Wednesday, July 15, 2020

DKT. NDUMBARO AFANYA ZIARA KATIKA MPAKA WA MKENDA, RUVUMA


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amefanya ziara katika eneo la mpaka wa Mkenda uliopo Wilaya ya Songea Vijijini Mkoani Ruvuma unaoinguanisha Tanzania na nchi Jirani ya Msumbiji. Ziara hii inalenga kibaini na kutatua changamoto mbalimbali ili kukuza biashara na uhusiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na nchi jirani ya Msumbiji. Katika ziara hiyo Dkt. Ndumbaro aliambatana na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi ya Wilaya ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Vijijini Mhe. Pololet Mgema. 

Akiwa mpakani hapo Dkt. Ndumbaro amefanya mazungumzo na watumishi wa Idara mbalimbali za Serikali walipo katika ofisi za mpaka huo kwa lengo la kusikiliza changamoto na mapendekezo yanayolenga kuboresha namna ya utoaji huduma kwa wakazi wa eneo la mpaka na watumiaji wa mpaka huo. Aidha, Dkt. Ndumbaro pamoja na kutoa ufumbuzi wa baadhi ya changamoto, na kuahidi kuzifanyia kazi changamoto zilizosalia amewataka watumishi kuendelea kufanya kazi kwa ubunifu, jitihada na uaminifu.

Dkt. Ndumbaro pia ametembelea Ofisi za mpakani kwa upande wa Nchi jirani ya Msumbiji na kufanya mazungumzo na Watumishi walipo katika Ofisi hizo. 

Mheshimiwa Ndumbaro, amewaeleza wakazi na watumishi waliopo mpakani humo kuwa Serikali inaendelea na hatua za kuzitatua changamoto kubwa zinazo changia ugumu wa utekelezaji wa majukumu ya kilasiku na kuadhiri mwenendo wa biashara mpakani hapo, ikiwemo ukosefu wa umeme, huduma ya mawasiliano na barabara ya kiwango cha lami na ujenzi wa Kitu cha Kutoa Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP)

Dkt. Ndumbaro amewapongeza Watumishi walipo mpakani kwa kazi nzuri wanayoifanya na amewahimiza Watumishi hao kuendelea kutekeleza Dilomasia ya Uchumi, kuendeleza uhusiano mwema na kushughulikia suala la Diaspora

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akisaini kitabu cha Wageni alipotembelea Ofisi ya Uhamiaji katika mpaka wa Mkenda uliopo Wilaya ya Songea Vijijini, Mkoani Ruvuma
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na Wafanyakaozi wanahudumu katika mpaka wa Mkenda. Kushoto ni Mhe. Pololet Mgema Mkuu wa Wilaya ya Songea Vijijini. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na Mkuu wa Wilaya ya Songea Vijijini Mhe. Pololet Mgema wakiwa katika picha ya pamoja baadhi ya wakazi wa mpakani Mkenda 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akipokelewa na Maafisa Uhamiaji wa upande wa Msumbiji alipotembelea ofisi za mpakani Mkenda za nchi hiyo wakati wa ziara.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akisaini kitabu cha Wageni alipotembelea Ofisi ya Uhamiaji za Msumbiji zilizopo mpakani Mkenda, Ruvuma
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na Mkuu wa Wilaya ya Songea Vijijini Mhe. Pololet Mgema wakiwa katika picha ya pamoja baadhi ya Watumishi wa Mpakani kutoka Tanzania na Msumbiji 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akiendelea na ziara katika maeneo mbalimbali ya mpaka

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akisisitiza jambo wakati wa mazunguzo na daadhi Wananchi waliojitokeza wakati wa ziara

Friday, July 10, 2020

TANZANIA, CHINA ZAAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO, KUKUZA MAENDELEO


Tanzania na China zimeahidi kuendeleza ushirikiano wa kidiplomasia ili kuhakikisha kuwa nchi hizo zinakuwa na maendeleo endelevu. 

