Wednesday, May 5, 2021

TANZANIA KUHAKIKISHA BIASHARA KATI YA TANZANIA NA KENYA INAINUA UCHUMI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kongamano la wafanyabiashara wa Kenya na Tanzania lililofanyika jijini Nairobi nchini Kenya alipokuwa kwenye ziara rasmi ya siku mbli nchini Kenya kwa mwaliko wa mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta.

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta akihutubia Kongamano la Wafanyabiashara wa Tanzania na Kenya lilifonyika jijini Nairobi tarehe 05/05/2021

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo huku wakisikilizwa na Waziri wa uwekezaji Mhe. Geoffrey Mwambe , Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda, na Waziri wa Utlii na Mambo ya Kale wa Zanzibar Mhe. Leyla Mohamed Musa Mawaziri hao walikuwa nchini Kenya kuhudhuriaa Kongamano la Wafanyabiashara wa Tanzania na Kenya

Baadhi ya viongozi kutoka Tanzania walioshiriki Kongamano la Wafanyabiashara wa Tanzania na Kenya lililofanyika jijini Nairobi

Baadhi ya wafanyabiashara kutoka Tanzania walioshiriki Kongamano la wafanyabiashara wa  Tanzania na Kenya lililofanyika jijini Nairobi na kuhudhuriwa na Marais  wa nchi za Kenya na Tanzania

Baadhi ya wafanyabiashara kutoka Tanzania walioshiriki Kongamano la wafanyabiashara wa  Tanzania na Kenya lililofanyika jijini Nairobi na kuhudhuriwa na Marais  wa nchi za Kenya na Tanzania

Baadhi ya wafanyabiashara kutoka Tanzania walioshiriki Kongamano la wafanyabiashara wa  Tanzania na Kenya lililofanyika jijini Nairobi na kuhudhuriwa na Marais  wa nchi za Kenya na Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameihakikisha jumuiya ya wafanyabiashara wa Tanzania na Kenya kuwa Serikali anayoiongoza itaendelea kuchukua hatua kuondoa vikwazo vya kibiashara vilivyopo ili kuimarisha sekta binafsi na hivyo kukuza uchumi wa nchi hizo.

Mhe. Samia alikuwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la wafanyabiashara wa Tanzania na Kenya lililofanyika jijini Nairobi nchini Kenya na kuhudhuriwa kwa pamoja na Rais Samia na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Kenya Me. Uhuru Kenyatta.

Amesema Serikali za nchi hizo zitahakikisha kunakuwa na sheria nzuri, uwazi, mifumo ya kodi inayoeleweka na mifumo thabiti ya Mahakama itakayoshughulikia kesi za biashara kwa haraka na uwepo wa mazingira mazuri ya uwekezaji katika nchi hizo

Amesema kufanyika kwa Kongamano hilo kumewezesha kuwepo kwa majadiliano ya pamoja kati ya Sekta Binafsi na Serikali, wafanyabiashara wao kwa wao na kuelezea kuwa ni kitu kizuri kwani kinachangia juhudi za kuinua na kuimarisha ukuaji wa biashara na sekta binafsi kwa maendeleo ya nchi zote mbili

Mhe. Rais Samia amesema Tanzania itaendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha kunakuwa na mazingira mazuri ya uwekezaji na kufanya biashara ili kuwawezesha wafanyabiashara kuendesha shughuli zao kwa amani na utulivu kwani Sekta binafsi ni muhimu katika ukuzaji wa uchumi kwa kutoa ajira, kuleta masoko, hufungua fursa mbalimbali na kuchagiza moyo wa ujasiriamali miongoni mwa wananchi.

Amesema Tanzania imedhamiria kwa dhati kuona Sekta binafsi imara inayoweza kukabiliana na changamoto za uchumi za dunia kupitia uanzishwaji wa viwanda na hivyo kuongeza ubora wa bidhaa zinazozalishwa nahivyo kutoa ajira na utajiri wananchi kitu ambacho wafanyabiashara wanatakiwa kukifikia.

