Tuesday, October 29, 2013

Mhe. Membe akutana na Mkuu wa chombo kipya cha EU kuhusu Usalama Majini



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Bw. Etienne de Poncins,  Mkuu wa Chombo kipya chini  ya Jumuiya ya Ulaya (EUCAP Nestor) kinachoshughulika  na utoaji mafunzo katika masuala ya Usalama  Majini kwa nchi za pembe ya Afrika. Bw. Poncins alifika Wizarani kwa ajili ya kuwasilisha rasmi ombi kwa Serikali ya Tanzania la kujiunga na Chombo hicho ambacho lengo lake kuu ni kutoa mafunzo, misaada ya kiufundi na kisheria ili kuziwezesha nchi washirika kukabiliana na matukio mbalimbali ya Uharamia na Ugaidi yanayotokea katika Bahari Kuu ikiwemo Pwani ya Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika.

Balozi wa Jumuiya ya Ulaya hapa nchini, Mhe. Filiberto Cerian Sebregondi (kulia) akimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) alipozungumza nao kuhusu masuala mbalimbali ya Usalama Majini.


Mhe. Membe akimsikiliza Bw. Poncins akielezea utendaji kazi wa Chombo hicho cha EUCAP Nestor.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dora Msechu (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kushoto) na Bibi Victoria Mwakasege, Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Ulaya na Amerika wakimsikiliza Bw. Poncins (hayupo pichani).

Mazungumzo yakiendelea

Mhe. Sebregondi akichangia jambo wakati wa mazungumzo kati ya Mhe. Membe na Bw. Poncins (hawapo pichani)

Maafisa kazini! Kutoka kushoto ni Bi. Zulekha Fundi na Bw. Frank Mhina, Maafisa Mambo ya Nje wakinukuu mazungumzo kati ya Mhe. Membe na Bw. Poncins (hawapo pichani).

Mhe. Membe akisisitiza jambo kwa Mhe. Sebregondi na Bw. Poncins baada ya kumaliza mazungumzo yao

 
Picha ya pamoja.
 




No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.