Friday, May 3, 2019

Wizara ya Mambo ya Nje kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Kilimo

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.)  amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini, Bw. Japhet Justine (kushoto). 

Mazungumzo kati yao yalijikita katika kuangalia namna ya kushirikana ambapo Bw. Justine amemweleza Prof. Palamagamba John Kabudi kuwa, Benki ya Maendeleo ya Kilimo itaendelea kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki hususan katika kuangalia fursa za masoko nje ya nchi kupitia Balozi za Tanzania. Masoko hayo  yatakuza biashara ya bidhaa ghafi za Tanzania nje pamoja na kuongeza thamani ya mazao yanayolimwa nchini.

Kwa upande wake,  Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi alimhakikishia ushirikiano Mkurugenzi huyo ili kuhakikisha mazao kutoka Tanzania yanapata soko nje ya nchi. Pia alimweleza kuwa, Wizara itaendelea kushirikiana na Benki hiyo katika kuweka mazingira mazuri ya kuvutia wawekezaji kutoka nje kwa ajili ya kuja nchini kuwekeza kwenye sekta ya kilimo kwani kuimarika kwa sekta hiyo  kutatoa fursa ya kuanzishwa kwa viwanda vya usindikaji mazao ndani ya nchi na kuzalisha ajira kwa vijana.

Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki zilizopo jijini Dar es Salaam tarehe 03 Mei 2019
Mhe. Prof. Kabudi akisisitizia jambo wakati wa mazungumzo  na Bw. Justine.

Thursday, May 2, 2019

Dkt. Ndumbaro akutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt Damas Ndumbaro (Mb.), amekutana na kufanya mazungumzo na  Kaimu Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), nchini leo tarehe 1 Mei, 2019, katika ofisi ndogo za wizara Kivukoni, Dar es salaam. Mazungumzo hayo, yalilenga kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na EU  kwa ajili ya mustakabali wa maendeleo ya pande hizo mbili. Baadhi ya masuala yaliyojadiliwa ni pamoja na Mkataba wa Ubia wa Kiuchumi katika ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), ushirikiano katika nyanja za elimu na udhibiti wa biashara haramu ya dawa za kulevya. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt Damas Ndumbaro (Mb.), akifafanua jambo wakati wa mazungumzo hayo.
Kaimu Balozi Stuart akielezea jambo wakati wa mazungumzo hayo.
Afisa Mambo ya Nje  wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Albert Philipo akifuatilia mazungumzo hayo.
Juu na chini mazungumzo yakiendelea.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt Damas Ndumbaro (Mb.) akiagana na Kaimu Balozi Charles Stuart mara baada ya mazungumzo.


Wednesday, May 1, 2019

Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje washiriki maadhimisho ya Mei Mosi jijini Dar es Salaam

Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Mhe. Paul Makonda (mwenye Tisheti ya bluu) na viongozi wengine akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema (wa pili kulia) wakiwa wamesimama kuwasalimu Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (hawapo pichani) walipopita mbele ya jukwaa kuu wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam tarehe 1 Mei 2019. Kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka 2019 ni  "Tanzania ya uchumi wa Kati inawezekana, wakati wa mishahara na maslahi bora ya wafanyakazi ni sasa".
Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakipita mbele ya mgeni rasmi (hayupo pichani) kwa shangwe na furaha huku wakiwa wameinua juu bango lao wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani (Mei Mosi)
Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa kwenye maadhimisho ya Mei Mosi jijini Dodoma
Ilikuwa ni shangwe na furaha kwa Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki waliopo jijini Dar es Salaam kuadhimisha siku yao ya wafanyakazi inayoadhimishwa duniani kote tarehe 1 Mei kila mwaka
Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki waliopo jijini Dar es Salaam wakiwa katika Picha ya pamoja.



Prof. Kabudi ashiriki maadhimisho ya siku ya Taifa la Uholanzi

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akihutubia kwenye kuadhimisha siku ya Taifa la Uholanzi, kulia ni Balozi wa Uholanzi nchini Mhe. Jeroen Verheul.

