Tuesday, September 27, 2022

SERIKALI, SEKTA BINAFSI WAKUBALIANA KUBORESHA MIFUMO KUWAFIKIA DIASPORA

Mkurugenzi anayeshughulikia masuala ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi James Bwana ameeleza kuwa Serikali imejidhatiti kufanya maboresho ya mifumo ya Tehama katika sekta za umma na sekta binafsi ili kuhakikisha fursa mbalimbali zinazopatikana nchini zinawafikia diaspora kwa wakati.

Hayo yameelezwa katika siku ya pili ya mkutano wa wadau wa sekta za umma na binafsi uliojadili masuala mbalimbali kuhusu ushiriki wa Diaspora katika shughuli za maendeleo ya Taifa uliomalizika leo tarehe 27 Desemba 2022 Jijini Dodoma.

Wadau wa mkutano huu wamepata fursa ya kushirikishana na kupeana uzoefu juu ya huduma mbalimbali wanazozitoa kwa diaspora, kutoa maoni ya namna bora ya kuboresha huduma na umuhimu wa taasisi kushirikiana ili kurahisisha utoaji wa huduma” alisema Balozi James

Miongoni mwa maeneo yaliyopendekezwa na wadau kwa ajili ya maboresho ni pamoja na: kuongeza kazi ya ukamilishwaji wa mapendekezo ya kupatikana kwa hadhi maalum kwa Diaspora, Uandaaji na ukamilishaji wa Sera na sheria ya Diaspora ya Tanzania, taasisi za fedha kuwa na huduma rafiki na zenye riba nafuu kwa Diaspora na ukamilishaji wa mfumo wa kidigitali wa kuhifadhi taarifa muhimu za watanzania wanaoishi na kufanya kazi nje ya nchi, ujulikanao kama “Diaspora Digital Hub”. Mfumo huu utawezesha kuwatambua Diaspora na mahitaji yao pamoja na kuongeza ubunifu katika utoaji huduma.

Maeneo mengine ni uharakishwaji wa mchakato wa kuwapatia Diaspora vitambulisho vya Taifa, kuwepo kwa siku maalum ya Diaspora ili kuwajengea uzalendo, Balozi za Tanzania nje ya nchi kusimamia kwa karibu changamoto mbalimbali za Diaspora, wadau kuwekeza zaidi katika kupata uzoefu kutoka mataifa mengine yaliyofanikiwa katika masula ya Diaspora, maboresho katika taratibu na sheria za ununuzi na umiliki wa ardhi na majengo, kuanzishwa kwa madawati maalum yanayohudumia Diaspora katika sekta za Umma na Binafsi hususan huduma za kidigitali.

Akifunga mkutano huo Naibu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Diaspora, Ofisi ya Rais – Ikulu Zanzibar, Bi. Maryam Ramadhan Hamoud amewahakikishia wadau kuwa Serikali ya mapinduzi Zanzibar itaendelea kutoa ushirikiano na uzoefu wake katika hatua mbalimbali za uandaji wa sera na sheria ya Diaspora kwa upande wa Tanzania bara kwa kuwa tayari Tanzania-Zanzibar ilishakamilisha taratibu hizo.

Mkurugenzi wa masuala ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi James Bwana akiongea na wadau kwenye mkutano wa kujadili masuala ya ushiriki wa Diaspora katika shughuli za maendeleo nchini uliomalizika tarehe 27 Septemba 2022 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa masuala ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi James Bwana akifurahia jambo wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya ushiriki wa Diaspora katika shughuli za maendeleo nchini uliokuwa ukiendelea jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa masuala ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi James Bwana akifuatilia jambo wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya ushiriki wa Diaspora katika shughuli za maendeleo nchini uliokuwa ukiendelea jijini Dodoma.

Afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Semeni Nandonde akichangia jambo kwenye mkutano uliokuwa ukijadili masuala ya ushiriki wa Diaspora katika shughuli za maendeleo nchini uliokuwa ukiendelea jijini Dodoma.
Mwakilishi kutoka Benki ya CRDB Bw. Joseph Haule akichangia mada kwenye mkutano wa kujadili masuala ya ushiriki wa Diaspora katika shughuli za maendeleo nchini uliokuwa ukiendelea jijini Dodoma.
Mwakilishi kutoka Exim Bank Bi. Mtenya Cheya akiwasilisha mada kwenye mkutano wa kujadili masuala yaushirikishwaji wa Diaspora katika shughuli za maendeleo nchini uliokuwa ukiendelea jijini Dodoma.
Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Bi. Victoria Saria akiwasilisha mada kwenye mkutano wa kujadili masuala yaushirikishwaji wa Diaspora katika shughuli za maendeleo nchini uliokuwa ukiendelea jijini Dodoma.
Mkutano wa kujadili masuala ya ushiriki wa Diaspora katika shughuli za maendeleo nchini ukiendelea.

Monday, September 26, 2022

TPA, BANDARI YA ANTWERP KUONGEZA USHIRIKIANO

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) pamoja na Bandari ya Antwerp ya Ubelgiji zimeahidi kuongeza ushirikiano ili kuongeza ufanisi katika shughuli za bandari pamoja na Chuo cha Bandari nchini.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Juma Kijavara amebainisha hayo wakati alipokutana kwa mazungumzo na Uongozi wa Bandari ya Antwerp ya Ubelgiji ulioongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bandari hiyo Bw. Kristof Waterschoot katika Ofisi za Mamlaka hiyo Jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia ugeni huo, Mhandisi Kijavara amesema umetembelea bandari hiyo kwa lengo la kuimarisha ushirikiano baina yao na kuona maeneo gani wanaweza kuanzisha ushirikiano na kukuza ufanisi wa huduma za bandari.

“Tumeona tushirikiane na wenzetu walioendelea zaidi katika bandari ili kuboresha ufanisi katika bandari zetu na maeneo tunayoona ni ya kipaumbele ni ushirikiano katika kuboresha Chuo chetu cha bandari, kuimarisha shughuli za bandari za kila siku, miundimbinu na masuala ya Tehama,”amesema Kijavara.

Pamoja na mambo mengine, Kijavara amesema kwa mwaka wa kalenda 2021 walihudumia meli 50 - 60 kwa mwezi lakini kutokana na kuongezeka kwa ufanisi, TPA inahudumia meli kati ya 65 - 80 kwa mwezi na kuchangia makusanyo kuongezeka kutoka Sh bilioni 70 - 75 kwa mwezi hadi kufikia Sh bilioni 90 - 100 kwa mwezi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bandari ya Antwerp ya Ubelgiji, Bw. Kristof Waterschoot amesema kuwa lengo la ziara yake nchini ni kuangalia maeneo ya ushirikiano baina ya Bandari ya Antwerp na Mamlaka ya Bandari ya Tanzania ili kuboresha zaidi ufanisi wa bandari pamoja na Chuo cha Bandari ili kuweza kuwajengea uwezo zaidi wanafunzi wanaosoma na watakaosoma katika chou cha bandari.

“Tunaamini ushirikiano baina ya Bandari ya Antwerp na TPA utaimarisha sekta ya bandari zetu na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za bandari kwa maslahi ya mataifa yetu,” amesema Bw. Waterschoot    

Uongozi wa Bandari ya Antwerp ya Ubelgiji umewasili nchini leo kwa ziara ya kikazi ya siku tatu ambapo mbali na kuitembelea Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), pia ujumbe huo utafanya ziara katika Shirika la Bandari Zanzibar (ZPC) pamoja na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Jijini Dodoma.

Balozi wa Ubelgiji nchini, Mhe. Peter Huyghebaert akifuatilia kikao baina ya Ujumbe wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Mkurugenzi Mkuu wa Bandari ya Antwerp ya Ubelgiji, Bw. Kristof Waterschoot kilichofanyika katika ofisi za Bandari Jijini Dar es Salaam 
Kikao kikiendelea baina ya Ujumbe wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na ujumbe wa Bandari ya Antwerp ya Ubelgiji kikiendelea katika ofisi za Bandari Jijini Dar es Salaam 

Mkurugenzi Mkuu wa Bandari ya Antwerp ya Ubelgiji, Bw. Kristof Waterschoot akieleza jambo wakati wa kikao kati yake na Ujumbe wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA). kikao hicho kilichofanyika katika ofisi za Bandari Jijini Dar es Salaam 

