Friday, December 13, 2019

TANZANIA, KENYA ZAAHIDI KUENDELEZA NA KUKUZA MAENDELEO

Tanzania na Kenya zimeahidi kuendeleza na kushirikiana katika kuhakikisha kuwa maendeleo baina ya nchi hizo yanakuwa kila wakati. 

Akihutubia sherehe za maadhimisho ya 56 ya Jamhuri ya Kenya, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amesema kuwa Tanzania na Kenya ni ndugu na nchi hizo zitaendelea kushikiana katika kuhakikisha kuwa maendeleo baina ya nchi hizo yanakuwa kila wakati.

"Sisi Tanzania na Kenya ni ndugu wa damu, kwa hiyo basi tunawatakia sana kila la kheri katika kuiletea Kenya maendeleo…lakini mjue kuwa maendeleo ya Kenya ni maendeleo ya pia ya Tanzania, maendeleo pia ya Uganda, ni maendeleo pia Burundi, maendeleo pia Rwanda na Maendeleo pia ya Sudani Kusini na ni maendeleo pia ya jumuiya ya Afrika Mashariki" Amesema Prof. Kabudi

Kwa upande wake, Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa umoja na mshikamano ambao imekuwa ikionesha kwa Kenya na kusema kuwa umoja huo umekuwa ni chachu ya maendeleo kwa Tanzania na Kenya.

"Napenda kuwafahamisha kuwa umoja na mshikamano wetu umekuwa chachu ya maendeleo baina ya mataifa haya mawili…..tukumbuke kuwa umoja ni nguvu na dhamira yetu ni kushirikiana na mataifa yote duniani. Na dhamira yetu ni kuishi kwa amani umoja na mshikamano ili kukuza uchumi wetu," Amesema Balozi Kazungu

Aidha, Balozi Kazungu amebainisha kuwa Tanzania itaendelea kuwa ya kipekee kwa taifa la Kenya kutokana na mshikamano ambao imekuwa ikionesha kwa nchi ya Kenya kijamii, kisiasa na kiuchumi.

"Itakumbukwa kuwa, mwezi Aprili 2019 Kenya tulipokutana na Tanzania jijini Arusha tuliweza kuondoa vikwazo vya biashara 25 kati ya 37, hii inadhihirisha ni kwa jinsi gani Kenya na Tanzania na ndugu ambao wanapenda kukuza na kuendeleza maendeleo ya biashara" ameongeza Balozi Kazungu.



Baadhi ya wageni waalikwa wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho ya miaka 56 ya Jamhuri ya Kenya jana jijini Dar es Salaam  

Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu akigonga glasi na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) ikiwa ni ishara ya upendo, umoja na mshikamano baina ya nchi hizo mbili mara baada ya kuzindua rasmi maadhimisho ya miaka 56 ya Jamhuri ya Kenya jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwasilisha hotuba yake wakati wa maadhimisho ya miaka 56 ya Jamhuri ya Kenya yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu


Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu akihutubia hadhara iliyojitokeza wakati wa maadhimisho ya miaka 56 ya Jamhuri ya Kenya jana jijini Dar es Salaam  
Baadhi ya wageni waalikwa wakiimba nyimbo za taifa za Tanzania pamoja na Kenya kabla ya kuanza rasmi kwa sherehe za maadhimisho ya miaka 56 ya Jamhuri ya nchi hiyo.





Wednesday, December 11, 2019

KATIBU MKUU AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA CHINA


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (kushoto) akisaini kitabu cha Wageni alipokutana kwa mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China Mhe. Chen Xiaoding (kulia) jijini Beijing, China Desemba 11, 2019. Dkt. Mnyepe yupo nchini humo kushiriki Mkutano wa Pili wa Jukwaa la Haki za Binadamu kwa Nchi zinazoendelea.

Dkt. Mnyepe amemuhakikishia Mhe. Chen kuwa, Tanzania itaendelea kudumisha ushirikiano na China kupitia Jukwa la Ushirikiano kati ya Afrika na China (Forum on China-Africa Cooperation - FOCAC). Aidha, kwa pamoja wamekubaliana kuendelea kushirikiana katika kuhakikisha kuwa, mageuzi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa yanakuwa na tija kwa chi zinazoendelea hususan nchi za Afrika.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (kushoto) naNaibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China Mhe. Chen Xiaoding wakiwa katika picha ya pamoja jijini Beijing, China.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (kushoto) akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China Mhe. Chen Xiaoding walipokutana kwa mazungumzo jijini Beijing, China Desemba 11, 2019 

KATIBU MKUU DKT. MNYEPE ASHIRIKI MKUTANO WA HAKI ZA BINADAMU BEIJING, CHINA.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe yuko nchini China kushiriki Mkutano wa Pili wa Jukwaa la Haki za Binadamu kwa nchi zinazoendelea unaofanyika jijini Beijing nchini humo. 

