Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Waandishi wa Habari ( hawapo pichani) juu ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kiamataifa katika Ofisi za Idara ya Habari (Maelezo). Wakati wa Mkutano huo Mhe. Membe alizungumzia masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutetea suala la Uraia wa Nchi mbili kwa Watanzania waishio ughaibuni kupitia Bunge Maalum la Katiba, Kuchaguliwa tena kwa Tanzania kwenye Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika, Nafasi ya Tanzania katika Ulinzi wa Amani duniani na kuendelea kudumisha Uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Rwanda. Wengine katika ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Rajabu Gamaha (wa pili kutoka kushoto), Balozi Simba Yahya (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati na Bw. Assah Mwambene Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo). |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.