Awali akizungumza katika Kongamano hilo Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta ameitaka jumuiya ya wafanyabiashara wa Tanzania na Kenya  kuchangamkia fursa za kibiashara ambazo hazijafikiwa katika nchi hizo ili kukuza biashara katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuleta maendeleo kwa watu wake.

Amewataka Mawaziri wanaohusika na biashara kukutana na kutatua changamoto zinazokwamisha ukuaji wa biashara katika nchi hizo ili kukuza uchumi na kuinua maisha ya wananchi wa nchi hizo na kuongeza kuwa ana imani kuwa hayo yote yakifanyika kwa pamoja bila ya kushindana ni wazi kuwa watakaoibuka washindi ni wananchi wa nchi hizo.

Amesema wawekezaji na wafanyabiashara wa Tanzania wanaweza kwenda kuwekeza nchini Kenya bila ya kudaiwa viza za biashara ili mradi wafate sheria kanuni na taratibu zilizopo. Amewagiza Mawaziri wanaohusika na mgogoro uliopo eneo la mpaka la Taveta hadi Namanga wakutane ili kuona nanma ya kuondoa changamoto na kutoa wiki mbili mahindi yaliyokwama huko yawe yameondolewa.

Mhe. Kenyatta pia amewataka Mawaziri wa Afya katika nchi hizo kukutana na kuangalia namna ya kuondoa changamoto iliyopo sasa upimaji wa virusi vya Corona na kutaka vyeti vilivyotolewa katik nchi moja vitambuliwe katika nchi nyingine.

 

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ASHIRIKI DHIFA YA KITAIFA KATIKA IKULU YA NAIROBI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  katika picha na Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta pamoja na Mke wa Rais Kenyatta Mama Margaret Kenyatta kabla ya kwenda kwenye Dhifa ya Kitaifa aliyoandaliwa na Rais Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya tarehe 04 Mei, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika picha ya Pamoja na Mke wa Rais Kenyatta Mama Margaret Kenyatta kabla ya kwenda kwenye Dhifa ya Kitaifa aliyoandaliwa na Rais Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya tarehe 04 Mei, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta wakielekea kwenye Dhifa ya Kitaifa aliyoandaliwa na Rais Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya tarehe 04 Mei, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama na Mwenyeji wake Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta pamoja na Mke wa Rais Kenyatta Mama Margaret Kenyatta wakati wa nyimbo za Taifa zikipigwa katika Dhifa ya Kitaifa aliyoandaliwa na Rais Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya tarehe 04 Aprili, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika Dhifa hiyo ya Kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima yake na mwenyeji wake Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya tarehe 04 Mei, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya Kitabu kutoka kwa Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta mara baada ya Dhifa ya Kitaifa iliyofanyika katika Ikulu ya Nairobi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta pamoja Mke wa Rais Kenyatta Mama Margaret Kenyatta mara baada ya Dhifa ya Kitaifa katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya tarehe 04 Mei 2021. picha na Ikulu


 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameshiriki dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima yake na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi iliyofanyika jioni ya tarehe 04 Mei,2021.

Katika siku ya pili ya ziara yake tarehe 05/05/2021 Mhe. Rais akiwa na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta atahutubia Mabunge ya Kenya na baadaye atafungua Kongamano la wafanyabiashara wa Kenya na Tanzania linalofanyika jijini Nairobi.

Mhe. Rais Samia yuko nchini Kenya kwa ziara rasmi ya siku mbili kufuatia mwaliko wa mwenyeji wake Mhe. Rais Kenyata anatarajiwa kurejea nyumbani tarehe 05/05/2021




