Friday, February 21, 2020

BALOZI IBUGE AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA KUWAIT NCHINI TANZANIA


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Balozi Mubarak Mohammed Alsehaijan katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Pamoja na mambo mengine, mazungumzo hayo yalijadili mambo mbalimbali ikiwemo kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na Kuwait kupitia Nyanja mbalimbali ikiwemo uwekezaji wa miradi na biashara pamoja na uundwaji wa tume ya kudumu ya pamoja ya ushirikiano.

Aidha, Mhe. Balozi Alsehaijan alitumia fursa hiyo kumkabidhi Katibu Mkuu, Balozi Ibuge salamu za rambirambi kufuatia ajali zilizotokea hapa nchini hivi karibuni.

Kwa upande wake Balozi Ibuge, alimweleza Mhe. Balozi Alsehaijan umuhimu wa kuendeleza jiji la Dodoma na kumkaribisha jijini Dodoma.

Mazungumzo hayo yamefanyika siku moja baada ya Ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania kusheherejea 59 ya Uhuru wake na miaka 29 ya ukombozi wa taifa hilo yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge, akimkaribisha Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Balozi Mubarak Mohammed Alsehaijan leo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Balozi Mubarak Mohammed Alsehaijan akimuelezea jambo Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge walipokutana katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

 
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge, akimulezea jambo Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Balozi Mubarak Mohammed Alsehaijan leo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Balozi Mubarak Mohammed Alsehaijan leo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam



VACANCY ANNOUNCEMENT



PRESS RELEASE

VACANCY ANNOUNCEMENT AT THE COMMONWEALTH SECRETARIAT

The Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation has received vacancy notification from the Commonwealth Secretariat inviting qualified Tanzanians to apply for the post of Economic Adviser-Trade Policy Analysis.

Application details can be found through the Secretariat’s website, http://thecommonwealth.org/jobs. Closing date for application is Friday 28th February, 2020.

“The Ministry encourages qualified Tanzanians to apply”.



Issued by:
Government Communication Unit,
Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation,
Dodoma.
21ST February, 2020.

Wednesday, February 19, 2020

UBELGIJI NA TANZANIA  ZAPANIA KUDUMISHA URAFIKI NA KUONGEZA USHIRIKIANO.
 Ubelgiji na Tanzania zimedhamiria kudumisha urafiki na kuongeza zaidi ushirikiano katika ubia wa maendeleo, uwekezaji, biashara, utalii na masuala mengine ya Kikanda na kimataifa. Hayo yalielezwa wakati wa mazungumzo baina ya Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Mheshimiwa Jestas Abuok Nyamanga na  Mfalme wa Ubelgiji, Mtukufu Philippe  wakati Balozi Nyamanga akiwasilisha Hati zake za utambulisho kwa Mfalme huyo katika kasri yake jijini Brussels  tarehe 6 Februari 2020.
Wakati wa utambulisho huo, Balozi Nyamanga aliwasilisha salaam za Mheshimiwa Dkt John Pombe Joesph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Mfalme huyo na kueleza jinsi Tanzania inavyoridhika na urafiki na ushirikiano mzuri uliodumu kwa miaka mingi baina ya nchi mbili na imedhamiria kuueleza ushirikiano huo na kupanua wigo wake.
Balozi Nyamanga katika mazungumzo hayo  amemweleza  Mfalme Philippe, juhudi za pekee zinazofanywa na serikali inayoongozwa na Rais Magufuli katika kuweka msingi wa uchumi wa viwanda;  kufungamanisha ukuaji wa uchumi na maendeleo ya watu; kuboresha mazingira wezeshi kwa uendeshaji wa biashara na uwekezaji; na kuimarisha usimamizi wa utekelezaji wa mipango mbalimbali  ya kitaifa, kikanda na kimataifa. 
Aidha, Balozi Nyamanga amemweleza Mfalme Philippe kuwa Tanzania imedhamiria kushirikiana na Ubelgiji hususan katika ubia wa maendeleo, biashara na uwekezaji wenye kuleta faida kwa pande zote.
 Kwa upande wake,   Mfalme huyo wa Ubelgiji ambaye kwa kuipenda Tanzania miaka ya nyuma  amewahi kuja Tanzania kwa mapumziko binafsi Zanzibar na kueleza kuwa Tanzania ni nchi muhimu kwa Ubelgiji na hivyo nchi yake itaendeleza ushirikiano zaidi na Tanzania katika kufanikisha mipango mbalimbali ya maendeleo nchini pamoja na kushirikiana katika masuala ya amani na usalama hususan kwa wa nchi za Maziwa Makuu na ajenda zingine zinazogusa maslahi ya nchi zetu mbili kimataifa. 
Ubelgiji ni miongoni mua Nchi zinazoongoza kwa uwekezaji nchini Tanzania ikiwa inashika nafasi ya kumi kati ya nchi zaikai ya 90 zilizowekeza nchini Tanzania. Aidha kutokana na ushirikiano mzuri uliopo Tanzania ni kati ya nchi 14 zinazoendelea duniani ambazo Ubelgiji imeingia nazo makubaliano maalum ya ushirikiano wa ubia wa maendeleo (Developmet Coop[eration Framework)


Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Mheshimiwa Jestas Abuok Nyamanga akiwa na  Mfalme wa Ubelgiji, Mtukufu Philippe mara baada ya kuwasilisha Hati zake za utambulisho kwa Mfalme huyo katika kasri yake Jijini Brussels - Ubelgiji Februari 06,2020.

Tuesday, February 18, 2020

Katibu Mkuu Mwaluko azitaka sekta zishirikiane kukabili maafa


Na. OWM, ZANZIBAR

“Tatizo la athari za maafa yanayotokana na majanga ya asili linahitaji ushiriki wa sekta zote ili kukabiliana nalo ipasavyo, katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)” Mwaluko.

Kauli hiyo imetolewa leo mjini Zanzibar na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko wakati alipokuwa anafungua kikao cha SADC cha Makatibu Wakuu wenye dhamana ya maafa katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), ambaye yeye ni mwenyekiti.

 Mwaluko amesema nchi zote za SADC zina uzoefu wa masuala ya maafa, hivyo ni matarajio yake kuwa kazi waliyopewa ya kuandaa nyaraka kwa ajili ya mkutano wa Mawaziri wenye dhamana ya maafa utakaofanyika siku ya Ijumaa tarehe 21 Februari 2020,  uweze kufikia malengo yake.

Katika kikao hicho, Makatibu Wakuu wataandaa nyaraka itakayo ainisha mikakati na programu za kukabiliana na maafa na mpango unaobainisha namna nchi za SADC zilivyojipanga kukabiliana na maafa yanapotokea katika ukanda huo.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mtendaji wa SADC wa Masuala ya Ushirikiano wa Kikanda, Dkt. Thembinkosi Mhlongo  alieleza kuwa athari za maafa zikiwemo vifo, uharibifu wa mali na miundombinu zimezikumba takribani nchi zote za SADC. Hivyo amesisitiza umuhimu wa nchi hizo kushirikiana kwa pamoja kuandaa mikakati ya menejimenti ya maafa.

Naye, Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar, Bw. Abdallah Hassan Mitawi amewaeleza  wajumbe wa kikao hicho kuwa nchi za SADC zimelipa umuhimu mkubwa suala la kukabiliana na athari za maafa na hilo linadhihirishwa na ushiriki wa nchi 15 kati ya 16 wanachama wa SADC katika mkutano huo.

Mkutano huo unaofanyika kwenye Hoteli ya Madinat AL Bahir iliyopo Mbweni, nje kidogo ya mji wa Zanzibar unatarajiwa kuhitimishwa kwa kikao cha ngazi ya Mawaziri tarehe 21 Februari 2020 ambapo Mgeni Rasmi atakuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein.

“Ushiriki wa kisekta kwenye Kupunguza madhara  ya maafa ni njia  bora ya kujenga Uhimili  katika ukanda wa nchi wanachama wa  Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)”
MWISHO.


Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko akifafanua umuhimu wa ushiriki wa kisekta kwenye Kupunguza madhara ya maafa, wakati akifungua kikao cha SADC cha Makatibu Wakuu wenye dhamana ya maafa katika ukanda wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), ambapo yeye ni mwenyekiti wa kikao hicho, leo tarehe 18 Februari 2020, Zanzibar.

Naibu Katibu Mtendaji wa SADC wa Masuala ya Ushirikiano wa Kikanda, Dkt. Thembinkosi Mhlongo akifafanua umuhimu wa Nchi  za SADC kuwa na mikakati ya kukabili maafa yanayo zikabili, wakati wa kikao cha SADC cha Makatibu Wakuu wenye dhamana ya maafa katika ukanda wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC, leo tarehe 18 Februari, 2020, Zanzibar
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar, Bw. Abdallah Hassan Mitawi akifafanua namna ya nchi za SADC zinavyoathirika na maafa ya asili, wakati wa kikao cha SADC cha Makatibu Wakuu wenye dhamana ya maafa katika ukanda wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC, leo tarehe 18 Februari, Zanzibar


Baadhi ya makatibu wakuu kutoka Tanzania, wakifuatilia kikao cha SADC cha Makatibu Wakuu wenye dhamana ya maafa katika ukanda wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC, leo tarehe 18, Februari, 2020, Zanzibar, (katikati), Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi,anayeshughulikia Mifugo,  Profesa Olesante Ole Gabriel (kulia kwake), Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Dkt. Faraij Mnyepe,  na Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio.

Baadhi ya maafisa waandamizi kutoka ukanda wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), wakifuatilia kikao cha SADC cha Makatibu Wakuu wenye dhamana ya maafa, leo tarehe 18 Februari, 2020, Zanzibar.


Baadhi ya maafisa waandamizi kutoka ukanda wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), wakifuatilia kikao cha SADC cha Makatibu Wakuu wenye dhamana ya maafa, leo tarehe 18 Februari, Zanzibar, Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali, Jimmy Matamwe,(kulia), Mkurugenzi wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa, Zanzibar , Makame Khatibu Makame na Naibu Mkurugenzi wa Kamisheni hiyo, Muhidin Ali Muhidin
Makatibu Wakuu wenye dhamana ya maafa katika ukanda wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC,wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo, leo tarehe 18, 2020, ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni “Ushiriki wa kisekta kwenye Kupunguza madhara  ya maafa ni njia  bora ya kujenga Uhimili  katika ukanda wa nchi wanachama wa  Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)”
Makatibu Wakuu na maafisa waandamizi wenye dhamana ya maafa katika ukanda wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC,wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo, leo tarehe 18, Februari, 2020, ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni “Ushiriki wa kisekta kwenye Kupunguza madhara  ya maafa ni njia  bora ya kujenga Uhimili  katika ukanda wa nchi wanachama wa  Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)”


NAIBU WAZIRI DKT.NDUMBARO AHITIMISHA ZIARA YAKE KATIKA ENEO LA USHOROBA WA MTWARA


Sunday, February 16, 2020

WAZIRI KABUDI: WATUMISHI FANYENI KAZI KWA BIDII NA USHIRIKIANO


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amewataka Watumishi wa Wizara hiyo kuchapa kazi kwa bidii na kuendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Katibu Mkuu mpya, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge.

Mhe. Prof. Kabudi ametoa rai hiyo jana jijini Dodoma wakati wa kikao na Watumishi wa Wizara ambapo pamoja na mambo mengine, kikao hicho kilitoa fursa ya kutakiana heri ya mwaka mpya 2020 na kumkaribisha Wizarani Katibu Mkuu Mpya, Balozi Kanali Ibuge.

Aidha, Mhe. Prof. Kabudi aliwaeleza watumishi hao kuwa, mwanzo wa mwaka ni kipindi kizuri cha kujipanga na kuweka mikakati ya namna bora ya kutekeleza majukumu  kwa ajili ya maendeleo ya Taifa ikiwa ni pamoja na kufahamu vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Joseph Pombe Magufuli.

