Wednesday, December 21, 2011

Mabalozi wapya wakaribishwa Wizara ya Mambo ya Nje

Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bwana John Haule leo amewakaribisha rasmi Mabalozi Wateule kwenye Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambapo Wakuu wa Idara na Votengo walieleza kwa kifupi kazi za Wizara kwa ujumla. 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bwana John Haule akiongoza kikao cha utambulisho kati ya Mabalozi Wateule na Uongozi wa Wizara Leo tarehe 21.12.2011

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara Bwana D. Mndeme akijitambulisha kwa mabalozi wapya wa Wizara.

Balozi Mteule nchini Misri, Mhe. Mohamed Hamza akijitambulisha kwenye Mkutano huo. Kushoto ni Balozi Batilda Burian anayeenda nchini Kenya.

Balozi Mteule wa Tanzania nchini Oman Mhe. Ali Saleh akijitambulisha kwa uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Balozi Mteule wa Tanzania nchini Msumbiji Mhe. Shamim Nyanduga

Balozi Mteule wa Tanzania nchini Uganda Mhe. Ladislaus Komba akijitambulisha
Katibu Mkuu wa Wizara Bwana John Haule akiongea na Mabalozi Wateule. Wa kwanza kushoto ni Mhe. Batilda Burian, Balozi Mteule wa Tanzania nchini Kenya.

Mhe. Grace Mujuma (wa kwanza Kulia), Balozi Mteule wa Tanzania nchini Zambia  

Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani Bw. Gabriel Mwero akijitambulisha kwa mabalozi wapya.


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Bw. Adrian Miyaye akijitambulisha.

Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bw. Katinda E. Kamando akijitambulisha kwa mabalozi wapya wa Wizara.


Kaimu Mkurugenzi Idara ya Asia na Australasia Bi. Naimi Aziz akijitambulisha kwa mabalozi wapya wa Wizara.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.