Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisalimiana na Mhe. Francisco Montecillo Padilla, Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa hapa nchini mara baada ya kuwasili Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumsalimia na kumpa pole kufuatia shambulio la bomu lililotokea Jijini Arusha tarehe 5 Mei, 2013 na kupelekea watu watatu kufariki dunia na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa. Balozi Padilla alikuwa miongoni mwa wageni waalikwa katika hafla ya ufunguzi rasmi wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, Jimbo Kuu la Arusha wakati tukio hilo linatokea. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.