Kadhalika amewataka kufanya kazi kwa bidii, kujitambua na kujenga umoja  na ushirikiano katika kutekeleza majukumu hayo kikamilifu.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge ameahidi ushirikiano kwa watumishi wa Wizara na kuwakumbusha kuwa kila mmoja ana wajibu mkubwa wa kuchangia maslahi mapana ya Taifa ilimradi kila mmoja atekeleze wajibu wake kwa kuendelea kujituma, kuwa tayari kurekebishwa, kuwa watiifu na kuwa tayari kupokea maelekezo.

"Watumishi wenzangu, kila mmoja hapa ana mchango mkubwa kwa maslahi ya Taifa letu. Ninasisitiza kuwa mwendelee kujituma, kufanya kazi kwa weledi, kuwa watiifu, kuwa tayari kurekebishwa na kuwa tayari kupokea maelekezo. Binafsi nitaendelea kutoa usikivu kwenu kama ilivyokuwa kwa watangulizi wangu" alisema Balozi Ibuge.

Kuhusu changamoto mbalimbali zinazoikabili Wizara, Balozi Kanali Ibuge amewataka Watumishi wote kushirikiana kuzitatua kwani hakuna changamoto ya kudumu endapo Watumishi wote watakuwa kitu kimoja.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiongea na Watumishi wa Wizara wakati wa kikao kilichofanyika jijini Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akiongea na watumishi wa wizara wakati wa kikao kilichofanyika jijini Dodoma

 Sehemu ya watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia kikao kilichofanyika jijini Dodoma 




NAIBU WAZIRI DKT.NDUMBARO AHITIMISHA ZIARA YAKE KATIKA ENEO LA USHOROBA WA MTWARA

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amehitimisha ziara yake katika Mikoa  inayopitiwa na mradi wa maendeleo wa kuboresha miundombinu ya Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (Mtwara Corridor). Mradi huu unahusisha ujenzi wa bandari ya Mtwara (ambao unaendelea kwa kasi), ujenzi wa barabara katika kiwango cha lami kuanzia Bandari ya Mtwara hadi bandari ya Mbamba Bay iliyopo Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma sambamba na ujenzi wa bandari hiyo.

Lengo la ziara hii ilikuwa ni kuangalia hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa miundombinu ya bandari na barabara katika ushoroba huo, kufanya mazunguzmzo na viongozi wa Serikali za Mikoa na Wilaya, ambapo Mheshimiwa Ndumbaro alitumia nafasi hiyo kuhimiza Mamlaka za Mikoa na Wilaya, kulinda na kuboresha uhusinao wa kidipolomasia na nchi tunazopakana nazo katika ukanda huo ili kujenga mazingira rafiki ya kibiashara, wakati huu ambao Serikali ya Awamu ya Tano imeboresha miundombinu inayowezesha kuzifikia nchi hizo kiurahisi zaidi.

Ujenzi wa miundombinu katika Ukanda wa Kusini mwa Nchi unachochea ukuaji wa biashara katika ukanda huo kwa kurahishisha usafirishaji na mawasiliano na kuzifikia kiurahisi Nchi jirani za Malawi, Kaskazini mwa Msumbiji na Zambia.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri wa Mambo Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Ndumbaro aliambatana na Balozi wa Malawi nchini Mhe.Glad Chembe Munthali, ambaye amefurahishwa na kuridhishwa na dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga mazingira rafiki ya kibiashara na nchi jirani kwa kuboresha miundombinu inayoziwezesha nchi hizo kunufaika na huduma za bandari nchini kiurahisi na kwa gharama nafuu. 

Kadhalika, nia ya Mhe. Munthali Balozi wa Malawi nchini, katika ziara hiyo ilikuwa ni kuangalia kwa namna gani wafanyabiashara kutoka nchini kwake watanufaika na uboreshwaji wa miundombinu ya ushoroba wa Mtwara katika kusafirisha bidhaa zao kwa muda mfupi na gharama nafuu. 

