Thursday, November 4, 2021

TANZANIA YAAHIDI KUIUNGA MKONO MAHAKAMA YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU NA WATU

 

Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akifungua Mdahalo wa Tano wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu jijini Dar es Salaam

 

Rais wa Mahakaama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Mhe. Jaji Imani Aboud akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mdahalo wa Tano wa Mahakama hiyo jijini Dar es Salaam

Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango (katikati) akiwa na viongozi mbalimballi meza kuu wakati wa ufunguzi wa Mdahalo wa Tano wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu jijini Dar es Salaam

 

Majaji na viongozi mbalimbali wa Serikali wakifuatilia ufunguzi wa Mdahalo wa Tano wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu jijini Dar es Salaam

Washiriki wa Mdahalo wa Tano wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu wakifuatilia ufunguzi wa mdahalo huo jijini Dar es Salaam

Mabalozi mbalimbali kutoka katika bara la Afrika wanaoziwakilisha nchi zao  Tanznaia wakifuatilia ufunguzi wa Mdahalo wa Tano wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu jijini Dar es Salaam 

 

 Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango (katikati) akiwa na viongozi mbalimballi katika picha ya pamoja baada ya kufungua Mdahalo wa Tano wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu jijini Dar es Salaam

 

 Na Waandishi wetu Dar,

 

Tanzania kuendelea kuiunga mkono Mahakama ya Afrika ya Haki za binadamu na watu katika kuhakikisha utoaji haki kwa wananchi unatekelezeka kwa wakati, uwazi na uadilifu.

Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amebainisha hayo wakati wa kufungua Mdahalo wa tano wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu jijini Dar es Salaam.

Amesema Tanzania itaendelea kuiunga mkono Mahakama hiyo katika kuhakikisha inatekeleza majukumu yake na kuongeza kuwa itaendelea kuwa mwanachama wa Mahakama hiyo kutokana na ukweli kuwa ni miongoni mwa nchi zilizoshiriki kikamilifu katika kuanzishwa kwa mahakama hiyo.

Ameongeza kuwa lengo la kuanzishwa kwa Mahakama hiyo ilikuwa ni pamoja na kuzisaidia Mahakama za nchi wanachama katika utoaji haki kwa kutekeleza maamuzi ya Mahakama hiyo na siyo kukinzana na Mahakama na sheria za nchi wanachama  kupitia utekelezaji wa maamuzi yake.

‘Tanzania itaendelea kuwa mwanachama, tulishiriki katika uanzishwaji wake, tutaendelea kuwa sehemu ya Mahakama hii kwa kuzingatia kuwa Mahakama hii ilianzishwa kwa lengo la kuzisaidia mahakama za nchi wanachama na sio kukinzana na mahakama na sheria za nchi wanachama,’ amesema Dkt. Mpango.

 Amewataka washiriki wa mdahalo huo kupitia majadiliano yao kuja na mapendekezo yatakayosaidia na kuwezeha upatikanaji wa haki kwa wananchi wote kwa wakati badala ya kukinzana na sheria za nchi wanachama.

Amesema utoaji haki kwa wananchi wote ndio jambo la msingi na kwamba mfumo wa utoaji haki  hauna budi kuimarishwa ili kutekeleza jukumu hilo kwa nguvu zote kwani imani ya wananchi kwa mfumo huo ndio msingi wa imani ya wananchi .

Awali akizungumza katika ufunguzi wa Mdahalo huo, Rais wa Mahakama hiyo Mhe. Jaji Imani Aboud amesema mdahalo wa mwaka huu umejikita katika kuangalia ufanisi na utekelezaji wa majukumu ya mahakama.  

Naye mwakilishi wa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Jaji Dkt. Deo John Nangela kutoka Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara amesema Tanzania ina mahusiano makubwa na taasisi za Kimataifa ikiwemo Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu na Mahakama nyingine zilizoko katika kanda na kuongeza kuwa Tanzania ni mdau katika mahakama hizo na itaendelea kuziunga mkono mahakama hizo katika kuhakikisha utoaji haki unapatikana kwa wakati na uwazi.

Mdahalo wa Tano wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu unahudhuriwa na majaji na Wanasheria wa Serikali kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Afrika na kauli mbiu yake inasema kujenga imani kwa mfumo wa mahakama wa Afrika.

 



Wednesday, November 3, 2021

BALOZI FATMA AFUNGA MKUTANO WA MAHAKAMA YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU NA WATU

 

Balozi Fatma Rajab akizungumza katika hafla ya kufunga Mkutano wa Kimataifa wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu uliofanyika jijini Dar es Salaam

 

Balozi Fatma Rajab (kushoto) akizungumza katika hafla ya kufunga Mkutano wa Kimataifa wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu uliofanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa wanasheria waandamizi kutoka katika nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kulia  kwake ni Rais wa Mahakama hiyo Mhe. Jaji Iman Abood kutoka Tanzania.

Balozi Fatma Rajab (kushoto) akizungumza katika hafla ya kufunga Mkutano wa Kimataifa wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu uliofanyika jijini Dar es Salaam

Balozi Fatma Rajab (katikati) akiwa meza kuu wakati wa hafla ya kufunga Mkutano wa Kimataifa wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu uliofanyika jijini Dar es Salaam

 

Washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu uliofanyika jijini Dar es Salaam wakifuatilia hafla ya ufungaji wa mkutano huo

Washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu uliofanyika jijini Dar es Salaam wakifuatilia hafla ya ufungaji wa mkutano huo. 