Makubaliano hayo yamefanywa na Balozi wa China nchini, Mhe. Wang Ke, wakati alipokutana kwa mazungumzo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge leo jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Ibuge amesema kuwa wamejadili masuala mbalimbali ikiwemo suala la namna ya kutekeleza nia ya Viongozi Wakuu wa nchii za China na Tanzania (Rais wa China, Mhe. Xi Jinping pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Joseph Pombe Maufuli) ya kupunguza madhara yatokanayo na ugonjwa wa COVID 19 ikiwemo kufutiwa na kusamehewa madeni.

Naishukuru Serikali ya China kwa uhusiano na ushirikiano ambao imekuwa ikionesha kwa Tanzania. Uhusiano huo umeendelezwa na viongozi wa pande zote mbili ambao umekuwa ukiimarika siku hadi siku na kuahidi kuwa serikali ya Tanzania itaendela kudumisha ushirikiano wake wa kidiplomasia kati yake na China.

Pamoja na mambo mengine, mazungumzo yalijadili masuala ya biashara na uwekezaji, mradi wa nyumba 25 za wataalum wa Afya zilizopo Osterbay jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake Balozi Wang Ke pamoja na mambo mengine, ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa jitihada ilizochukua katika kukukuza uchumi wake hadi kufikia uchumi wa kati, pamoja na mapambano dhidi ya COVID 19.

"Leo nimekutana na Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje, Balozi Brigedia Jenerali Ibuge na kuongea mambo mbalimbali ya ushirikiano na tunaipongeza Serikali ya Tanzania kwa jitihada  ilizochukua katika kufanya kazi kwa bidii na kukuza uchumi wake hadi kufikia uchumi wa kati, pamoja na hatua ilizochukua katika kupambana na janga la COVID 19 ambapo tumefurahishwa kuona janga la COVID 19 limeisha," Amesema Balozi Ke.

Balozi Ke ameongeza kuwa wamekubaliana katika maongezi hayo pia kuendeleza ushirikiano wa kufanya kazi kwa pamoja kwa manufaa ya mataifa mawili (Tanzania na China) ili kuhakikisha uhusiano na ushirikiano unazidi kukua na kuimarika.

 Tanzania na China zimekuwa zikishirikiana katika sekta za kilimo, biashara na uwekezaji, miradi ya mikopo nafuu na misaada, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Uchukuzi, Afya, Utalii na utamaduni. 

China na Tanzania zilianzisha mahusiano rasmi ya kidiplomasia mwaka 1964.


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akiongea na Balozi wa China nchini, Mhe. Wang Ke, wakati walipokutana kwa mazungumzo leo jijini Dar es Salaam

Balozi wa China nchini, Mhe. Wang Ke akiongea na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge wakati Walipokutana kwa mazungumzo leo jijini Dar es Salaam 



Tuesday, July 7, 2020

NUMBER OF FRENCH TOURISTS SURGE TO 56,000

The number of French tourists visiting Tanzania increased from 21,000 in 2016 to 56,000 last year, thanks to the Tanganyika Expeditions Agency and Axium by Parker operators, who have been organising trips.

Speaking at a meeting with French tour operators and tourism professionals in Paris recently, Tanzanian Ambassador to France Samwel Shelukindo told participants that the government of Tanzania had lifted restrictions on commercial flights and quarantine measures imposed on travellers since May 18, this year.

He noted that international airlines, including Ethiopian Airlines, Qatar Airways and KLM had already resumed flights to Tanzania.
"As it is the case in other countries, Tanzania was also affected by the Covid-19 pandemic, but now coronavirus cases have dropped significantly, thanks to the commitment and efforts made by the government under the leadership of our President John Magufuli and Tanzanian people who understood the challenge and complied with preventive measures to fight against the covid-19 pandemic," said the ambassador.

He added that the Ministry of Natural Resources and Tourism had developed national standard operating procedures (SOPs) for the management of Covid-19 in tourism business and invited potential tourists to consult the embassy.

"In this respect, I would like to underline that Tanzania has started receiving tourists. All precautions and preventive measures are taken to receive tourists and enable them to have an unforgettable stay. The government has also created an enabling environment to attract tourists." 

