Mhe. Balozi Batilda S. Burian akishiriki katika zoezi la utolewaji wa damu pamoja na Watanzania wengine aliyoambatana nao, mapema leo mjini Nairobi.
Mhe. Balozi Batilda S. Burian akishiriki katika zoezi la utolewaji wa damu pamoja na Watanzania wengine aliyoambatana nao, mapema leo mjini Nairobi.
WATANZANIA WAISHIO KENYA WAITIKIA WITO WA KUJITOLEA
DAMU KWA AJILI YA WAATHIRIKA WA TUKIO LA UGAIDI, NAIROBI KENYA
Mhe. Balozi Batilda S. Burian, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania nchini Kenya, ameongoza umati wa Watanzania waishio hapa Nairobi leo
kujitolea damu kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tukio la Ugaidi
lililotokea Tarhe 21 Septemba 2013 Nairobi Kenya, ambapo hadi sasa zaidi
ya watu 62 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 179 wamejeruhiwa vibaya na
wengi wao bado wanaendelea kupata matibabu katika hospitali za Aga Khan
University Hospital, Hospitali ya Nairobi ( Nairobi Hospital), na Hospitali ya
MP Shah.
Katika tukio hilo pia Mtanzania, Bwana Vedastus Nsanzungwanko,
Meneja, Child Protection, UNICEF ni mmoaa wa wale walioathirika na tukio hilo
ambapo alijeruhiwa kwa risasi na magrunet katika miguu yake yote
miwili. Hivi sasa Bwana Vedastus amelazwa katika hospitali ya Aga Khan, Nairobi
na anendelea kupatiwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri.
Picha na
maelezo kwa hisani ya Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini
Kenya
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.