Thursday, August 22, 2013

Mhe. Membe apokea msaada wa Magari ya kubebea wagonjwa kutoka Korea Kusini

Na Zainabu Abdalah

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama Mkoani Lindi Mheshimiwa Bernard Membe. Jana amekabidhiwa msaada wa magari manne ya kubebea wagonjwa kwa ajili ya wananchi wa Majimbo ya Nchinga na Ruangwa ya mkoani Lindi na Balozi wa Korea nchini, Mhe. Chung Il.

Hafla hiyo imefanyika nyumbani kwa Balozi huyo Osterbey Dar es Salaam na ilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Serikali za Mitaa naTawala za Mikoa (Tamisemi) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ruangwa, Mheshimiwa Kassim Majaaliwa na Mheshimiwa Said Mtanda, Mbunge wa Jimbo la Mchinga, Lindi.

Magari hayo manne ya kubebea wagonjwa yaliyokabidhiwa ni kwa ajili ya vituo vinne vya Afya vilivyopo katika Majimbo hayo ambavyo ni Sokoine, Kitomani, Ruangwa na Milola.

Waziri Membe ameishukuru sana Serikali ya Korea Kusini kwa msaada huo na kuahidi kuwa utatumika vizuri kama ulivokusudiwa. Aidha, alisema Serikali ya Tanzania itaendelea kudumisha ushirikiano mzuri uliopo na Serikali ya Korea Kusini ambao ulianza miaka mingi iliyopita.

 

 

 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.