 Mkutano huu ulioandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya China kwa kushirikiana na Ofisi ya Habari ya Baraza la Taifa la nchini humo, unalenga kuzikutanisha  nchi zinazoendelea kwa lengo la kubadilishana taarifa na kujadili kwa pamoja masuala ya Haki za Binadamu.

Dkt. Mnyepe  ambaye pia aliwasilisha salaam za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika Mkutano huo amesema, Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi zingine duniani katika kulinda na kutetea Haki za Binadamu na utawala bora sambamba na kuendelea kuheshimu, na kufuata Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu kutoingilia masuala ya ndani ya nchi.

Akizungumza katika mkutano huo Dkt. Mnyepe, ameelezea hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano ambazo kwa kiasi kikubwa zimechangia kuboresha mazingira ya upatikanaji wa huduma za msingi kwa wananchi. 

Hatua hizo ni pamoja  na utelezaji wa sera ya elimu bure, uboreshwaji wa mazingira ya uwekezaji na biashara, kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma za afya, na ujenzi wa miundombinu ya barabara na nishati ambayo itarahisisha na kupunguza gharama za upatikanaji wa huduma kwa wananchi.

Aidha, Katibu Mkuu Dkt. Mnyepe katika mkutano huo ameendelea kusisitiza dhamira ya Tanzania ya kuitaka Jumuiya ya Kimataifa kuondoka vikwazo dhidi ya Zimbabwe. 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe akizungumza kwenye Mkutano wa Pili wa Jukwaa la Haki za Binadamu kwa nchi zinazoendelea unaofanyika jijini Beijing, China.
Sehemu ya hadhira iliyojitokeza kwenye Mkutano wa Pili wa Jukwaa la Haki za Binadamu kwa nchi zinazoendelea wakifuatilia hotuba iliyokuwa ukitolewa na Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe akizungumza kwenye Mkutano wa Pili wa Jukwaa la Haki za Binadamu kwa nchi zinazoendelea unaofanyika jijini Beijing, China.    

Saturday, December 7, 2019

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

EURO MILIONI 140 KUWANUFAISHA WAKULIMA WA MAHINDI NA KOROSHO WA NCHI ZA AFRIKA,CARIBBEAN NA PACIFIC (ACP) TANZANIA IKIWEMO.
Jumla ya Euro milioni 140 zimetengwa ili kuwanufaisha wakulima wa mazao ya korosho na mahindi katika mpango maalum wa kutoa mikopo,kujenga uwezo katika uzalishaji,masoko,uwekezaji na kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao hayo kwa wakulima wa nchi za Afrika,Caribbean na Pacific jambo litakalosaidia kupunguza umasikini na njaa katika nchi hizo.

Akizungumza katika mkutano wa 110 wa nchi za Afrika,Caribbean na Pacific uliofunguliwa na makamu wa rais wa Kenya Mhe. William Ruto jijini Nairobi nchini Kenya,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amesema Tanzania imetoa hoja ya kutaka mazao ya korosho na mahindi kuongezwa katika mazao ya vipaumbele kwa nchi za ACP jambo ambalo limeridhiwa na kuungwa mkono nan chi za Benin na Burkinafaso.

Ameongeza kuwa kukubalika kwa hoja hiyo iliyowezesha mazao hayo kuingizwa katika moja ya mazao ya vipaumbele kwa nchi za ACP Serikali ya Tanzania itajipanga kupitia wizara husika ili kuandaa mapendekezo ya namna ambayo wakulima wa Tanzania watanufaika na program hiyo sambamba na mazao mengine yakiwemo pamba,miwa na kahawa.

Aidha,Waziri Kabudi amesema kuwa kupitia program hiyo maalum ya ACP  wakulima wa korosho na mahindi watawekewa mikakati ya kusaidiwa katika uzalishaji,kutafutiwa masoko na mbinu za uwekezaji sanjari na kuongeza mnyororo wa  thamani na kusaidiwa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi yanayoweza kuathiri uzalishaji wa mazao hayo.