Ujumbe wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na katika pichaa ya pamoja na Ujumbe wa Bandari ya Antwerp ya Ubelgiji

Ujumbe wa Bandari ya Antwerp ya Ubelgiji ukipata ufafanuzi wa shughuli mbalimbali za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ulipofanya ziara katika bandari hiyo leo Jijini Dar es Salaam




WIZARA YA MAMBO YA NJE YATOA WITO KWA WADAU KUFUNGUA HUDUMA MAALUM KWA DIASPORA


Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imekutanisha wadau wa sekta ya umma na  binafsi katika mkutano wa kujadili masuala ya diaspora na ushirikishwaji wao ili waweze kuchangia maendeleo ya Taifa kwa ufanisi zaidi.

Akifungua mkutano huo  wa siku mbili tarehe 26 na 27 Septemba 2022, Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Agness Kayola ameeleza kuwa madhumuni ya mkutano  huo ni  kujadili namna wadau hao watakavyoweza kuongeza huduma za taasisi zao kwa diaspora ili kuleta ushirikiswaji wenye tija katika maendeleo ya Taifa.

“Mkutano huu umewakutanisha wadau wanaotoa huduma mbalimbali kwa Diaspora na wale ambao hawana huduma bado, lakini ni Wadau wanaoweza kuwa na mchango muhimu katika kuongeza ushiriki wa Diaspora wa Tanzania kwenye masuala ya maendeleo ya taifa’’ alisema Balozi Kayola.

Pia akaeleza kupitia mkutano huo wadau watapata fursa ya kushirikishana juu ya masuala mbalimbali muhimu, kama vile Fursa za Uwekezaji nchini; Vigezo vya Kusajili Wawekezaji Wazawa na Wawekezaji Wageni, wakiwemo Diaspora wenye Uraia wa nchi nyingine; Fursa za Uwekezaji kwa Diaspora na nini kifanyike kuongeza Uwekezaji kutoka kwa Diaspora wa Tanzania.

Naye Mkurugenzi wa masuala ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi James Bwana ameeleza kuwa mkutano huo umezikutanisha taasisi za fedha, kampuni za simu za mikononi, taasisi za umma na binafsi za ujenzi wa nyumba za makazi kama vile Shirika la nyumba la Taifa (NHC), Hamidu City Park, KC Land na wengine.

Vilevile ameeleza kuwa kupitia mkutano huo Serikali na wadau wa sekta binafsi wataweza kujadili namna mataifa mengine duniani yalivyofanikiwa katika eneo la ushirikishwaji wa diaspora ikiwa ni hatua ya kuboresha huduma za sekta binafsi katika kuchagiza ari na hamasa ya diaspora kuchangia katika maendeleo ya Taifa.

"Takwimu zinaonesha nchi kama China, India, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Ghana, Nigeria zilivyofanikiwa katika eneo la dispora hivyo, hatuna budi kuongeza ubunifu ili kufanikisha mikakati yetu ya kitaifa kwa kuunganisha nguvu ya diaspora na sekta binafsi" alisema Balozi Bwana.

Kwa upande wa Naibu Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Diaspora, Ofisi ya Rais – Ikulu, Zanzibar, Bi. Maryam Ramadhan Hamoud ameeleza kuwa mkutano huo utawafahamisha wadau kuhusiana na mchango wa Diaspora katika sekta mbalimbali hususan Afya, Elimu, Uwekezaji na umuhimu wa Diaspora katika kuchangia maendeleo ya nchi kupitia fedha wanazotuma nyumbani (Remittances).

Mbali na hayo Bi. Maryam aliongeza kuwa, wadau watapata fursa ya kutambua huduma mbalimbali za misaada ya kijamii, Sayansi na Ubunifu, ambayo huletwa nchini na Wafadhili kupitia uratibu wa Diaspora.

