Sehemu ya Masanduku yenye miili ya askari saba wa Jeshi la
Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliofariki dunia hivi karibuni mjini
Darfur nchini Sudan wakati wakilinda amani, yawasili nchini leo kwenye Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wanananchi wa Tanzania (JWTZ)
wakiwa wamebeba moja ya masanduku saba yenye miili ya askari wa jeshi hilo
waliofariki dunia mjini Darfur wakati wakilinda amani.
Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wanananchi wa Tanzania (JWTZ)
wakipakia moja ya masanduku saba yenye miili ya askari wa jeshi hilo
waliofariki dunia mjini Darfur wakati wakilinda amani.
Askari hao waliuwawa kwa shambulio la kushtukiza na kundi la
waasi wakati wakiwa kwenye kazi yao ya kulinda amani nchini Sudan.
Jeshi la JWTZ lilioa taarifa likisema kuwa tukio hilo ni
pigo kubwa kwa nchi yetu ya Tanzania ikiwa ni la kwanza kutokea tangu Tanzania
ilipoanza kuchangia walinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa mwaka 2007.
Picha na maelezo kwa hisani ya www.issamichuzi.blogspot.com
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.