Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Seif Sharrif Hamad, akisaini Kitabu cha Wageni alipotembelea Banda la Maonesho la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Maonesho ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanafanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 15 hadi 16 Aprili, 2014 na kuzihusisha Wizara na Taasisi za Muungano. Lengo la maonesho hayo ni kuwaeleza wananchi mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 50 ya Muungano, changamoto na namna ya kuzikabili pamoja na matarajio ya baadaye kuhusu Muungano huo. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.