Mwaka 2010, Serikali ilianzisha Kitengo cha Diaspora chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ilianzishwa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Uratibu wa Masuala ya Diaspora katika Ofisi ya Rais Ikulu – Zanzibar. Jukumu kubwa la Ofisi hizi mbili, ni kusimamia, kuratibu na kushughulikia masuala yanayohusu Ushiriki wa Diaspora katika shughuli za Maendeleo ya nchini.
Mkurugenzi wa masuala ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi James Bwana akiongea na wadau kwenye mkutano wa kujadili masuala yaushirikishwaji wa Diaspora katika shughuli za kiuchumi nchini uliofanyika jijini Dodoma
Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje naUshirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Agnes Kayola akifunguamkutano wa wadau kujadili masuala ya ushirikishwaji wa Diasporakatika shughuli za maendeleo nchini uliofanyika jijini Dodoma
Mkurugenzi wa masuala ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi James Bwana akifuatilia majadala uliokuwa ukiendelea kuhusu ushirikishwaji wa Diaspora katika shughuli za maendeleo nchini uliofanyika jijini Dodoma
Meza kuu; Mkurugenzi wa masuala ya Diaspora katika Wizaraya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki BaloziJames Bwana (kushoto) Kaimu Naibu Katibu Mkuu Balozi Agnes Kayola (katika) na Naibu Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano waKimataifa na Diaspora, Ofisi ya Rais – Ikulu, Zanzibar, Bi. Maryam Ramadhan Hamoud wakifuatilia mkutano
Sehemu ya wadau wakifuatilia mkutano wa kujadili masuala yaushirikishwaji wa Diaspora katika shughuli za maendeleo nchini uliofanyika jijini Dodoma
Sehemu ya wadau wakifuatilia mkutano wa kujadili masuala yaushirikishwaji wa Diaspora katika shughuli za maendeleo nchini uliofanyika jijini Dodoma
Meza Kuu wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadauwalioshiriki mkutano wa kujadili masuala ya ushirikishwaji wa Diaspora katika shughuli za maendeleo nchini uliofanyika jijini Dodoma

BALOZI MULAMULA AZUNGUMZA NA WAFANYAKAZI UBALOZI WA NEW YORK


 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akizungumza na wafanyakazi wa Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa jijini New York

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Mhe. Prof. Gaston Kennedy (kushoto) na Balozi na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Mhe. Dkt. Suleiman Ali Suleiman (kulia) alipokutana na wafanyakazi wa ofisi hiyo jijini New York
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi ya Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa jijini New York

Balozi na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Mhe. Dkt. Suleiman Ali Suleiman (wa tatu kulia) akizungumza katika kikao cha Mhe Waziri Mulamul alipokutana na wafanyakazi wa Ofisi ya Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa jijini New York

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akizungumza na wafanyakazi wa Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa jijini New York

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Ofisi ya Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa jijini New York

 

 



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amekutana na kuzungumza na wafanyakazi wa Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa jijini New York na kuwataka kutanguliza uzalendo na kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za utumishi wa umma wakati wa kutekeleza majukumu yao kwa faida ya nchi.

Balozi Mulamula pia amewataka watumishi hao kusimamia matumizi mazuri ya fedha za Serikali katika kutekeleza majukumu yao kwenye vituo vya uwalikishi wa nchi na kutangaza kazi mbalimbli zinazofanywa na ubalozi ili kuonesha kazi zao na hivyo kuonesha umuhimu wa uwakilishi katika Umoja wa Mataifa na mchango wao katika Diplomasia ya Uchumi.

"Hapa New York mna kila sababu ya kujitangaza, nyinyi hapa mnamuingiliano mkubwa, ni nyumbani kwa Umoja wa Mataifa, lazima  muoneshe faida ya nyinyi kuwakilishaa nchi kwenye Umoja wa Mataifa, onesheni mchango wenu katika shughuli za diplomasia ya uchumi na mashirika ya kimataifa,"alisema Balozi.


