Friday, November 29, 2013

Wakurugenzi wa Sera na Mipango wapigwa msasa kuhusu maandalizi ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia



Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais-Tume ya Mipango, Bw. Philp Mpango akiwakarabisha Wakurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara na Taasisi nyingine za Serikali pamoja na wageni waalikwa katika kongamano ambalo mzungumzaji alikuwa Balozi Celestine Mushy, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kongamano hilo lilifanyika jengo la Golden Jubilee jijini Dar es Salaam. 


Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akiwasilisha mada yake kwa wajumbe. Mada hiyo ilihusu mchakato wa kuandaa Malengo ya Maendeleo Endelevu na Agenda ya Maendeleo baada ya mwaka 2015 ambao ni mwaka wa mwisho wa kutekeleza Malengo ya Milenia (Sustainable Development Goals and Post 2015 Development Agenda). Balozi Mushy alisisitiza umuhimu wa taasisi zote husika kushiriki katika vikao vya maandalizi vya mchakato huo au wakishindwa kushiriki waandae taarifa za maandishi ili watakaoshiriki waziwasilishe.


Balozi Mushy akiendelea na mada yake.


Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nao wakisikiliza mada.


Balozi Mushy akibadilishana mawazo na mmoja wa wajumbe wa kongamano hilo baada ya kumaliza kazi ya kuwasilisha mada.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.