Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Umoja wa Mataifa itakayoanza kuadhimishwa tarehe 17 hadi 24 Oktoba, 2014. Wiki hiyo ambayo huadhimishwa kila mwaka itajumuisha matukio mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mjadala wa Wazi utakaofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tarehe 22 Oktoba, 2013 na maonesho ya shughuli mbalimbali za Umoja wa Mataifa na Wizara ya Mambo ya Nje yakayofanyika Viwanja vya Karimjee tarehe 23 na 24 Oktoba, 2013 . Kilele cha maadhimisho hayo ni tarehe 24 Oktoba ambapo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) atakagua Gwaride rasmi na kupandisha Bendera ya Umoja wa Mataifa. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni "Tanzania ya Kesho Tunayoitaka". Mwingine katika picha ni Alberic Kacou, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.