembelea na kujionea namna kituo cha kutolea huduma kwa pamoja mpakani cha Mtukula (OSBP) kinavyofanya kazi na kufanya Mkutano wa pamoja uliowashirikisha wadau mbalimbali kutoka Tanzania na Uganda. Mkutano huo umefanyia Mpakani mwa Tanzania na Uganda eneo la Mtukula.

Dkt. Ndumbaro akizungumza na Mhe. Waganda kabla ya kufanya mkutano wa pamoja na wadau mbalimbali. Wengine katika picha ni wajumbe walioongozana na Naibu Mawaziri hao.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt.Ndumbaro (Mb.) akizungumza kwenye Mkutano na wadau mbalimbali pamoja na jumuiya ya wafanya biashara walio hudhuria mkutano huo.

Naibu Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki wa Uganda, Mhe. Maganda naye akizungumza na wadau pamoja na jumuiya ya wafanya biashara walio hudhuria mkutano huo

Wadau kutoka upande wa Tanzania wakisikiliza kwa makini  wakati Naibu Mawaziri, Mhe. Dkt. Ndumbaro na Mhe. Maganda walipokuwa wakizungumza kwenye mkutano uliyofanyika mpakani wa Tanzania na Uganda-Mtukula
Mhe. Dkt. Ndumbaro akiwa na Mhe. Maganda wakisikiliza kwa makini michango mbalimbali ya wadau iliyokuwa ikiwasilishwa kwenye mkutano.
Mwakilishi wa jumuiya ya wafanya biashara akichangia mada kwenye mkutano
Mmbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Uganda naye akichangia mada wakati wa mkutano huo ukiendelea.

Ujumbe wa Uganda nao wakifuatilia mazungumzo hayo kwa makini.
Viongozi wa pande zote mbili walipata fursa ya kuzungumza na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari waliohudhuria mkutano huo na kuwaelezea yaliyojiri kwenye mkutano.
Dkt. Ndumbaro pamoja na Mhe. Maganda wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mkutano.
Viongozi hao wakifanya ziara kwenye maeneo mbalimbali ya kituo hicho cha pamoja na kujione namana watendaji wanavyo fanya kazi kwa umakini kwa kutumia vifaa vya kisasa katika kupambana na mambo mbalimbali ikiwemo namna ya udhibiti wa magonjwa ya mlipuko.
Dkt. Ndumbaro pamoja na Mhe. Maganda wakimsikiliza Afisa wa ukusanyaji mapato kutoka Tanzania Bw. Mohamed Shamte alipokuwa akielezea namna kituo hicho cha pamoja kinavyo fanya kazi. Naibu Mawaziri hao walijione namna watendaji wanavyofanya kazi kwa umakini kwa kutumia vifaa vya kisasa katika kupambana na mambo mbalimbali, ikiwemo udhibiti wa magonjwa ya mlipuko kama vile Ebola..
Dkt. Ndumbaro pamoja na Mhe. Julius wakiendelea na kukagua  Kituo ili kujionea namna watendaji wake wanavyotoa huduma kwa wananchi wa pande zote mbili.
Katika picha ni jengo la Kituo cha kutolea hudmua kwa pamoja Mtukula mpakani mwa Tanzania na Uganda.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Akizungumza kwenye mkutano huo, Mhe. Dkt. Ndumbaro alisema lengo la ziara yao katika kituo hicho cha kutolea huduma kwa pamoja Mtukula ni pamoja na kujionea mafanikio na kubaini changamoto zinazokabili utendaji wa kazi na kuzipatia ufumbuzi. 

Akiainisha mafanikio makubwa yaliyofikiwa na kituo hicho , Dkt. Ndumbaro alieleza namna mizigo mbalimbali ikipita kwa wakati kwa kuzingatia taratibu zote zilizopo pamoja na wafanyabiashara kati ya nchi hizi mbili wakifanya biashara zao bila vikwazo vyovyote vile.

Pamoja na mambo mengine Dkt. Ndumbaro alitumia fursa hiyo kuwajulisha wadau mbalimali waliohudhuria mkutano huo, kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imeanzisha safari za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), kutoka Dar es Salaam, Arusha mpaka Enttebe, Uganda. Mafanikio hayo yametokana na mahusiano mazuri ya kidiplomasia yaliyopo baina ya Tanzania na Uganda na pia kupitia Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. 

Kwa upande wake Mhe Maganda, alifurahishwa na hali ya kituo hicho namna huduma zinavyotolewa. Aidha, aliahidi kuwa Serikali ya Uganda itaongeza watendaji kazi kwenye kituo hicho ili kuwezesha upande wa Uganda kufanya kazi masaa 24 kama ilivyo kwa upande Tanzania. Pia alisisitiza nchi yake kuendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali ya Ushirikiano.
    