Amewapongeza kwa namna mnavyoshirikiana na Diaspora wa Tanzania walioko jijini New York, na kuawataka waendeleze ushirikiano huo kwani wao ni walezi  na wasaidizi wao panapohitajika jambo la kufuatilia
 

Nimeona mna ushirikiano sana na Diaspora wa hapa,  muendelee kuwashirikisha na muendelee kuwa walezi, washauri na msimbague mtu, sisi kama Wizara tunapenda kuwaona mkiwa pamoja, mshirikiane na Idara ya Diaspora katika kutekeleza suala hilo," alisema Balozi Mulamula



Sunday, September 25, 2022

TUNATHAMINII NA KUTAMBUA MCHANGO WA INDIA: BALOZI MULAMULA

z

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula Balozi Mulamula akizungumza wakati wa hafla maalum ya kuadhimisha miaka 75 ya Jamhuri ya India katika Umoja wa Mataifa iliyofanyika kwenye Ofisi za Ubalozi wa kudumu wa India katika Umoja wa Mataifa jijini New York.

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula Balozi Mulamula akiwa na washiriki kutoka mataifa mbalimbali  katika hafla maalum ya kuadhimisha miaka 75 ya Jamhuri ya India katika Umoja wa Mataifa iliyofanyika kwenye Ofisi za Ubalozi wa kudumu wa India katika Umoja wa Mataifa jijini New York.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mhe. Amin Juma Mohamed akizungumza wakati wa hafla maalum ya kuadhimisha miaka 75 ya Jamhuri ya India katika Umoja wa Mataifa iliyofanyika kwenye Ofisi za Ubalozi wa kudumu wa India katika Umoja wa Mataifa jijini New York.

Waziri wa Mambo ya Nje wa visiwa Vya Jamaica Mhe. Kamina Johnson Smith akizungumza wakati wa hafla maalum ya kuadhimisha miaka 75 ya Jamhuri ya India katika Umoja wa Mataifa iliyofanyika kwenye Ofisi za Ubalozi wa kudumu wa India katika Umoja wa Mataifa jijini New York.


Baadhi ya washiriki wa  hafla maalum ya kuadhimisha miaka 75 ya Jamhuri ya India katika Umoja wa Mataifa katika picha ya pamoja kwenye hafla hiyo iliyofanyika kwenye Ofisi za Ubalozi wa kudumu wa India katika Umoja wa Mataifa jijini New York.


Baadhi ya washiriki wa  hafla maalum ya kuadhimisha miaka 75 ya Jamhuri ya India katika Umoja wa Mataifa katika picha ya pamoja kwenye hafla hiyo iliyofanyika kwenye Ofisi za Ubalozi wa kudumu wa India katika Umoja wa Mataifa jijini New York.


 

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amesema Tanzania inathamini na kutambua mchango mkubwa wa India katika kuendeleza miradi ya maji na afya nchini na hivyo kusaidia jiotihada za Tanzania katika kutekeleza malengo endelevu ya Umoja wa Mataifa na dira ya Tanzania ya Mwaka 2025 .

Balozi Mulamula ametoa kauli hiyo katika hafla maalum ya kuadhimisha miaka 75 ya Jamhuri ya India katika Umoja wa Mataifa iliyofanyika kwenye Ofisi za Ubalozi wa kudumu wa India katika Umoja wa Mataifa jijini New York.

 

“TANZANIA inathamini na kutambua mchango wa India katika kuisaida serikali kutekeleza mipango yake ya maendeleo, na tunaamini kuwa ushirikiano uliopo utakuwa zaidi na zaidi kwani ushirikiano huo ni matunda ya uhusiano wa nchi za kusini na kusini,”

 

Amesema uhusiano na Indi unachangia juhudi za Tanzania kufikia malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa ya Afya na ustawi wa watu na maji safi na salama na hivyo kuchangia utekelezaji wa dira ya Tanzania ya mwaka 2025 na kuongeza kuwa ni mmoja ya wawekezaji wakubwa nchini ambaye anachangia asilimia 16 ya biashara ya Tanzania na kuchagiza utekelezaji wa dira yetu ya 2025.

 

Ametaja miradi inayonufaika na ushirikiano huo kuwa ni usambaza maji Dar es Salaam hadi Chalinze wenye thamani ya Dolla za Marekani Milioni 178 ambao unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba mwaka huu. 