Prof. Palamagamba ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alitumia fursa hiyo kuelezea mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na Uholanzi katika sekta mbalimbali zikiwemo Kilimo, Elimu, Biashara na Ujenzi wa Miundombinu. Pia alilipongeza taifa hilo kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania kwenye kuleta maendeleo nchini.

Aidha, Prof. Kabudi alieleza kuwa Tanzania inaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji ili kuwavutia wawekezaji wa Uholanzi kuja kuwekeza nchini kwa wingi, ambapo alieleza kuwa mpaka sasa Uholanzi ni miongoni mwa nchi 10 zinazoongza kwa uwekezaji nchni, ambapo imewekeza jumla ya miradi 159 Tanzania.

Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Makamu wa Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Mabalozi mbalimbali wanao ziwakilisha nchi zao hapa pamoja na wawakilishi wa mashirika ya Kimataifa. 

Prof. Palamagamba John Kabudi akiendelea kuhutubia  kwenye maadhimisho hayo. 
Sehemu ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchni zao hapa pamoja na wageni mbalimbali wakimsikiliza kwa makini Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani) alipokuwa akihutubia.
Juu na chini ni sehemu nyingine ya wageni waalikwa aliohudhuria maadhimisho hayo wakisikiliza hotuba hiyo ya Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Hayupo pichani).



Prof. Palamagamba John Kabudi(Mb.) akigonganisha glasi na Mhe. Balozi Jeroen Verheul kwa kuwatakia viongozi wa Tanzania na Uholanzi Nguvu na Afya Njema.
Prof. Palamagamba John Kabudi(Mb.) akigonganisha glasi na Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal.
Prof. Palamagamba John Kabudi akizungumza na Mabalozi pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria maadhimisho hayo.
Sehemu Nyingine ya wageni waalikwa wakisalimiana na kubadilishana mawazo wakati wa maadhimisho hayo yakiendelea. 
Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria maadhimisho hayo.









Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje washiriki maadhimisho ya Mei Mosi kwa kishindo jijini Dodoma

Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,  Mhe. Dkt. Binilith Mahenge (katikati) na viongozi wengine akiwemo Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula (kushoto) wakiwa wamesimama kuwasalimu Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (hawapo pichani) walipopita mbele ya jukwaa kuu wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma tarehe 1 Mei 2019. Kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka 2019 ni  "Tanzania ya uchumi wa Kati inawezekana, wakati wa mishahara na maslahi bora ya wafanyakazi ni sasa".
Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakipita mbele ya mgeni rasmi (hayupo pichani) kwa shangwe na furaha huku wakiwa wameinua juu bango lao wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani (Mei Mosi)
Sehemu ya wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa kwenye maadhimisho hayo
Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa na bango la Wizara wakati wa maadhimisho ya mei Mosi jijini Dodoma.
Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa kwenye maadhimisho ya Mei Mosi jijini Dodoma
Ilikuwa ni shangwe na furaha kwa Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  kuadhimisha siku yao ya wafanyakazi inayoadhimishwa duniani kote tarehe 1 Mei kila mwaka
Wafanyakazi waWizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa na ari katika kuadhimisha siku yao
Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakijumuika na wenzao duniani kote kuadhimisha Mei Mosi

Sehemu nyingine ya Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Juu na chini ni umati wa Wafanyakazi kutoka Wizara, Sekta na Taasisi mbalimbali wakiadhimisha siku ya wafanyakazi duniani


Wafanyakazi wa Wizara ya Mabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa jukwaani wakati wa maadhimisho ya Mei Mosi
Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani
Sehemu nyingine ya Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa uwanjani wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani
Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki walishiriki kwa wingi kuadhimisha siku yao


Sehemu nyingine ya wafanyakazi hao wakiwa kwenye maadhimisho ya Mei Mosi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma
Ni nyuso za tabasamu kama zinavyoonekana kwa Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki waliposhiriki kikamilifu maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani
Watoto hawakuachwa nyuma na wazazi wao ambao ni Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuja kuadhimisha siku ya mfanyakazi duniani kama inavyoonekana pichani
Juu na chini ni sehemu ya Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani
Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiungana na wafanyakazi wengine kuimba wimbo wa mshikamano "Solidarity Forever" kama wanavyoonekana pichani


Picha ya pamoja