Program hiyo ya ACP imetajwa kuwa mkombozi kwa nchi hizo katika jitihada za kupunguza umasikini na ukosefu wa chakula kwa kuwa  unalenga zaidi wakulima wa chini na wa kati hususani wanawake na vijana.

Mazao mengine yaliyopo katika mpango wa nchi za Afrika,Caribbean na Pacific kwa muda mrefu sasa licha ya kuwa Tanzania haijatumia fursa hiyo kikamilifu ni pamoja na Pamba,kahawa na cocoa kwa nchi nyingi za Afrika nan dizi,miwa,kava na raum kwa nchi za Caribbean na Pacifiki.

Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Kenya Balozi Pindi Chana amesema Ubalozi wa Tanzania Nchini humo unafuatilia kwa ukaribu mkutano huo kwa kuwa utatoa fursa mbalimbali ambazo zitaiwezesha Tanzania kunufaika nazo hususani kupitia mazao ya kilimo jambo ambalo litasaidia kupunguza umasikini na ukosefu wa ajira hususani kwa akina mama na vijana.

Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

MHE.WILLIAM RUTO AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA MAWAZIRI WA ACP

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. William Ruto akifungua Mkutano wa 110 wa Baraza la Mawaziri kwa Nchi za Afrika,Caribbean na Pacific (ACP) katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta (KICC) unaoendelea Nairobi-Kenya
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika mkutano wa Baraza la Mawaziri wa nchi za Afrika,Caribbean na Pacific (ACP) unaoendelea Katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Kenyatta (KICC) Jijini Nairobi,Kenya

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa anajadiliana jambo na Balozi anayeiwakilisha Tanzania Nchini Ubelgiji na Jumuiya ya Ulaya (EU) Balozi Jestas Nyamanga wakati wa Mkutano wa 110 wa nchi za Afrika,Caribbean na Pacific (ACP) ukiendelea Katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Kenyatta (KICC) Jijini Nairobi-Kenya.

Balozi wa Tanzania Nchini Kenya Balozi Pindi Chana akiwa anafuatilia mijadala mbalimbali katika mkutano wa 110 wa Baraza la Mawaziri wa nchi za Afrika,Caribbean na Pacific (ACP) unaoendelea Katinka ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Kenyatta (KICC)  Jijini Nairobi - Kenya



Friday, December 6, 2019

MAPENDEKEZO YA TANZANIA ACP YAUNGWA MKONO

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwasilisha hoja ya Tanzania katika Mkutano wa 110 wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Afrika,Carribean na Pacific (ACP) katika ushirikiano na Jumuiya ya Ulaya unaofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kenyatta (KICC) Nairobi, Kenya.
Nyuma ya Prof. Kabudi ni Balozi wa Tanzania Nchini Ubelgiji na Jumuiya ya Ulaya Balozi Jestas Nyamanga.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa anafuatilia mkutano wa Baraza la Mawaziri wa  nchi za Afrika,Carribean na Pacific (ACP).
Nyuma ya Prof. Kabudi ni Balozi wa Tanzania Nchini Kenya Balozi Pindi Chana akifuatiwa na  Balozi wa Tanzania Nchini Ubelgiji na katika Jumuiya ya Ulaya Balozi Jestas Nyamanga


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa anajadiliana jambo na Balozi wa Tanzania Nchini Ubelgiji na katika Jumuiya ya Ulaya Balozi Jestas Nyamanga (aliyesimama) akifuatiwa na Balozi wa Tanzania Nchini Kenya Balozi Pindi Chana pamoja na baadhi ya maafisa wa Ubalozi na wa Wizara ya Mambo ya NJe na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kenyatta (KICC) Nairobi Kenya.

                        TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

TANZANIA YATOA MAPENDEKEZO YAKE KATIKA MKUTANO WA ACP NA KURIDHIWA NA BARAZA LA MAWAZIRI WA NCHI ZA ACP.

Tanzania imetoa mapendekezo makuu matatu na yamekubaliwa katika kikao cha mashauriano baina ya Mawaziri wa Baraza la Nchi za Afrika,Carribean na Pacific kilichoanza leo jijini Nairobi, Kenya. 

Mapendekezo hayo ya Tanzania yametolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Prof. Palamagamba John Kabudi katika Mkutano wa 110 wa Baraza la mawaziri wa wa Nchi za Afrika,Carribean na Pacific katika ushirikiano na Jumuiya ya Ulaya ambao utafuatiwa na Mkutano wa tisa wa wakuu wa Nchi na Serikali katika jiji la Nairobi Nchini Kenya na kuongeza kuwa Tanzania imetoa mapendekezo hayo ili kutodhoofisha umoja wa ACP hususani katika kipindi hiki ambacho nchi hizo ziko katika majadiliano ya kina na Jumuiya ya ulaya kuhusu mkataba mpya wa ushirikiano baada ya mkataba wa sasa unaofikia ukomo Februari mwakani.

