Tuesday, July 2, 2013

Mhe. Rais Obama atembelea Mitambo ya Symbion na kuzindua mpango wa maendeleo ya nishati Afrika



Rais wa Marekani, Mhe. Barack Obama akizindua rasmi Mpango Maalum wa Maendeleo ya Nishati Barani Afrika ulioanzishwa na Marekani  (Power Africa Initiative) wakati alipotembelea Mitambo ya Kufua Umeme ya Symbion iliyopo Ubungo Jijini Dar es Salaam katika siku yake ya pili ya ziara ya kitaifa hapa nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Mhe. Rais Obama wakati wa uzinduzi huo. Wengine katika picha ni Mhe. Prof. Sospeter Muhongo, Waziri wa Nishati na Madini na Mhe. Said Mecky Sadick, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Mhe. Rais Kikwete, Mhe. Muhongo, Mhe. Sadick na Balozi wa Marekani hapa nchini, Mhe. Alfonso Lenhadrt wakimsikiliza Mhe. Rais Obama.

Wageni mbalimbali wakiwemo Maafisa Waandamizi kutoka Serikalini wakimsikiliza Mhe. Rais Obama (hayupo pichani).

Wageni mbalimbali wakiwemo Maafisa Waandamizi kutoka Serikalini wakimsikiliza Mhe. Rais Obama (hayupo pichani). Mstari wa kwanza kutoka kulia ni Balozi Dora Msechu, Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Balozi Liberata Mulamula, Msaidizi Mwandamizi wa Rais katika masuala ya Diplomasia na Balozi wa Tanzania nchini Marekani.

Mhe. Rais Kikwete akiteta jambo na Mhe. Prof. Muhongo.

Mhe. Rais Obama akizungumza na Prof. Muhongo mara baada ya kutangaza Mpango Maalum wa Maendeleo ya Nishati Barani Afrika ulioanzishwa na Marekani  (Power Africa Initiative).

Mhe. Rais Obama akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Sadick

Mhe. Rais Obama na Mhe. Rais Kikwete wakiwa katika eneo la Mitambo ya Symbion.

Mhe. Rais Obama na Mhe. Rais Kikwete wakimsikiliza mmoja wa Wataalam aliyebuni kifaa mfano wa mpira ambapo kinapojaa upepo kwa kupigwa huweza kusababisha nishati ya umeme ambayo hutumika kwa matumizi mbalimbali kama kuchaji simu na kuwasha taa.

Mhe. Rais Obama na Mhe.Kikwete wakijaribu kupigiana kifaa hicho mfano wa mpira.
Mhe. Rais Obama na Mhe. Rais Kikwete wakiangalia kifaa hicho kikiunganishwa kwenye moja ya taa kabla ya kuwashwa.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.