Miradi mingine ni usambazaji wa bomba la maji kutoka Ziwa Victoria hadi  Tabora, Igunga, na Nzega uliozinduliwa mwezi January 2021; kusambaza bomba la maji kwenda katika miji ya Tinde na Shelui na vijiji vya jirani wenye thamani ya dola milioni 10.64 za Marekani ambao unaotarajiwa kukamilika mwezi Oktoba 2022; na mradi wa ujenzi wa mfumo wa usambazaji maji katika miji 28 Tanzanian wenye thamani ya dola milioni 500 za Marekani ambao utekelezaji wake unatarajiwa kuanza mwezi Disemba 2022.
 

Kuhusu sekta ya Afya Balozi Mulamula amesema Tanzania inaishukuru India kwa mchango wake kwa Tanzania kujiweka tayari kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa COVID 19 hasa kwa kuwekeza katika ujenzi wa vituo vya afya, kuongeza nguvu ya watumishi wa afya nchini na kuongeza uwezo wa nchi kutengenza dawa, ugavi, chanjo na vifaa tiba.
 

Tarehe 15 Agosti 2022 India  iliadhimisha miaka 75 ya kuwa Jamhuri na miaka 76 tangu ipate uhuru  ipate Uhuru wake.




Saturday, September 24, 2022

BALOZI MULAMULA AKUTANA NA MAWAZIRI WA UFARANSA NA RWANDA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Waziri wa Nchi, Maendeleo, Kifaransa na Ushirikiano wa Kimataifa wa Ufaransa Mhe. Chrysoula Zacharopoulou walipokutana katika Ofisi za Ubalozi wa Ufaransa Umoja wa Mataifa jijini New York ikiwa ni moja ya mikutano ya pembeni inayoendelea sambamba na Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa nvhini Marekani.

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiangalia kitabu cha taarifa alichopatiwa na  na Waziri wa Nchi, Maendeleo, Kifaransa na Ushirikiano wa Kimataifa wa Ufaransa Mhe. Chrysoula Zacharopoulou walipokutana katika Ofisi za Ubalozi wa Ufaransa Umoja wa Mataifa jijini New York.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akimuelezea kuhusu zawadi ya picha aliyompa Waziri wa Nchi, Maendeleo, Kifaransa na Ushirikiano wa Kimataifa wa Ufaransa Mhe. Chrysoula Zacharopoulou walipokutana katika Ofisi za Ubalozi wa Ufaransa Umoja wa Mataifa jijini New York.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula na ujumbe wake katika picha ya pamoja na Waziri wa Nchi, Maendeleo, Kifaransa na Ushirikiano wa Kimataifa wa Ufaransa Mhe. Chrysoula Zacharopoulou walipokutana katika Ofisi za Ubalozi wa Ufaransa Umoja wa Mataifa jijini New York.





Waziri Mulamula alipokutana na  Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Mhe. Vincent Biruta jijini New York na kujadiliana juu ya masuala yenye maslahi baina ya nchi zao.

Waziri Mulamula akiwa na Balozi wa Tanznia nchini Marekani Mhe. Dke Elsie Kanza (wa kwanza kulia) walipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Mhe. Vincent Biruta jijini New York na kujadiliana juu ya masuala yenye maslahi baina ya nchi zao.

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amekutana na kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Mhe. Chrysoula Zacharopoulou katika Ofisi za Ubalozi wa Ufaransa Umoja wa Mataifa jijini New York.

Katika mazungumzo yao viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali ya kimaendeleo na namna ya kuendelea kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania  na Ufaransa na namna ya kuendeleza sekta za uchukuzi, muindombinu, kilimo,  biashara na uwekezaji nchini.

Viongozi hao pia wamejadiliana namna ya kuongeza ujazo wa biashara kati ya Tanzania na Ufaransa na kuihusisha sekta binafsi katika harakati za kuinua uchumi wa Tanzania.

Katika tukio jingine Waziri Mulamula amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Mhe. Vincent Biruta jijini New York na kujadiliana juu ya masuala yenye maslahi baina ya nchi hizo.

Viongozi hao wajadili namna wanavyoweza kushirikiana kupitia sekta ya biashara, uwekezaji na uchukuzi na hivyo kuchangia harakati za ukuzaji wa uchumi wan chi hizo.

Viongozi hao wako jijini New York kuhudhuria Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa  Mataifa (UNGA) unaoendelea nchini Marekani.