Tuesday, May 4, 2021

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS UHURU KENYATTA AMUALIKA KUWA MGENI RASMI MIAKA 60 YA TANZANIA BARA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta alipowasili katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya tarehe 04 Mei, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha Wageni baada ya kuwasili katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya ambako yupo katika ziara rasmi ya siku mbili nchini Kenya kwa mwaliko wa Rais wa nchi hiyo Mhe. Uhuru Kenyatta.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta wakati wakielekea kwenye mazungumzo ya Pamoja na Ujumbe wa Tanzania na Kenya.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta wakati nyimbo za Taifa za Tanzania na Kenya zilipopigwa mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya tarehe 04 Mei, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshima liloandaliwa na Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya tarehe 04 Mei, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta wakati wakielekea kwenye mazungumzo ya Pamoja na Ujumbe wa Tanzania na Kenya.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta mara baada ya mazungumzo yao katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya na amemualiaka kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara yatakayofanyika tarehe 9 Disemba 2021.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari baada ya kumaliza mazungumzo yao Mhe. Rais Samia amesema wamekubaliana kukuza na kuimarisha uhusiano wa kiuchumi, kibiashara, kidugu, kihistoria na wa kirafiki uliopo baina ya nchi mbili.

Mhe. Rais Samia amesema kuwa wamekubaliana kutekeleza miradi ya pamoja ya kimkakati ikiwamo miradi ya usafiri na usafirishaji wa watu na bidhaa na kuangalia jinsi ya kupata nishati ya umeme na gesi kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine ikiwa ni pamoja na ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi kutoka Dar es salaam hadi Mombasa na kusisitiza kuwa ni wakati wa kuitekeleza miradi hiyo kwa vitendo.

Mhe. Rais amesema kuwa wamekubaliana kuimarisha miundombinu ya usafirishaji kwa kujenga barabara, kuimarisha usafiri wa majini katika ziwa Victoria, reli na anga na kushughulikia uondoaji wa vikwazo vya biashara visivyo vya kodi na kuagiza Tume ya pamoja ya Ushirikiano (JPC) kukutana kushughulikia vikwazo hivyo ili kuondoa mivutano na misuguano  inayokwamisha juhudi za kukuza uchumi kwa nchi hizo. 

Amesema Tanzania imejipanga kwa nguvu zote kuwekeza nchini Kenya ili kukuza ujazo wa biashara na kuongeza miradi ya uwekezaji kutoka kampuni 30 za watanzania zilizowekeza mtaji wenye thamani ya Shilingi bilioni 19.3 za Kenya ambazo ni sawa na Shilingi bilioni 410.2 za Tanzania na kutoa ajira kwa wakenya 2640.

Amesema Kenya ni miongoni mwa nchi zilizowekeza nchini kwa kiwango kikubwa ambapo kampuni 513 za nchi hiyo zimewekeza nchini mtaji wenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 1.7  ambazo ni sawa na Shilingi trilioni 3,888 na kuzalisha ajira  51,000  kwa watanzania na amemuhakikishia mwenyeji wake kuwa atawashawishi wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania kuwekeza kwa wingi nchini Kenya.

Awali, akizungumza katika mkutano huo Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta alimuhakikisha Rais Samia kuwa Kenya itaendelea kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja na Tanzania ili kutimiza lengo la kuziletea maendeleo nchi hizo na kuongeza kuwa Kenya itaendeleza juhudi za kukuza na kuimarisha uhusiano na ushirikiano uliopo baina ya nchi mbili hizo ili kuinua uchumi kupitia sekta mbalimbali kama vile biashara, uwekezaji, madini, nishati, mifugo, usafirishaji, ulinzi na usalama kwa manufaa ya nchi zote mbili na watu wake.

Mhe. Kenyata amekubali mualiko wa kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara na kuahidi kuungana na Watanzania wakati wa maadhimisho hayo yatakayofanyika nchini tarehe 9 Disemba, 2021.

Mhe. Rais Samia yuko katika ziara rasmi ya siku mbili nchini Kenya kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Kenya.

 

RAIS SAMIA AWASILI JIJINI NAIROBI KWA ZIARA YA RASMI YA SIKU MBILI NCHINI KENYA

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuka kutoka katika ndege ya Shirika la Ndege Tanzania alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta kuanza ziara rasmi ya siku mbili nchini Kenya kufuatia mwaliko wa mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Mhe. Raychelle Omamo alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi kuanza ziara rasmi ya siku mbili kufuatia mwaliko wa mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta.