Mapendekezo ya Tanzania yaliyokubaliwa na kuingizwa kama sehemu ya maazimio ya Baraza la Mawaziri ni hoja ya kutokuruhusu wanachama washiriki nje ya wanachama wa ACP, (Associate members),kutoingiza wanachama watazamaji kutoka katika makundi yaliyoganyika kutoka katika serikali zao na ambazo  hazitambuliwi  na mamlaka za serikali za nchi wanachama pamoja na kutaka majadiliano ya kisiasa baina ya nchi za ACP na Umoja wa Ulaya kuendelea kusalia katika mamlaka za serikali za Nchi za Afrika,Carribean na Pacific badala ya kuyaamishia katika Bunge la ACP.


Ameitaja sababu nyingine kuwa ni kuepuka mivutano isiyo na tija kati ya Nchi za Afrika,Carribean na Pacific na Nchi za Jumuiya ya Ulaya hususani katika nyakati ambazo nchi hizo zinahitaji mshikamano mkubwa zikiwa zinapita katika  kipindi muhimu cha kujenga uchumi na ustawi wa jamii ya nchi zao na pia kujenga wigo wa kuaminiana baina ya Nchi wanachama.

Ameongeza kuwa majadiliano baina ya Nchi wanachama wa ACP ni muhimu ili kupitia upya mkataba wa George Town,mkataba ambao ndiyo ulianzisha Kundi la ACP na kusainiwa katika jiji la Goergetown nchini Guyana mwaka 1975. Nchi za ACP zimekubaliana kufanya mabadiliko makubwa ya Mkataba huo ili kujenga Umoja wa ACP unaoendana  na mabadiliko ambayo yamejitokeza ulimwenguni na masuala mbalimbali ya Kimataifa ambayo yanahitaji mtazamo mpya.

Prof. Kabudi amesema katika muktadha huo wa majadiliano, Tanzania imetoa mapendkezo hayo matatu ambayo yote yamekubaliwa na kuungwa mkono na  nchi zote 79 wananchama wa ACP  jambo linaloonesha kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaheshimika sana  katika masuala ya kimataifa.

Akizungumzia juu ya faida ya Mkutano huo wa Nchi za Afrika,Carribean na Pacific , Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji ambaye pia anaiwakilisha Tanzania katika Jumuiya ya Ulaya Balozi Jestas Abuok Nyamanga amesema kuwa mkutano huo unatumika kama kutoa fursa kwa nchi 79 wanachama wa ACP kutathmini changamoto mbalimbali zinazokabili nchi hizo, kuweka mikakati ya pamoja na kuwa na sauti ya pamoja katika kusimamia utekelezaji wa mikakati hiyo na katika majadiliano na Jumuiya ya Ulaya. Alisema kuwa miongoni mwa masuala yatakayojadiliwa na kuwekewa mikakati ya pamoja ni pamoja na masuala yanayohusu uwekezaji, viwanda na biashara; uongezaji wa mnyororo wa thamani katika mazao ya kilimo, kuongeza uwezo na wigo wa ukusanyaji wa kodi. Mkutano huo pia unajadili namna ya kuwaongezea uwezo wafanyabiashara wadogo,kuongeza ubunifu na matumizi sahihi ya teknolojia  na kukabiliana na mabadiliko ya tabiachi. Masuala yote hayo ni moja ya kipaumbele cha serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu hii ya tano inayoongozwa na Dkt John Pombe Magufuli.

Amehitimisha kwa kusema katika mkutano huu Katibu Mkuu wa ACP anatarajiwa kuchaguliwa ili kuweka mfumo mpya wa kiuongozi utakaosaidia wanachama wa ACP kupita katika ushirikiano kwa miaka  mingine ijayo katika ushirikiano baina ya nchi za Afrika,Carribean na Pacific na Jumuiya ya Ulaya.  



Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliaono ya Serial,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
06 Desemba,2019
Nairobi - Kenya.

CALL FOR APPLICATION FOR INCLUSION IN THE SADC SECRETARIAT DATABASE OF FREELANCE INTERPRETERS








Thursday, December 5, 2019

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI INASHIRIKI KATIKA MAONESHO YA VIWANDA DAR ES SALAAM




Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inashiriki katika Maonesho ya Nne ya Viwanda yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE).

