Mhe. Bernard K. Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa akiwa kwenye mazungumzo na
Mhe. Mark Simmonds, Waziri wa Uimgereza
anayeshughulikia masuala ya Afrika kwenye Wizara ya
Mambo ya Nje ya Uingereza leo tarehe 11 Juni 2014.
Pamoja na mambo mengine, Mawaziri hao wamezungumzia
maazimio ya Mkutano wa Kimataifa kuhusu Ukomeshwaji
wa Udhalilishaji wa kijinsia kwenye maeneo yenye
Migogoro (''End Sexual Violence in Conflict") unaoendelea
mjini London, Uingereza. Tanzania inashiriki Mkutano huo
kufuatia mualiko wa Serikali ya Uingereza kutokana na
mchango mkubwa wa Tanzania katika kufanikisha kuwepo
kwa Tamko la Umoja wa Mataifa linalo husu suala hilo
(Declaration of Commitment to End Sexual Violence in
Conflict). |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.