Waziri wa Michezo, Utamaduni na Urithi Mhe. Amina Mohammed akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi


Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan akielekea katika jengo maalum lililopo katika Uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta alipowasili jijini Nairobi kuanza ziara rasmi ya siku mbili nchini Kenya.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitia saini kitabu maalum mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi nchini Kenya.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Raychelle Omamo alipowasili jijini Nairobi kuanza ziara rasmi nchini Kenya.


Baadhi ya Watanzania wakisubiri kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Rais Samia Suluhu Hasssan alipowasili jijini Nairobi kwa ziara rasmi ya siku mbili nchini Kenya.


Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akiwasalimia baadhi ya Wafanyabiashara wa Tanzania waliopo Kenya alipowasili jijini Nairobi kwa ziara rasmi ya siku mbili nchini Kenya.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi nchini Kenya kuanza ziara rasmi ya siku mbili kufuatia mwaliko wa mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta.

Alipowasili jijini Nairobi Mhe. Rais Samia alilakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Mhe. Raychelle Omamo na Waziri wa Michezo, Utamaduni na Urithi Mhe. Amina Mohammed.

Baada ya kuwasili Mhe. Rais Samia aliekea hotelini kwa ajili ya mapumziko kidogo na baadaye alielekea Ikulu ya Nairobi kwa ajili ya kupokelewa rasmi na Mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta ambapo alikagua gwaride na kupigiwa mizinga 21 kwa heshima yake.

Akiwa Ikulu jijini Nairobi Mhe. Rais alifanya mazungumzo ya faragha na mwenyeji wake Mhe. Rais Kenyatta na baadaye walifanya mazungumzo rasmi ambayo yalihudhuriwa na wajumbe wa pande zote mbili.

Baada ya kumaliza mazungumzo yao viongoazi hao walizungumza na waandishi wa habari na baadaye Mhe. Rais Samia alikwenda kuweka shada la maua katika Kaburi la Baba wa Taifa la Kenya hayati Mzee Jomo Kenyatta.

Jioni Mhe. Rais atahudhuria dhifa ya Kitaifa ambayo imeandaliwa kwa heshima yake na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta.

Kesho tarehe 05/05/2021 Mhe. Rais akiwa na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta atahutubia Mabunge ya Kenya na baadaye atafungua Kongamano la wafanyabiashara wa Kenya na Tanzania linalofanyika jijini Nairobi.

Mhe. Rais anatarajiwa kurejea nyumbani siku hiyohiyo ya tarehe 05/-05/2021

Monday, May 3, 2021

MAANDALIZI YA MKUTANO WA 12 WA BARAZA LA KISEKTA LA MAWAZIRI WA FEDHA WA EAC YAANZA JIJINI ARUSHA

Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Fedha na Uchumi pamoja na Mkutano wa Mawaziri wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Mashauriano ya Kibajeti unafanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 3 hadi 7 Mei 2021.


Mkutano huo ambao umeitishwa na Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, umetanguliwa na kikao cha Ngazi ya Wataalam kutoka Sekta za Fedha na Uchumi unaofanyika kuanzia tarehe 3 hadi 5 Mei 2021 na kufuatiwa na kikao cha Makatibu Wakuu tarehe 6 Mei 2021 kabla ya kuhitimishwa na Mkutano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri mnamo tarehe 7 Mei 2021.


Mkutano huo wa 12 pamoja na mambo mengine una lengo la kupokea na kujadili taarifa za Kamati zinazoshughulikia masuala ya Fedha pamoja na kufanya mashauriano ya awali ya Bajeti ya Mawaziri wa Fedha na masuala ya Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Vilevile, utapokea Taarifa ya Utekelezaji wa Maazimio mbalimbali yaliyofikiwa wakati wa Mkutano wa 11 wa Baraza hilo la Kisekta.


Ujumbe wa Tanzania kwenye kikao cha ngazi ya Wataalam unaongozwa na Bw. William Mhoja, Kamishna wa Uchambuzi wa Sera kutoka Wizara ya Fedha na Mipango. 