Kupitia Maonesho hayo, Wananchi wanaelimishwa kuhusu majukumu ya Wizara na utekele zaji wake na namna wizara na balozi za Tanzania zinavyofanya kazi ya kuvutia watalii na wawekezaji kuja nchini kutembelea vivutio vya kitalii na kuwekeza nchini.

Maonesho hayo ni utekelezaji kwa vitendo  kwa azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga Uchumi wa Viwanda ili kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2021.

Kauli mbiu ya maonesho hayo ya Tanzania sasa Tunajenga Viwanda inalenga kujenga na kuimarisha utamaduni wa Watanzania kutambua, kununua na kuthamini bidhaa zinazozalishwa nchini.

Maonyesho ya Nne ya Viwanda yanahusisha wadau wa Sekta ya Viwanda na yataonesha fursa zilizopo katika katika sekta ya viwanda na yatatoa fursa kwa wadau kuzungumza na kujadili  namna ya kujenga mahusiano endelevu ya biashara.


Maonyesho hayo pia yatawezesha kufanyika  kwa mikutano ya wafanyabiashara ambayo itawakutanisha wauzaji na wanunuzi .


Afisa wa Wizara akiwa ndanii ya Banda la Wizara tayari kwa ajili ya kuwahudumia wananchi watakaotembelea Maonesho ya Nne ya Viwanda yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Ukuzaji Biashara Tanzania (TANTRADE) yaliyoanza tarehe 5, Desemba 2019 katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam
Maafisa wa Wizara wakiwa ndanii ya Banda la Wizara tayari kwa ajili ya kuwahudumia wananchi watakaotembelea Maonesho ya Nne ya Viwanda yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Ukuzaji Biashara Tanzania (TANTRADE) yaliyoanza tarehe 5, Desemba 2019 katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.

Maafisa wa Wizara wakiwa ndani ya Banda la Wizara tayari kwa ajili ya kuwahudumia wananchi watakaotembelea Maonesho ya Nne ya Viwanda yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Ukuzaji Biashara Tanzania (TANTRADE) yaliyoanza tarehe 5, Desemba 2019 katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.
 
 

Tuesday, December 3, 2019

TANZANIA KUIMARISHA, KUENDELEZA USHIRIKIANO NA FALME ZA KIARABU (UAE)

Serikali ya Tanzania imeahidi kuendeleza ushirikiano wake na Falme za Kiarabu (UAE) katika sekta za biashara, miradi ya maendeleo, utalii, utamaduni, usafirishaji, kilimo na afya.

Akiongea katika maadhimisho ya 48 ya Falme za Kiarabu (UAE) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam jana Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amesema kuwa ili kukuza na kuendeleza ushirikiano baina ya nchi hizo mbili ni muhimu pia kupanua maeneo ya ushirikiano kati ya nchi zetu mbili hyaakiwemo ya utalii, kilimo na miradi mbalimbali ya maendeleo.

"Tayari tumeanza maandalizi ya mkutano wa pili wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Falme za Kiarabu (UAE) ambao utafanyika hapa nchini Tanzania mwaka 2020, baada ya mkutano wa kwanza wa JPC ambao ulifanyika Desemba 2016 Abu Dhabi wakati ambao, makubaliano hayo yalipo sainiwa," Amesema Prof. Kabudi

Prof. Kabudi aliongeza kuwa, makubaliano hayo yaliyosainiwa Abu Dhabi ni pamoja na Mkataba wa Ushirikiano kwenye Huduma za Usafiri wa Anga (BASA) na Mkataba wa ushirikiano katika sekta ya Utalii. Tunatarajia kupanua wigo wa ushirikiano wetu katika mkutano ujao wa JPC.

Kama moja ya Makati wa uwekezaji, tuko tayari kuhakikisha kuwa wawekezaji wanawekeza Tanzania. Aidha, mbali na maboresho ya mfumo wa udhibiti wa biashara Tanzania 'Blue Print' yaliyoanza Julai, 2019, tunafanya mashauriano ya ndani mkataba wa kuepusha na na tozo za ushuru mara mbili; na makubaliano ya mkataba wa pamoja juu ya kukuza na kuendeleza ulinzi wa uwekezaji aambapo kwa makubaliano haya ni chanzo cha Falme za Kiarabu (UAE)  kuwekeza Tanzania.