BALOZI MULAMULA ASHIRIKI MKUTANO WA AMANI NA USALAMA WA AU

 

 

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Robert Kahendaguza aliposhiriki katika  Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Afrika uliofanyika katika Ofisi za Uwakilishi za Umoja wa Afrika kwenye Umoja wa Mataifa Jijini New York.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Robert Kahendaguza akizungumza  katika  Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Afrika uliofanyika katika Ofisi za Uwakilishi za Umoja wa Afrika kwenye Umoja wa Mataifa Jijini New York tarehe 23/09/2022

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Mhe. Mussa Faki Mahamat (kushoto ) katika meza kuu wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Afrika uliofanyika katika Ofisi za Uwakilishi za Umoja wa Afrika kwenye Umoja wa Mataifa Jijini New York tarehe 23/09/2022

Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Afrika uliofanyika katika Ofisi za Uwakilishi za Umoja wa Afrika kwenye Umoja wa Mataifa Jijini New York wakifuatilia mkutano huo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula ameshiriki katika Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Afrika uliofanyika katika Ofisi za Uwakilishi za Umoja wa Afrika kwenye Umoja wa Mataifa  Jijini New York.


Akizungumza katika mkutano huo Balozi Mulamula ameuhakikishia Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Kimataifa kuwa Tanzania iko tayari na itaendelea kushirikiana na jumuiya hizo kushughulikia changamoto za amani na usalama.


Amesema utayari huo wa Tanzania unakwenda sambamba na kufanya mapambano dhidi ya ugaidi wa aina zote lazima uwe kipaumbele katika nchi zote na kutoa wito wa kuanzishwa kwa kamati ya mawaziri  ya kukabiliana na ugaidi kama ilivyokubaliwa wakati wa mkutano wa AU uliofanyika mjini Malabo.
 
Amesema vita dhidi ya ugaidi na vitendo vya kihalifu vinahitaji nguvu ya kushirikiana pamoja kwa ngazi zote kuanzia taasisi, nchi, kanda na taasisi za kimataifa na kusisitiza juu ya umuhimu wa kuunganisha kazi ya uangalizi ya Umoja wa Afrika  na Baraza la Usalama la Umoja wa Afrika ili kuwa na uratibu wa pamoja.
 
Amezisihi nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kusaini na kuridhia mikataba muhimu kama  Mkataba wa  kuzuia na kupambana na ugaidi; Mkataba wa Umoja wa Afrika wa ushirikiano wa kuvuka mipaka na Mkataba wa Afrika wa  Ulinzi wa Usafiri majini,usalama na maendeleo ili kuimarisha nguvu katika kupambana na ugaidi, vitendo vya kidhalimu.

Friday, September 23, 2022

FILAMU YA THE ROYAL TOUR ILIYOTAFSIRIWA KWA KIJAPAN YAZINDULIWA JAPAN

Wageni wanaotembelea Banda la Tanzania katika Maonesho ya Kimataifa ya Utalii yanayoendelea nchini Japan wakiangalia Filamu ya "The Royal Tour"
Wageni wanaotembelea Banda la Tanzania katika Maonesho ya Kimataifa ya Utalii yanayoendelea nchini Japan wakiangalia Filamu ya "The Royal Tour" huku wakiburudika kwa kula vyakula vya Kitanzania
Sehemu ya Filamu ya "The Royal Tour" ikimuonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan alivyokuwa akiapa kushika wadhifa huo
Banda la Tanzania limependeza kweli kweli ambapo linavutia wageni wengi kulitembelea.

 

DKT MPANGO AHUTUBIA BARAZA. KUU LA UMOJA WA MATAIFA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Philip Mpango akihutubia Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jijini New York nchini Marekani.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Philip Mpango akihutubia Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) jijini New York.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Philip Mpango akihutubia Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA).


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (kushoto) Waziri wa Nchi Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa Zanzibar Mhe. Masoud Ali Mohammed , Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu na Mama Dionisia Mpango Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakifuatilia hotuba ya Makamu wa Rais Dkt. Mpango katika Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijijini New York nchini Marekani 

 


 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema Tanzania inaamini diplomasia na meza za mazungumzo ni chombo bora cha kutatua migogoro duniani na kwamba nchi zina wajibu wa kuzingatia utatuzi wa migogoro kwa njia za amani ili kulinda ustawi wa watu watu na kuepuka athari zinazoweza tokana na migogoro duniani.

