TAARIFA KWA WATANZANIA
WAISHIO KATIKA MAENEO YA UWAKILISHI WA UBALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA NCHINI AFRIKA KUSINI
Mhe. Radhia N.M.
Msuya, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania nchini Afrika Kusini anawatangazia watanzania wote waishio katika
maeneo ya uwakilishi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini
Afrika Kusini yaani Afrika Kusini,
Lesotho, Botswana na Namibia kuwa wanaombwa kujiandikisha kupitia anuani ya
Ubalozi ifuatayo: administration@tanzania.org.za
ili kurahisisha msaada wakati watanzania wanapopatwa na shida mbali mbali.
Sambamba
na taarifa hii, Mheshimiwa Balozi anapenda kuzishukuru Jumuiya za watanzania
waishio katika maeneo ya uwakilishi wake kwa ushirikiano wa dhati wanaoutoa kwa
Ubalozi wao katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku ya kuimarisha
mashirikiano na nchi za uwakilishi huo.
Tunawashukuru
na kuwatakia heri ya mwaka mpya, 2013!
Ahsanteni.
Imetolewa na,
Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Pretoria,
JAMHURI YA
AFRIKA KUSINI
17 Januari,
2013
Unapojibu tafadhali taja:
TZPR/I.20/I
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.