Aidha, kwa nyakati tofauti Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius G. Byakanwa, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mndeme na Mkuu wa Wilaya Nyasa Mhe. Isabela Chilluba wameelezea utayari wao wa kuratibu na kusimamia shughuli na fursa za biashara zinazotokana na maboresho ya miundombinu katika ukanda huo.

Ziara hii ni mwendelezo wa jitihada zinazofanywa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa  kushirikiana na Mamlaka mbalimbali za ndani katika utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi ambayo pamoja na mambo mengine inalenga kukuza biashara na kuvutia uwekezaji nchini.   

Ujenzi wa barabara ya Mtwara hadi bandari ya Mbamba Bay kwa kiwango cha lami unafikia ukingoni, mkandarasi anaendelea na ujenzi wa sehemu iliyosalia (Mbinga hadi Mbamba bay) ambapo anataraijia kukabidhi barabara hiyo Septemba, 2020.

Ujenzi wa miundombinu katika ushoroba wa Mtwara umeleta mapinduzi makubwa ya maendeleo ya uchumi na kijamii katika Mikoa ya Kusini mwa Tanzania sambamba na kuliongezea Taifa mapato.  
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius G. Byakanwa (kulia) wakiwa kwenye mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius G. Byakanwa akielezea jambo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro kwa kutumia kielelezo cha ramani, walipokuna kwa mazungunzumzo wakati wa ziara ya Dkt.Ndumbaro katika ushoroba wa Matwara. 
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius G. Byakanwa (kulia) na Balozi wa Malawi nchini Mhe.Glad Chembe Munthali (kushoto) wakiwa katika mazungumzo walipokutana wakati wa ziara ya Mhe. Dkt. Ndumbaro katika Mkoa huo
Kutoka kulia ni Mhe.Dkt. Damas Ndumbaro Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  Balozi wa Malawi nchini Mhe.Glad Chembe Munthali, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius G. Byakanwa, Bw. Alfayo Kidata Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara, na Mhe. Evod Mmanda Mkuu wa Wilaya ya Mtwara wakiwa katika picha ya pamoja.
Mhe.Dkt. Damas Ndumbaro Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  akisalimiana na Wafanyakazi wa Bandari ya Mtwara alipotembelea Ofisi za Bandari hiyo wakati wa ziara yake mkoani humo.
Mhe.Dkt. Damas Ndumbaro Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akizungumza na wafanyakazi wa Bandari ya Mtwara (hawapo pichani). Aliwahimiza kujituma na kuongeza ubunifu ili kuongeza  ufanisi na tija wa bandari hiyo ambayo ukarabati wa kuiboresha unaendelea.
Mhe.Dkt. Damas Ndumbaro Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiwa na Watendaji wa Bandari ya Mtwara na Viongozi wa Mkoa alipotembelea eneo la bandari ya Mtwara
Kutoka kushoto; Mhe.Dkt. Damas Ndumbaro Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Christina Mndeme Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, na Mhe.Glad Munthali Chembe Balozi wa Malawi nchini wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma. 
Mhe.Dkt. Damas Ndumbaro Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akisalimiana na Mhe. Isabela Chilluba Mkuu wa Wilaya ya Nyasa alipowasili wilayani humo kwa ziara ya siku moja
 Mkuu wa Wilaya Nyasa Mhe. Isabela Chilluba akitoka maelezo kwa Mhe.Dkt. Damas Ndumbaro Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  na Ujumbe wake katika moja ya fukwe na eneo la bandari ya Mbamba Bay iliyopo katika Ziwa Nyasa. 
Picha ya pamoja 


Wednesday, February 12, 2020

BALOZI IBUGE AKUTANA, AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI WA SHIRIKA LA IOM


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Uhamaji (IOM), kanda ya Kusini mwa Afrika Bw. Charles Kwenin katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Pamoja na mambo mengine, mazungumzo hayo yalijadili mambo mbalimbali ikiwemo maandalizi ya Majadiliano kuhusu Uhamaji katika kanda ya Kusini mwa Afrika yanayotarajia kufanyika chini ya uenyekiti wa Tanzania kama Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).