Mhe. Dkt. Mpango amesema hayo jijini New York alipohutubia Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) alipomuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

“Tanzania inaamini kuwa diplomasia na meza za mazungumzo ndiyo chombo muhimu na ni vitu vikuu vya kuzingatia wakati wa  kutatua migogoro duniani, Mataifa yanapaswa kuzingatia kuwa yanahaki na wajibu wa kulinda maisha ya binadamu hasa watoto na wanawake lakini pia lazima wahakikishe ustawi wa watu wote , ni muhimu  kutafuta suluhu au kutatua migogoro kwa njia za amani, hii inasaidia kuepuka athari zitokanazo na migogoro hiyo kama vile ongezeko la bei za chakula na mafuta na kushuka kwa uzalishaji wa kilimo na viwanda duniani kote,“ alisema Dkt. Mpango.

Makamu wa Rais pia amepongeza juhudi za Umoja wa Mataifa katika kukuza lugha mbalimbali duniani ikiwemo tamko la kihistoria la Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu na Sayansi (UNESCO) lililoitaja "7 Julai" kuwa Siku ya Lugha ya Kiswahili Duniani na kuwezesha lugha hiyo kuadhimishwa kwa mara ya kwanza duniani na hivyo kuitambua arsmi kimataifa.

Amesema Tanzania inajivunia kushiriki katika shughuli za kulinda amani ambapo imechangia Askari katika misheni 5 kati ya 16 zilizopo za kulinda amani duniani na kuahidi kuwa  itaendelea kuchangia zaidi iwapo itaombwa kufanya hivyo na kuiomba Umoja wa Mataifa kuongeza uungaji mkono wake kwa juhudi za kikanda katika za kujenga na kulinda amani.

 

Kuhusu mabadiliko ya tabia nchi Dkt. Mpango amesema nchi za Afrika zinahitaji mabadiliko ya haki na utaratibu katika kufikia matumizi ya nishati mbadala kwa kuzingatia hali za Maisha ya watu wa bara hilo wenye changamoto mbalimbali za upatikanaji wa nishati hizo na kutoa wito wa kuondolewa kwa upinzani dhidi ya ufadhili wa kimataifa katika utekelezaji wa miradi ya mageuzi katika nchi za Afrika ambayo inalenga kutumia rasilimali ikiwemo gesi kwa ajili ya nishati na matumizi mengine katika kufikia maendeleo.

 

Amesema biashara ya hewa ukaa barani Afrika inapaswa kufanyika kwa uwazi na kuwanufaisha wananchi waliotunza mazingira na misitu inayozalisha hewa hiyo kwa matumizi ya dunia na kuongeza kuwa Tanzania ni moja ya iliyowekeza zaidi katika uhifadhi wa misitu ambapo asilimia 30 ya eneo la ardhi ya taifa hilo imehifadhiwa.

 Kuhusu mapambano ya ugonjwa wa COVID 19, Dkt. Mpango amesema amezishukuru nchi na jumuiya za kimataifa zilizoshirikiana na Tanzania kupambana na janga hilo kuanzia utoaji wa vifaa vya uchunguzi, dawa, programu za msaada wa chanjo, ambazo zimekuwa muhimu katika kushinda vita dhidi ya janga hilo na kuwezesha nchi kufikia asilimia 60 ya kuchanja watu wake hadi sasa na kuongeza kuwa kuchelewa kwa Afrika kupata chanjo za ugonjwa huo kunasisitza hitaji la Nchi za Kiafrika kufanya kazi pamoja katika ukuzaji wa masuluhisho asilia kupitia utafiti wa pamoja wa kisayansi.

Ametoa wito kwa mataifa kuweka vipaumbele vya vitendo hasa kwenye malengo ya maendeleo endelevu ambapo amayasihi mataifa kujitolea kufanya kazi kwa karibu na Umoja wa Mataifa na Nchi Wanachama wake, kwa nia ya ushirikiano na mshikamano wa kimataifa kuelekea mustakabali endelevu.