"UAE imekuwa ikisaidia katika ufadhili wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayolenga kusaidia juhudi za Tanzania kufikia maendeleo ya kiuchumi na kijamii kama vile ufadhili wa ujenzi wa barabara kutoka Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi (ADFD). Ni matumaini yangu kuwa Mfuko utaendeleza usaidizi na kuelekeza miradi mingine ya maendeleo," Amesema Prof. Kabudi.

Kwa upande wake, Kwa upande wake, Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Tanzania, Balozi, Khalifa Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi amesema kuwa Falme za Kiarabu zitaendeleza ushirikiano baina yake na Tanzania kindugu, kidiplomasia, kiuchumi na kuhakikisha kuwa ni wa kudumu.

"Napenda kuwafahamisha kuwa Falme za Kiarabu (UAE) utaendelea kuwekeza hapa nchini Tanzania ikiwa ni ishara ya kukuza uchumi. Tutaendelea kuwaeleza wawekezaji fursa zilizopo Tanzania ili waendelee kuja kuwekeza" Amesema Balozi, Mohamed Al-Marzooqi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwasilisha hotuba yake wakati wa maadhimisho ya 48 ya Falme za Kiarabu (UAE) yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam



Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Tanzania, Balozi, Mhe. Khalifa Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi akihotubia wageni waalikwa katika maadhimisho ya 48 ya Falme za Kiarabu (UAE) yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam
Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Tanzania, Mhe. Balozi, Khalifa Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi akimpongeza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) mara baada ya kumaliza kuhutubia wageni waalikwa katika maadhimisho ya 48 ya Falme za Kiarabu (UAE) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam


























Baadhi ya wageni waalikwa wakiimba nyimbo za taifa za Tanzania pamoja na ya Falme za Kiarabu (UAE) kabla ya kuanza rasmi kwa maadhimisho







Tanzania na Namibia Zajizatiti kukuza Biashara baina yao


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akisalimiana na Waziri wa Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa wa Namibia, Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah mara baada ya Mhe. Nandi-Ndaitwah kuwasili katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere kwa ajili ya kushiriki mkutano wa Tume ya Kudumu ya  Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Namibia.
Naibu Waziri Mkuu naWaziri wa Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa wa Namibia, Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa AAfrika Mashariki, Dkt. Faraji K. Mnyepe.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa wa Namibia, Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah akiangalia picha za matukio ya wapigania uhuru wa nchi za Kusini mwa Afrika ikiwemo Namibia.

Naibu Waziri Mkuu naWaziri wa Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa wa Namibia, Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah akiweka saini Kitabu cha Wageni alipowasili Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwasilisha hotuba yake wakati wa kuhitimisha Mkutano wa pili wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Namibia leo jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa wa Namibia, Balozi Selma Ashipala-Musavyi, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa wa Namibia, Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb), Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko, (Mb) pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa, (Mb)
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa wa Namibia, Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah akiwasilisha hotuba yake wakati wa kuhitimisha Mkutano wa pili wa Tume ya Kudumu ya pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Namibia leo jijini Dar es Salaam. Wenginine kutoka kushoto ni  Katibu Mkuu wa Wizara ya Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa wa Namibia, Balozi Selma Ashipala-Musavyi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb), Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb), Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko (Mb) pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb)
Baadhi ya Makatibu Wakuu, maafisa waandamizi wa Serikali, maafisa wa Serikali pamoja na waandishi wa habari wakifuatilia ufunguzi wa mkutano wa JPC leo jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri Kuu na Waziri wa Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa wa Namibia, Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb) wakiweka saini Hati ya Makubaliano ya kushirikiana katika Utamaduni, Sanaa na Michezo kati ya Tanzania na Namibia. 

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa wa Namibia, Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb) wakibadilishana Hati ya Makubaliano ya kushirikiana katika Utamaduni, Sanaa na Michezo kati ya Tanzania na Namibia.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa wa Namibia, Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah wakisaini Hati ya Makubaliano ya kushirikiana katika Masuala ya Utalii kati ya Tanzania na Namibia

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa wa Namibia, Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah wakibadilishana Hati ya Makubaliano ya kushirikiana katika Masuala ya Utalii kati ya Tanzania na Namibia.

Meza kuu katika picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb), Balozi wa Namibia nchini Tanzania Mhe. Theresia Samaria Naibu Waziri Mkuu na Waziri Wizara ya Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa ya Namibia, Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb), Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko, (Mb) na Waziri wa Viwanda Mhe. Innocent Bashungwa, (Mb) Pamoja na Makatibu Wakuu, na Viongozi waandamizi wa Serikali.