Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan M. Mwinyi akitia sahihi kwa niaba ya Serikali,Mkataba wa Kimataifa wa Kudhibiti Biashara ya Silaha ( ATT) Tanzania ilikuwa kati ya nchi 67 za kwanza ambazo zimetia sahihi katika siku ya kwanza ya uzinduzi wa tukio hilo la kihistoria. Baada ya Mkataba kutiwa sahihi nchi zaidi ya 50 kama sheria zinavyotaka utaanza kufanya kazi rasmi baada ya siku 90. Mkataba huu ambazo umechukua zaidi ya miaka sita hadi kupatikana unalenga katika pamoja na mambo mengine kusimamia na kuratibu biashara ya silaha zikiwamo mizinga ya kivita, magari ya deraya, ndege za kivita, helkopta za mashambulizi, meli za kivita na silaha ndogo na nyepesi. vile vile mkataba unalenga kudhibiti silaha zisiangukie mikononi mwa makundi ya kihalifu yakiwamo ya kigaidi.
TANZANIA YAWEKA HISTORIA YATIA
SAHIHI MKATABA WA KUDHIBITI
BIASHARA YA SILAHA
Na Mwandishi Maalum
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa miongozi mwa
nchi za kwanza kutia sahihi Mkataba wa Kimataifa wa Kudhibiti Biashara ya Silaha Duniani ( ATT)
Utiaji sahihi
wa tukio hilo la kihistoria umeziduliwa
jana jumatatu ( Juni 3) hapa Makao Makuu
ya Umoja wa Mataifa. Ukishuhudiwa na viongozi
mbalimbali akiwamo Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon.
Katika tukio
hilo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliwakilishwa na Balozi Ramadhan M. Mwinyi, Naibu Muwakilishi
wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.
Utiaji sahihi wa mkataba huo
unafanyika ikiwa ni takribani miezi miwili kupita tangu Baraza Kuu la
Umoja wa Mataifa lilipoupitisha kwa kuupigia kura 154 za ndiyo na hivyo
kuhitimisha majadiliano ya uundwaji
wa mkataba yaliyodumu kwa takribani
miaka sita.
Kutiwa sahihi kwa
Mkataba huo sasa kunafungua fursa
ya kuanza kufanya kazi rasmi baada ya
siku 90, kwa sababu zilikuwa zikihitajika sahihi
50 ili upate baraka ya kuanza rasmi. Lakini idadi hiyo
imepitiliza katika siku ya kwanza ya utiaji wa sahihi na kufikia nchi 67.
Dhumuni kuu
la mkataba pamoja na mambo mengine ni kusimamia na
kuratibu biashara ya silaha za aina mbalimbali zikiwamo, mizinga ya kivita,
magari ya deraya, ndege za kivita,
helkopta za mashambulizi, meli za kivita, makombora pamoja na silaha ndogo
ndogo na nyepesi.
Aidha Mkataba pamoja
masuala mengineyo hautaingilia uhuru wa nchi kununua silaha kwa matumizi yake ya ndani na haki ya kujilinda na kulinda
mipaka yake, vilevile mkataba hauzui nchi kufanya biashara ya kusafiri aina
yoyote ya silaha ilimradi inazingatia sheria na taratibu zilizomo ndani ya mkataba ikiwa ni pamoja na taratibu ambazo
nchi yenyewe imejiwekea.
Matumaini ya Jumuiya ya Kimataifa ni kwamba
utekelezaji wa mkataba na kama
utaekelezea ipasavyo utasaidia sana
kudhibiti silaha zisiangukie mikononi mwa makundi mbalimbali ya kihalifu
yakiwamo ya kigaidi.
Akizungumza mara baada ya kutia sahihi, Balozi Ramadhan Mwinyi aliungana na wasemaji
wengine katika kukaribisha hatua hiyo
muhimu. Huku akieleza kwamba kwa Tanzania kutia sahihi ni uthibitisho wa
utayari wake wa kuutekeleza kwa kuzingatia masharti na matakwa yanayoendeana
na mkataba huo.
Akasema
Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi za mwanzo kutia sahihi mkataba
huo kwa kuwa ilikuwa moja kati ya nchi zilizodhamini
Azimio la Kuanzishwa kwa Mkataba na pia ilishiriki kikamilifu katika
majadiliano yote yaliyozaa mkataba huo.
Balozi Mwinyi akaeleza pia kuwa kufanya kazi kwa Mkataba
huo kutachangia katika amani ya Kimataifa, amani na usalama wa Kikanda na pia utachangia sana
katika kupunguza madhara yatokanayo na
biashara haramu na holela ya silaha lakini pia
utasaidia katika kukuza na kuimarisha uhusiano mzuri miongoni mwa nchi wanachama.
Katika hatua
nyingine Muwakilishi huyo wa Tanzania amesisitiza haja na umuhimu wa uwepo wa fursa sawa kati ya
wasafirishaji wa silaha na waagizaji wa silaha na kwamba Mkataba huo usidhibiti au kuzuia
biashara ya silaha ambayo ni halali na kwamba mkataba haupashwi kuingilia au
kwa namna yoyote ile au kuadhiri uhuru na haki ya nchi kujilinda na
kulinda watu wake.
Tanzania pia imekaribisha misaada ya kiufundi katika
maandalizi ya utekelezaji wa mkataba huo hasa
kwa nchi zinazoendelea.
Nchi hizo 67
ambazo zimetia sahihi ni , Albania, Antigua and Barbuda, Argentina,
Australia, Austria, Bahamas, Belgium,
Belize, Benin, Brazil, Burkina Faso, Burundi, Chile, Costa Rica, Cote D’ Ivoire, Croatia, Cyprus, Czech
Republic , Denmark, Djibout, na Dominica Republic.
Nyingine ni Estonia, Finland, France, Germany, Greece,
Grenada, Guyana, Hungary, Iceland, Italy, Jamaica, Japan, Latvia, Liechtenstein, Lithuania, Luxembourg, Mali, Malta,
Mauritania, Mexico na Montenegro.
Mataifa mengine ni
Mozambique, Netherlands, New Zealand, Norway, Palau, Panama, Portugal,
Republic of Korea, Romania, Saint
Lucia, Saint Vincent and the Grenadines,
Senegal, Seychelles, Slovenia,
Spain, Suriname, Sweden, Switzerland, Togo,
Trinidad and Tobago, Tuvalu, United Kingdom of Great Britain and
Northern Ireland, United Republic of Tanzania na Uruguay.
Habari na picha kwa hisani ya Mrs. Maura Mwingira, Ubalozi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, mjini New York, nchini Marekani
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.