 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Fatma Rajab amefunga Mkutano wa siku tatu wa Kimataifa wa Utekelezaji wa maamuzi ya  Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo pia uliangalia changamoto ambazo nchi wanachama wa Umoja wa Afrika unakabiliana nazo katika kutekeleza maamuzi yanayotolewa na Mahakama hiyo na kuzitafutia njia ya kukabiliana nazo pamoja na matarajio ya kuanzishwa kwa Mahakama hiyo.

Akizungumza wakati wa kufunga Mkutano huo Balozi Fatma amewataka washiriki wa mkutano huo kuyachukua yale yote waliyokubaliana katika mkutano huo ili kuziwezesha nchi zao kutekeleza maamuzi yanayotolewa na Mahakama hiyo kwa ufanisi.

Mkutano huo ulianza Novemba  Mosi umehudhuriwa na Wanasheria waandamizi kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Afrika.

Tuesday, November 2, 2021

MKUTANO WA 32 WA BARAZA LA MAWAZIRI LA KISEKTA LINALOSHUGHULIKIA MASUALA YA AFRIKA MASHARIKI NA MIPANGO WAFUNGULIWA JIJINI ARUSHA

Mkurugenzi Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi (kati) akiongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa maandalizi ngazi ya wataalamu unaofanyika jijini Arusha, Tanzania tarehe 1 na 2 Novemba 2021.

Mkutano huo wa ngazi ya wataalamu na mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu utakaofanyika tarehe 3 na 4 Novemba 2021 ni sehemu ya mikutano ya maandalizi kuelekea Mkutano wa 32 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango utakaofanyika tarehe 5 Novemba 2021. 

Wataalamu wengine waandamizi walioambatana na Balozi Mbundi ni pamoja na Mkurugenzi wa Uendeshaji Sera Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Agnes Meena (kushoto) na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Mipango katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Justin Kisoka.

Mwenyekiti wa Mkutano ngazi ya wataalamu Dkt. Alice Yalla kutoka Kenya akiongoza mkutano huo unaofanyika jijini Arusha, Tanzania tarehe 1 na 2 Novemba 2021.

Ujumbe wa Uganda ukifuatilia mkutano.

Ujumbe wa Burundi ukifuatilia mkutano

 

Ujumbe wa Kenya ukifuatilia mkutano

Monday, November 1, 2021

MKUTANO WA KIMATAAIFA WA MAHAKAMA YA AFRIKA YA WATU NA HAKI ZA BINADAMU WAANZA DSM


 

 Waziri wa Nchi , Katiba, Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman akifungua Mkutano wa Kimataaifa wa Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi  jijini Dar es Salaam


Washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu wakifuatilia ufunguzi wa mkutano huo

Washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu wakifuatilia ufunguzi wa mkutano huo

Washiriki wa Mkutano wa Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Mhe. Haroun Ali Suleiman na Rais wa Mahaka ya Afrika baada ya ufunguzi wa Mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salaam


Mmoja wa viongozi wanaoshiriki katika mkutano huo akizungumza kitu na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu Mhe. Jaji Iman Abood baada y aufunguzi wa mkutano huo jijini Dar es Salaam

Waziri wa Nchi , Katiba, Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman akizungumza na mmoja wa viongozi wanaoshiriki mkutano huo baada ya ufunguzi rasmi.


Na mwandishi wetu, Dsm


Mkutano wa Kimataaifa kujadili utekelezaji wa maamuzi ya Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu, changamoto na matarajio yake umeanza jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo wa siku tatu umefunguliwa na Waziri wa Nchi Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora  wa Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussien Ali Mwinyi.

Akifungua mkutano huo Mhe. Suleiman amezitaka nchi za Afrika kuhakikisha Mahakama hiyo inakamilisha malengo ya kuanzishwa kwake.

"Mahakama ya Afrika ni taasisi yetu sote, tumeiunda sisi wenyewe na kwa maana hiyo naamini kuwa ni kwa maslahi yetu sote Waafrika tunajukumu la kuhakikisha taasisi hii haishindwi kufikia malengo yake" alisema Mhe. Suleiman na kuongeza kuwa   hakuna mtu atakayenufaika iwapo Mahakama hiyo itafeli au kuwa taasisi isiyotekeleza kazi ya kulinda na kukuza haki za binadamu barani Afrika.

Amesema malengo ya Mahakama hiyo yataweza kufikiwa iwapo tu Serikali zote za bara la Afrika zitatelekeza kikamilifu maamuzi ya Mahakama hiyo.

" Niwaambie  kuwa namna moja kuu ambayo Serikali zitawezesha Mahakama hii kufikia malengo yake ni kwa kutekeleza kikamilifu maamuzi yanayotolewa" alisema na kuongeza kuwa kufanya hivyo kutaionesha dunia kuwa nchi za Afrika zinachukua hatua kulinda na kukuza haki za binadamu kwa nguvu zote.

Awali akizungumza katika mkutano huo,  Rais wa Mahakama ya Afrika Mhe. Jaji Iman Abood alisema mkutano huo umelenga kuangalia namna bora ya kuboresha utendaji kazi wa mahakama hiyo na changamoto zinazopitia nchi katika kutekeleza maamuzi yanayotolewa na Mahakama hiyo na hivyo kuja na suluhisho la pamoja ili kuziwezesha nchi zote kutekeleza maamuzi hayo.

Mkutano huo unashirikisha  nchi wanachama wa Umoja wa Afrika na unahudhuriwa  wanasheria waandamizi kutoka katika Serikali za nchi za Afrika kwa lengo la kuangalia utekelezaji wa maamuzi yanayotolewa na Mahakama hiyo kwa nchi wanachama pamoja na changamoto zinazopitia nchi hizo na kutafuta namna ya kukabiliana nazo na matarajio yaliyopo kutokana na kuwepo kwa mahakama Mahakama hiyo.