Sunday, June 30, 2013

Matukio mbalimbali katika mkutano wa Smart Partnership Dialogue

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza  na Waziri Mkuu wa Algeria, Mhe. Abdelmalek Sellal Mazungumzo hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Mhe. Sellal yupo nchini kuhudhuria Mkutano wa Majadiliano kwa Manufaa ya Wote (Global 2013 Smart Partnership Dialogue).

Mhe. Rais Kikwete akisaini kitabu cha wageni alipombelea Banda la maonesho la Kampuni ya MaxMalipo kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Kampuni hiyo huku Maafisa wa kampuni hiyo wakishuhudia . Maonesho hayo yanafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere huku mkutano wa Majadiliano kwa Manufaa ya Wote (Global 2013 Smart Partnership Dialogue) ukiendelea.


Mhe. Rais Kikwete akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Bw. Juma Rajabu, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MaxMalipo kuhusu namna kampuni hiyo inavyorahisisha malipo ya huduma mbalimbali kwa wananchi kwa teknolojia ya hali juu.

Mhe. Rais Kikwete akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Bw. Lusaju Mwamkonda, mmoja wa Maafisa kutoka Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) ya namna Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ulivyoeenea ndani na nje ya Tanzania ikiwemo nchi za Burundi, Rwanda n.k. Kushoto kwa Mhe. Rais ni Dkt. Kamugisha Kazaura, Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL.

Mhe. Rais Kikwete akizungumza na Watendaji mbalimbali alipotembelea Banda la Maonesho la TTCL. Kulia kwa Mhe. Rais ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Makame Mbarawa.

Mhe. Rais Kikwete na Mhe. Mbarawa  katika picha ya pamoja na Watendaji wa TTCL alipotembelea banda hilo.

Mhe. Rais Kikwete akipata maelezo  kutoka kwa mmoja wa Maafisa Watendaji alipotembelea Banda la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa (NIMR) kuhusu  namna Taasisi hiyo inavyojishughulisha na utafiti wa magonjwa pamoja na madawa.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani)  kuhusu mkutano wa Majadiliano kwa Manufaa ya Wote (Smart Partnership). Mkutano huo unafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuanzia tarehe 28 Juni hadi 1 Julai 2013. Kushoto kwa Balozi Sefue ni Mkurugenzi wa Commonwealth Partnership for Technology Management (CPTM), Dkt. Andrew Taussig.


Mhe. Membe akiteta jambo na Meneja wa Mkutano wa Majadiliano kwa Manufaa ya Wote, Bibi Rosemary Jairo.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Fatuma Mwasa(kushoto) akifurahia jambo na Mkuu wa Sekretarieti ya Maandalizi ya Mkutano wa Majadiliano kwa Manufaa ya Wote (Smart Partnership), Bibi Victoria Mwakasege.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.