Balozi Modest Mero, Balozi wa Tanzania katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Geneva akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Bw. Roberto Azevedo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara ya Kimataifa Duniani yaani World Trade Organisation(WTO) mjini Geneva, Uswisi.
Balozi Modest Mero, Balozi wa Tanzania katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Geneva katika mazungumzo.
Picha ya pamoja Balozi Mero, Mama Mero na Bw. Azevedo.
Mheshimiwa Balozi Modest Mero, Balozi wa Tanzania katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Geneva amewasilisha hati za utambulisho kwa Bw. Roberto Azevedo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara ya Kimataifa Duniani yaani World Trade Organisation(WTO) mjini Geneva, Uswisi.
Katika mazungumzo, Mkurugenzi Mkuu amemfahamisha Mh. Balozi kuwa Shirika la Biashara Duniani liko katika hatua za mwisho kukamilisha majadiliano ya mikataba ya Biashara ya Kimataifa katika maeneo matatu kwa pamoja ikiwa ni masuala ya Kilimo, Maendeleo na Uwezeshaji Biashara.
Aidha, Mkurungenzi Mkuu alielezea mahusiano mazuri aliyonayo na nchi yetu kwa kipindi kifupi akiwa kama Mkurugenzi Mkuu, na kuwa aliliona hilo wakati wa kampeini yake alipokuja nchini kuomba kura yetu. Ni kwa mantiki hiyo na imani aliyo nayo kwa Tanzania, Mkurugenzi huyo ameomba Tanzania itumie ushawishi wake ili kufanikisha mkutano wa Mawaziri wa Biashara utakaofanyika mjini Bali Indonesia kuanzia tarehe 3-6 December 2013, ili kupitisha mikataba ya Biashara katika maeneo matatu yaliyotajwa hapa juu.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.