Pia katika Mkutano huo wadau walitoa pongezi kwa viongozi wa Serikali za pande zote mbili kwa kuanzisha kituo hicho cha kutolea huduma kwa pamoja mpakani Mtukula, ambapo walisema kuanzishwa kituo hicho kumeongeza chachu ya maendeleo kwa wafanyabiashara wa pande zote mbili ambapo wamekuwa wakisafirisha bidhaa zao kwa wingi bila kupata changamoto kulinganisha na hapo awali kabla ya kuanzishwa kwa kituo hicho.

 Kadhalika wadau walitoa pongezi kwa watendeji waliopo kituoni hapo kwa upande wa Tanzania, kwa kutoa huduma nzuri kwa masaa 24 kwenye kituo hicho ambapo, imepelekea wafanyabiashara kutokupoteza muda mwingi wafikapo mpakani hapo. 


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
9 Februari 2019















Thursday, February 7, 2019

Wabunge wa EALA walivyotoa Elimu ya Mtangamano wa EAC

Mkurugenzi Mkazi wa Trade Mark East Africa (TMEA), Bw. John Ulanga akitoa mada kwa Wabunge wa Tanzania katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) kuhusu shghuli za taasisi hiyo. Alisema taasisi yake inashirikiana na Serikali kuboresha miundombinu mbalimbali kwa madhumuni ya kuhakikisha kuwa biashara katika nchi za EAC inafanyika bila vikwazo.

Waheshimiwa Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakijadili kwa pamoja na Mkurugenzi wa TMEA kuhusu mchango wa taasisi hiyo katika kuboresha mwenendo wa biashara baina ya Tanzania na nchi nyingine za EAC.

Waheshimiwa Wabunge wa EALA wakijadili mada iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mkazi wa TMEA.

Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam

Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania katika Bunge la EALA, Mhe. Dkt. Abdallah Makame (kulia) akijadili jambo na Makamu Mkuu wa Chuo cha Dar Es Salaam mara baada ya kuwasili katika chuo hicho kwa ajili ya kutoa elimu kwa wanafunzi kuhusu EAC. 

Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania katika Bunge la EALA, Mhe. Dkt. Abdallah Makame (kulia) akipata chakula cha mchana na wanafunzi wa UDSM katika Cafteria Namba moja ya Chuo hicho. Mwenye nguo za bluu ni Mbunge mwenzake wa EALA, Mhe. Pamela Maasay.

Wanafunzi wa UDSM wakipata chakula cha mchana ambapo Wabunge wa EALA walijumuika nao katika chakula hicho.

Mbunge wa EALA, Mwalimu Josephine Sabastian (kushoto) akibadilishana mawazo na wanafunzi wa UDSM wakati wakipata kwa pamoja chakula cha mchana Cafteria.
Waheshimiwa Wabunge wa EALA wakiwa katika meza kuu kwenye Ukumbi wa Nkurumah kwa ajili ya kuongea na wanafunzi kuhusu fursa za EAC.
Mbunge wa EALA, Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe akiwasilisha mada kuhusu EAC kwa wanafunzi wa UDSM.

Waheshimiwa Wabunge wa EALA wakiongea na wanafunzi wa UDSM kuhusu fursa za Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Wanafunzi walioshiriki kwenye mazungumzo na Wabunge wa EALA. Mwenye suti ya bluu ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam.
Washiriki wengine katika mazungumzo hayo.


Wanafunzi wakiuliza maswali na kutoa maoni namna Watanzania watakavyofaidika na Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki



Waheshimiwa Wabunge wa EALA wakikabidhi bendera ya EAC kwa viongozi wa UDSM ili iwe inapeperushwa chuoni hapo. Walitoa wito kwa taasisi nyingine, hususan za Serikali kupeperusha bendera hiyo.
Mkutano na Asasi za Kiraia
Mbunge wa EALA, Mwalimu Josephine Sabastian akitoa elimu kuhusu EAC kwa wawakilishi wa Asasi za Kiraia zilizopo hapa nchini.



Majadiliano baina ya Wabunge wa EALA na wawakilishi wa Asasi za Kiraia kuhusu ushiriki wa asasi hizo katika masuala ya EAC.

Wabunge wa EALA na wawakilishi wa Asasi za Kiraia wakiimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Wabunge walisisitiza umuhimu wa wimbo huo kupigwa katika shughuli rasmi za Serikali.
Mdau akifanya tafrisi ya lugha ya ishara kwa watu wenye ulemavu wa kusikia.