French tour operators listening to Tanzanian Ambassador's  speech   
Tanzanian Ambassador to France H.E Samwel Shelukindo addressing French tour operators during a meeting that took place in Paris, France recently.
Participants listening to Ambassador Shelukindo's  speech during a meeting with French Tour Operators that took place in Paris recently.  

Monday, July 6, 2020

KATIBU MKUU BALOZI BRIGEDIA JENERALI IBUGE ATEMBELEA BANDA LA WIZARA SABASABA


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, ametembelea banda la Wizara katika maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) 2020 yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Akiwa katika banda la Wizara Balozi Ibuge amewataka Watanzania kuendelea kuchapa kazi zaidi ili kuyaona matunda ya nchi kuwa katika kundi la uchumi wa kati.

''Sasa nchi yetu imeingia katika uchumi wa kati ambao unamaanisha kila mtu aendelee kupiga juhudi zaidi ya pale alivyokuwa anafanya ili tuendelee kupaa kuliko hivi ambavyo tumefikia sasa'' amesema Balozi Ibuge.

Amesema Tanzania sasa ina Balozi 43 na Balozi ndogo tatu na ni mwenyeji wa Balozi 63 na Mashirika ya Kimataifa 30 ikiwa ni namna ya kuipeleka Tanzania katika anga za kimataifa tukionyesha mafanikio vivutio vyetu na vitu vingine vyote tunavyovifanya ili kujiletea maendeleo huku tukiimarisha mahusiano ya kimataifa.

Akiwa katika maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), Balozi Ibuge ametembelea banda la Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC) na makampuni matatu ya Kigeni yanayoshiriki maonesho hayo.


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Wizara katika maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) 2020 yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, akizungumza na watumishi alipotembelea banda la Wizara katika maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) 2020 yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, akiangalia jarida linaloelezea utekelezaji wa dipolomasia ya uchumi linalochapishwa na Wizara alipotembelea banda la Wizara katika maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba).
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, katika picha ya pamoja na watumishi walioko kwenye banda la Wizara katika maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba)

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, akijadili jambo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dkt. Ave Maria Semakafu walipotembelea moja ya banda kwenye maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba).
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dkt. Ave Maria Semakafu wakimsikiliza mfanyabiashara kutoka Siria anayeshiriki maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) 2020 yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) katika maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) 2020 yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam

Nafasi ya Kazi katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola


Sunday, July 5, 2020

DKT. NDUMBARO ATEMBELEA BANDA LA WIZARA SABASABA


Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, ametembelea banda la Wizara katika maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) 2020 yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Akiwa katika banda la Wizara Dkt. Ndumbaro amewataka watumishi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na maarifa zaidi ili kuiletea sifa Serikali na kuendelea kuimarisha mahusiano ya kimataifa.

"Kwa kuwa sisi tunafanya kazi ya kuiwakilisha Tanzania katika nchi za Nje na kuhakikisha mahusiano ya kimataifa yanaimarika hatuna budi kufanya kazi kwa bidii na maarifa yetu yote, hili ni jukumu letu hivyo ni lazima tuhakikishe tunalitekeleza kwa ufanisi na ufasaha," Amesema Dkt. Ndumbaro

Akiwa katika maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), Dkt. Ndumbaro ametembelea pia banda la Bunge, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Dodoma na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.


Watumishi wa Wizara wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro, alipotembelea banda la Wizara katika maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) 2020 yanayoendelea jijini Dar es Salaam.




Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ndumbaro, akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Wizara katika maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) 2020 yanayoendelea jijini Dar es Salaam.




Thursday, July 2, 2020

PROF. KABUDI ATETA NA MJUMBE MAALUM WA MAZIWA MAKUU



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Prof. Kabudi ateta na Mjumbe Maalum wa Maziwa Makuu

Dodoma, 2 Julai 2020
Tanzania inaamini katika umoja wa jumuiya ya kimataifa kwenye kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazoikabili dunia ikiwemo mlipuko wa ugonjwa wa Corona.

Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) alipofanya mazungumzo kwa njia ya mtandao na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye eneo la Maziwa Makuu, Balozi Huang Xia.

Viongozi hao walitumia fursa hiyo kubadilishana mawazo katika masuala mbalimbali yanayotokea duniani, ikiwa ni pamoja na mikakati na mbinu bora za kukabiliana na janga la ugonjwa wa Corona na athari zake katika uchumi kwenye eneo la Maziwa Makuu.   

Balozi Huang alielezea hatua mbalimbali anazozichukua zikiwemo kuongea na taasisi za kimataifa za fedha na wadau wengine kwa ajili ya kuzihimiza kutoa misaada kwa nchi za Maziwa Makuu ili ziweze kukabiliana na janga la ugonjwa wa Corona na athari zake za kiuchumi na kijamii. Licha ya kukutana na taasisi hizo, Balozi Huang pia amefanya mashauriano na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Maziwa Makuu kuhusu janga la Corona. Kwenye mashauriano hayo Mawaziri wamesisitiza umuhimu wa kuandaa mkutano wa Mawaziri kwa njia ya mtandao ili kujadili, pamoja na mambo mengine mikakati ya kukabiliana na ugonjwa wa Corona na hali ya usalama katika eneo la Maziwa Makuu.

Kwa upande wake, Prof. Kabudi aliunga mkono wazo la kuwa na mkutano wa Mawaziri wa nchi za Maziwa Makuu na kuelezea matumaini yake kuwa, mkutano huo utatoa mawazo mazuri yatakayosaidia ufumbuzi katika changamoto zinazoikabili dunia ukiwemo ugonjwa wa Corona.

Aidha, Prof. Kabudi alitoa maelezo kuhusu mikakati iliyochukuliwa na Serikali ya Tanzania katika kudhibiti ugonjwa wa Corona. Alisema moja ya mikakati hiyo ni tangazo la maombi ya siku tatu kwa nchi nzima lililotolewa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, maombi ambayo yaliyohusisha imani zote.  Tangazo hilo  lilionekana ni jambo geni kwa watu wengi duniani lakini kwa Tanzania, nchi yenye waislamu na wakristo takribani nusu kwa nusu, lilikuwa ni muhimu na uamuzi huo haukuifanya Tanzania kupuuza maelekezo mengine yanayotolewa na wataalam wa afya.   

Mazungumzo hayo yalihitimishwa kwa Mhe. Waziri kuahidi kuwa, Tanzania itashirikiana kwa karibu na ofisi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika uamuzi wake wa kuandaa mkakati maalum wa kuzuia migogoro na kuimarisha amani na utulivu kwenye eneo la nchi za maziwa makuu.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akizungumza kwa njia ya mtandao na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye Ukanda wa Maziwa Makuu, Mhe. Balozi Huang Xia kuhusu ushirikiano katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona na masuala ya amani na usalama katika ukanda huo. Mazungumzo hayo yalifanyika Prof. Kabudi akiwa jijini Dodoma huku Balozi Huang Xia akiwa jijini Nairobi, Kenya.
Sehemu ya ujumbe ulioambatana na Mhe. Prof. Kabudi ukifuatilia mazungumzo kati ya Prof. Kabudi na Balozi Huang Xia (hawapo pichani). Kulia ni Bw. Magabilo Murobi, Katibu wa Waziri na Bw. Ali Ubwa, Afisa Mambo ya Nje.




Monday, June 29, 2020

VACANCY ANNOUNCEMENT



PRESS RELEASE


VACANCY ANNOUNCEMENT

Dodoma, 29 June 2020

The Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation has received vacancy notification from the Commonwealth Secretariat inviting qualified Tanzanians to apply for the post of Assistant Research Officer-International Trade Policy Section.

Application details can be found through the Secretariat’s website, http://thecommonwealth.org/jobs. Closing date for application is Wednesday 8 July 2020.


“The Ministry encourages qualified Tanzanians to apply”.



Issued by;
Government Communication Unit


Friday, June 26, 2020

MKUTANO WA MAWAZIRI WA KAMATI YA SADC YA ASASI YA USHIRIKIANO WA SIASA, ULINZI NA USALAMA (TROIKA) WAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM


Mkutano wa Mawaziri wa Kamati ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ya Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama kwa ngazi ya Mawaziri umefanyika kwa njia ya Mtandao (Video Conferencing) na kujadili masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama.

Mkutano huo umefanyika chini ya Uenyekiti wa Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara ya Kimataifa wa Jamhuri ya Zimbabwe, Mhe. Sibusiso Busi Moyo na utakutanisha Mawaziri wenye dhamana ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mambo ya Ndani, Ulinzi pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kutoka nchi wanachama wa SADC. Ujumbe wa Tanzania umeongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi.

Mkutano huo umehudhuriwa na nchi 16 wanachama wa SADC ambazo ni Angola, Afrika Kusini, Botswana, Comoro, DRC, Eswatini, Lesotho, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Madagascar, Namibia, Visiwa vya Shelisheli, Zambia, Zimbabwe na Mwenyekiti Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (katikati), kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Nchi George Simbachawene na mwisho kushoto ni Katibu  Mkuu Wizara ya Ulinzi, Dkt. Faraji Mnyepe wakifuatilia mkutano kwa njia ya video conference, Jijini Dar es salaam

Mawaziri pamoja na baadhi ya Makatibu Wakuu/Maafisa waandamizi kutoka Tanzania wakifuatilia mkutano kwa njia ya Video Conference, jijini Dar es Salaam

Mkutano ukiendelea  





IMF YAAHIDI KUIPATIA TANZANIA FEDHA ITAKAYOIHITAJI


Shirika la Fedha Duniani (IMF) limeahidi kuipatia Tanzania fedha itakayoihitaji ili iweze kuendelea kukabiliana na athari zitokanazo na janga la Covid 19 kwa ajili ya kuimarisha uchumi wake.

Mkurugenzi Mkazi wa IMF nchini Tanzania Bw. Jens Reinke ameyasema hayo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi leo katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam.

Pia Bw. Reinke ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hatua madhubuti inazozichukua katika kukabiliana na janga la Covid 19 ili kuepusha madhara ya kiuchumi na kijamii.

Mazungumzo hayo pia yamelenga miradi ya maendeleo, msamaha wa madeni kwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania, ushirikiano baina ya IFM na Tanzania, biasara na utalii. 
  
Kwa upande wake, Prof. Kabudi ameishukuru (IMF) kwa msamaha wa madeni ambao umetolewa kwa Tanzania na nchi nyingine, fedha zitakazoziwezesha nchi hizo kuendelea kukabiliana na Covid 19.

"Tumeongelea mambo mbalimbali yanayohusu ushirikiano hasa katika kuimarisha uchumi wetu baada ya janga la covid 19, usirikiano kati ya Tanzania na IMF unafahamika na tumekubaliana baadhi ya mambo ambayo tutayafanyia kazi kwa kina ili tuweze kuimarisha uchumi wetu baada ya corona hasa katika sekta ya utalii, biashara na miundombinu," amesema Prof. Kabudi.

Katika hatua nyingine, Waziri Kabudi amekutana na kumuaga Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Nguyen Kim Doanh ambaye amemaliza muda wake wa utumishi na amemtakia maisha mema na kumsihi kuendelea kuwa balozi mwema kwa Tanzania nchini Vietnam na duniani kwa ujumla.

"Kwa niaba ya Serikali napenda kukuhakikishia kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Vietnam katika nyanja mbalimbali za kimataifa ikiwemo kuiunga mkono Vietnum katika kugombea nafasi mbalimbali katika Masirika ya KImataifa," Amesema Prof. Kabudi.

Nae Balozi Doanh ameishukuru Tanzania kwa ushirikiano ambao imekuwa ikimpatia alipokuwa akitekeleza majukumu yake nchini wakati wote na kuahidi kuwa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili utaendelea kuimarishwa.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Kabudi akisalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa IMF nchini Tanzania Bw. Jens Reinke 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi akimuelezea jambo Mkurugenzi Mkazi wa IMF nchini Tanzania Bw. Jens Reinke leo katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam 


Mkurugenzi Mkazi wa IMF nchini Tanzania Bw. Jens Reinke akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi leo katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi akiongea na Balozi wa Vietnam  nchini, Mhe. Nguyen Kim Doanh ambaye amemaliza muda wake wa utumishi nchini Tanzania 


Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Nguyen Kim Doanh akipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Kabudi  


Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Nguyen Kim Doanh akimkabidhi zawadi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Kabudi  



Thursday, June 25, 2020

PROF. KABUDI AKUTANA, KUMUAGA BALOZI WA IRELAND NCHINI TANZANIA


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi, amekutana na kumuaga Balozi wa Ireland nchini, Mhe. Paul Sherlock ambaye amemaliza muda wake wa utumishi na amemtakia maisha mema na kumwambia kuwa ni matarajio yake kuwa atakuwa balozi mwema kwa Tanzania nchini Ireland na kwingineko duniani.

Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine, Prof. Kabudi amesema kuwa Ireland imekuwa na uhusiano mzuri wa kidiplomasia na Tanzania hasa katika kuunga mkono jitihada za kuimarisha sekta mbalimbali nchini ikiwemo miradi ya maendeleo, elimu, kilimo, afya pamoja na biashara na uwekezaji.

“Kupitia uhusiano imara kati ya Tanzania na Ireland hivi karibuni tulivyopatwa na janga la covid 19, Ireland imetoa msaada wa Euro milioni 1.5 ambapo baadhi ya fedha hizo zilipelekwa Shirika la Afya Duniani ofisi ya hapa Tanzania na Shirika la Chakula duniani ofisi ya hapa nchini kwa ajili ya kununua chakula lakini pia kwenda katika mfuko wa Benjamini Mkapa kwa ajili ya kuajiri wafanyakazi na kujenga vituo vya afya ili kutusaidia kupambana na Covid 19,” Amesema Prof. Kabudi.


Waziri Kabudi amemhakikishia Balozi Sherlock, kuwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Ireland utaendelea kuimarika hasa katika sekta ya uwekezaji na biashara, na kutoa wito kwa Serikali ya Ireland kuja kuwekeza hapa nchini katika sekta za kilimo, viwanda hasa vya nguo pamoja na ujenzi.  

Aidha, Balozi Sherlock ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushirikiano ambao imekuwa ikimpatia alipokuwa akitekeleza majukumu yake nchini na kuahidi kuwa ushirikiano uliopo utaendelezwa hasa ikizingatiwa kuwa nchi hizo mbili zimekuwa na uhusiano wa kidiplomasia kwa miaka 40.

" Natumaini kuwa serikali ya Ireland kupitia uhusiano wake na Tanzania itaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania za kukabiliana na changamoto mbalimbali na kuhakikisha kuwa inasonga mbele kimaendeleo," amesema Balozi Sherlock.

Tanzania na Ireland zimetimiza miaka 40 ya uhusiano wa kidiplomasia tangu Serikali ya Ireland ilipofungua ubalozi wake nchini Tanzania mwaka 1979.  


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi akiongea na Balozi wa Ireland nchini, Mhe. Paul Sherlock wakati alipokuwa akimuaga katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam



Balozi wa Ireland nchini, Mhe. Sherlock akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Kabudi katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Kabudi akimkabidhi zawadi ya picha ya mlima Kilimanjaro Balozi wa Ireland nchini, Mhe. Sherlock katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam



Balozi wa Ireland nchini, Mhe. Sherlock akimuonesha moja ya picha katika kitabu alichompatia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Kabudi kama zawadi  



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Kabudi akimkabidi zawadi ya kitabu cha picha Balozi wa Ireland nchini, Mhe. Sherlock