Sehemu ya Wajumbe wa kikao cha Wataalam wakiwa wamesimama kabla ya kuanza kikao chao ili kumkumbuka aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliyefariki dunia mwezi Machi 2021


Kamishna wa Uchambuzi wa Sera kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. William Mhoja (kushoto) akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano wa majadiliano kwa ngazi ya wataalam ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Fedha na Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika jijini Arusha tarehe 7 Mei 2021. Mkutano wa Wataalam unafanyika kuanzia tarehe 3 hadi 5 Mei 2021 na kufuatiwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu tarehe 6 Mei 2021. Kulia ni Bw. James Msina, Kamishna Msaidizi, Idara ya Fedha za Nje anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Kikanda, Wizara ya Fedha na Mipango.

Bw. James Msina, Kamishna Msaidizi, Idara ya Fedha za Nje anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Kikanda kutoka Wizara ya Fedha na Mipango akichangia jambo wakati wa kikao cha  wataalam wanaoandaa Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

Mkuu wa Idara inayoshughulikia masuala ya Fedha katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Pantaleo Kessy (kushoto) akichangia jambo wakati wa kikao cha wataalam

Ujumbe kutoka Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Uganda wakishiriki mkutano wa ngazi ya wataalam ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa  12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika jijini Arusha tarehe 7 Mei 2021

Mjumbe kutoka Burundi akishiriki mkutano wa wataalam

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Elias Bagumhe akishauriana jambo na mjumbe kutoka Tanzania wakati wa kikao cha wataalam

Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia majadiliano yaliyokuwa yakiendelea

Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania kwenye kikao hicho

Ujumbe ulioshiriki kikao cha waatalam


Saturday, May 1, 2021

MATUKIO KATIKA PICHA: WATUMISHI WA WIZARA YA MAMBO YA NJE WASHIRIKI MEI MOSI, DODOMA

Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, wameungana na Wafanyakazi wengine wa Wizara, Taasisi, Mashirika na Sekta binafsi  kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani  iliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.  

Maadhimisho hayo yameongozwa na Mkuu wa Mkoa  wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge akiambatana  na Viongozi na Watendaji wengine wa Serikali.
Sehemu ya Watumishi wa Wizara wakiwa katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani jijini Dodoma
Sehemu ya Watumishi wa Wizara wakiwa katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani jijini Dodoma
Sehemu nyingine Watumishi wa Wizara wakiwa katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani jijini Dodoma
Sehemu nyingine Watumishi wa Wizara wakiwa katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani jijini Dodoma
Sehemu nyingine Watumishi wa Wizara wakiwa katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani jijini Dodoma
 Watumishi wa Wizara wakiwa katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma
Watumishi wa Wizara wakiwa katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma


WIZARA YA MAMBO YA NJE YASHIRIKI MEI MOSI KITAIFA JIJINI MWANZA

Na Mwandishi wetu, Mwanza

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imeungana na Wizara, Taasisi, Mashirika na Kampuni binafsi katika kushiriki maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Mwanza.

Maadhimisho hayo yameongwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiambatana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Husein Kattanga, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Mb), Mawaziri wa wizara mbalimbali pamoja na Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama.

Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wameongozwa na Waziri wake Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb), Naibu Waziri Mhe. Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk (Mb) pamoja na Katibu Mkuu Mhe. Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge.

Kaulimbiu katika maadhimisho hayo ni Maslahi bora, Mishahara juu, Kazi iendelee.

Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa katika maandamano ya siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Mwanza


Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa katika maandamano ya siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Mwanza


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  akiongoza meza kuu kushuhudia maandamano ya Watumishi wa Umma na binafsi waliokuwa wakipita mbele ya jukwaa kuu wakati wa kilele cha siku ya wafanyakazi duniani (hawapo pichani) iliyoadhimishwa kitaifa katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Liberata Mulamula (Mb) akiteta jambo na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Mbarouk Nassoro Mbarouk (Mb) wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani iliyofanyika jijini Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba


Sehemu ya Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali wakifuatilia maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani iliyofanyika kitaifa jijini Mwanza


Sehemu ya Mawaziri wa Wizara mbalimbali na Wakuu wa taasisi mbalimbali wakifuatilia maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani iliyofanyika kitaifa jijini Mwanza