Majadiliano hayo yanatarajiwa kufanyika kabla ya mwezi Agosti, mwaka 2020 hapa nchini yakiwa na dhamira ya kujadili usimamizi wa masuala ya uhamiaji ili kuwezesha uundwaji wa sera zenye uwiano miongoni mwa nchi wanachama wa SADC.

Aidha, Balozi Ibuge amewahakikishia wajumbe wa IOM, utayari wa Tanzania kuwa nchi mwenyeji wa Majadiliano hayo.




Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Uhamaji (IOM), kanda ya Kusini mwa Afrika Bw. Charles Kwenin akiongea na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge leo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akiwaelezea jambo Mkurugenzi wa Shirika la (IOM), kanda ya Kusini mwa Afrika Bw. Charles Kwenin akiongea pamoja na Mwakilishi wa IOM hapa nchini Dkt. Qasim Sufi leo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge (watatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa (IOM), Bw. Charles Kwenin, Mwakilishi wa IOM nchini Dkt. Qasim Sufi pamoja na Afisa Uhusiano na Sera wa IOM, Bi. Naomi Shiferaw. Wengine kulia mwa Katibu MKuu ni watumishi wa Wizara, Bw. Hangi Mgaka na Gloria Ngaiza.  






Tuesday, February 11, 2020

BALOZI KANALI IBUGE AKUTANA,KUFANYA MAZUNGUMZO NA SEKRETARIETI YA SADC

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge amekutana na kufanya mazungumzo na Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

Pamoja na mambo mengine, Katibu Mkuu alipokea taarifa ya ziara ya Sekretarieti ya SADC na kuwahakikishia ushirikiano wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hususan Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika kufanikisha mikutano yote ya SADC kipindi cha Uenyekiti wa Tanzania.

Ujumbe huo wa Sekretarieti ya SADC una wajumbe watano ukiongozwa na Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala wa SADC, Bibi. Bodo Tanrely Radaody Ravarosy ambao wapo nchini kwa ajili ya maandalizi ya mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa SADC unaotarajiwa kufanyika tarehe 10 - 11 Machi, 2020, Jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine, ujumbe huo ulipata fursa ya kukutana na Katibu Mkuu Balozi Ibuge na kumpa taarifa ya maandalizi ya mkutano huo.

Mwezi Augosti, 2019 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Joseph Pombe Magufuli alipokea rasmi Uenyekiti wa SADC katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi wanachama.

Aidha, hatua hiyo ilifuatiwa na mikutano mbalimbali ya kisekta iliyofanyika na inayoendelea kufanyika hapa nchini kwa kipindi cha kuanzia mwezi Septemba 2019 hadi Agosti, 2020 ambapo hadi sasa imeshafanyika mikutano mitatu ya kisekta.

Mikutano hiyo ni pamoja na Mkutano wa Mawaziri wa SADC wenye dhamana ya masuala ya Tehama, Habari, Uchukuzi na hali ya Hewa, Mkutano wa Pamoja wa Mawaziri wa Sekta ya Afya na VVU na UKIMWI pamoja na mkutano wa pamoja wa Mawaziri wa Mazingira, Maliasili na Utalii.
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akiongea na Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala wa SADC, Bibi. Bodo Tanrely Radaody Ravarosy leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akiwa katika picha ya pamoja na Sekretarieti ya SADC pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara

Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akiagana na Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala wa SADC, Bibi. Bodo Tanrely Radaody Ravarosy

DKT. NDUMBARO, BALOZI IBUGE WASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO YA RAIS MSTAAFU WA KENYA HAYATI DANIEL ARAP MOI

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) pamoja na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge wamesaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Kenya nchini kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Kenya, Daniel Arap Moi aliyefariki 4 Februari, 2020.   

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) akitoa salamu za pole kwa baadhi ya wafanyakazi wa Ubalozi wa Kenya Jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Kenya, Hayati Daniel Arap Moi

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) akisaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Kenya Jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Kenya, Hayati Daniel Arap Moi

 
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, wizara hiyo, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akisaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Kenya Jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Kenya, Hayati Daniel Arap Moi

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) pamoja na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Ubalozi wa Kenya Jijini Dar es Salaam mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo